Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, amesema Marehemu Levy Mwanawasa wa Zambia ameishi na kuwatumikia wananchi wa Zambia kwa mapenzi, kujitolea, heshima na kwa dhati kubwa na wananchi wa Zambia wanaweza kumlipa hilo kwa kumuenzi katika matendo yake haya.

Rais Kikwete amewaambia waombolezaji katika viwanja vya bunge mjini Lusaka leo wakati wa Misa ya kumuombea Marehemu iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimataifa, viongozi wa dini na wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini.

“Ameishi maisha yake na kuwatumikia watu wake kwa mapenzi, heshima na kwa ustaarabu, kitu mnachoweza kumrudishia ni kumuenzi, fuateni na tekelezeni yale aliyobakiza”.

Rais Kikwete ametoa salamu hizo kwa niaba ya viongozi wa Afrika watu wake na Tanzania ambapo amewaambia wananchi wa Zambia kuwa Mrehemu Mwanawasa alikuwa rafiki na mwenzake kama alivyokuwa kwa viongozi wengine katika ukanda huu na duniani kwa ujumla.

“Yeye na mimi tulipatana sana kama ilivyo kawaida kwa viongozi wa nchi mbili rafiki na majirani, siku zote tulikuwa tunawasiliana na kila mara kulipotokea jambo linalotuhusu sote tulishauriana na kwa kweli utamaduni huu ulikwenda vizuri kwa faida ya nchi zetu mbili” amesema na kumuelezea kuwa alikuwa kiongozi wa kutumainiwa na rafiki mkubwa kwa Watanzania, nchi jirani Afrika na dunia kwa ujumla na kwamba Tanzania na bara la Afrika limepoteza mtu muhimu”.

Rais Kikwete amesema viongozi na waombolezaji wamekuja kutoka karibu na mbali na Zambia kuja kuwafariji wa Zambia na kumshukuru Mungu kwa maisha na aliyomjalia Mwanawasa.


Premi Kibanga,
Lusaka, Zambia

03 September, 2008

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...