John Mashaka akisoma hotuba yake alioiandaa kwenye kongamano la Tuwajali wenzetu lililofanyika jumatatu ndani ya viwanja vya Mnazi mmoja, Dar. Mashaka ambaye alikuwa akiishi na kusoma nchini Marekani amerejea nyumbani (Tanzania ) hivi karibuni na kuanza kujishughuliza na kazi za kijamii,ikiwemo kutoa misaada mbalimbali katika vituo vya watoto yatima na wenye virusi vya Ukimwi
Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo, kamanda wa polisi zoni maalumu ya dar afande Selemani Kova akimpongeza mwanaharakat John Mashaka kwa hotuba nzuri
John Mashaka akiwa na baadhi ya wazee baada ya kuwapa msaada wa vitu mbalimbali yakiwemo mablanketi.Mashaka katika hotuba yake alioisoma jumatatu alisema kuwa "Nilizaliwa humu nchini, nayafahamu matatizo ya watanzania walio wengi, ambayo siyo mahitaji ya kifahari bali mahitaji muhimu ya kumudu maisha.Nimeamua kujishugulisha na hizi shuguli ili kulipa fadhila,Ninaamini sitakuwa nimewatendea haki binadamu wenzangu iwapo nitazamisha kichwa changu katika starehe na maisha ya kifahari nikasahau niliowaacha nyumbani wakiteseka kwa njaa na umasikini".
Mwanaharakati John Mashaka akikabidhi misaada kama uonavyo pichani alipotembelea kwenye moja ya kituo cha watoto wa yatima hivi karibuni jijini Dar.Mashaka amerejea hivi karibuni nchini Tanzania akitokea nchini Marekani alikokuwa akiishi, ambapo kwa hapa nyumbani ameamua kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kijamii kama viel kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu,wazee pamoja na watoto wenye virusi vya ukimwi.
kwa habari zaidi za mwanaharakati huyu nenda
na

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 52 mpaka sasa

  1. Sasa huyu JOHN MASHAKA amerudi bongo kimoja au amekuja likizo,nilisoma habari zake kuwa anafanya kazi katika financial Services firm moja huko USA.

    ReplyDelete
  2. UBUNGE LAKINI HUPATI, LABDA UGOMBEE U-PADRI AU U-SHEIKH

    ReplyDelete
  3. teh teh teh sun grass kwenye kivuli, suti bongo 100 degrees that so fun that nigga is crezy acha ubishoo wewe sura mbaya

    ReplyDelete
  4. Mimi nilikuwa nadhani watu wanotoka majuu wanakuwa watambuzi wa mambo zaidi yetu tulio bongo, la hasha huyu jamaa naona amedandia gari kwa mbele!

    kitendo cha huyu jamaa kwenda ktk mkutano na kusoma hotuba direct from his laptop mimi naona ni kitu cha kishamba.

    ReplyDelete
  5. Kusoma presentation, sijui paper kwenye laptop?? A big no no, angeprint copy labda kungekuwa na Ppoint ndo asome kwenye laptop!

    Hiyo bluetooth(???) sikioni kwenye presentation?? na sunglasses?? It is not polite. Labda mimi mshamba kuh watu wa majuu!!

    ReplyDelete
  6. Hongera sana john!!
    usiwasikiliza hawa waosha vinywa, hawaangalii nini unafanya wanaangalia nini umevaa au wewe sura nzuri kweli watu wengine pumbavu.

    na raiti kama wangekuwa wao wangekuwa baa na wanawake wa kila aina. tujifunze njisi ya kuishi na wengine msiwe tu na roho mbaya zenye kujaa wivu.

    mmenisikitisha sana mnajuwa kiasi gani hao wanaopokea huo msaada wanavyoshukuru au lipi jema hapa duniani?? binadamu afanye nini ndiyo mridhike?

    sunglsses kwenye kivuli unachotaka wewe nini?

    huyu anatumia hela zake kusaidia wasio na uwezo, na wengine wanatumia hela za wavuja jasho kwenda kuchezea nje ya nchi je yupi bora????????

    muombeni radhi wote mlio mponda bila sababu. mnakera sana wa tz. mnaonyesha kweli mmetoka ktk malezi hafifu.

    ReplyDelete
  7. Show Off Kibaaao FALA, Next time Print your Sh!t au ndio una-go-green?, haimake sense uwe na blue tooth kwenye mkutano, ni sawa na kutafuna GUM huku unahutubia. Huyu jamaa fiksi nyingi.

    HOW OLD IS HE Anyway?, mbona mambo anayofanya ni ya kitoto!?, From what i have read a while back jamaa ni professional fulani, ila the way he present himself hapo Na-wonder ni nani amempatia kazi HUKO USA!!, au ni manager wa MacD!?....Man! some people, never grow up..&..are jus ignorant to the CORE!!...hata kama wako Educated...ish!

    Kweli ukivipata ukubwani.........(malizia mwenyewe)

    hizi ni Cent zangu mbili tuu, na michuzi uziweke usinibanie this time, mi natoa maoni yangu tuu.

    BooSt3D.

