Na John Nditi, Morogoro

MAHAKAMA ya Mwanzo ya Nunge ya Manispaa ya Morogoro, imemhukumu omba omba maarufu Matonya Mazengo, kutumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka amri iliyomzuia kuendelea kufanya kazi ya kuomba mitaani.

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu, amethibitisha kuhukumiwa kwa Matonya baada ya kufikishwa Mahakamani na Idara hiyo Mei 19, mwaka huu baada ya kukiuka masharti aliyopewa ya kumtaka asiendelee na shughuli za kuomba omba katika mitaani ya Manispaa ya Morogoro.

“ Ni kweli alikamatwa na askari wa Mgambo wa Manispaa ya Morogoro na kuletwa kwetu sisi wa Idara ya Ustawi wa Jamii ili kupata ushauri wetu kwa kusudio la kumfikisha Mahakamani” alisema Ofisa huyo wa Mkoa wa Ustawi wa Jamii

Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro, Matoya awali alikamatwa na Askari wa Mgambo wa Manispaa mwishino mwa mwaka jana katika zoezi la kuwaondoa ombaomba mitaani na kutakiwa kujaza fomu ya kula kiapo cha kuacha kuomba mitaani na kubalia Kambi ya Wazee wasiojiweza ya Fungafunga ya Mjini hapa.

“ Matoya alikula kiapo cha kuacha kuomba na kurudishwa Mkoani Dodoma pia aliahidi endapo akirudi Morogoro ataishi katika Kambi ya Wazee wasiojiweza na iwapo atajihusisha na kuomba basi apelekwe Mahakamani afungwe jela” aliongeza kusema Ofisa huyo.

Kwa mujibu wa Ofisa huyo , Matonya aliamua kurudi tena Mkoani Morogoro mwanzoni mwa Mei mwaka huu na kuendelea kukaa eneo la daraja la Shani Cinema na kufanya shughuli za kuomba omba kwa staili ya kulala chali chini katika eneo hilo la Daraja.

Alisema kufuatia kuwepo kwake katika eneo hilo na kuendelea na kazi hiyo , alikamatwa na Askari wa Mgambo na kufikishwa katika Ofisi za Ustawi wa Jamii na baadaye kufikishwa Mahakamani.

Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa Idara ya Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Matoya amepelekwa katika Kambi ya Wazee wasiojiweza ya Funga Funga akisubili fedha za kumsafirisha kurudi makwao.

“ Hiki kifungo cha nje cha mwaka mmoja ni kuachakutembeea mitaani kwa kazi ya kuomba…tukizipata fedha kutoka Halmashauri ya Manispaa sisi Idara ya Ustawi wa Jamii kutamsafirisha kurudi nyumbani kwao Mkoani Dodoma” alisema Ngungamtitu

Kwa mujibu wa Ofisa huyo, ombaomba wengi waliorudishwa makwao wamerudi tena na kubadili mfumo wa uombaji wa kukaa barabarani ambapo kwa sasa wanapita katika maeneo ya Mahoteli, Baa na Migahawa wakiongozana kwa zamu kwa ajili ya kuwaomba wateja.

Hivyo kutokana na kushamiri kwa hali hiyo, Ofisa huyo ameushauri Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuchukua hatua kwa kuwaelekeza Askari wa Mgambo kuendesha msako katika maeneo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. NCHI YENYEWE KUTWA TUNAOMBAOMABA KWA WAHISANI IWAJE MATONYA ANANYIMWA HIYO HAKI. WANZA MATONYA NI CELEBRITY MBONA MANAMTELEKEZA

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2008

    Michuzi naomba upost contacts za mwanasheria anayeweza kumsaidia huyu mzee na gharama zake ili wanaglob wamsaidie

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2008

    Hivi kuna Wakosaji na Mafisadi wangapi WANAPETA? mbona mnapenda kuonea WANYONGE?? OMBAOMBA, mnamfunga MAJAMBAZI yako mtaani!!Kwa hiyo akirudia kuomba inakuwaje mnampeleka Jela kabisa au??? Fuatilieni Mambo ya msingi...

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2008

    Kwa kweli hata mimi sipendi michango ila ntachangia,AU NADHANI tumsaidie kiaina nyingine asirudi mtaani kuomba omba. ndio kusaidiana maisha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2008

    si bora huyo anayeomba!mafisadi wanaiba hawafungwi!leo Matonya anaomba anafungwa?Tanzania hakuna Haki

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2008

    Inaonekana wadau wengine hawasomi makala kwa ufasaha,Matonya amefungwa kifungo cha nje na sio gerezani, sasa kuna mdau anataka mwanasheria amsaidi.Sasa asaidiwe nini zaidi ya hivyo kuwekwa kwenye nyumba ya wazee na kurudishwa kwao Dodoma.

    Matonya ni mzee sana na hakuna hakimu yoyote duniani anaweza kuwa katili na kumfunga Gerezani kwa kosa hilo la kipuuzi kwani ombaomba wapo hata Ulaya na duniani kote kwa ujumla.Kama Nchi yetu inaomba fedha hata za bajeti unategemea wananchi nini wafanye kama nawao (wasiojiweza) kuishi mitaani kuombaomba kama chokoraa wa kenya.

