Tovuti kubwa na maarufu inayoshughulika na masuala ya urembo ya Global Beauties, leo imetoa utabiri wake wa warembo wa Miss Earth 2008 yanayofanyika Manila, Philippines. Mashindano haya yanayojumuisha takriba warembo 90 ni kati ya mashindano makuu duniani (yaani Grand Slam).

Katika tovuti ya Global Beauties, Miriam amewekwa namba 2 katika uchambuzi wa awali wa wataalam wa masuala ya urembo (soma:

/earth/2008/e08_tree.htm).
Nafasi hii ni ya juu na inaonyesha mafanikio ya Miriam Odemba katika mashidano haya. Hata hivyo Afrika inatabiriwa kufanya vyema mwaka huu kwani warembo wengine kutoka Botswana na Sudan ya Kusini pia wamewekwa katika utabiri huu wa 16 bora.

Lakini Miriam kawaacha mbali warembo hawa na wenzake wote isipokuwa mrembo wa Romania. Hii ni dalili njemakwani hata mwaka jana mrembo wa Miss Universe Tanzania 2007 Flaviana Matata aliwekwa katika orodha hii ya GLobal Beauties kama mrembo anayetabiriwa kufanya vizuri, na ikawa hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hivi haya si mashindano ya nachural byuti? Mbona wanawake wetu wa afrika (karoso msudani) wana nywele bandia?

    ReplyDelete
  2. This is pure nonsense

    ReplyDelete
  3. jamani waswahili hamuachini hila kwani kinachoshiriki hayo mashindano ni nywele au mtu?

    ReplyDelete
  4. nakubaliana na mdau aliyesema "this is pure nonsense" miriam kama haukufanikiwa wakati zile za face of africa mama sahau
    umetanga tanga na njia na sasa uko huku jamani wadada wa kitanzania fanyeni mambo ya maana shule ni muhimu miss earth or whatsover won't take you anywhere get up na uangalie nini unataka and go for it na wadau wa urembo angalieni mbele

    ReplyDelete
  5. Wewe hapo juu unaona gere! kwani umeambiwa haja soma?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...