Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM kilichofanyika ikulu jijini Dar leo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Hivi wazee hii habari ya kuendesha vikao vya chama ikulu inakuwaje??? Si ni nyumba ya kiongozi wa wananchi wote? Au ndio imekuwa nyumba ya kiongozi wa chama?? CHADEMA, NCCR, TLP na wengineo na wapewe ruksa ya kufanya vikao vyao phapo pia basi maana wanao wanachama ambao ni watanzania pia...
    Yaani hawana hata aibu ya kutenganisha chama na serikali..ovyooo

    ReplyDelete
  2. VIKAO VYA CCM VINAFANYIKA IKULU SIKU HIZI...HIVI KIKWETE ANATUPELEKA WAPI JAMANI..???!!!

    ReplyDelete
  3. Vikao vya CCM visifanyikie Ikulu. Hivi hakuna ofisi za CCM? Haya ni matumizi mabaya ya Ikulu. Tafakari.

    ReplyDelete
  4. Bwana michuzi na wadau ningependa kufahamishwa kuhusu haya mambo.... ni kweli hii ni sawa kikao cha chama kufanyika katika ikulu ya taifa? nilifikiri ikulu ni ya wananchi yote yani serikali na mambo yakichama ayausiki na serikali!
    naomba tu watu wanalolijua hili wafafanue

    ReplyDelete
  5. Nchi yao, chama chao, rais wao, ikulu yao, bunge lao wembe ni ule ule...aibu tupu nchi hii. Chama na serikali tofauti yake ni nini?

    ReplyDelete
  6. Bwana Michuzi. Katika katiba nyingi za vyama vingi si haki kwa chama tawala kutumia kutumia rasilimali za umma kuendeshe shughuli za chama. Ikulu ni ya watanzania ambao wengi wao sio CCM. Hayo maji wanayokunywa, umeme na gharama nyingi zinahusu hivi vikao vinalipiwa na bajeti ipi? ya chama au serikali?

    ReplyDelete
  7. MSAADA TUTANI (MAONI)

    Wadau,
    Mimi hii habari ya Kikwete, Rais wa nchi kufanyia kikao cha CCM ndani ya Ikulu, imenishangaza sana. Nimesoma Sayansi ya Siasa hapo UDSM, lakini nijuavyo mimi hiki kitu ktk nchi ya ki-demokrasia hakiruhisi kabisa, kutumia mali za serikali na wananchi kwa ujumla kwa manufaa ya chama.Kwa mnaokumbuka vizuri kesi ya Dr.Kabourou na Azim Premji mwaka 1994 ktk uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kigoma mjini, Kabourou miongoni mwa mambo mengine alimshitaki Rais Mwinyi ambaye alitumia mali za serikali kama ndege, magari ya STH, kulala ikulu ndogo ya Kigoma huku akifanya shughuli za kichama, kampeni ya CCM...Kwa mujibu wa Jaji Mchome, vitendo hivyo viliathiri uchaguzi, hivyo Kabourou kuibuka kidedea.Sasa hili nalo vipi tena wadauz?????Tulijadili jamani.

    Mimi hainiingii akilini kuona Ikulu inafanyiwa vitendo hivi. Kwanini wasiende kwenye jengo lao la CCM pale Umoja wa Vijana CCM walitumie, au wakakodi Ubungo Plaza na kwingineko??Matumizi ya mali zetu kwa shughuli za chama ni ubakaji wa demokrasia.Hii kwa watu wengi huwatishia kuona Chama kinazidi kushika hatamu.Kuna kitabu kipya kimetoka sasahivi cha Bwana MAKULILO, Alexander, PhD Student at Lepzig University, Germany kiitwacho TANZANIA: A De Facto One Party State? Unaweza kuipata kazi hiyo kupitia links hii, www.target.com/TANZANIA-Facto-One-Party-State/dp/3639086988

    MAKULILO Jr,

    ReplyDelete
  8. hivyo vikao vya CCM Ikulu kivipi? washauza jengo la Umoja wa Vijana sasa imebaki kutumia ofisi za serikali kufanyia vikao vyao

    ReplyDelete
  9. Nilisikia kuwa Mzee Makamba alifiwa na Mwanae "Kimweri".
    Kumbe amesharudi kazini?

    Kama ni kweli: Pole Mzee wetu.

    ReplyDelete
  10. I don't get it kwanini kikao cha CCM kifanyike Ikulu. Sisi wananchi wa kawaida ambao we have nothing to do with CCM we are paying for CCM bills. Please Mr Kiwete tusamehe sisi walala hoi, hatuna hizo hela za kuwalipia wanasiasa bills zao. Mdau Ukerewe.

    ReplyDelete
  11. Mbona huyu Kikwete anachanganya vitu.Mambo ya chama yanafanywa Ikulu kwa nini?Ikulu ni ya wananchi hivyo mambo yote ya serikali yanapaswa yafanyike hapo na siyo ya chama.Jamani muwe wastaarabu.