    POPO

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2008

    Yaani Halmashauri imekosa la kufanya mpaka kumg'ang'ania Matonya.
    Kuna vitu vingi vya kufanya na wamuache mzee wa watu aendelee kuomba.
    Kumrudisha kwao sio tatizo, wangemtafutia kitu cha kufanya.
    Omba omba wapo kila sehemu hata huku Ulaya wapo, sasa iweje Matonya ananyanyaswa?
    Kuweni na huruma jamani!!!!!!!!!
    Mwenzetu ndio kazi yake.
    Kaka Paul, UK

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2008

    Hakuna anaeupenda umasikini na kama kungekuweko mfumo ambao utawasaidia watu wenye kipato cha chini Matonya sidhani kama angependa kujidhalilisha. Hivi badala ya kukasirinia tulikoangukia tukasirikie tuliko jikwaa.
    Je tuna mfumo utakao/unao saidi ombaomba? Kama upo unafanikiwa au ndio kama jela?
    Kwanini serikali isifilisi mafisadi wote halafu wawapatie ombaomba waone kama Matonya atarudi Samora! Na kama akirudi atakuwa katika Prado kama Papaaa ... nanihiiiii!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 23, 2008

    Ninavyofahamu kaka Michu ni kwamba kweli Matonya ni Omb...mba. Ila aliamriwa na manispaa kuacha kuomba na akahifadhiwa katikanyumba ya Wazee ya Nunge(Morogoro kuna kituo cha watu waiojiweza)ili akae na wazee wenziwe na kusaidiwa na jamii kama kawaida kwani mahitaji hayatoshi toka serikalini
    Ni kawaida makundi tofauti hujuika kwenda kutoa misaada mbalimbali katika kituo hicho..ikiwa ni chakula,mavazi,pesa kidogo za kujikimu(kama wanazo watoaji)na mahitaji mengine ya kawaida.
    Matonya alikiuka agizo hilo na kuamua kurudi mtaani na kuendelea kuomba..kufikishwa kwake mahakamani ni jitihada ya manispaa kumuondolea uwezekano wa kupatwa na mabalaa mengine..ikumbukwe kuwa Matonya ni mtu mwenye umri sasa ni sio kijana tena...hivyo anatakiwa kutunzwa kama wengine...yeye hataki anarudi barabarani....hivyo labda kumfunga kifungo cha nje kutamsaidia naye apumzike...na si kwamba amefungwa eti sababu ni ombaomba..la hasha sidhani hivyo..nafikiri waale wenye utaalamu na masuala ya jamii mtaungana nami...

    Mwisho kama nilivyoeleza, watu wote jamani ni vizuri kama unajisikia una ziada kidogo ukapeleka msaada kidogo kwa wazee wetu wa Nunge pale Morogoro, ili akina Matonya baada ya kuhifadhiwa hapo wapumzike na kumalizia siku zao wakitunzwa na jamii..inawezekana si ulaya tu wanaweza fanya mabo haya...hata sisi kwa kuanzia tunaweza fanya taratibu...Nasema hivyo kwani nilipokuwa Morogoro nilikuwa naenda hapo kama mmoja wa kikundi na kusaidiana na wazee hao,moja ya shughuli yetu ilikuwa kuwalimia shamba lao dogo na bustani zilizopo maeneo hayo...hatukuwa na uwezo sana hivyo tulijitolea kwa nguvu zetu na muda wetu kidogo tulioweza kuupata...natmai bado makundi tofauti yanafanya hivyo kwa wazee wa Nunge....

    Ni hayo tu

    Nyaningedere

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2008

    Yaani mmemwona Matonya tuu? mwacheni, keshazoea kuomba omba akikaa maisha yanakuwa boring.

    Kuna mengi ya maana ya kufanya kuliko kumfatilia .....eti Matonya...

    Malibe

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 24, 2008

    Huyu jamaaa Matonya Mazengo napenda kujuana naye tafadhali post picha yake kwenye blog yako and turn him into a celebrity it can be done. I want to send him a suit and some money tell me how

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 24, 2008

    nyie watu mko vipi!!?!?!?!especially wewe Tarehe May 23, 2008 8:48 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

    MATONYA AFUNGWEEEE BWANAAAA...TENA HAWA MACHOKORAA WAONDOLEWA BARABARANI.WANALETA VISNGITI, MUDA WA KUKAA NA KUOMBA ANGEENDA KULIMAA SI ANGEPATA HELA!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 24, 2008

    Unawezaje kumkamata mtu kwa kuwa maskini? Toka lini umasikini ukawa kosa la jinai?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 24, 2008

    You let Balali go free and you are dealing with poor Matonya what a shame. At least he doesn't steal from people like mafisadi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 24, 2008

    anon 12:47 punguani kweli wewe, hiyo hela ya suit,si ukatoe charity jamani!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 26, 2008

    Nchi yenyewe OMBAOMBA,Leo unashangaa Mze Matonya kuwa Ombaomba,huu siyo Unafiki huu?Kwanza ikatazeni Serikali Kuu kama ubavu huo mnao,iache mara moja tabia ya kukutana na wahisani wa nje kila mwaka KUOMBAOMBA KAMSAADA?Tabia hiyo chafu itakwisha lini?Mkisha fanikiwa kulitekeleza hilo sasa washukieni wakina Matonya,hapo tutawaelewa.Majahili wakubwa nyie!Ufisadi aaa hamuuoni ila ombaomba !Hebu Oneni haya kwanza Mafisadi wakubwa nyie!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...