wengi mmekuwa mnakusikia tu, lakini hapa ndipo uwanja wa fisi maarufu kuliko viwanja vya sehemu zingine, eneo la tandale. ni uwanja wa wazi ulio katikati ya nyumba za wenyeji ambapo mchana panakuwa tulivu kama inavyoonekana.

mambo huanza mara tu jua linapozama ambapo vimeza vya biashara mbalimbali kama vile samaki, mahindi na hata chai kwa maharage na mikate huwekwa na pia meza za karata tatu na kamari zingine huwsapo pia.


mwanga ni wa vibatari na taa za chemli huchomoza kila mahali. usiku unapokuwa mkubwa biashara kubwa nazo huanza. wauza vilaji vikali ikiwa ni pamoja na wauza bwimbwi na makahaba husogea na kujibanza pembeni kusubiri wateja. vibaka wakubwa kwa wadogo nao hawachezi mbali. makelele ya mtu kupigwa loba sehemu hiyo ni ya kawaida kabisa, kama ilivyo muziki wa mchiriku ambao unapazwa kwa sauti ya juu na vikikolea watu hulisakata rhumba kama kawaida.


serikali ya mkoa wa dar umeshapiga marufuku viwanja vya fisi ingawa habari zinasema amri hiyo ni kama kutaka kunguza nyumba kwa maji ya moto. mambo ni aluta kontinyua. na hapo ndipo mwanamuziki nyota wa kundi la destiny child alitembelea mchana wa leo na kuongea na wenyeji pamoja na kutembelea mojawapo ya nyumba ya makahaba ambao wengi ni vijana bado.
fungua globu ya uwanja wa fisi kwa kubofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2008

    Michuzi, i love Mchiriku !! huo ndiyo muziki asili wa kwetu, Mimi natoa hoja, unaonaje wewe uukuze huu Muziki kama Taji Liundi alivyokuza Bongo Flava ?
    Mdau issa, south africa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2008

    ingia YOU TUBE,alaafu bofya hyena square(tanzania)utalia machozi - sir GOD has been so unjust

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2008

    kwakweli inasikitisha sana.hii movie imeonyeshwa sana huku europa mi nimdau wa sweden waliirusha kwenye luninga kwa kweli inasikititisha kuona maisha maisha ya nyumbani.mungu akuzidishie huyo moyo wa kueleimisha wa tu eliza.mdau sweden.göteborg

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2008

    Nimeona hiyo documentary ya Hyena Squre pale EastAfricanTube yaani inatia huruma sana kuona bado wenzetu wanaishi kwenye maisha ya dhiki yaliyojaa magonjwa na umasikini wa hali ya juu. Angalia hapa http://www.eastafricantube.com/media/9686/JITAMBUE_PT.1/

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2008

    kumbe uwanja wa fisi ndio hyena square sio hyena grounds au stadium hamna noma square imetulia

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2008

    Daaa kweli maisha sio kitu cha kuchezea kila mtu anapita kwenye bara bara yake anayojua mwenyewe

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 18, 2008

    Kaka Michuzi asante sana kwa hii habari. Hiyo link ya hyena square imeninyenyekeza sana. Wengine tumejaliwa maisha mazuri sana inatubidi tushukuru sana. Lakni pia tujiulize ni namna gani tunaweza kusaidia katika kubadilisha hii hali. Kama asemavyo ano. 11:08, You are humbled by what you see. Asante sana sana. (Son of a peasnat)

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 18, 2008

    Anony wa 17 June 11:08 kama umelia machozi haukunizidi mimi. kwa sababu zifuatazo.

    Yule binti ambaye ameathirika aitwaye ELIZA bila kuficha mimi nimeshawahi kulala naye mara mbili, kwa kifupi nilikuwa mteja sana wa uwanja wa fisi.najua wako wengi watakao lalamika au kulaumu, lakini wacha niseme.

    Hakuna mtu yoyote ambaye akikutana na mimi ana kwa ana ataamini kuwa nimeshawahi kuwa mteja mkubwa pale uwanja wa fisi, naweza kutembea huku nimefumba macho nikakupeleka kila kona mahali pale.na maeneo ya jirani na pale, sijajua mwanamke yupi amabye sijampitia ajiuzaye mahali pale.

    Huku nikiwa nasoma chuo kikuu cha DSM nakumbuka siku moja nikakutana na prof mmoja accidentally uzuri mimi namfahamu lakini yeye hanijui na ni profesa ambaye anafahamika sana.

    Sijatoa maelezo haya ili kunogesha globu hii bali nadhani ni wakati mwingine mzuri wa kuelezana ukweli bila kunyoshea wengine vidole.

    sikujua kuwa ELIZA yupo katika hali hiyo wala haikunishtua maana nilipoamua kuacha nilipima kama mara saba kwa nyakati tofauti na mahali tofauti,Kipindi kandoro anapiga marufuku nilikuwa tayari nimeamua kuachana na maisha ya aina hii,achilia mbali sababu ya heshima au la,nikaja nikatambua hata kama tutajitahidi kwa namna gani kuukataa ukweli lakini hali inabaki palepale we HUMAN WE HAVE INFALLIBLE NATURE, hata biblia inasema wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa MUNGU.