    ReplyDelete
  12. yaani hawa jamaa wa ccm wamejisahau kabisaa kuwa hiyo ni nchi ya vyama vingi na wengine hawana vyama kabisa ila wote hao wanamiliki hiyo ikulu kupitia kodi zao.Hawa mafisadi inabidi tuwaamshe ikifika 2010....subiri tu

    ReplyDelete
  13. Nchi inaelekea pabaya. Kikwete rafiki yangu na rais wangu, kipindi hiki naona mambo yanakuendea vibaya utadhani umenusa Zebaki (mmHg). Siamini kama kwa busara zako na hekima za watu kama akina Kingunge mngethubutu kufanyia vikao vya CCM Ikulu.

    Siamini kama ni wewe unaeongoza hicho kikao. Tunakoelekea kwa sasa siko.

    Juzi Pinda 'alionywa' kule bungeni kutotumia mambo ya kiserikali kichama. Wewe awali watu waliwahi kukupigia kelele kwa u-ccm wako kwenye mambo ya kitaifa. Sasa umegeuka, unaelekea kubaya zaidi. HAPANA MKUU, UMEKOSEA.

    Siamini kama nyote mliokaa hapo ndio wale wale mnaojua kushupaa nyakati vyombo vya habari vikifanya kazi zake lakini kwa hili la kutofuata katiba na misingi ya utawala bora mwaliona sahili.

    Tumekwisha. Naapa... CHAMA KIFANYIE MIKUTANO IKULU!!!!! Dunia hii hii ya demokrasia, na nchi hii hii yenye KHANGA ZILIZOANDIKWA WE CHERISH DEMOCRACY? No, come on!@

    ReplyDelete
  14. WOTE MMESAHAU KUWA CHAMA NDIO KILISHINDA UCHAGUZI KIKAUNDA SERIKALI NA HIYO SERIKALI IKO CHINI YA CHAMA.

    MWENYEKITI WA CHAMA ANA MAMLAKA YA JUU YA SERIKALI, HATA MKUU WA MKOA HAFUI DAFU MBELE YA MWENYEKITI WA CHAMA WA MKOA NI BOSI KWAKE KWA SABABU CHAMA NDICHO KINACHOTAWALA.

    SASA NINI MAANA YA CHAMA TAWALA

    uliyesoma political science chuo kikuu, hebu tuelezee maana ya chama tawala na mfumo mzima ulivyo.


    pili Raisi ana mamlaka ya kumualika amtakae huko Ikulu.

    tatu, hao CHADEMA, wakishinda huo uchaguzi unafikiri hiyo Ikulu itakuwa mali ya Mbowe tu? Na Chadema watafanya hivyo2 labda wakitaka kuwa wanafiki wafanye vikao vya siri, kwa sababu chama chao ndio kitakuwa kinatawala. Na Mungu apishie mbali mwenyekiti mwingine wa chadema aje ndio ashinde, lakini akishinda huyo Mbowe sijui kutakuwaje huko Ikulu, hakuna kiongozi hata mmoja wa Chadema atakayetia mguu wake labda atoke kaskazini.

    ReplyDelete
  15. Mdau uliyosomea siasa ya jamii UDSM nafikiri haukuielewa vizuri!maana ikulu ni makao ya kiongozi wa serikali ya chama kilicho madarakani hivyo vikao kama cha kamati kuu hata mazungumzo baina ya rais na viongozi wake yanawezekana kabisa kufanyika hapo>kitu ambacho kinaweza kutushtua ni pale halmashauir kuu au mkutano mkuu wenye mamia ya watu utakapofanyikia ikulu!vilevile kuhusisha kufanyika mkutano huo ikulu ni vyema tuangalie je kuna gharama za mkutano chama kimedai serikali?maana naona hao wajumbe wa kamati kuu wengi wao ni mawaziri na viongozi wandaamizi wa nchi ambao vikao vingi wanakuwa ikulu hivyo kulalamika kwetu ni matokeo ya kutoweza kutofautisha hali halisi na udhanifu
    nzehe

    ReplyDelete
  16. Jana nilijaribu kutuma ujumbe, ila labda kuna mahali nilikosea, maana ujumbe haukuingia ukumbini. Ujumbe wangu ulikuwa ni wa kuuliza kama ni sahihi kikao cha chama chochote cha siasa kufanyika Ikulu. Mimi ni Mtanzania ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa, na niliona ni bora niulize hilo suali baada ya kukerwa na kitendo cha CCM.

    ReplyDelete
  17. Wewe mtoa maoni wa 11:48AM acha ufala wako wa kutokujua maana ya chama tawala huku ukimtaka mtu aliyesoma political science akufafanulie kwa ushindani.

