Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka nchini leo jioni (25 Mei, 08) kuelekea Japan kuhudhuria mkutano wa nne unaohusu maendeleo ya Afrika, ujulikanao kama Tokyo International Conference on African Development (TICAD) utakaofanyika katika jiji la Yokohama.

Kabla ya kuhudhuria mkutano huo, Rais Kikwete atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Yasuo Fukuda, tarehe 27 Mei, 08 kuzungumzia mahusiano na ushirikiano wa nchi mbili hizi katika maswala ya kiuchumi na kidiplomasia na pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Kikwete anatarajiwa kumweleza mwenyeji wake juu ya maendeleo na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika na kujadili utatuzi wake.

Japan ni mshirika mkubwa wa maendeleo ya Tanzania ambapo Japan ni moja ya nchi zinazoisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchangia katika bajeti na pia imechangia katika misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula, barabara na maji

Mkutano wa nne wa TICAD utaanza tarehe 28-30 Mei, ambapo viongozi wote wa bara la Afrika wamealikwa kuhudhuria pamoja na viongozi wa Japan, wakuu wa mashirika mbalimbali ya kimataifa duniani kama vile Umoja wa Mataifa, mashirika ya fedha duniani, taasisi sizizo za kiserikali kutoka bara la Asia na Afrika, nchi rafiki na wenza katika maendeleo duniani.

Mbali na mkutano wa TICAD Rais pia atashiriki mikutano na makongamano mbalimbali yanayohusu uchumi, miundo mbinu, maendeleo na maswala mbalimbali yanayohusu utunzaji wa mazingira barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Aidha Rais Kikwete ataongoza mkutano utakaojadili tatizo la chakula duniani ambapo atazungumzia swala hili kwa kina hususan katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo barani Afrika na hatimaye atashiriki katika kupitisha azimio la Yokohama.

Rais pia anatarajia kutumia nafasi hiyo kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Afrika watakaohudhuria mkutano huo.

Rais atafuatana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Benard Membe, Waziri wa Fedha - Mhe. Mustapha Mkulo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zanzibar - Mhe. Haroun Suleiman, Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko - Mhe. Cyril Chami na Mbunge wa Muleba Kusini na Mwenyekiti wa Kamati Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama - Mhe. Wilson Masilingi.

Rais anatarajiwa kurejea Dar-es-Salaam tarehe 31 Mei, 2008.



Imetolewa na Ikulu-Dar-es-salaam
25.05.08

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2008

    Ama kweli Tanzania Raisi tumepata. Kila kukicha kiguu na njia.Maisha bora kweli yatapatikana? Mafisadi nao wanazidi katanua akiondoka. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2008

    mzushi tu nae hana lolote, yaani kama juha. mimi ananiudhi kweli anavyokumbatia ufisadi. really I hate him for that. Ukimficha mwizi nawe ni mwizi tu vile2. Michuzi usinibanie kwani sijamtukana mkuu, nakereka tu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2008

    Michuzi mwambieni mh. Raisi atulie ili ashughulikie matatizo makubwa yanayoikumba nchi kwa wakati huu kwa kupunguza safari.Aliomba kazi ili awatumikie watanzania lakini sasa hizo safari za mara kwa mara hatufiki mbali watanzania. Maisha bora tutakuwa tunayasikia kwa wenzetu.Uwenyekiti wa OAU isiwe kisingizio kwani hata kabla hajapata huo uwenyekiti alikuwa kila kukicha yeye kiguu na njia.Nchi ina matatizo makubwa sana ambayo yanahitaji kushughulikiwa kwani bila ya yeye kutulia nyumbani watanzania tutegemee maisha mabovu kuliko awamu yoyote ile ambayo ilishawahi kutokea. Kama ni kuomba mabalozi wanakazi gani? kwanini wasifanye hiyo kazi ya kuomba kwa matajili kuliko yeye kubeba vyeo vya ubalozi na uraisi kwa wakati mmoja. Kwani amekuwa miongoni mwa maraisi wazurulaji barani afrika. Kasi mpwa na nguvu mpya imehamia kwenye safari baadala ya kuwatumikia watanzania.Hao washauri wake kwanini wasimshauri apunguze safari kwani 2010 hiyoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2008

    umefika wakati tanzania tujisifu kuwa na rahis mtalii,rahis wetu anapenda sana utalii anaenda sana nje karibu kila siku.Watanzania inabid tupende utalii nas twende sana nje,tuige mfano wa rahis wetu,nashukuru uwa aend pekeyake anaenda na mawaziri hiyo yote kuonyesha anajal mawaziri ambao sisi wenyewetuliwachagua kwa kura zetu,hongera sana rahis we kata anga tu usijali si walipaj wa kod zitakusaidia katika kusafiri we na baraza lako la mawaziri.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2008

    Raisi ashauriwe apunguze safari za kila mara ili ashughulikie matatizo yanayoisibu nchi ukiwemo ufisadi na mfumuko wa bei ambayo yamerudisha nyuma jitihada za watanzania kujiletea maendeleo. Safari hizo hazionyeshi manufaa yoyote kwa nchi. Watanzania hatukumchagua kwa kazi ya kusafiri.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2008

    Huyu jamaa anakatisha tamaa sana aisee, yaani habari za ufisadi kwenye magazeti zinafunika udhaifu wake katika utendendaji kazi.....

    Yaani hata akialikwa kwenye kajimkutano kadogo tu lazima aende! Nahisi ofisini kwake "in-tray" itakuwa imejaa mafaili mengi sana yanayosubiri kupitiwa na kusainiwa......

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2008

    nyie mnalalamika nin rahis kusafiri,wivu umewajaa,mlitaka msafiri nyie,matatizo ya wananchi siyo wenyenchi.we safiri tu president usijali maneno.
    ukiwa tz wakat huu watakuuliza sana maswali ya ufisad bora uende mbali ukipenda nawewe badilisha urahia upate pakukimbilia baadaye.
    kwa kusafiri tu nakupa hongera.
    wakati unasoma ulikuwa na ndoto ya kusafiri wakati ndio huu usilaze damu we safiri,safari njema

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2008

    Raisi amekuwa mtalii, yetu macho na maskio.Utalii huu utaleta maisha bora kweli au maisha mabovu kwa watanzania.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2008

    anon wa 11:38 HUIJALI NCHI YAKO WEWE. samahani kwa kusema ivi ila huyu JK,kwa kweli is the most hopeless and helpless president in the country's history. ivi AMEFANYA NINI LA MAANA, zaidi ya kkuunda baraza jipya every 2 months, kuaccept watu kujiuzulu na ufisadi?TAFADHALI MTU MWENYE FACTS NAOMBA ANIJIBU KWA UFASAHA

    AMINA YUSUF

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 26, 2008

    na wasi wasi muda mfupi ujao president wetu ataenda kutembea sayari nyingine

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 26, 2008

    rais wetu JK,ni tourist kwa lugha ya kigeni. ni mtu anaependa kujua nchi zingine zikoje,nasikia keshawahi kwenda pluto na mars pia

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 26, 2008

    Mtalii JK katembelea Japan.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 27, 2008

    mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, rais wetu hendisamu!! na kupata uenyekiti wa sijui nini ya afrika nadhani ni kwa vile wenzie wako busy in their countries the only idle person gets to get the job... mweee.
    Michuzi, Mkapa amepasua ukimya huko kijijini kwake kuhusu tuhuma zake, naomba kama una habari kamili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...