    Niko ulaya na famili yangu nzuri Yesu amenibadilisha kiasi kuwa nimesahau kabisa mambo ya uwanja wa fisi,kabla ya kuoa tulipima na ninaamini vifaa vya wenzetu huku havina wasiwasi kwa kifupi SINA, lakini sijisifu wala kujona mjanja kwa kutumia kondom, sifikirii wala siamini eti zinasaidia wangapi wanavaa na bado wanapata??

    Mungu ameniepushia mbali huu ugonjwa, moja ya vitu ninavyomwomba MUNGU anisaidie anipe fedha nisaidie watoto yatima, nisaidie akina dada kama hawa wanaoteseka na kufikia kufanya biashara kama hizi.nyota ya binti huyu imefifishwa kungali mapema.JAMII nzima inapaswa ilaumiwe.

    TUMEJIWEKEA STANDADI ZETU ZA MAISHA NA DHAMBI, tunapowaona malaya tunawaona wanadhambi, kumbe na sisi tunakula rushwa, huyu anaua na anaona sawa, huyu anadanganya na anona sawa.ILI MRADI KILA MWANADAMU ANAJIONA HANA DHAMBI, ILI KUJILINDA NI RAHISI KULAUMU WENGINE !!! Yesu alisema hu nani wewe utoaye kibanzi kwenye jicho la mwenzio huku unaboriti kwenye jicho lako??

    inaonekana Dini tunaziparamia kama kweli wangekuwako waislamu na wakristo safi wanaofuata dini zao barabara wasingekuwepo watoto wa mitaani, wasingekuwepo machangudoa.Dini ni fasheni kuitwa Bakari na John, basi tumefika KUMBE MUNGU ANATAKA TUONDOE HALI ZETU ZA UBINAFSI NA KUISAIDIA JAMII, .ELIZA AMEATHIRIKA LAKINI IMPACT YAKE KATIKA JAMII NI KUBWA NA HAITASAHAULIKA , NI RAHISI KUMSAHAU ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MWAKA 80.

    JAMII TUAMKE TUSAIDIE KILA ANAYEIHITAJI MSAADA JIRANI YETU, MSAADA SO LAZIMA FEDHA BALI HATA MAWAZO MAZURI, TUTAPUNGUZA VIBAKA, MAJAMBAZI,MAKAHABA, MAANA LEO AMEATHIRIKA ELIZA HUJUI KESHO ATAPATA NANI.

    HATUKO SALAMA KATIKA JAMII INAYOUMWA, HAKUNA TAJIRI NDANI YA MASKINI, WALA HAKUNA WA KUJIVUNA TANZANIA.

    NITARUDI TU KUENEZA INJILI YA BWANA YESU ALIYENIPONYA NA KILA ATAKAYESOMA UJUMBE HUU, AFIKIRIE MARA MBILI NA APITIE HIYO UTUBE ATAELEWA NASEMA NINI.

    MICHUZI ASANTE

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 18, 2008

    Ujue nilikua najiuliza maswali mengi kwa kujaribu kulinganisha haya maelezo ya uwanja wa fisi na hilo Vogue ninaloliona katika picha (cha kufurahisha zaidi, Vogue lenyewe ni jeupe). Akili yangu ilikua bado haipata uhusiano wa hilo Vogue na hayo mazingira.

    Nimepata jibu baada ya kusikia kua Kelly alitembelea hapo (nadhani hiyo picha ilipigwa wakati wa ziara yake).

    Ignorant,
    Jeremani

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 18, 2008

    Nyie Wadauhuko Juu Ongeeni Tu Lakin Hiki Sisi Ndio Las Vegas Yetu Yaani Wenyewe Tumerizika Kinoma Hata Rais Anaipenda Sema Anaona Aibu Kwa Wadhifa Wake Tu Uongoooo????? Job true true

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 18, 2008

    I see opportunity in this situation!


    Hii sehemu inafaa ibomolewe na ijengwe garden kama Champs Elysee la Paris. Itakuwa sehemu nzuri basi ya kufanya hata maonesho ya jeshi siku za taifa, badala ya kutumia uwanja wa Taifa kama nchi iliyochanganyikiwa. Hata wahindi wana garden kama Elysee kwa ajili hiyo "India Gate"


    Dawa siyo kuwachimba mkwara hawa wakazi wa UWF kwani hiyo ni nguvu ya soda tu. Dawa ni kuwacompesate na kutafuta sustainable alternative use ya hiyo sehemu.


    Mifano mizuri ya sehemu mbovu zilizobadilishwa ni masaiti ya; Millenium Dome London na Opera House ya Sydney.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 18, 2008

    dah anon wa 7:09 kama unayoyasema ni ya kweli,its about time i wake up and start doing right!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 18, 2008

    Vijisenti vya mbunge wa Bariadi vingefanya kazi kiasi gani uwanja wa fisi?Au Richmonduli tungeleta hela zetu tungefanya mangapi?Mi niko ulaya lakini bado hua napenda kununua mademu mitaa hiyo so life goes,wateja tupo

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 18, 2008

    Kwakweli nimesoma Comment zote lakini za Anon 17 June 11:08 ndio umenikata maini.

