Mmiliki na mwendeshaji wa kampuni ya TK Media (wachapaji wa gazeti la Jitambue) bwana MUNGA TEHENAN amefariki jana jumatatu saa mbili na nusu asubuhi katika hospitali ya Shree Hindu Mandal ya jijini dar es salaaamu alikolazwa kwa muda mfupi kwa kusumbuliwa na moyo.
Hayati Munga alikuwa muelimishaji wa utambuzi kwa njia ya darasa pale kimara na kwa njia ya vitabu, kanda, CDs TV na kwa njia ya gazeti (Jitambue).

Kwa mujibu wa familia yake, mazishi ya Hayati Munga yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya Kisutu (karibu na jengo la uvccm-dsm)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2008

    Poleni KWETU SOTE tukiwemo wasomaji na wasikilizaji wa habari zake za Jitambue. Yaani Mwandishi wa JITAMBUE kafa bila kujitambua kuwa atakufa na wala kutambua siku ya kufa.Pole Kwetu sote wasomaji,waandishi na wasambazaji wa habari na magazeti ya Jitambue.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2008

    Rest in Eternal Peace Munga

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2008

    mungu amlaze mahali pema peponi munga tehenan,amen

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2008

    Poleni sana kwa msiba huo mkubwa.Rambirambi ziwafikie ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu popote pale walipo.Kila chenye uhai kitaonja mauti.Mungu alitoa na sasa Mungu ametwaa kilicho chake.Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi,Amina.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2008

    ooh jamani,namkumbuka Munga wakati akisimamia kipindi cha jitambue enzi hizo TVT,alikuwa ana kipaji sana cha kuchambua mambo ya jamii.nimesikitika kweli,RIP brother

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2008

    KUMUENZI MAREHEMU TUNA HAJA YA KUFUATA YOTE ALIYOKUWA AKIFUNDISHA,
    BWANA ALITOA NA AMETWAA,JINA LAKE LIHIMIDIWE,
    BOFYA http://www.tkmedia.co.tz/Archives.htm
    MOJA YA MAKALA YAKE KUHUSU KIFO:
    Hivi karibuni nimesoma kuhusu mtu anayedaiwa kuwa mzee kuliko wote duniani kwa sasa. Mtu huyu mwenye umri wa miaka 111, ambaye ni Mjapani, alipoulizwa maoni yake, alisema, hataki kufa. Nilianza kujiuliza, hivi ni lini kifo kitakuwa ni jambo la hiari na lenye kupendeza? Lakini, hata hivyo, mbona maisha ni mafupi sana, hata kama mtu atapewa miaka 200 ya kuishi!

    Binafsi, napenda kufurahia maisha yangu, lakini najua kwamba maisha ni mafupi sana. Watu wengine wanakiona kifo kama tatizo kubwa linalowazonga.

    Watu wengi ambao walishaaga dunia kama vile mababu wa mababu zetu mimi nahisi kama wanaishi vizuri tu huko walikoenda.

    Ni kujisumbua kukikataa, kukiogopa au kukiona kifo kama ni tatizo kubwa ajabu. Wengi wa waliokufa wanakiona kifo sawa na mtu aliyemaliza shule na kufuzu. Inabidi hivi sasa tubadilike na tukione kifo kama mtu aliyepitiwa na usingizi wenye jinamizi na kuamkia kwenye ulimwengu wenye amani na usalama.

    Lazima wote tufe! Lazima tuishi maisha haya tuliyoyazoea na baadaye tuondoke twende tukaishi maisha mapya ambayo hatukuyazoea. Tujue kwamba maisha tuliyoyazoea ni ya muda tu, na maisha ambayo hatukuyazoea ni ya muda mrefu.

    Kama umetafakari kwa makini nafikiri umeshaona kwamba hakuna binadamu anayeishi milele. Mamilioni ya watu wanaoishi duniani ni wafu watarajiwa.

    Wengine wanajitahidi kusogeza maisha yao mbele lakini iko siku itawadia na wataondoka, watake wasitake. Nahisi kwamba watu hung’ang’ania maisha ya dunia kwa sababu hawajui maisha baada ya kufa yakoje.

    Wazo langu ni kwamba kifo si chanzo cha mateso. Chanzo cha mateso ni raha za muda ulizonazo duniani. Unaona kwamba kifo kitakuondolea raha hizo.

    Hivi mtu ambaye yuko kwenye maumivu makali ya kupigwa risasi na damu inamwagika kwa kasi bado atatamani aishi? Atataka afe ili aondokane na maumivu makali anayoyapata.

