Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda kikagua gwaride aliloandaliwa baada ya kuwasili Accra, Ghana, kihudhuria Mkutano wa Sita wa Jumuiya ya Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pasific (ACP)
Waziri Mkuu Mh.mMizengo Pinda na Mkewe Tunu wakitembelea Uwanja wa Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Ghana, Kwame Nkurumah jijini Accra walikokwenda kuhudhuria Mkutano wa Sita wa Jumuiya ya Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (ACP) jijini Accra. Nyuma yao ni Mnara uliojengwa kwenye kaburi la kiongozi huyo
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mh. Philip Marmo (kushoto) wakiwa katika Mkutano wa Sita wa Jumuiya ya Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pasific (ACP) uliofunguliwa leo na Rais wa Ghana, John Kofuor jijini Accra Ghana
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Philipo Marmo (kushoto) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr. Theodorous Kamala katika Mkutano wa Jumuiya ya Wakuu wa Nchi za Afrika, Carribean na Pasifiki (ACP) uliofanyika jijini Ghana leo
Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu wa New Papua Guinea, Michael Somare jijini Accra, Ghana, ambako wote wanahudhuria Mkutano wa sita wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (ACP).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Nchi inaitwa Papua New Guinea,ni vizuri kuwa unahakikisha spelling kabla hata ya kupeperusha.

    ReplyDelete
  2. Hivi huyu jamaa kavaa sketi, au ?

    ReplyDelete
  3. ndio huko wanaume wanavaa sketi kama vile wamasai wanavyo vaa shuka!

    ReplyDelete
  4. Hilo ndilo vazi la taifa kwa visiwa hivi vya Papua new Guinea,Fiji Samoa n.k ni kama sketi fulani hivi ila jamaa wanajivunia na vazi lao la taifa...na sie hapa bongo tuwe tunavaa mavazi yetu kukuza utamaduni wetu..

    ReplyDelete
  5. mbona huyo wa guinea kavaa skirt?

    ReplyDelete
  6. VIONGOZI WETU WAONE KUWA SIKU ZA KUKUMBATIA MAVAZI YA WAKOLONI ZIMEKWISHA. WAAFRIKA TUNAWEZA KUVAA MAVAZI YA ASILI YETU NA KUPENDEZA PIA. SIO SUTI KILA KUKICHA. KUANZIA KIPAIMARA, KUOA / KUOLEWA, MAOFISINI HADI KUFA NI SUTI TU ZA NINI?

    PINDA ANA LA KUJIFUNZA HAPO KWA VIONGOZI WA AFRIKA YA MAGHARIBI.

    ReplyDelete
  7. ACP ni Jumuiya muhimu sana kwetu kiuchumi na kibiashara.hususan katika kujenga msimamo wa pamoja baina ya nchi changa za jumuiya hiyo na nchi zilizo endelea zaidi kwa viwanda duniani.Ulikuwa ni mkutano muhimu sana kwetu watanzania.Labda katika mkutano mwingine utakaohusu mambo ya malaria na ukimwi labda mawaziri wetu wa masuala ya uchumi na viwanda na biashara ndiyo watakao chaguliwa wakatuwakilishe!In Tanzania no wonder a Medical Doctor can become a District Administrator!

    ReplyDelete
  8. Michu na Wadau

    Kuna taarifa eti ziliwahi kutangazwa na BBC sina hakika kama ni sahihi kwamba huko Papua New Guinea kuna lugha ya asili inafanana sana na lugha ya Kinyamwezi cha zamani ingawa lugha hiyo hivi sasa imechanganyika na baadhi ya lugha za huko je habari hizi ni za kweli?

    Mdau Muddy

    ReplyDelete
  9. Hapana, sio skirt wala vazi la taifa bali alitoka kuoga. Hiyo ni taulo. Inasemekana alihisi joto ghafla akaingia bafuni fasta! Hehehe...

    ReplyDelete
  10. Huku scotland hiyo wanaita KIRT ni vazi asilia lililo expensive sana.

    ReplyDelete
  11. anon hapo juu 2:12pm hicho kivazi sio kirt ni kilt ukisema kirt ushaleta maana nyengine asante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...