    ReplyDelete
  8. MSUKUMA NI MSUKUMA TU

    ReplyDelete
  9. Achane Wivu wenu huo, yeye amesaidia watu wasiojiweza au mlitaka akawanunulie bia baa mnywe hadi basi ndo mumsifie?? Mashaka endelea na moyo huo huo wenye wivu wafie mbele

    ReplyDelete
  10. hehehe...wabongo mnanikata mbavu! Sometimez elimu peke yake haisaidii!

    ReplyDelete
  11. Mi mara ya kwanza nilifikiri ni Kipofu !!! Mpaka nilipo-scroll down na kuona hizo picha zingine alizozipiga bils sun glasses, ndo nikatambua kuwa ni lack of Social Skills tu, ila jamaa sio kipofu.

    ReplyDelete
  12. Hahaha JM nashukuru kwa mchango wako wa mablankenti lakini kaka mbona unachemsha mapema hivi?

    JAMANI KUSOMA HOTUBA NA BLUUTUTHI? ina maana ulitegemea Call wakati unatoa hotuba?

    nikuambie unapotoa misaada usiwe na Mengi kuita makamera wakuuze watu wanatoa kimya kimya.kitu kingine kama unataka ubunge sahau kalalale juu ya mkuki bagamoyo ndio SHIKAMOO JAZZ watakuachia

    ReplyDelete
  13. Dah lakini kweli aisee? yaani..

    1: Sunglasses?
    2: Bluetooth Headset?

    This guy used to work at Wall Street in New York??? you must be kidding me.. i mean, c'mon

    Buffalo,
    New York

    ReplyDelete
  14. sina mengi ya kusema ila nataka kutumia nafasi yangu kwa kumshukuru mwenyezi mungu kwa kumpa hekima kijana john mashaka. bila shaka umebarikiwa na mwenyezi MUNGU wenye wivu haawatabadirisha baraka zako.Hongera mwana kwetu.

    ReplyDelete
  15. wewe anony wa september 10,08,11:10 AM

    unaesema msukuma ni msukuma tu, ulitaka msukuma awe kama kinyonga awe anabadirika badirika????

    sasa wewe nani mbona hujajitambulisha au bibi yako alipatikana kila kona ukapoteza ukabila??

    waache wenye kabila zao watese!!

    ReplyDelete
  16. Michu hebu tuwekee sound cript basi nasi tumsikilize

    ReplyDelete
  17. anon wa sept 10 1:52 umenichekesha sana mi si msukuma ila jibu ulilompatia swahiba nadhani linamfaa kwa hapa, maana naona analeta dharau kwa makabila ya wengine.

    Sina tatizo na uhuru wa john mashaka juu ya presentastion yake kama ametumia tekelinalokujia hapo au vipi gani mi ninachofurahia ni zaka yake tu alotoa kwa kusaidia wanaohitaji msaada kutoka mfukoni mwake, tujifunze mazuri.

    ReplyDelete
  18. kweli watanzania tuna mambo kweli badala ya kusifia kitendo chake cha kujitolea kuwasaidia watu nyie mnaanza kuponda eti mara blue tooth, jamani kutoa ni moyoni wala si urembo au kabila analotoka mtu.
    Wengine hapa mnatamani mngekuwa nyie lakini Mungu hakuwapa nyie kwani alijua mna roho mbaya. Hongera kijana na usiache kujitolea kwani hao ni wabongo na wengi wao wana njaa kali kazi yao kukandikia kila kitu hata kilicho kizuri. Na Mungu akauzidishie

    ReplyDelete
  19. HA HA HA HA WABONGO WATU WABAYA SANA ,SIKU JOHN MASHAKA ALIPOTELEWA HUMU ZAMANI KWENYE MIKUTANO NA WAZUNGU ALIPEWA SIFA NYINGI SANA KWAMBA TUWAKILISHE NA HONGERA KIBAO ALIZIPATA.LEO HII JOHN MASHAKA KARUDI NYUMBANI KUTOA MISAADA ANASHAMBULIWA.KWELI SISI WATANZANIA WIVU NI KITU AMBACHO KITAENDELEA KUTURUDISHA NYUMA MILELE.WEWE KAMA HUKO MAJUU NA HUWEZI KUFANYA ALIOFANYA HUYU JAMAA HUTAKIWI KUMUONEA WIVU INATAKIWA HIWE CHANGAMOTO KWAKO HILI BAADAE HUWEZE KUSAIDIE FAMILIA YAKO NA WATU WENGINE KAMA UTAWEZA.MANAKE UKWELI HALISI WATU HATA NDUGU ZAO HAWAWEZI KUWASAIDIA ITAKUWA WATU WENGINE?.
    WATANZANIA WENZANGU TUSIPOTEZE MDA KUMSHAMBULIA MTU KWA KUVAA MAWANI SEHEMU FLANI AU KILE UNAJUAJE LABDA ANAMATATIZO YA MACHO NA ANAJALRIBU KUJIKINGA NA MIALE YA JUA ? HAYO YA SUTI WAKATI WA JOTO MBONA WATU WANAVAA SUTI KWENDA KANISANI NA WABUNGE PIA WANAVAA WATU WENGI TU HAU KANISANI KUNA BARIDI? ACHENI HOJA ZA KIJINGA KAMA HUONI CHA MAANA JAMAA LAICHOKIFANYA JUST MOVE ON.
    mdau mzawa

