kelly rowland wa destiny child akilengwalengwa na machozi alipokuwa akihadithia aliyoyaona na kuyasikia uwanja wa fisi huko tandale leo. uzalendo ilimshinda na machozi yalipomzidia ikabidi aondoke ghafla kwenye mkutano wake na waandishi wa habari hoteli ya kempinski alikofikia
kelly rowland wa destiny kids akizuru mojawapo ya nyumba wanamoishi wakazi wa uwanja wa fisi sehemu za tandale

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2008

    Hapa ni makao makuu ya nchi! jee huko Newala hali ikoje? na serikali inasema inaleta maendeleo kwa wananchi wote ndiyo haya maendeleo yenyewe? na tu takribani miaka 50 ya UHURU, tutafika kweli jamani, tuacha kudanganyana na tufanye kweli, hii hali inatisha nyinyi MR POLITICIANS mnaendelea kutudanganya na mnajenga MBEZI BEACH migorofa na kuendesha mishangingi hiyo ni sawa kweli MR AND MRS POLITICIANS.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2008

    Kaka Mithupu ni destny childs not "kids" na wewe nawe mmmh !

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2008

    don bother about these black americans wanafiki wakubwa,whys is she crying?kama mnakumbuka 1985 michael jackson na wengine walianzisha kundi la USA FOR AFRICA wakaimba WE ARE WORLD.ujumbe mzuri mzuri wa kuisaidia AFRICA ulizia kipi walichosaidia?kama sio kuuza milions of copies ili kulipia surguries za kubadilisha pua,
    lets hope for the best ila AFRICA we are very far behind,we need many years kufika level ya hawa exploiters,they stagnated africa.anyone who can remember the world history,back 15th century we had the same level of development.why the gap is increasing?its so so sad,
    ally.UK.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2008

    Alichokiona hakitofautiani sana na yanayojiri kati ya Beverly Hills na South Central LA.

    Kuna wakazi wa South Central LA ambao hawana maji wala vyoo, ila wao wana unafuu kwamba welfare programs zao zinafanya kazi kikwelikweli kwani wafanyakazi wa social welfare hawashindi kwenye semina na mikutano kujaza matumbo yao, bali wanakaa ofisini na kufanya kazi walizoajiriwa.

    Masikini wa South Central Los Angeles pia wana advantage nyingine ya kupata "vijisenti" & coupons kutoka serikalini kukidhi mahitaji machache ya kila siku.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2008

    Bwana michuzi Shikamoo mzee.Hii habari ni nzuri ingawa inasikitisha.Ni sawa na ileeee ya Darwin's Nightmare ya Mwanza.Angalia sana Sirikali isije ikakurarua makucha.

    OMBI:Hii Habari umeirukia Mwishoni wakati Kelly tayari yupo Hyena square haujatueleza alitoka US mahsusi kwa ajili ya hii square au alikuwa anapita tu bongo au huku TZ ndiko asili yake?Tafadhali Sheikh.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2008

    Hii ni skendo!! nchi inaweza kuchafuliwa kama ilivyochafuliwa na sinema ya mapanki.
    Najua umasikini wetu ndiyo unaotufanya tuwaonyeshe wageni kila kitu/mahali ki(pa)baya ili watuonee huruma na kuweza kupata misaada. Duh!! kweli umasikini ni kama laanaaa, masikini hana heshima, hana thamani.
    Mimi nadhani waafrica tubadilike kidogo kwani kama umasikini na uchangudoa upo kila nchi duniani. Kama lengo ni kusaidiwa kwa kuonyesha udhaifu wetu sasa tuache kwani africa inafahamika kwa mabaya na ya watu wakusaidiwa siku zote lakini misaada haikutusogeza mbali na haitotutoa katika umasikini wetu kama hatutojitegemea wenyewe. Hii ni skendo, ni aibu lakini nitashangaa wengine wakifurahia

