Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Bongo hatuwezi kuendelea sababu ya watu wachache. Angalia dunia nzima mafuta yameshuka zaidi ya nusu bei,crude oil ilikuwa $147 a barrel mpaka $62. Hapa USA mafuta yalifika hadi $4 a gallon of 4-5 liters sasa ni chini ya $2.

    Bongo tuko karibu na visima lakini bei inatia kichefuchefu.
    Mdau USA

    ReplyDelete
  2. Heri wewe Mdau wa USA umesema labda Watanzania watazinduka na kulivalia Njuga suala hili.Galoni moja ya Marekani ni karibu Lita 3.71 hivi kama sikusahau.Kwa bei hiyo ya $2 kwa galoni maana yake ni kwamba Lita Moja ya Petroli itauzwa kwa bei ya shilingi 660/=.Hapa kwetu Lita moja bado inauzwa kwa bei ya shs.1,590/= na zaidi(?).Kulikoni?Hawa watu kama hawataki kushirikiana na serikali katika kupunguza mfumuko wa bei nchini KWANINI HAWAACHI KUFANYA HIYO BIASHARA YA MAFUTA?WAKAFANYE BIASHARA NYINGINE.Bidhaa ya Mafuta ni Nyeti mno kumruhusu mfanyabiashara yeyote ajitengenezee faida kubwa bila kujali athari zake kiuchumi.Nitawalaumu wafanya biashara ya vituo vya petroli LAKINI WA KULAUMIWA ZAIDI NI SERIKALI YENYEWE KWA UZEMBE NA KUTOJALI!Kodi inayotozwa kwenye bidhaa ya mafuta ni kubwa mno!Kwanini iwe hivyo?Hivi kweli Wizara ya Fedha hawatambui athari zake katika uchumi?Upo umuhimu wa KUIPIGA DEKI WIZARA NZIMA YA FEDHA!wafanyakazi hapo hawatufai kabisa.Kwanini bidhaa za mafuta zikiwemo petroli,dizeli,mafuta ya taa na gesi zisitozwe kodi kabisa?This is a vital Input into Production of goods and services.Na badala yake kodi itozwe katika hizo Final Goods and Services?Huu Uchumi wenzetu hapo Hazina mliusomea wapi?Wa kuvurga uchumi na kusababisha machafuko katika mfumo mzima wa uzalishaji mali!Matokeo yake,wawekezaji katika Viwanda wamezidi kutukimbia na kwenda nchi za jirani na baadaye kuziuza bidhaa hizohizo hapa kwetu Tanzania.Matokeo yake karibu kila bidhaa hapa nchini hivi sasa imepandishwa Bei na Bei zinapandishwa kila siku!Ukichanganya pamoja kushuka kwa shilingi dhidi ya Dola uchanganye na bei kubwa ya petroli na dizeli basi mfumuko wa bei siyo huu tunaoimbiwa kila siku na serikali(?),ni mkubwa zaidi!Hili linadhihirika jinsi kila siku noti ya shs.10,000/= inavyozidi kupoteza uwezo wa kununua kiasi cha bidhaa zilezile ulizoweza kununua jana sokoni au katika supamaketi!Sisi wote soko letu moja.Kwa hiyo katika hili hakuna wa kutudanganya.Jambo la kujiuliza hapa,inakuwaje serikali yetu iliyochaguliwa kidemokrasia na wapiga kura wenyewe ikisha ingia madarakani inapoteza kabisa mawasiliano na wale walioiweka madarakani hadi muda mfupi tu karibia ya uchaguzi ndipo kauli tamutamu zinapoanza kusikika?Hivi watanzania wataendelea kugeuzwa Mataahira hadi lini kwa visingizio vya Bei inapangwa na Nguvu za Soko(Price shall be determined by Supply and Demand)?.Hata pale inapodhihirika wazi kwamba kuna Mkono wa TATU(mkono wa Mafisadi) zaidi ya ile miwili ya supply na demand,na bado serikali ikabaki inachekelea tu kwa kejeli na dharau!Huku watu wakinyonywa Vipato vyao ambavyo ni duni tayari?Nakushukuru sana mdau wa USA.Nakuomba sana uwe unatupostia bei ya rejareja ya petroli ya huko USA kila siku,hilo litawafanya watu wetu hapa watambue ni jinsi gani wanavyoibiwa na wafanya biashara wa mafuta kwa baraka ya serikali yao wenyewe!Hii kama siyo Hujuma ni nini?Ipo haja ya kuwamulika na kuwachambua Maofisa wote walioko katika nafasi nyeti za maamuzi huko ngazi za juu.Usije kuta serikali imekaliwa na Mamluki wa kisiasa bila ya sisi wenyewe kujua!Lets not assume that everything will always be all right!

    ReplyDelete
  3. This is yet another another proof of how Dead the Tanzanian economy is right now after decades of economic mis-planning!Are Tanzanians sensitive to any price irritations?Or price hikes?If they are,if at all,you would expect a reaction to that!A serious drop in the consumption of the pricehiked item or outright riots!Is the Tanzanian Disposable Income sensitive to any price changes?I doubt.Utafikiri ndiyo kwanza tumepata Uhuru wetu Jana toka kwa Waingereza,kwa jinsi tunavyo yaendesha mambo yetu!Matatizo makubwa.Umuhimu wa kubadilisha Viongozi kila baada ya muda mfupi lazima utiliwe mkazo ili Taifa lisivie na kushupaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...