    ReplyDelete
  20. Kwa niaba ya wahitaji tunashukuru kwa msaada wako na mola akujalie upate maradufu.

    kwa niaba ya mahakimu wa mahakama za ustaarabu tafadhali uwe makini unapotaka kujitambulisha katika majukwaa kwa madhumuni ya kisiasa. ndg. yangu ni vema uwe makini sana unavyojiwakilisha katika kadamnasi na pia katika matumizi ya mara kwa mara ya vyombo vya habari vinginevyo muulize Sarah Palin maana bado kitambo kidogo 'lipstick zake mwenyewe' zinaanza kumpaka pasipotakiwa!

    ReplyDelete
  21. Ama kweli kwenda shule sio kuelimika!

    ReplyDelete
  22. Kweli watanzania wengine bwana hata waende shule ushamba unabakia palepale jamaa utafikiri katokea moshi. sasa kutoa sijui viblanketi ndo huite kadamnasi au masifa tu. Mimi naona kukaa sana marekani wabongo wengine akili zinaruka ila hawajitambui

    ReplyDelete
  23. Bwana Mashaka hapo unaonekana kama Body Guard sema tu-2 huna kifua!?

    Actually hiyo picha ya kwanza nilidhani unamsaidia bosi kuishusha laptop, anyway..

    why did they let go like that? i mean someone is responsible.

    halafu hapo juu, kumbukeni presantation ni kitu cha muhimu sana.. acheni kufananisha degedege na mashetani!? sijui mnaamanisha kwasababu mimi hapa natoa US Dollar 2 ($2) kila mwezi kwenda Oxfarm hili wasaidie watoto hapo Africa lakini sijawahi kuchukua picha na kuleta hapa!?

    mnakuja kasi?

    Buffalo,
    New York

    ReplyDelete
  24. NIMESOMA SPEECH YAKO BWANA MASHAKA KULE KWA MICHUZI JR!. TWO QUICK COMMENTS,

    1 YOU CRAFTED YOUR SPEECH KAMA -UNAJI -INTRODUCE IN THE LARGE ARENA (I BELIEVE THATS THE UNDERLYING IDEA , BUT THE AUDIANCE IS THAT ONE YOU CLAIM "IN NEED OF BASIC NEEDS",MEANING- THIS SPEECH IS TOO HIGH CALIBER FOR THEM TO GRASP THE UJUMBE!!!!!!. WHY NOT A SIMPLE SPEECH?

    2.I CAN READ THE FINE PRINTS ON WHERE YOU ARE HEADING BUT, MY USHAURI WA BURE; TAKE OFF THE SUIT JACKET (COAT), ROLL OUT THE SLEEVES TAKE OFF THAT EARPIECE, TAKE OFF THAT EXPENSIVE CELL PHONE, TAKE OFF THOSE DOLCE AND GABANA GLASSES---THEN PREACH WHAT YOU WANT TO PREACH.OTHERWISE YOU WILL BE MUTING WHAT YOU HAVE SAID ON YOUR SPEECH.
    OTHERWISE NENDA DODOMA KWAWATISHE WALE WANAJUA VALUE YA WHAT U HAVE VERSUS THE CONTENT OF YOUR SPEECH MAYBE THEY WILL GIV U A ROOM

    PR wa NAPE.

    ReplyDelete
  25. I am not a hater na sio muosha kinywa na naomba nianze kwa kumpongeza jamaa kwa jambo jema alilofanya na pia kuwa namfagilia sana Mashaka. Sikumjua mwanzo mpaka alivyowekwa humu na katika tovuti nyingine miezi kadhaa iliyopita na nikasikia habari zake kwa watu wanaomfahamu. Napenda kusikia/kuona wabongo wakijiwezesha na kupepea vema bendera pindi wawapo nje.

    Ila kuna mambo mawili aliyofanya hapa si ya kistaarabu. La kwanza kubwa ni kuvaa miwani ya jua wakati anatoa hotuba; tena wengi anaoongea nao hapo ni wazee waliomzidi umri. That is considered very rude.
    La pili ni bluetooth earpiece... sidhani kama alikuwa anaitumia muda huo, ya nini sikioni. Kwani angepigiwa simu angepokea hapo? Lakini hii sio bigi deal sana.

    Kuhusu mengine kama sijui kavaa suti wakati jotom hapo mi naona watu mnaenda too far. Ni uhuru wake, kama ye anaona joto analimudu we inakuhusu nini? Mwisho we uliyedai hapati ubunge... kwanza kakuambia anagombea; na hata kama atakuja kugombea,... kama we hutampigia jisemee mwenyewe. Wapo wengine watakaompigia kura.

    PS: Nshimimana aka Dumisane, hiyo aliyo nayo jamaa ni earpiece sio handset

    ReplyDelete
  26. Kumbe huyu mtu alikua anapalilia njia ya kurudi bongo.

