jk akiongoza maelfu ya wadau kuishangilia taifa stars mara baada ya kipyenga cha mwisho kulia. japokuwa kila mmoja alitamani kuchukua pointi zote tatu muhimu, lakini hako kamoja ka sare na moja ya timu kali kuliko zote barani afrika si haba ati. wadau mwasemaje?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2008

    Kwa upande wangu naona timu yetu inafanya vizuri sana baada ya miaka 2 tu. Tuendelee kuipa moyo, tukisoda kwenye south basi zinazokuja tutaenda tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2008

    kwa kweli wamejitahidi sasa inabidi waendelee na moto huo huo washinde mechi zilizobaki za marudiano

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 15, 2008

    Michuzi unafahamu,washabiki ni kama barafu,kwenye baridi huganda zaidi kwenye jua kali huyeyuka, leo Maximo shujaa,tukifungwa hafai hiyo inakubalika popote duniani.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 15, 2008

    Katika hali ya kawaida ya kimchezo nadhani sio mbaya sana kutoa suluhu na timu yoyote ile ukiachilia mbali hawa vigogo wa soka barani Africa na Dunia nzima kwa ujumla.Kama ulivyosema, lengo la kila timu iingiapo uwanjani ni kujinyakulia pointi 3 muhimu.Sasa ikitokea kinyume cha hapo, kuna mambo muhimu ya kuyaangalia kwa kuzingatia msimamo wa kila timu katika kundi husika,ndipo timu iweze kufurahia sare.
    Sasa,kwa hali halisi ya kimashindano Cameroon ndio wamenufaika zaidi na matokeo hayo.Kwao huo ni ushindi japo wao walitegemea wapate pointi 3 ili waweze kujiimarisha kileleni.Lakini ukweli unabaki kwamba haya matokeo kwao ni mazuri.Ni mazuri kwa sababu kuu 2.
    Moja, wamepata pointi moja zaidi na hivyo kuzidi kujika kileleni katika kundi letu.
    Lakini la pili ni kwamba wametoa sare ugenini jambo ambalo kisoka ni muhimu sana.Tukumbuke hata walipohojiwa baadhi ya wachezaji wa Cameroon,walikiri kwamba Taifa Stars ndio wana nafasi ya kushinda mchezo wa huo kwani watakuwa wakicheza nyumbani huku karai likitapika(uwingi wa mashabiki).
    Kwa hiyo kama tunazungumzia aliyenufaika na matokeo hayo,basi ni dhahiri wapinzani wetu wamenufuika nayo.Sisi tumeumia kwa kweli.
    Najua hoja inayojengwa hapa ni kwamba tumeweza kutoa sululu na vigogo wa soka barani Afrika,sawa nakubaliana hilo.Lakini je,suluhu hiyo inafaida yoyote kwetu hasa kwa kuangalia matokeo mabaya ya mechi zilizotangulia?Jibu ni hapana.Ilipaswa tutoke uwanjani tumeinamisha vichwa chini huku tukitafakari kibarua kigumu sana kilicho mbele yetu katika mustakabali mzima wa kutimiza ndoto za kwenda kwa mzee Madiba kushiriki fainali za kombe la Dunia.Najua hakuna lisilowekana katika soka ili mradi tu kuwe na mikakati madhubuti ya kuaandaa timu yetu vema.Lakini naanza kupata hofu kama kitendo cha kutoa sare na Cameroon tena nyumbani kwetu tunashangilia kwamba ni ushindi? Sina hakika kama tutafika kweli!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 15, 2008

    ikiwa mambo yenyewe tunafurahi kiasi hichi kwa draw..... hii inanikumbusha kwetu "kufungwa tufungwa lakini chenga twawala!"

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 15, 2008

    Kumbe kikwete anavalia saa mkono wa kuume halafu ni nyeusi hadi mkanda. .mmmmmmmnnn afadhali amesaidia tumetoa droo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 15, 2008

    Kama tukiamini tutaweza. Nakumbuka mashamsham ya Kakakuona miaka ya tisini. Tuipe moyo timu yetu na labda tupunguze kidogo kulekeza fikra zetu za mpira Old Trafford, Anfield na kwingineko. Kabla hujasema - naelewa mapenzi ya klabu si sawa na ya taifa lakini pale mtu unapokuwa na mapenzi na timu inayochangia wachezaji kwenye timu ya taifa fulani unakuwa pia na mapenzi ya dhati kwa timu hiyo. Mimi Mara Spurs japo haina wachezaji kwenye timu ya taifa...