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 18, 2008

    Hapo tunaweza kusema ni moja ya kumi ya maisha na hali halisi ya Watanzania walio wengi, tena jaribu kufikiria kuwa hapo ni mjini Dar, je huko kusikofika magari!
    Sioni ajabu yule ambaye amezaliwa na kukulia katika hali nzuri akateremsha machozi. Sioni ajabu, viongozi wetu wanaposikia watu wanashindia matunda wakakanusha! Kwani alishiba hamjui mwenye njaa, Na hawezi kuamini kuwa wapo watu wananjaa. Mtu kama huyo hajui njaa, hajui kuwa watu wengi wanaishi kwa mlo mmoja tena wakubahatisha na mbaya zaidi ni wakujaza tumbo tu.
    Wengi watasema ni sababu ya uvivu. Lakini angalia kipato cha Mtanzania wa kawaida. Kipato hiki kimelundikiwa makodi ya kila namna(kodi zilizojificha). Sasa hivi nauli juu(kwasababu tunataka super-profit), na nani anayepanda daladala kama sio mkazi wa Uwanja wa fisi, Mbagala au malalahoi kwa ujumla, bei za vyakula juu, elimu nzuri juu, dawa mahosipitalini mmmh, sisemi. Sasa huyu Mtanzania mnategemea atajiendeleza vipi. Akakopeje mtaji wa kujikimu, ilihali hana dhamana! Pesa za Kikwete alizotoa zimeishia kwa wajanja na anaishi hapa mjini!....
    Kwahiyo hapo uwanja wa fisi ni sehemu ya `maonyesho' ya hali halisi ya Watanzania walio wengi, fikeni mjionee wenyewe, na tunaomba wakija `WADHUNGU' muwakaribishe `uwanja huo wa maonyesho wa hali halisi ya Mtanzania'. Msione aibu...huenda tukapata misaada...
    m3

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 18, 2008

    you people!always with criticism! hata mimi mwenyewe ningelia. we unaelinganisha uwanja wa fisi na marekani mbumbumbu kweli!

    ila mbona kelly rowland katoka kama mbongo hapo!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 18, 2008

    we anony unaeitwa Ally wa Uk,unachuki binafsi na hao watu kwani Afrika ni Tanzania pekee inayohitaji msaada? au watoa misaada lazma watoe kila nchi ya Afrika? ni choice yao tu hivyo usipende kujumuisha wamarekani weusi wote kuwa ni wanafiki wakubwa, mbona juzi kwenye sullivan tumeona jesse jackson akiongoza harambee ya michango kwa ajili ya manyata primary school ya Arusha? na kiasi cha $50,000 kilipatakina? waswahili tuna msemo kutoa ni moyo hivyo wapo wenye moyo wa kutoa na wasio nao pia.mbona hata hapa bongo hiyo ipo hivi unadhani wote wanaosaidiwa na serikali mfano yatima hawana ndugu zao wenye uwezo kwenye ukoo wao wa kuwasaidia kabisa? jibu si wote wenye kuhitaji kusaidiwa na serikali hawana ndugu wenye uwezo wa kuwasomesha n.k lkn ni moyo wa mtu.na sio lazma mtu atoapo msaada ajitangaze wengine hawapendi kujitangaza wajulikane kwenye vyombo vya habari. wapo watu wanatoa misaada na hawapendi kujitangaza hadharani.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 18, 2008

    Mnajua bwana kuna umaskini wa aina mbili...kuna absolute poverty na relative poverty. Hapa uwanja wa fisi ni absolute poverty...wa marekani ni relative poverty. Huwezi kulinganisha hata kidogo. Pili, kumjibu yule aliyeongelea kuhusu Michael Jackson na ile USA FOR AFRICA...kwanza ile ilikuwa ni kusudi la Ethiopia. Pili sie wengi tulio na afadhali tutaangalia mara moja na kutoa chozi...kesho umeshasahau. Huo ndo ubinadamu. Bongo bwana hata matajiri wana njaa! Kuna tofauti kati ya njaa na kutafuta maisha bora. Kutafuta maisha bora ndo kuendelea...lakini njaa ndo inatuumiza. Mimi naona lazima tujifunze kutofautisha ivyo viwili. Mfano mzuri ni Mengi...ndio ni tajiri...lakini hachoki kutafuta maendeleo zaidi. Lakini pia anatoa msaada wa kunyanyua wengine. Sio kana kwamba wewe ni tajiri au ni nafuu kuliko wenzako inakuwa imetosha. Lazima uendelee kutafuta maisha bora. Njaa inakuwa pale unapotafuta kwa lazima na kwa kudidimiza wenzako. Viongozi wengi sana wanafanya ivyo...ndo ufisadi huo! Na hiyo inakuwa na 'trickle-down effect' mpk kwa watumishi wadogo. Mfano mzuri ni polisi...hasa hasa traffic police. Kwa nini aombe rushwa?...anajua ile 20,000 itaenda kuliwa huko juu tu. Hali hii kweli inatuumiza sana. Swali ni jinsi ya kuondokana nayo!