    Kweli akili kichwani kwako.

    Wale wengine na matawi ya CCM na wengine tulianza kuona topic nyingi tu za kujieleza kwenye blog....nikajiuliza mbona watu wengi tu wanatoa misaa lakini hawajitangazi?

    Sasa ile big job kweli ameiachia? Mimi naona ile ingezidi kuingiza Dola nchini mwenu na kusaidia wengi zaidi.

    Kazi yake ile I am sure alikua anapokea six figures saa huko bongo kweli atapata kazi ya kumlipa $100,000 per year.

    Mimi ningekua na kazi ile kweli ningefanya na kila siku napeleka 50,000 kwa hao watu kuwapa mitaji na knowledge ya kusurvive.

    Mablanket yanaisha. Na kesho yakiisha tena sijui huyo mtu asubiri msamaria mwingine tena kuwapa misaada.


    ReplyDelete
  27. Mweeeee blue tooth, sunglasses

    Sio kosa lake ...alikua anaishi North Carolina na alisema yeye ni bank investors akasema anafanya Wall street, NY.

    Angeishi NY City kweli asingetoa hiyo presentation kwa makeke hivyo. Sunglasses na bluetooth za nini ndugu yangu?

    Unapoteza maana ya misaada yako.

    Mdau NY City

    ReplyDelete
  28. John Mashaka, thanks for helping the people in need! There are many who still needs our support but I'm afraid that still majority of them are forgotten. Thanks for showing the way and keep it up!

    Mdau,
    Gothenburg,
    Sweden.

    ReplyDelete
  29. Suala si wivu, suala ni jinsi alivyowakilisha hiyo misaada.

    Kutoa misaada ni jambo jema, na kila mmoja anajua. Lengo kuu ni kusaidia ambao hawana uwezo.

    Lakini wakati mwingine inaweza kuwa na lengo lililojificha kama kutafuta umaarufu, kujenga jina nk

    Kama alikuwa na nia ya kutoa msaada angeweza kwenda kutoa msaada kimya kimya ikaisha, hapo lengo ingekuwa ni kusaidia

    Lakini kwa kuwa kuna waandishi wa habari, basi iko wazi kuwa kaamua kufanya hilo kama tukio la wazi kwa jamii (Public)

    Kwa mantiki hiyo basi, alipaswa kutumia akili yake kujenga mwonekano sahihi kwa jamii. Angeweza hata kuchukua muda na kuvaa mavazi sahihi, kuchapisha risala, na kuvaa kirahisi tu, na bado watu wangemuelewa.

    Hao wanaosema kuwa baadhi ya watoa maoni wana wivu, sidhani kama ni wivu, ni suala la kukubali kukosolewa pale unapofanya mambo mbele ya jamii.

    Nadhani nimeeleweka.
    Pengine ushauri wa bure, sisi bado ni waTanzania, hivyo kama unaenda kusoma risala hadharani, jenga taswira sahihi.

    ReplyDelete
  30. MTU MSOMI ATA-COMMENT NAMNA HII:

    MOJA:HONGERA BWANA MASHAKA KWA KUSAIDIA JAMII.MUNGU AKUZIDISHIE DAIMA.HILO NI JAMBO ZURI NA LA KUTIA MOYO.KEEP UP THE GOOD WORK.

    MBILI:AS LONG AS ULIKUWA UNAITUMIA TECHNOLOGY HIYO KUKUSAIDIA NA MIWANI KUKUKINGA NA JUA,THEN NO BIGGY.OTHERWISE WAS JUST SHOW OFF.

    AGAIN KEEP UP THE GOOD WORK, THAT'S ALL WHAT MATTERS.

    ReplyDelete
  31. DON'T HATE CONGRATULATE.
    Jamaa hayo makolombezwa mengine yote that's his swagger.
    Suti kama haikupi joto wewe inakusumbua nini? Sawa sawa na pili pili hiko shambani wewe unalalamika inakuwasha.
    Mawani kavaa yeye yana husiano gani na misaada aliyotoa?
    Bluetooth hiko sikioni kwake mbona haikumzuia kusoma speech yake?
    Speech hiko kwenye laptop mnajuaje kama hakupata mda wa kuprint au hakuwa na printer?
    Kwahio hivyo vya juu vyote ndio mmeviona vya kukosoa kiasi cha kwamba huo msaada aliotoa hauna maana? Ndio mnafisadiwa kwa ajili ya akili ndogo.
    Watu wangapi wanafanya fujo hapo za kijinga na hawatoi misaada hamuambii kitu ?

    ReplyDelete
  32. Michuzi, umenibania comment yangu niliyoitoa leo asubuhi juu ya huyu jamaa.
    lakini sio mbaya wewe ndo mwenye blog.
    Powa jamaa anajua analofanya na atajifunza mwenyewe hali ya kibongo.

    ReplyDelete
  33. I hate misaada Mungu anisamehe kama nakosea kwa hili. Cha muhimu sio misaada nchini. Tunahitaji knowledge ya kuweza kusurvive. Hivi mablanket na vyandarua vikiisha ndio basi tena.Walaendeleaje na maisha au wanaotoa ni kwa malengo yao na wakipata wala hamna follow up.