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 15, 2008

    hapa hamna cha kufanya vizuri au kutoka kidedea wala nini manake hii mechi ilikuwa ya taifa stars kushinda. draw unatoka ugenini sio nyumbani. angalia uganda wamewafunga angola nyumbani, malawi wamewafunga egypt nyumbani, rwanda wamewafunga morocco nyumbani. hizi ndo gemu tutakazokuja kujutia kwa nini watukushinda

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 15, 2008

    hayo mapesa wanayotapanya kwenye mpira kwanini yasitumike kusaidia wanafunzi wa chuo kikuu mlimani?

    au kwanini wasiwekeze pesa hizo kwenye kufundisha waalimu wa shule za sekondari?

    kwanini tunajenga uwanja wa mpira wa kifahari wakati shule zetu na vyuo vyetu havina maktaba na maabara?

    WATANZANIA NANI KATUROGA??!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 15, 2008

    Ni kweli kwa kuwa-hold wale jamaa (Simba wasioshindika) ni hatua moja kubwa sana kwa timu yetu na nchi yetu.Wanastahili sana pongezi na Maximo pia pongezi kwake maana nadhani hata wao Cameroon wanajiuliza mara 2x2.
    Pamoja droo hiyo bado ninaamini kuwa uwezi wa kuwashika kwao pia tunao na kupata ushindi japo wa ka-goli kamoja kwani ktk soka hamna linaloshindikana.
    Pamoja na timu yetu kuwa ktk kiwango ambacho kwa mwenye macho yeyote aliona kuna watu (Mamluki) bado wanakera sana.Mi nawaomba hawa mamluki wasio jua mpira na wasiokuwa na hata chembe ya uzalendo wasiwe wanakuja uwanjani maana kuna siku atakufa mtu pale uwanjani.Naongea hivi kwa kuwa imenikera sana baada ya jana kumuona mamluki mmoja akiwa amevaa jezi ya cameroon wakati akiwa amekaa jukwaa la watanzania!Nilitamani nimrushe chini lkn kwa kuwa mimi ni mzalendo nikaamini next time atajifunza.
    Kwa watanzania tulivyo pamoja na kiwango kilichoonyeshwa jana bado kama ingetokea mchezaji mmoja akafanya kosa wale jamaa wakatufunga basi wangegeuka na kuanza kuwashangia kameruni maana kuna waliokuwa wakitamka hivyo wakati tukienda uwanjani. Nawaaombeni watanzania tuwe na moyo wa kizalendo wa kweli hata kama tutafungwa goli 100!Kuna watu walikuwa wanamlaumu maximo lkn baada ya mechi walimshangilia!Tusipende kuyaona mazuri bila kuwa tumeayaandalia mazingira ya kuyapata.
    Tumpe support kocha na timu yetu mi naamini baada ya miaka kama 3 tanzania tutakuwa na timu ya kujivunia na kupata mafanikio tunayoyataka.Lkn kama tutakuwa kila wakati tunamlaumu kocha! Real we can't reach any success maana ataondoka huyo ambaye ameshawajua vizuri wachezaji wa kitanzania na atakuja mwingine kuanza upya! sasa sijui tutakuwa tunafanya nini?
    Shuma the real tanzanian

    ReplyDelete
  11. Mungu amesaidia maana kile kikosi cha Cameroun kinatisha.Sipati picha mpaka Dan Mrwanda alimnyanyasa Rigo Song

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 15, 2008

    Watanzania wengi hatuna uzalendo na hii haipo kwenye mpira peke yake bali katika michezo yote na hata katika bidhaa tunazozitumia. Watu wengi wanaona kila linalofanywa na watanzania ni la kubezwa kwa kufananisha na nchi zilizoendelea bila kujua kwamba kitu muhimu katika kufikia maendeleo ni kutanguliza uzalendo pamoja na kujithamini na kuthamini chako. Hili ni tatizo kubwa sana kwa watanzania kwani imefikia kila kitu kizuri lazima kifanywe na wageni na siyo wazawa na hili linasababisha tuwe nyuma kimaendeleo kila siku huku tukikumbatia bidhaa mbovu kutoka nje, wataalam wabovu kutoka nje pamoja na utendaji mbovu wa viongozi kwa sababu hawajiamini kama wanaweza kufanya vitu vizuri.
    Kila mafanikio yanahitaji kuwekeza pesa pamoja na muda, waulizeni hao waliofanikiwa kwenye mpira kama walifika hapo walipo ndani ya miaka miwili!! Wote mnakumbuka tulipoteza muda mwingi sana kwa kuwashabikia Rage,Ndolanga na Wambura na tukasahau kucheza mpira. Tuwe wavumilivu na tujipe muda ili tuyafikie mafanikio. Ili tuyafike maendeleo ya kweli, uzalendo ni muhimu sana. Nakumbuka kuna mbunge 1 alishawahi kusema kwamba waingereza walifika hapo walipo kwa kuonyesha uzalendo kwamba kitu bora ni kile kilichozalishwa Uingereza.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 15, 2008