    Kifo ni rafiki yetu wa kweli. Kifo kinatutahadharisha kwamba tusiyategemee sana maisha tunayoishi. Kifo kinatukumbusha kwamba kila dakika tuliyonayo inapaswa itumike ipasavyo. Somo kubwa tulipatalo kutokana na kifo, inabidi liwe kwamba maisha baada ya kifo ni ya furaha na watu tukubali kifo, tuwe tayari wakati wowote kufa.

    Hebu jiulize swali lifuatalo: ‘Hivi niko tayari kufa sasa hivi?’ Kama jibu lako ni hapana, ni kitu gani kinachokufanya utake kuendelea kuishi? Unaogopa kufa au unaogopa kupoteza mali zako ulizochuma kwa jasho?

    Ukweli ni kwamba kama kifo kipo na haijulikani kitakufika lini, haina haja wewe kuogopa kwa sababu una umri mdogo au una mali nyingi. Uoga huu ni kwa sababu hatujajiandaa kufa. Kama unataka suluhu na kifo basi jiandae kufa.

    Siyo lazima uwe tajiri sana, na baada ya kufikia lengo hilo ndiyo uwe muda muafaka wa kufa. Hivi sivyo. Sijatimiza yote niliyopanga, lakini niko tayari kufa sasa hivi. Ndiyo maana siogopi kifo na wala sikioni kifo kama janga. Kifo ni sehemu muhimu kwenye maisha yangu!

    Kweli kuna mambo mengi sijayafanikisha, lakini juhudi nilizofanya zilikuwa sahihi. Sasa tatizo liko wapi hadi nidhani nastahili kufa baada ya mafanikio tu! Malengo yangu yalikuwa mazuri sana lakini sikuyatimiza kama nilivyopanga.

    Hapa cha msingi ni malengo kuwa mazuri lakini kama binadamu nina kikomo cha uwezo wangu. Maumbile hayakutaka kila nililotakla liwe kukamilika.

    Hii inatosha kukufariji na kujua kwamba umetenda uliyopaswa kufanya, na hii inatosha kukikaribisha kifo kikuchukue bila woga, kwamba kuna kitu hukukitimiza.

    Ukishajua hivi hutakiogopa kifo na utaishi maisha yenye furaha uwe na umri mdogo, maskini au tajiri.

    Kuogopa yanayohusu kifo hilo ndilo janga la kweli, lakini kifo kamwe si janga. Kwani, aliyekwambia kwamba, kifo kina ubaya ni nani? Ni dini yako, ambayo inakutishia kuhusu moto, majoka na hasira za Mungu! Dini ingekwambia, baada ya kifo ni amani na furaha tupu isiyo na mwisho, usingethamini maisha haya ya shida ya kidunia.

    Maisha baada ya kifo ni ya milele. Kama ni ya milele yataweza vipi kuwa ni maisha ya shida na mashaka? Maisha ya shida na mashaka ni ya yale yenye muda maalumu, tena mfupi.

    Kila mmoja anataka kutimiza jambo fulani na anafukuzana na muda katika kutaka kufanya hivyo. Ndiyo maana kifo kinatazamwa kama adui.

    Kama nilivyosema awali, kila mtu amefundishwa kuwa kifo hatima yake ni shida na mateso, ni hofu na vitisho. Mimi siamini kwamba, kwa Mungu mwenye upendo na huruma na usamehevu kunaweza kuwa katika mazingira ya aina hiyo. Jela za binadamu ndiyo ziko hivyo kwa sababu wana visasi, siyo kwa Mungu!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 06, 2008

    Bwana amaetoa, na Bwana ametwaa, jna la Bwana lihimiduwe. Kwa kweli tutakukosa sana bwana Munga. Nasikitika kumpoteza mkombozi wa wanyonge, mtanzania mwenye nia ya kuhelimisha Watanzania wenzake. Umeondoka na kutuacha katika kipindi kigumu ambacho nchi imegubikwa na wimbi la mafisadi.

    Kuondoka kwako ni msiba mkubwa kwa taifa. Umpumzike kwa amani. Amina.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 06, 2008

    Inna lillah waina ilayhi rajiun,

    Aise ni msiba mkubwa.Huyu Munga nimesoma nae pale Chuo kikuu Mlimani na pamoja na rafiki yangu Chikoko. Na baadae nilishirikiana nae alipokuwa anachapisha gazeti.Mungu ampe malazi pema.Aise yaani kifo, we acha tu!

    Rambirambi zetu zifike.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2008

    Du! Jamaa kafa bila kumuona uso! Nilitamani san siku moja kuonanan nae. Ni miongoni mwa watu walionisaidia sana kimaisha kwa makala zake. Kuna wakati aliandikia Dar Leo makala za Saikolojia. Kwa kweli alikuwa mtu.