    Kuna mtu alisemaga ukitaka kumsaidia mtu usimpe samaki, mpe ndoana akavue.

    Na elimu yako usingetumia hiyo hela kununua mablanket. Ungefungua taasisi ya information and skill assessing. Hao watu wawe na mahali pa kuweza kuwasaidia kupata knowledge ya kuweza kuwaondoa katika umasikini huo.

    Honesty kuna maskini na walemavu wengine wanaweza kupatiwa knowledge wakaweza wakaendeleza maisha.

    Asante kwa kuwapa Blanket lakini blanket na press conference, the way you present this and that mshikaji noma sana.

    Hayo ni maoni yangu tu I am not a hater

    ReplyDelete
  34. Im not a player hater
    Wabongo kweli tunapenda kuponda na kukandia vya kwetu,watu wetu.Najuwa bongo ni sehemu ya joto lakini si tatizo kwa mtu kupiga suti.Hii si mara ya kwanza kumuona mtu akipiga suti kama Mashaka.SUTI ni vazi la heshima na linalokubalika katika weather yoyote ile duniani.
    sina uhakika kama hiyo suti ilitengenezwa kwa lengo la kuvaliwa afrika au la ninachojuwa ni kuwa suti zinatengenezwa kwa kuendena na weather ya eneo fulani.Mfano suti iliyoshonwa kwa lengo la kuvaliwa sehemu ya joto inaweza kuwa nyanya ktk sehemu ya baridi.Scroll down kwenye picha ya Nyerere na waandishi mnaona ni wangapi walivaa suti kama Mashaka na jiulizeni maswali wenyewe.Acheni kuwa mnasema PUMBA ili mradi mseme tu.Mbona marekani kipindi cha Summer watu kibao wanavaa suti? Hivi angevaa kaplii na fulana,or traki suti, chini ana ndala ama sendozi si mngesema ni kutokuwa na heshima?Wabongo bwana.
    Lakini hiyo ya kusoma toka kwenye laptop ni over-showing bro.Kwa nini hukwenda kama wengine wanavyofanya?Anyway hizi ndizo za wabongo.Kujionyesha kwiiingi.
    I doubt huyu jamaa anafanya kazi Wall street(NY) kama wengi wanavyodai.Nilivyosikia mara ya kwanza huyu jamaa ni banker na anaishi somewhere in
    North Carolina sasa Wall street na NC wapi na wapi?Au NC kuna branch ya wall street?I dont believe it.

    ReplyDelete
  35. Ano. September 10, 2008 4:59 PM Mimi na wewe kwanza kabla ya jamaa na misaada ya serengeti lager sasa wewe unasema jamaa kama katoka Moshi, r u out of ur mind? Unajua watu wanaotoka Moshi wewe? Jiangalie na please usirudie tena kufananisha wakuja wenu na Moshi. Ona sasa madubwena kibao, no social skills at all.
    Unajua za mwizi 40 unaposema uongo unakamatwa kirahisi sana trust me na ndio haya yanatokea sisemi mengi ila wadau juu wameshasema. Kama alitoka mfukoni kwake haya, kama aliandika proposal akapata fungu haya, kama alichangisha watu wa ofisini kwake maana wanatoa tu hapa who care kama msaada utapata sana na kama ni serengeti na yeye wako kwenye PR deal haya time will tell.But atleast ameonesha utu, sio kama hao ubongo wa flava wenu kila siku kulewa na kupiga watu mwisho jela. But hatua mbadala ni ujenga watu in skills na knowledge ya kusimama wenyewe maana kama ni hivi watataka tena after sometimes ikichakaa. meaning watakuwa omba omba for life mpo hapo!!
    Ila mshikaji anachechekesha kwikwikwikwikwikwi

    ReplyDelete
  36. Jamaa ameandikisha Charity US kapewa mahela ndio anagawa Bongo sio katafuta ..... msione vinag'aa!!!! Ulimwengu wa kwanza Charity dili muulize jamaa wa mambo ya michezo (Jina namuhifadhi...)

    ReplyDelete
  37. Huyu bwana, ni sawa sawa na westerns who are using African problems to make a living for themselves not for Africans he has just set up “The John Mashaka Charitable Foundation” you can Google to get his website, Fanya wema nenda zako, kuna wabongo wanafanya mazuri and never even seen. Picha, na video is to be used for fundraising purpose, Mashaka just be Mashaka, Kijijini kwanu wanahitaji maji, to mention few..

    Ok mewapa Unga bulanketi, vikiisha je? …. AFRICA DOES NOT NEED AID, WE NEED TRADES TECH THEM HOW TO FISH…. Amen

    ReplyDelete
  38. KAMA NI MSUKUMA BASI LAZIMA ATAKUWA AMECHANGANYA NA MHAYA, EITHER UPANDE WA BABA AU MAMA, MAANA HIZI SHOW OFFS NI TABIA ZA WATU WA KURE KWETU.... Hiyo wall street ulikuwa unafanya kama mfagiaji or? tunaomba CV!