    Mpira kujiamini tu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 15, 2008

    hapa hamna cha kufanya vizuri au kutoka kidedea wala nini manake hii mechi ilikuwa ya taifa stars kushinda. draw unatoka ugenini sio nyumbani. angalia uganda wamewafunga angola nyumbani, malawi wamewafunga egypt nyumbani, rwanda wamewafunga morocco nyumbani. hizi ndo gemu tutakazokuja kujutia kwa nini watukushinda

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 15, 2008

    Nilienda uwanjani jana ili kujionea mwenyewe nini kitakachotokea na pia kuangalia hasa timu yetu jinsi ilivyo hasa baada ya kutoiona kwa muda ikicheza LIVE. Niliyoyaona ni kama yafuatayo:
    1) Kocha Maximo anastahili pongezi, kwa muda aliokaa na timu na hali halisi ya timu ilipofikia
    2) Tanzania kwa ujumla hatuna STRIKERS, kuna haja kuwekwa kwa mkakati maalum wa kuwatafuta na kuwafundisha ikibidi kuwa na kocha maalum kwa strikers tu.
    3) Wachezaji wetu wanahitaji kujenga miili yao ionekane kama ya wachezaji, kwa maoni yangu kabla ya soka kwanza waingizwe GYM for BODY BUILDING. Jana walivyokuwa ni kama mfano wa TEMBO na DUME LA PAKA. Maana wakiguswa tu huko kuanguka kwao ni mail tatu
    4)Wakati umefika sasa kwa Maximo, TFF, Serikali kwa maana ya wizara ya utamaduni na michezo,kukaa na kuulizana hasa ni kipi alichokikosea JUMA KASEJA hadi leo hii asiitwe ndani ya timu pamoja na makosa ya wazi aliyoyafanya IVO MAPUNDA jana. Tushukuru mungu jana mungu alikuwa upande wetu, akicheza kama alivyocheza jana IVO huko YAUNDE, nafikiri tutafungwa si chini ya goli 4. Kuna story kuwa Maximo anasema ati Kaseja tatizo lake ni ufupi, lakini ninavyomfahamu mimi Kaseja pamoja na ufupi wake hana tatizo la kufungwa mipira ya juu. Wakati umefika sasa WAKAZIONGEA SABABU HALISI; KWA PAMOJA NA KUMSAMEHE AREJEE KUNDINI. Haiingii akilini KIPA BORA WA TANZANIA ASIWEMO NDANI YA TIMU YA TAIFA KWA SABABU TU NI MFUPI???. LEO hii Katibu mkuu wa TFF akiulizwa swali la Kaseja kutokuwepo Taifa stars, kupitia kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1, alijibu kuwa KOCHA MKUU WA TAIFA STARS NDIO ANAJIBU LA KWANINI KASEJA HAYUMO TAIFA STARS. SIamini kama kweli hali ndio hiyo

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 15, 2008

    A Kenyan woman in Mauritius has been arrested along with two Tanzanian boxers and four officials after they were busted trying to smuggle heroin worth a reported USD $1.8 million into Mauritius.

    The woman, whose name has not yet been released, appeared to be the contact in Mauritius for the Tanzanians who had just arrived in the island for the African boxing championships with the heroin. They were arrested as they attempted to hand over the drugs to the Kenyan woman by placing them outside near their hotel.
    Source: http://breakingnewskenya. wordpress.com.
    Taifa Stars mnatakiwa kuwa makini na hoteli za ufukweni mtakapofikia Mauritius, kwani pwani zao zimejaa wageni kibao toka sehemu mbalimbali duniani kama 'watalii' pia ni 'mizungu ya unga'
    Mdau
    Port-Louis

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 16, 2008

    Maximo aondoke hana jipya.kama angekuwepo Boban basi wangepatana vizuri na kina Ngassa.

    kocha aa chuki sana na wachezaji.
    Kaseja anasema mfupi jee Omar Mahadhi aliyechaguliwa timu ya Africa alikuwa mrefu?

