Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), moja ya benki zinazoongoza nchini imechaguliwa kuwa miongoni mwa benki 7 zitakazoshindania Tuzo za Benki Bora Afrika.

Tuzo za Benki Bora Afrika zinatoa heshima kwa juhudi za mageuzi ya kiutendaji, mifumo ya kisasa ya ufanisi na utendaji pamoja na ukuaji wa sekta ya kibenki barani Afrika. Tuzo hizi zinakusudia kusimika uwezo wa taasisi za kibenki zinazoongoza barani Afrika na watendaji wake ambao wanazidi kupanua uwezo wao katika sekta ya mabenki ulimwenguni.

Akizungumzia tukio hilo la kihistoria kwa benki hiyo na wadau wake, Mkurugenzi Mkuu wa NBC Christo de Vries alisema, “Haya ni mafanikio ya hali ya juu kwa NBC na utamaduni wetu wa ufanyaji kazi. Tuzo za Benki Bora Afrika zinawatunuku watendaji waliofanikiwa zaidi katika nyanja ya mabenki barani Afrika na kwetu sisi hii ni hatua kubwa katika njia tuliyoanza kuipitia tangu tulipoanza shughuli zetu hapa nchini.”

Tuzo za Benki Bora Afrika zinatambua mchango wa watu na taasisi za fedha zinazofanya juhudi za kuleta maendeleo barani Afrika na kusherehekea mafanikio ya mageuzi ya sekta hii nyeti. Tuzo zitatolewa kwa washindani waliochangia ufanisi mzuri katika sekta hiyo barani humu kwa mwaka 2007 katika makundi mbalimbali 17.

Uteuzi huu unaiweka NBC kwenye kundi moja na benki nyingine kubwa 6 Afrika nzima ambazo ni Attijariwafa Bank, Banco International de Mozambique, Intercontinental Bank, Oceanic Bank, Standard Bank na Zenith. Utaratibu wa kumchagua mshindi utafanyika mjini Washington DC, Marekani.

“Sote tunatambua kuwa kuchaguliwa huku kusingewezekana bila ya mchango mkubwa toka kwa jamii nzima ya NBC. Hatua hii imekuja wakati ambapo benki hii inapata changamoto tele toka kwa benki zingine mbalimbali na mazingira yanayobadilika kila wakati.
Itakubalika kuwa kuchaguliwa huku kutatoa msukumo mkubwa kwetu sote kama wafanyakazi na benki yetu kwa ujumla,” aliongeza de Vries, akigusia nafasi NBC iliyomo katika soko la mabenki nchini Tanzania ambapo benki hiyo imekuwa ikiendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...