    ReplyDelete
  39. wewe bwana mdogo Ano september11, 2008 1:19 usilete za kuleta hapa kwanza inaonekana hata moshi yenyewe huijui labda hukunielewa namfanananisha na wafanya biashara wa moshi lakini akisema ametoka marekani halafu amefanya kazi wall street NY basi hajaribu kurekebisha image yake maana anaonekana kama vile katokea moshi teteteteee

    ReplyDelete
  40. haya john mashaka huyo, kakaa huko us na mapesa yote kaona bongo kuna dili karudi nyie mtabaki kuyoyoma tu humu ndani,na ku beba maboksi mwenzenu ndio huyo.Mtumie akili uko majuu sio kushangaa maghorofa tu nakutoboa vipuli mambo ya mtoni si kusoma speech kwenye vijikaratasi mwenzenu ana taka kuonyesha alivyo jifunza kwenye kazi yake ya kistaarabu tembeeni babu muone ukizoe kufanya ofisini uta act kiofisi ofisi ukizoea kubeba maboksi utavaa hata bukta kwenye mkutano. Unaishi kutokana na hadhi,ndio raha ya kitabu hiyo jamani bakini hukohuko us mpaka maghorofa ya waangukie wenzenu bongo wanapeta tu na masuti.

    ReplyDelete
  41. Inawezekana kuna walakini katika kuvaa mawani na bluetooth lakini hiyo isichukuliwe kama a big deal. Pia anaweza kuwa anania ya kujijengea jina hata kama ni kwa ajili ya kisiasa lakini kwani kuna ubaya gani? You have to start somewhere. Kikubwa ni kwamba anaonekana ana lengo zuri la kutaka ku-make a difference katika jamii. Fikiria pia angeweza kutulia quitely na kufurahia maisha yake.
    Tukosoane kwa nia ya kupeana moyo so that he/we can make it better next time
    Niliona link zifuatazo about him
    http://www.wsoctv.com/family/15032767/detail.html
    http://www.mashakafoundation.org/

    ReplyDelete
  42. Huyu kijana, na hiyo bluethooth yake naona ameishi sana na wanaigeria. Nnaigeria akishaweka hiyo utamsikia hata ukiwa 100km, my sister ooooooh, my brother ooooooh me ade bought a new BM from the box but no petrol in my car ooooh darling.......labda alikuwa akisubiri simu toka kwa kimwana.
    J. London

    ReplyDelete
  43. Okay...nadhani ameshapata pigo la kutosha. Huyu jamaa kusema kweli ni mkali. Mimi nilikuwa simfahamu kabisa...lakina baada ya ku-google jina lake...inaelekea ni mtu mwenye roho nzuri. Hata hivyo sitabadilisha maoni yangu niliyotoa mwanzo...kwa maana sidhani alilofanya ni jambo la busara. Lakini nakupa big-up kwa kazi yako nzuri. Kama huna any interior motives kama vile urais, ubunge na hasa ufisadi basi may God richly bless you in your work....

    mtoto

    ReplyDelete
  44. kunawatu wamechonga sana kuhusu jm. eti kama anatoa msaada inabidi awe kimya.
    sasa angalieni rais anatoa futari kwa yatima lakini wamemtoa ktk news sio rahisi kuwakibia kina michuzi hatakama hutaki.

    ila pia sio vibaya kwani nabidi watu waone ili wafate mfano.

    mashaka umebarikiwa sana!!!

    ReplyDelete
  45. Raisi ni raisi na ni documentation zake hata atakapo maliza kazi atakuwa na kumbukumbu.

    Sasa kila mtu anayetoa kidogo bongo akapiga picha na kuleta huku si tutabanana tu hapa kwa sana?

    Huyo anayesema anatumia laptop kutoa presentation yake kwa vile ni msomi. Presentation na projector iko wapi? Tofautisha speech na presentation.

    Hizo presentation ndio Monday morning meetings za wengi huku kwa hiyo tunaelewa tunachokisema.

    Show off blue tooth za nini?

    Au bongo big deal kuonekana mtu wa network sana? Wenzako tunaishi na blackberry na kila kitu kinajisort huko. Kama nina meeting/presentation ninaput in my blackberry na any phone inayokuja itapelekwa direct inakohusika na huo muda ni kuwa niko busy na mambo muhimu.

    Kutoa ni moyo lakini kupave the road kutumia migongo ya watu sio vizuri.