    Robert carlos mrefu? staz imetoka draw kwa uchawi si mpira.

    hatuwezi kushangilia draw dunia nzima itatucheka.Kocha wa Chelsea kafukuzwa.Maximo aondoke aje mwingine. au aende Yanga timu ya Rais wetu na yeye anajipendekeza kuweka wachezaji wa Yanga hata kama hawana kitu.

    Mapunda sio kipa yeye anamngangania ndio alitufungisha mechi zote. yeye anasema kaja kuweka foundation basi msingi tunao tunamshukuru ampishe mwingine aje kuendeleza.

    kusema kuwa kazoea wachezaji hata huko aendako atawazoea. hata AVRAM GRANT aliwazoea kina TERRY NA ASHLEY COLE.

    timu inatumia pesa nyingi lakini tunachopata kidogo.

    na hao majambazi TFF wanakula pesa tu.

    kama Kaseja ni mfupi mbona Yanga wamemchukua na Mapunda wanae.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 16, 2008

    ligi kuu ya vodacom wafungaji bora ni katende kutoka uganda,anafuatiwa na sunguti kutoka kenya,kile kizazi cha kina maajabu,kitwana,masement,tino,makumbi juma akipo tena jamani itachukua muda kupa watu kama hao kama vile nyerere mwingine labda baada ya miaka mia,Maximo anastaili sifa na alio ya fanya kwa kipindi iki kifupi ana staili sifa majungun na fitna zinatoka kwa kina mzizay na kundi lake tuna lijua na watanzania wa penda maendeleo ya soka tuta zidi kumuunga mkono maximo na kumbeba kama jana wenye wivu wajinyonge BIG UP ALLY BUSHIRI NA MAXIMO ALUTA CONTINUA TASO,TENGA BENDERA NA WENGINE.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 16, 2008

    WATANZANIA TUSIWE WENDAWAZIMU, SARE SI KITU CHA KUFURAHIA NI SAWA NA KUFURAHIA KUSHIRIKI NA USHINDI SI MUHIMU! HATUKUMUAJIRI MAXIMO ILI ATUWEZESHE KUTOKA SARE, DUNIANI KOTE SOKA NI USHINDI NA SI SARE. KOCHA ANAYECHEKELEA SARE NI YULE AMBAYE KIWANGO CHAKE NI CHA CHINI NA ANAJUA KUWA UJUZI WAKE NI MDOGO KULIKO MPINZANI WAKE HIVYO KWAKE SARE HUWA NI FURAHA NA SHANGWE KAMA ALIVYOFANYA MAXIMO. NCHI NYINGI ZINAZOJUA MPIRA NI NINI KOCHA ANAYETOKA SARE KILA MARA HUFUKUZWA.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 16, 2008

    TBC 1 KULIKONI? MNAWEKA WAPIGA PICHA WENYE MAKENGEZA NA KUFANYA KAMERA ZITAFUTE MPIRA MBONA ITV ILIKUWA AFADHALI KIDOGO. TBC 1 TUFUTENI WAPIGA PICHA WENYE UJUZI NA WEPESI WA KUFUATILIA MPIRA KWENYE KAMERA NA SI KUTUMIA MUDA MREFU KUTUONESHA JK BADALA YA MPIRA. UBORA WA KITUO CHA TV NI UBORA WA PICHA IRUSHAZO.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 16, 2008

    Nyie mnaompigia debe kaseja mnajidanganya , kaseja si mzuuuri saaana kama mnavyodhani, angekuwa mzuri enyimba wasingemtungua seven oclock kwenye mechi mbili isitoshe sasa hivi asingekuwa hapa bongo hata hao enyimba wangemchukua hata Yanga ( hasa Madega ) wamechemka.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 16, 2008

    Habari za saa hizi, kwa kweli kwa mechi ya juzi stars ilihitaji kushinda. N kuhusu wafungaji si kweli kwamba hakuna wapo wengi tumeona kwenye Taifa Cup kulikuwa na vipaji vingi tu ambavyo laiti kama kungekuwa na utaratibu wa kuendeleza soka vingetusaidia. Wa kuwlaumu ni TFF kwani hawana programu endelevu kwani kama wangekuwa nazo tungeona mikakati mbali mbali kuhusiana na vijana walioonyesha vipaji katika michuano ya Taifa.