    Jambo jingine, harusi yake na yangu zilikuwa sawa japo hatukuambiana, wala kujuana. Yaani harusi za watu wenye uwezo lakini simple!!!! mnafunga kanisani halafu watu wanaimba kisha mnakwnda nyumbani!!!

    Binafsi nitamkumbuka sana. Nawapa pole wote waloguswa kwa karibu. Mungu awape faraja ya kweli,

    Amen

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2008

    Do! Hizi ni habari za kusikitisha.
    Nimemfahamu Munga kwa mara ya kwanza pale alipopata zawadi KWANZA ya kuwa mwandishi bora wa riwaya ya kiswahili, mwaka 1997 pale Goethe Institute-DSM. Hadithi yake ya "RAIS WA KESHO"

    Baada ya hapo kitabu hicho kilichapwa na Ndanda Publishers, lakini kwa sababu zisizofahamika, kitabu hicho kilichapwa nakala chache sana na pia hakikuwahi kuwekwa sokoni. Ingawa pesa za uchapaji wa kitabu hicho kwa nakala nyingi zilitolewa toka kwa mdhamini wa zawadi ile.

    Mwaka 2004 nikishirikiana na Mswedish fulani tulikitafsiri kitabu hicho kwenda kwenye lugha ya Kiswedish kikitwa "PRESIDENTKANDIDATEN" na kinasabazwa na Books-on-Demand,Visby. Kitabu hicho ambacho pia kilitumia mchoro wangu kwenye cover ya mbele. kimependwa na waswedish wengi hasa wale waliowahi kufanya kazi Tanzania au kusihi Tanzania, na kuifahamu nchi hii


    Nimekuwa nikimtumia Munga kwa ushauri mbalimbali, pia kwenye projects zangu mbalimbali.

    Ni Pengo kubwa kwa waandishi wa vitabu, wanafalsafa, wanasaikolojia, na wapenzi wa ubunifu kama sisi. Munga alikuwa bado kijana na mpenda maendeleo wa aina yake. Amechangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya watu binafsi hasa wale waliowahi kujadiliana nae, kusoma, au kufuatilia maandishi yake kisaikolojia.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2008

    Asante Kaka Michuzi kwa taarifa. Kwa kweli nimesikitika sana kwa msiba wa Mr. Munga. Binafsi niliweza kumjua wakati wa vipindi vyake vya Jitambue kupitia TVT. Nilikuwa ninapenda jinsi alivyokuwa akiviendesha vipindi hivyo kwa upeo wa juu. Yaani unaona kabisa ni mtu aliyetulia na anajua ni nini anachokifanya. Bila shaka Watanzania waliokuwa wanaviangalia, wengi walinufaika.

    Napenda kuwapa pole wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mkubwa walioupata. Mungu awape moyo wa uvumilivu. Hayo ndiyo maisha yetu sisi wanadamu.

    Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2008

    Mungu ailaze roho ya Marehemu Munga mahali pema peponi. Kwa kweli Munga ni mtu mwenye kipaji cha pekee. nasema hivyo kwa kuwa watu wengi amewasaidia kisaikologia na mimi nikiwa mmoja wapo kupitia gazeti la JITAMBUE lililokuwa likitoka kila j.5. nakumbuka mara ya kwanza kumjua Munga kuna kijana mmoja nilikuwa nafanya nae kazi sasa mimi nikawa nilikuwa fastreted akaniambia nisome gazeti la JITAMBUE ambalo lilikuwa likitoka kila J.5. kwa kweli nilisona na nilijitambua kweli kupitia hilo gazeti na kila nilichokuwa kikisoma kila j.5 na kuangalia kwenye TVT, kilikuwa kinanihusu mpaka nikapata relief. sikuchoka nikaendelea kulisoma sana tu. BUT Munga amekufa imeniuma sana jamani. ngoja nimweleze rafiki yangu nae tulikuwa tukisoma nae. poleni sana wafiwa jamini, naona mnavyoumia ndio mimi pia naumia hivyo hivyo.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 08, 2008

    Dah!! nimeshtushwa mna habari hiyo .. mimi namfahamu Munga Toka yupo Uhuru na mzalendo ..MPAKA TUKAANZISHA gazeti la Cheche mimi nikiwa mmoja wa waanzilishi pamoja na marehemu alinisaidia sana katika kutunga maswala ya poroja kwani alikuwa namba wani kwa mabo ya porojo

    mungu amlaze pema pepeponi

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 08, 2008

    jamani poleni sana wafiwa alikuwa natoa mafunzo mazuri sana kwa bei poa ambayo huku ulaya kuyapata ni gharama kubwa sana kwa kweli alinisaidia sana mimi kujitambua vizuri tu poleni sana wafiwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...