Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. salaam bro michu,

    Nina swali dogo tu

    kwanini hela yetu unapenda kuiita na kuilinganisha na madafu,kwa nini hailinganishwi na vitu vyenye mvuto na ujumbe zaidi wenye kuongeza tija kwa taifa na kwa nini watu wengi wanapenda kutukuza hela ya kigeni kuliko hela yetu ya tanzania,Kwani ni kweli kwamba Madafu ndo kitu pekee chenye kulinganishwa na hela yetu tu.Je mtindo huu si unaonyesha jinsi gani wengi wetu walivyo watwana wa mambo ya kigeni zaidi bado.

    naomba ufafanuzi bro michuzi kama hutamaindi

    ReplyDelete
  2. ANON WA 1 TAKE IT EASY,HAUJUI SLANG NINI

    ReplyDelete
  3. Hizi picha za obama zitatoka kesho kenye times magazine.

    Hebu weka hii link watu waone huyu mpiga picha wake alikua anampiga picha toka kabla hayawa big shot

    Very intimate and good memories

    asante

    http://digitaljournalist.org/issue0810/callie-bp.html

    ReplyDelete
  4. Uchumi wetu licha ya "Kengele Nyingiiiiii" bado uchumi wa Minazi "Coconut Republic".Sasa hivi(2008)Watanzania ni masikini zaidi kuliko walivyokuwa miaka 20 iliyopita!Amini usiamini.Katika Masoko ya Hisa ya Ulimwenguni Tanzania hatumo(?).Utakuta katika kulinganisha ufanisi wa ukuaji au uporomokaji wa mauzo au thamani za hisa katika soko rasmi la Hisa na Mitaji katika kila nchi KWA KANDA YA AFRIKA YA MASHARIKI utazikuta ni nchi za KENYA;UGANDA;na MAURITIUS tu ndizo zinazolinganishwa,na Tanzania haimo.Siyo kwasababu hawaijui au hawaipendi Tanzania bali ni kutokana na ukweli kwamba Soko la Hisa la Tanzania liko shaghalabaghala!Huwezi kulitumia ili kupima kiwango cha ukuaji na mwelekeo wa uchumi hata kidogo!Viongozi wetu watakupa takwimu za Pato la Taifa "amabazo mara nyingi ni za kughushi" ili kukuthibitishia kwamba uchumi wetu ni imara na umezidi kukua mwaka hadi mwaka!Shillingi yetu imekuwa ikiitwa ikutani kama fedha za Madafu kutokana na kupoteza thamani yake katika soko la kimataifa.Thamani ya Leo ya Dola Moja ya Marekani ni sawa na Shillingi za Kitanzania zipatazo shs.1,259/= kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania.Bei yao ya kununulia ni shs.1,246/=kwa Dola moja na bei ya kuuzia ni shs.1,271/=.Lakini katika maduka ya kubadilishia fedha za kigeni bei ya kununulia ni shs.1,278/=kwa Dola(shs.1,246/=BOT),na bei ya kuuzia ni shs.1,294/=(shs.1,271/=BOT).Noti za Dola Moja zinanunuliwa kwa bei ndogo zaidi ya shs.1,100/= kuliko ile ya Dola Mia Moja kwa sababu wasafiri wengi hawapendi kuchukua Dola Moja Moja zinasumbua.Ukilinganisha hata na sarafu zingine za nchi za Kiafrika ambazo kwa hakika uchumi wetu ni "Tajiri Zaidi" tofauti na "uchumi imara zaidi" kuliko wao bado utakuta sarafu yetu ya shilingi ina thamani ndogo zaidi kuliko sarafu za nchi hizo kama Kenya;Burundi na hata Uganda ukilinganisha na jinsi sarafu yao ilivyopanda chati kwa kasi zaidi na huku ya kwetu ikidorora kwa kupiga chapuo(marktime)palepale ilipoganda!Shillingi Moja ya Kenya hii leo ina thamani sawa na Shillingi 18 ya Tanzania(?);Faranga(Burundi Franc)Moja ya Burundi ambayo ilipaswa kuwa sawa na shillingi yetu ina thamani sawa na shillingi 1/20 za Tanzania(?);shillingi moja ya Uganda ina thamani swa na senti 76 za Tanzania(karibu sawa na shs.1/=).Kwanini shillingi yetu inapungua thamani kiasi hicho ikilinganishwa na sarafu hata za nchi zingine masikini zaidi za Afrika kuliko hata sisi wenyewe ni maelezo marefu kidogo.Lakini kikubwa zaidi ni kwasababu hatuna sekta imara ya viwanda,ni kama HAKUNA.Tunalazimika kununua mahitaji yetu mengi muhimu kutoka nchi zingine za nje,hapa kwetu tumekubali kuweka sera kandamizi kwa ukuaji wa viwanda.Matokeo yake siyo tu sarafu itazidi kudharaulika duniani katika soko la fedha za kimataifa,soko la Hisa na Mitaji la kimataifa BALI HATA AJIRA ZA HAPA NCHINI TUMEDIRIKI KUZI UZA NCHI ZA NJE (we have also decided deliberately and nakedly even to export domestic jobs overseas and in consequence compounding even much worse domestic unemployment to our people and still wanting to Tax the same jobless to finance social infrastructures!).HAPA NDIPO TULIPO SASA WATANZANIA WENZANGU.Umeshawahi kumsikia Kikwete akizungumzia habari hii toka aingie madarakani?Habari Ndo Hizo Wabongo!-tonny-

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...