    Je ni nini yalikuwa madhumuni ya Taifa Cup?? ilikuwa ni kuchezesha timu za mikoa na kuishia hapo hapo au kulikuwa na madhumuni makuu ya michuano ilee?? nadhani kama wangeitumia ile michuano vizuri Taifa lingenufaika.

    Kuhusu Kaseja kusema ukweli mimi binafsi ni mpenzi wa Kaseja lakini kwa sasa na kutokana na michuano ya Taifa na Ligi kwa kweli kipa anaestahili kuongezwa Stars ni golikipa wa JKT Ruvu na Timu ya Mkoa wa Pwani Enock Mkama. Pia kuna mchezaji kama Mwinyi Kazimoto ambae amekuwa man of the match mara kadhaa mbali na huyu kiungo mchezeshaji Mohammed Banka ameonyesha kiwango cha juu kwenye ligi ya Vodacom na hata kwenye Michuano ya Taifa Cup. Kusema kweli uozo ni wa TFF badala ya kusimamia soka wao wanasimamia maslahi yao binafsi kwa kuweka viingilio vikubwa katika mechi badala ya japo wangeweka mikakati ya kuifunga Cape Verde.

    Kuhusu wafungaji kuna Mgosi alikuwa mfungaji bora Taifa Cup na Kijuso namba mbili pia hata waliomo kwenye Taifa stars yenyewe sio wabaya ispokuwa ni kwamba kocha anashindwa kuipatia combination ya uchezaji akilipatia hilo magoli yatapatikana.Kingine ningependa kuomba watanzania tuache unazi wa Usimba na Uyanga mpaka kwenye timu ya Taifa.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 16, 2008

    Mijitu Mingine bwana,

    Eti inafurahia sare kwa kua ni dhidi ya Cameruni ya kina Etoo,

    Yaani Etoo mmemuona Kifaaaaa!!!!!!?????,

    Kwa taarifa yenu ile ni michongo tu ndo maana akachezea Barca, lakin kiuchezaji Etoo ni fala tu kama mafala wengine.

    Kakabwa na Nsajigwa mpaka akawa haonekani kama yupo.

    Pale ilikua tuwapige bao wale wasen..@e na sio droo,

    Mi sikuona timu ya kutuzuia tusifunge sema tu umakini haukuwepo kwa Staz.

    Anyway, Maximo kayaona hayo yote, na uhakika pale Mjini Younde lazima Mrwanda, Ngassa na Gabriel kila mtu apige yake kama matatu hivi kabla ya kuishushia mvua ya magoli Cape verde

    Mimi

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 16, 2008

    KAKA MICHUZI KWA KWELI NIMEKERWA NA HUYU ANON WA Tarehe June 16, 2008 12:12 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
    NA MAONO YAKE NI HAYA HAPA CHINI

    Maximo aondoke hana jipya.kama angekuwepo Boban basi wangepatana vizuri na kina Ngassa.

    kocha aa chuki sana na wachezaji.
    Kaseja anasema mfupi jee Omar Mahadhi aliyechaguliwa timu ya Africa alikuwa mrefu?

    Robert carlos mrefu? staz imetoka draw kwa uchawi si mpira.

    hatuwezi kushangilia draw dunia nzima itatucheka.Kocha wa Chelsea kafukuzwa.Maximo aondoke aje mwingine. au aende Yanga timu ya Rais wetu na yeye anajipendekeza kuweka wachezaji wa Yanga hata kama hawana kitu.

    Mapunda sio kipa yeye anamngangania ndio alitufungisha mechi zote. yeye anasema kaja kuweka foundation basi msingi tunao tunamshukuru ampishe mwingine aje kuendeleza.

    kusema kuwa kazoea wachezaji hata huko aendako atawazoea. hata AVRAM GRANT aliwazoea kina TERRY NA ASHLEY COLE.

    timu inatumia pesa nyingi lakini tunachopata kidogo.

    na hao majambazi TFF wanakula pesa tu.

    kama Kaseja ni mfupi mbona Yanga wamemchukua na Mapunda wanae.