    ReplyDelete
  11. MACHOZI YA MAMBA NINI NASKIA HATA MAMA ALIOMBANAYO KURA

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 18, 2008

    kwa suala la misaada nchi zetu za africa zinasaidiwa sana jamani tuache unafiki jiulize kwa mwaka huu tu tz imepata misaada kiasigani..tatizo si misaada ila matumizi ya hiyo misaada most haiwafikii walengwa,ulaya wapo mafisadi serikalini si kama hakuna ila tofauti wenzetu ukikamatwa utashitakiwa na utarudisha pia pesa zikitolewa kwaajili yakitu fulani 98%zitatumika huko,turudi makwetu msaada utatolewa kwa wagonjwa na zi sinunuliwe hata panadol so lamuhimu hapa ni jinsi ya kuwabadilisha hawa viongozi ili tukaribie kidogo kwenye maendeleo ya kweli mi naamini hata ukiwa na kidogo lakini ukawa na plan nacho basi utaendelea so first tutokomeze mafisadi then mabadiliko tutayaona

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 18, 2008

    msemaji wa 18/06/08 saa 2:56 amesema ukweli na point zake ni za kisomi! missaada kupewa tupewe imepatikana kwanjia gani isiwe issue matumizi ndo iwe issue imetumikaje? je walengwa wamefaidika? utakuta ako kabinti machozi yatazaa matunda lakini hayo matunda baada ya kwenda kambi ya chupa yanaenda....... nyumbani anakotoka..... mipangomiji! tupo hapo wadau!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 18, 2008

    Nyie maruhuni mkome kabisa kuita uwanja wa Fisi mahali ambapo binadamu wenzenu tunaishinaishi.

    Ndio maana watakatifu wa Mungu watu waliookoka tunapenda kuita mahali hapo Uwanja wa Sifa kuheshimu binadamu wenzetu wanaoishi hapa.

    Lakini nyie maruhuni washirikina wapenda uchawi hadi bungeni mnapenda kuita uwanja wa fisi sijui kwa nini? Au mnakumbuka mafisi yenu mnayopanda usiku mkienda kuwanga ?.Au kwenye hilo eneo la Uwanja wa fisi ndiko huwa mna-Park fisi wenu mkishatoka kuwanga? Kwa nini mg`ang`anie kuita uwanja wa fisi shenzi nyie?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 18, 2008

    As much as i luv her...huyu Dada naona kapata REALITY CHECK ya hali halisi in teh world..sio all about bling bling na fame. Kuna watu wanasota....hiyo sure ilivyo i say ni PRICELESS....sorry Kelly thats a reality check my girl....be BRAVE!

    ReplyDelete
  16. NGOJA NIINGIE MITINI HIVI SISI WATANZANIA UMATONYA UTATIISHA LINI SISI NI MATAJIRI SIO OMBA OMBA HATA KIDOGO MSIJILEGEZE. NDIO MAANA MATONYA ATAKUWA MKURUGENZI WA REPOA MWAKA HUU MWISHONI AANZE KUFUNDISHA KOZI YA KUONDOA UMASIKI VYUO VIKUU DUNIANI KAMA ALIVYOTABIRI PROF DR J.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 18, 2008

    Watanzania bwana, tulilokalia ni mabishano tu! sasa inahusu nini hapa kubaruzana kuhusiana na misaada au kuufananisha uwanja wa fisi na Beverly Hills ya Marekani. La muhimu ni kwamba tatizo letu la kwanza watanzania wengi ni wabishi na washindani, suala ambalo linatufanya tusahau tatizo halisi na kujadili pambizoni mwa tatizo. Uwanja wa fisi tutake tusitake kweli ni janga, tena la watanzania wote, hiyo ni sehemu moja tu ya nchi yetu inayonyesha hali halisi ya Watanzania wengi. Tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa linachangiwa na kuzorota utendajikazi wa serikali yetu kwa kiasi kukubwa, kukosa elimu watu na kipato cha chini mno cha Watanzania. Bila kubishani inabidi tukubali uwanja wa fisi ni kitovu cha matatizo kibao likiwa tatizo kubwa la Ukimwi. Ni bora serikali yetu ijirekebishe na kuanza kuwafikiria wananchi wake na viongozi kuacha kula pesa za mapato ya serikali bila kujali hali mbaya ya kimaisha inayomkabili mwananchi. Pia wananchi wenyewe tufungue macho kuhusu suala zima la kuwachaguzi viongozi wanotuongoza.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 19, 2008

    sawa tumeshakubaliana kuwa ni uwanja wa fisi ni tatizo! Mimi napenda kuuliza mbona twailalamikia sana serikali? Ukiitegemea sana serikali utakuwa kilema. Yani kila siku kwenye habari utasikia wananchi wanaomba serikali iwasaidie. Serikali yenyewe ndo iyo...imejaza mafisadi, bado tu mwataka iwasaidie?...Watu lazima waje na solutions zao wenyewe! Kuna vitu vya kutegemea serikali, kama ulinzi, elimu lakini sio mazingira bora ya kuishi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...