    Wewe ndio wale wale mnaotaka tufungue miradi ya maji tukiwa na sare za CCM sio? Wewe ndio wale wale mnaotaka shule za kata zilizojengwa chini ya serikali ya CCM zitumiwe kwa mikutano ya kichama siyo? Sasa unatete mkutano wa chama ufanyike Ikulu. Fala wewe.

    Michuzi samahani, neno fala sio baya sana kiivo, naogopa kumuita mjinga.

    ReplyDelete
  18. wabongo inabid tupunguze kulaumu,ebu tuangalie gharama ambazo kikwete angetumia kutoka dar es salaam kwenda chimwaga hizo ni kodi zetu sisi na sio za chama kaliona hilo kapunguza gharama,nambie mawaziri wangapi ambao ni wajumbe wa kikao hicho wangetumia magari ya serikali na mafuta kwenda dodoma je kiasi gani tumeokoa kwa kikao hicho kufanyika dar es salaam?fedha wanazotumia ccm ni fedha za walipa kodi wa tanzania kwa sababu wanalipwa ruzuku kutoka serikalini lazima tujue kuwa ccm ndo serikal na serikal ndo ccm mpk hapo watanzania watakapoamua kufanya mabadiliko,la muhimu tumeokoa kiasi kikubwa sana cha pesa kwa kikao kufanyika hapo sababu rais ingembidi arudi tena dar sababu ya kupokea wageni kutoka denmark,hebu tuangalie rais ana msafara wa watu wangapi ambao wote wangelipwa posho kutokana na safari hiyo, tuache lawama tumezidi sasa kila kitu kwa nn huwa hatufikirii kwanza na wewe unayejiita msomi ulifundishwa kupinga huko udsm unashindwa kufikiria kwanza kwamba pesa watakazotumia ccm popote pale ni za watanzania na wanapoamua kubana matumizi ni kwa ajili ya watanzania na sio wana ccm.Ni ayo tu nawakilisha

    ReplyDelete
  19. Du yaani buku lako MAKULILO, Alexander, PhD Student at Lepzig University, Germany kiitwacho TANZANIA: A De Facto One Party State? Unaweza kuipata kazi hiyo kupitia links hii, www.target.com/TANZANIA-Facto-One-Party-State/dp/3639086988

    Bei yake $76 (dola sabini na sita) watakisoma kina Kingunge walioifanya ikulu kuwa jumba la mikutano ya CCM. je sisi walalahoi huweze kutupunguzia toka TSHs 76,000 kiwe Tshs 7,600 ili tuelewe uchambuzi wako Ndugu Makulilo.

    Mdau
    Malampaka Tanzania.

    ReplyDelete
  20. Matumizi ya Ikulu kwa manufaa ya chama ni totally wrong, lakini twende mbele na turudi nyuma....hata kama wangekodi ukumbi wowote mlipaji ni serikali in a way ambayo raia wasingejua. Viongozi wa juu wote wa CCM wanawalinzi(Bodyguards) ambao ni waajiliwa wa serikali. Naii hata tufanyeje ni concept ambayo kila cha kitatumia. Watanzania tukubali matokeo tu.

    ReplyDelete
  21. Hapa kinachofanyika ni jeuri ya "HAMTAWEZA KUFANYA LOLOTE" kama ilivyo ktk masuala mengine ya kifisadi yanayotokea.

    ReplyDelete
  22. JAMANI HAPO KULIA KWA JK SI NAFASI YA MH A.A.K MBONI HAYUPO? MISUPU TUFAHAMISHE KAMA ANA UDHURU

    ReplyDelete
  23. kudadadeki walhaiiiii,,,,raha kwa kwenda mbele
    kila mtu na nafasi yake na time lake,,ata nyie woooote apa mkiingia ikulu tu,,,weupeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  24. Na wewe mdau wa nov 2, 2:50, mie siwezi kukuita neno lolote baya maana hujui ulisemalo, yeye ni msomi wa political science angetumia usomi wake kutuelimisha na siye mantiki na maana ya chama tawala, maana kila mahali duniani si Tanzania tu kuna chama kinachotawala na vyama vya upinzani, sasa wewe hapo umeona ubishi ni nini? Kwani ni mara ya kwanza kwa vikao vya chama kufanyikia Ikulu tangu nchi hii iingie kwenye mfumo wa vyama vingi? Acheni kung'ang'ania kila kitu kwa nini? Kwa nini? Na si lazima pia kila mtu awe na mawazo na mtazamo unaoutaka wewe. Mie nimemuuliza Makulilo wewe kimekuwasha nini?

    Makulilo mwenyewe anaweza kujibu akaelezea jinsi system ilivyo na inavyofanya kazi. Na kama ni mapungufu anaweza kutuelezea namna inavyotakiwa kufanywa kuyarekebisha, wewe mwenzangu na mie unachemkwa nini? ''Kuuliza si Ujinga ila Ujinga ni kujifanya unajua wakati hujui!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...