    KWA KUKUSAIDIA TU NI KWAMBA KAMWE MAXIMO HATOONDOKA NA NI HAKI YETU KUFURAHIA DROO TULIYOIPATA KWA SABABU KWENYE KUNDI LETU NI SISI TU NDIO TUMETOA DROO NA CAMEROON,, MAURITUIS WAMEPIGWA TATU (3)CAPE VERDE WAMEPIGWA (2)TANZANIA WAMETOA DROO SASA HAKUNA HAJA YA KUSHANGILIA HAPO?? GROW UP DOGO PALE KWENYE MAFANIKIO NI VYEMA UKAJENGA MAZOEA YA KUWAPA MOYO WAPIGANAJI WAKO KULIKO KUTOA COMMENTS ZENYE KUWAVUNJA MOYO, NA KAMWE USIMLAUMU MAXIMO KWA JINSI ANAVYOFANYA LENGO LAKE NI KULETA HESHIMA KWENYE TIMU YA TAIFA NA UKUMBUKE KUWA HII NI NATIONAL TEAM SIO CLUB SO KWA MAAMUZI ALIYATOA JUU YA HARUNA MOSHI BOBAN NI SAHIHI KABISA LAZIMA WACHEZAJI WAWE NA NIDHAMU NA HIYO NDIO NGUZO YA MPIRA DUNIANI KOTE.. REJEA KWENYE FAINALI ZA AFRICA ZILIZOPITA AMBAZO ZILICHEZWA GHANA, ELHADJI DIOUF ALITOROKA KAMBINI AKAENDA NIGHT CLUB WHILE TIMU ILIKUWA INAKABILIWA NA MECHI SIKU MBILI ZINAZOFUATA JE ULIMUONA UWANJANI?? NA KAMA ULIFUATILIA VYOMBO VYA HABARI ULIPATA REPORT GANI JUU YAKE?

    HEBU NIAMBIE KUNA TIMU GANI YA TAIFA HAPA TANZANIA AMBAYO IMEWEZA KUKUSANYA MASHABIKI WENGI KAMA YA SASA HIVI? KWA KUKUSAIDIA TU TIMU ZILIZOPITA ZILIKUWA HAZIWEZI HATA KUKUSANYA MASHABIKI 5,000 KWENDA KUIANGALIA TIMU YAO NA NDO MANA IKAITWA KICHWA CHA MWENDA WAZIMU, WE UNAONA KABISA TIMU IMEBADILIKA VIJANA WANAJUA KUFUNGUA VYUMBA WANATULIA PALE WANAPOKUWA NA MPIRA ALAFU UNALETA CHUKI ZAKO BINAFSI WHY?

    MBONA HUSEMI KUHUSU EMANUEL GABRIEL MWAKYUSA THE WAY ALIVYOKOSA NAFASI NZURI ZA KUFUNGA HAPA NYUMBANI WAKATI WA MECHI NA MAURITIUS NA PIA AMERUDIA HAYO HAYO KULE CAPE VERDE MBONA HUGUSII HAYO? MBONA HUJASEMA KUHUSU SWEDI THE WAY ALIVYO WEKA MPIRA KIFUANI KUTAKA KUMRUDISHIA KIPA IVO MAPUNDA NA MCHEZAJI WA MAURITIUS AKAUWAHI NA KUFUNGA BAO LA KWANZA? AU WEWE UNAANGALIA MPIRA KWENYE TV ALAFU NDO WA KWANZA KUTOA LAWAMA ULITAKA IVO AFANYAJE PALE WAKATI BEKI WAKE NDO AMESABABISHA MAKOSA YOTE YALIYOPELEKEA KUFUNGWA GOLI LA KWANZA NA MAURITIUS?? TOA FITINA ZAKO HAPA ZA USIMBA NA UYANGA KWENYE TIMU YA TAIFA KAMA YANGA WAPO WENGI KWENYE TIMU YA TAIFA BASI HAO NDO WALIOONEKANA NI BORA, NA KAMA KASEJA ANGEKUWA MZURI BASI ASINGEFUNGWA BAO NYINGI NA ENYIMBA NA SIMBA INGEKUWA INAFIKA ANGALAU NUSU FAINALI KWENYE MASHINDANO YA CLUB BINGWA AU CAF SO DONT CAME UP HERE NA KUTULETEA HOJA ZILIZOFIFIA TIMU HAIJENGWI KWA MIAKA MIWILI BWANA INAHITAJI MUDA SANA KUFIKA PALE WALIPO CAMEROON, GHANA, NIGERIA,IVORY COST SO JIFUNZE KUPITIA WENGINE...