    Na mimi niweke picha za mabati ya shule tuliomalizia kuweka kwenye shule mwezi wa saba humu? Kwanza wala sikuchangisha kaelfu moja kangu tu ndio hako kalinunua mabati na sister akatoa hela a ujenzi.Big deal? NO kwa vile nilitoa rohoni na wala siwezi kumtangazia mtu kuwa nimefanya hivyo

    ReplyDelete
  46. Nyinyi picha za misaada hamzitaki mnaponda ,kila kitu mnaponda,
    Hapa nimeona kwanini the utamu anatoa picha zenu za ajabu hili watu wamwamge siri zenu manake hata angetoa picha zenu za maana bado watu wanaponda tu..
    Kama wewe huwezi kutoa msaada nyamaza tu jisaidie mwenyewe.
    Sasa watoto yatima kuwapa chakula kuna ubaya gani? Mnasema atoe ndoano wakavue,hao watoto wataweza kufanya kitugani hapo nchini kwetu ambapo mtu ana digrii tu anasota? Tufikirieni jamani.
    Hao wazee na mnajua nchi hilivyo tupa wazee wetu ,mnamlaumu kwa kuwapa mablanketi wazee wajikinge na baridi na mbu kwamba wakatafute wenyewe kwa nchi gani watanzania?
    Mbona tunapenda kuleta utani kila mahari kwanini jamani? Kama mtu huna cha maana kuongea kwanini usiende kwenye post nyingine ukaandike unachotaka?
    Kwanini kunapotokea jambo la maana hatupendi kupongeza na tunatafuta sababu za kijinga?
    Kama wewe mungu kakujalia unaweza kumudu maisha basi sio kila mtu kuna watu wanahitaji msaada.
    Mbona wamarekani wanatoa misaada ya vyandarua wanapongezwa? Yani huyu mashaka kutoa blanketi ndio mshamshambulia kiasi hichi?
    Mbona wabunge wanawapa mipira na jezi hili muwapigie kura na bado mnapiga ?

    ReplyDelete
  47. Mashaka au rafiki zako hawana haja ya kuendelea kubishana.
    Kazi yako ya kutoa msaada ni nzuri sana period.Kuvaa suti katika shughuli kama hiyo au hata kama unakwenda chooni si tatizo period!

    Mafujo yako ya kuvaa miwani myeusi tiii wakati wa hotuba na ma-bluututhii na ka laptop bila multimedia projector ndio hayana majibu mpaka kesho.

    Mimi mpiga kura (kama ulivyokwisha nieleza madhumuni yako toka mwaka jana)nakusubiri useme tu kuwa samahani nilichanganya masomo basi tuendelee mbele. Wewe na wanaokutetea kutundika blue tooth mkingángána na hayo hata itabidi tuanze uchunguzi wa hiyo misaada yako maana tutaanza kuwa na wasiwasi nawe. Ukikosea, unasema tu kumradhi basi yanaisha tunaendela, kwani nani hakosei hapa ulimwenguni?

    ReplyDelete
  48. Karibu nyumbani Mzee Mwanakijiji, ujue ukileta habari zako za Jamiiforums huko watakukamata sasa hivi wakijua wewe ndio Invisible- be careful.

    ReplyDelete
  49. Ano.September 11, 2008 11:48 AM,
    Gotcha, but usiseme sijui Moshi please, right! I am nah lake wale wanaokataa kwao. Sisi tulianza kuja huku kutafuta uhuru na Nyerere unajua hilo? so hakuna jipya mtu mtu wa foundation na kamba za wall street... namean? siku ingine ukuwepost...kuwa makini.
    Peace outta

    ReplyDelete
  50. Ano September 11, 2008 2:41 PM,
    You are very true. Thank you for link. Nilijua tu kuna kitu kama hii.

    ReplyDelete
  51. FAMOUS MASHAKA JOHN.
    NDUGU ZANGU WATANZANIA TANGU KIJANA HUYU AINGIE KATIKA BLOG NA WEB SITE MBALIMBALI NILITENGEMEA WATANZANIA WENZANGU WANGEJITAHIDI SANA KUMPA KIJANA HUYU MAWAZO KWENYE MAZURI NA MAPUNGUFU YAKE ALIYONAYO KAMA MWANADAMU WA KAWAIDA NIMEONA KIJANA HUYU AMEJITAHIDI SANA KATIKA KUJITOLEA KUSIMAMA KWENYE MAJUKWAA KUZUNGUMZA MENGI ALIYOTAKA KUZUNGUMZA KUNA MAPUNGUFU AMBAYO KILA MTANZANIA ANAONA KATIKA KONA MBALIMBALI KILICHOTAKIWA HAPA NI KUTOA MAWAZO TOFAUTI YENYE MSINGI WA KUKOSOA KWA KUTUMIA LUGHA ZA KISTARABU KABISA ZITAKAZOMSAIDIA.

    KWA UZOEFU WANGU NAELEWA UNAPOKUWA KIONGOZI HUWEZI KUELEWA KAMA WANANCHI WAKO WANAKUFATA AU WANAKUMBIZA. NILIVYOMULEWA MASHAKA ALICHOTAKIWA

    (1) NI FANYA STUDY ZA KUTOSHA KABLA YA KUPANDA JUKWAANI KWAMBA WATANZANIA WANAHITAJI NINI,

    (2) KUWA MUWAZI ZAIDI KWA WATANZANIA KUJINADI KWA SERA ZA UKWELI NA UWAZI ILI JAMII IELEWE KWAMBA UNATOA MISAADA INATOKA WAPI NA NI KWA NIA GANI

    (3) KAMA KIONGOZI NAKWENDA KUNADI SERA ZANGU OUTLOOK YANGU IWEJE KWA WATANZANIA.