    Kwanza ubarikiwe kwa kupewa ufahamu maana wewe ni sawa na yule mtu aliyejenga nyumba juu ya mwamba, sio kwamba nakusifia bali sifa nampa Yesu.

    Kwanza Mimi ni kama wewe, sijawahi kukatiza mitaa ya Uwanja wa fisi kutafuta starehe ila nilikatiza baada ya kusikia sifa zake lakini mimi mitaa yangu ilikuwa ni ya Ohio, Kinondoni na kati kati ya jiji na kuna nyakati sio mara moja au mbili nilipatwa na ajali mbaya ya kupasukiwa na Condom nikiwa na hawa wakina dada.
    Kwakeli sio jambo la kujisifia lakini yote ni mapito.

    Nipo ulaya kama wewe, nimeamua kubadili tabia kabisa na kitu ninachotaka kusema UHURUMA peke yake haimsaidii mtu, Bali matendo ndio kikuu. Unajua mtu MBINAFSI hana faida katika jamii lakini MTOAJI ndio anayetakiwa, mfano MUNGU alimtoa mwanae pekee afe kwaajili yetu, ili sisi tujitoe kwaajili ya wenzetu inatupasa tuamini na kutenda kwani IMANI bila ya matendo IMEKUFA.

    PESA hazimsaidii mtu wala UTAJIRI ni UBATILI mtupu, kwani TAJIRI atakufa kwa shinikizo la moyo kwa kufikiria na kulinda utajiri wake, ila Mtu mwenye UPENDO wa KWELI ama upendo wa ROHONI huyo ndio TAJIRI WA KWELI.
    Angalia huyu dada Elisa baada kuona kwamba matarajio hakuna, kaona ni bora ajitoe kusaidia wengine, ukiangalia hana hela wala siyo tajiri lakini ana upendo kwa wenzie.

    TUWAPENDE WENYE UKIMWI, TUWAANGALIE YATIMA NA WAJANE, Tusizi angalie dhambi zetu ila tuwasamehe wale wanao tukosea na kuwaomba radhi wale tunaowakosea ili MUNGU nae atusamehe MATHAYO 6:14-15 Hii ni mizani, unataka Mungu akusamehe, kwani wewe umesamehe wangapi?

    MATHAYO 6:19-20 tengeneza hazina ya kweli isiyo haribika kwa kuwa mtu mwema na mwenye upendo, kwani pale hazina yako ilipo ndio moyo wako ulipo MATHAYO 6:21.

    Mbarikiwe sana.

    PASTOR. (EBENEZER CHRIST CHURCH).

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 18, 2008

    MKUU WA WILAYA YA TEGETA BOSI WAKO KANDORO ALISEMA AMESAFISHA KILA KITU PALE UWANJA WA FISI SASA TUSAIDIE KUMUULIZA IMEKUWAJE TENA MBONA KAMA MWANZO MAMBO KAMA KAWA,NA HATARI ZAIDI KTK HUO UWANJA KUNA HUDUMA ZA NGONO MPAKA TSH.200 JE TUTAPONA???

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 18, 2008

    Mimi ni mwanaume mtu mzima, lakini baada ya kuangalia hii video ya hyena square kwenye youtube nimejikuta machozi yananidondoka kama mtoto mdogo!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 18, 2008

    nyinyi wote mlioguswa na habari hizi, inawapasa kuwasaidi hawa wakina dada pamoja na watoto yatima kwa hali na mali ingawa ni jukumu letu sote!!

    Mwenyezi Mungu anamakusudi yake kwenu ndio maana hadi leo hii mpo salama

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 20, 2008

    ebwana...kweli inasikitisha! Lkn napenda kuwauliza hao wanaosema 'they can see opportunity'...hiyo miji kama Sydney, London, nk uliyoitaja haina maeneo ya umalaya kama uwanja wa fisi. Mkiuvunja uwanja sio mwisho wa mchezo...issue ni jinsi ya kuumaliza mchezo huu. Na hii inabadilishwa na tabia za watu. Nchi zilizoendelea kuna malaya. Nenda Vegas utakuta malaya njiani...sehemu inaiingaza hela namna ile! Hapa ni mambo ya supply na demand...mkiweza kuua demand, supply nayo lazima itaisha peke yake tu! Mimi sidhani kwa kuuvunja huu uwanja au kupabadilisha itasaidia kitu...lazima kuna jawabu lingine! Mkumbuke umalaya ni moja ya biashara za zamani sana...hata kwenye biblia inazungumzia tokea kitabu cha Mwanzo! Unajua mimi binafsi sijawahi kutembea na malaya lakini kuna kipindi kweli wanavutia! Penda usipende...human nature iyo! swali ni jinsi gani tutapambana nayo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...