    PILI HAPA USITULETEE MIFANO YA KLABU HAPA TUPU NA NATIONAL TEAM SO UKIWA UNATOA MIFANO NI VYMEA UKAEGEMEA KWENYE NATIONAL TEAMS SIO KUTUAMINI OOH GRANT ALIONDOKA AKALETWA MWENGINE OOH HUYU AONDOKE AJE MWENGINE GROW UP DOGO HII NI NATIONAL TEAM SIO CLUB, NENDA KAJIFIKIRIE THEN UJE HAPA TUENDELEE KUJIBIANA KWA HOJA.
    TAIFA STARS OYEE MAXIMO OYEE

    TUNA HAKI YA KUFURAHIA KWA SABABU TUMEPATA DROO NA TIMU BORA SANA BARANI AFRICA NA DUNIANI PIA.

    WILLY UDSM

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 17, 2008

    Waungwana wenzangu , tunapaswa kuacha tabia ya kujifananisha na wale waliotuzidi sana soka..hatuna professional yoyote yule wa maana..wenzetu Cameroon walipanga timu nzima inayocheza soka ulaya..hata wale walioingia kipindi cha pili wanacheza ulaya pia..na tunapaswa kuacha pia kujiongopea kwamba eti na sisi kwa sasa tunaweza kucheza kombe la dunia

    kwa kifupi bado hatujawa na wachezaji ambao wanaweza kumfanya Marcio Maximo akaonekana hajui kufundisha..timu ile ya Cameroon ina wachezaji wanaofundishwa na makocha wa kiwango cha juu kule kocha wao wa taifa , Mzee Oto Pfister..kwa hiyo wachezaji wale au hata wadau wa soka wa Cameroon wanayo jeuri ya kusema kuwa kocha huyu wa taifa hatufai..lakini sisi wachezaji wetu ni hawa hawa wanaofundishwa na makocha ambao hawakai kwenye timu zaidi ya mwaka mmoja..na pia waungwana wenzangu tuachane na ile tabia ya kuwadharau makocha..tukumbuke kwamba Athumani Iddi anacheza namba nane kwa sasa , ni kwa sababu ya kocha wa kibrazil aliyembadilisha kutoka nafasi ya beki.

    Kiwango chetu cha soka kiko chini sana kiasi kwamba bado hatujaweza kuwa na wachezaji bora watakaomfanya Maximo aonekane hajui kitu..tunawazungumzia akina Mgosi na Kazimoto waliongara kwenye taifa cup..wakati taifa cup yenyewe ilikuwa na timu kama Lindi..timu iliyofungwa magoli kumi katika mechi moja!!.

    Kushindwa kwenda kombe la dunia au kombe la mataifa ya afrika mwaka 2010 sio sababu tosha ya kumfukuza Maximo..mbona hatukuwahi kwenda kwenye kombe la dunia kabla hajaja Maximo?..mbona ni mara moja tu katika historia ya taifa letu tulipowahi kushiriki mashindano ya mataifa huru ya afrika?..kushindwa kwenda afrika ya kusini mwaka 2010 au angola mwaka huo huo wa 2010 sio sababu ya kisayansi ya kuweza kuukata mchango mkubwa wa Maximo katika kulifanyia mapinduzi soka letu.

    Mpira wa bongo hauwezi kufanyiwa mapinduzi makubwa ikiwa simba na yanga bado zinaendeshwa kiswahili mpaka leo hii..wajuaji weeengi wamejaa kwenye timu zetu, wengine wanapelekwa na njaa zao wengine hawaeleweki wanafuata nini..kwa ufupi soka la vilabu vyetu ni vurugu tupu.

    Huyo jamaa anayemkata Maximo anashangaza sana kwa sababu hata huyo Mziray ambaye alikuwa ni adui mkubwa wa Maximo..kwa sasa anamuunga mkono na anayakubali mabadiliko yanayoonyeshwa na stars...usimba na uyanga hauna faida yoyote ile kwa sababu ni mwendelezo wa majungu na fitina zisizokuwa na mpango wowote ule

    Narudia tena ..bado hatujawa na wachezaji bora kiasi cha ubora wa Maximo kushindwa kuonekana..wachezaji wetu si ndio wale wanaorudia makosa yale yale kila siku hata baada ya kufundishwa mara mia kwa siku?.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...