    (4) KUJUA WATANZANIA WENGI TUNA LEVEL GANI YA ELIMU NA UPEO WA KUELEWA NA KUCHANGANUA MAMBO

    KWA WATANZANIA WANAOPENDA KUMJUA MASHAKA NA KUJUA NI NINI ANACHOFANYA MASHAKA WAKO NA FOUNDATION INAYOITWA JOHN MASHAKA FOUNDATION WAKO BOEARD DIRESTORS WAFUATAO, MASHAKA ,LA TASHA,MARTIN LATONYA NA MARIA FOUNDATION HIYO IKO SUPPORTED NA JAMES, CATHERINE ARNY NA ESTER WOTE WAKO WACHOVIA BANK NDICHO KINACHOPELEKEA YEYE KUPATA WATU WANYE MOYO KUJITOLEA NA KUDONATE WANACHOJISIKIA.

    USHAURI WANGU BINAFSI KWA MASHAKA USISIKILIZE SANA MANENO YA WATU NA KUWA MUWAZI ILI WATU WAKUELEWE MANAKE WATANZANIA HAWAELEWI MARA WENGINE WASEME UNATAKA KUWA RAIS MARA UBUNGE MARA UMAARUFU LAITI UNGEWAPA UKWELI HUU WANGEKUWA NA MAWAZO.
    PILI PUNGUZA KIDOGO SHOW OFF KUWA NA MAADILI YA UONGOZI USIWE NA ATITUDE YA KISANII NA KUJISHOW KWA KWA SISTER DU WATAKUCHANGANYA SANA HASWA HAPA JIJINI
    TATU JINADI KAMA ORGANIZATION NA SIO KAMA MASHAKA JOHN KAMA NINGEKUWA NA UWEZO WA USHAURI NISINGESEMA UJIITE JOHN MASHAKA FOUNDATION KWA SABABU UNAPOKUWA NA ORGANIZATION NI JUMUIYA ONDOA MUONEKANO WA BINAFSI KUNA MAJINA MAZURI TU KAMA LIGHT OF AFRICA, FUTURE OF AFRICA, KOMBOA AFRICA, ETC.

    USHAURI KWA WATANZANIA MSIWE NA JELOUS NA LUGHA MBAYA KAMA KUNA MTU AMBAYE ANGETAKIWA KUTOA LUGHA MBAYA KWA MASHAKA MIMI NINGEKUWA WA KWANZA KABISA KWANI APRIL 2,2008 FIANCEE WANGU BILA KUSHAURIANA NA MIMI ALITOA AHADI LIVE BONGO CELEBRITYKWAMBA ALIFANYA MEETING NAE MWAKA 2007 ATAMSAIDIA IN SETTING UP NGO NA LIVE ALIAHIDI KUMTUMIA MAIL PERSONALLY KUHUSIANA NA MAMBO HAYO.
    KWA HIVYO WATANZANIA TUMUUNGE MKONO KIJANA WETU


    UKITAKA KUPATA HABARI KAMILI KWA FOUNDATION YAKE BOFYAwww.johnmashakafoundation.org

    BALTAZAR
    WWW.KIPEPEOTOURS.COM

    ReplyDelete
  52. Jamani katika maoni yoote kweli mzee wa kipepeo funika ametoa maoni mazuri sana kijana huyu au sijui ni mzee wa kipepeo anaonekana ni kichwa sana michu you need this guy keep him closer he sees things from different angle and easy access for info and he deliver the right msg au kaka kipepeo ulishakuwa CIA nini manake kwa kweli umejitahidi sana man kutulewesha wabongo unajua huyu kijana anajinadi sana kama vile aonekane ana mahela mengii kumbe anakuja kutamba na hela za donation,Ila bro Kipepeo itabidi demu wako au kama una mpango wa kuomuoa inabidi umpige stop kali asifanye mazoea na huyu jamaa unajua huyu mshikaji hata hapa states ana tabia za Nigeria unawea kujikuta mama katoa gari jamaa anatembelea, manake jamaa ana lugha bwana unaweza kuona Kijana si ndio huyu kumbe ni bonge la msanii yaani kma vile wahaya manake pia totoza ndio zake haswa kamdemu wako ni mweupe hahahahaha pole man, mchunguze fiancee wako sana asizoeane na huyo mshikaji kama ni rafiki basi jua ndio hivyo tena na kwa nini demu wako amzoee mwanaume hivyo mpka kujilipua live kutoa misaada usikute faida ya kipepeo unagawana na mashaka nusu kwa nusu,
    POLE KAKA WANAWAKE SIKU HIZI HATUITAJI USHAURI KWA WAUME ZETU TUNAPIGA CHINI KWA CHINI ILA SALI SANA KAKA MAMA AWE MUWAZI KWAKO SIO MISAADA YA KISIRI WALA SIO KUDELETE SENT,DELIVERY MSGS,RECEIVED AND CALLS,
    HAHAHA ILA NAMJUA DEMU UNAEMZUNGUMZIA JINA LINAANZA NA E, WALIJIRUSHA SANA LAST YEAR WHEN THE GUY WAS ARROUND.
    BIG TIME MAN
    NYC

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...