
Mdau na Mpenzi wa Masnep
Stewart
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Asante sana Mdau.
ReplyDeleteHii picha nimefurahia sana, nimekuwa nikisafiri na Mhashamu Askofu Msaidizi Method kilaini Katika simulizi zake za historia ya kanisa katoliki (au uinjilishaji kwa ujumla) Duniani, Afrika , na sasa tuko Tz ,na alishatupeleka (kihistoria) mpaka Peramiho. Hii picha imenifanya niamini kwamba Kweli wa Benedictine walifanya kazi.
Asante sana.
Mdau Kiwoso
Asante sana Mdau.
ReplyDeleteHii picha nimefurahia sana, nimekuwa nikisafiri na Mhashamu Askofu Msaidizi Method kilaini Katika simulizi zake za historia ya kanisa katoliki (au uinjilishaji kwa ujumla) Duniani, Afrika , na sasa tuko Tz ,na alishatupeleka (kihistoria) mpaka Peramiho. Hii picha imenifanya niamini kwamba Kweli wa Benedictine walifanya kazi.
Asante sana.
Mdau Kiwoso
aiseeee si mchezo kitu balaa ile noma
ReplyDeletekuna kikwangua anga kingine wadau kipo itengule mwakujua???maeneo ya malangali iringa uwezi amini,,oldest jengoz adi leo zaishi,chekshia sasa majengo yetu ya mitaa kati dar yavoanguka wakati yaendelea na ujenzi,,
WIZI MTUPUUU
Daah naona hii ingeitwa peramiho twin tower tokea tunakuwa nasikia tu peramiho kumbe kumetulia itabidi siku moja niwe tourist ktk nchi yangu manake hata siijui mikoa kibao
ReplyDeleteAsante sana mdau kwa picha nzuri ya Peramiho yetu. kwa sisi tuliokulia maeneo ya jirani na hapo tunapafurahia sana na leo umenifanya nipakumbuke zaidi, ungetelemka na pale bondeni seminari kuu maarufu kama "major". Du kupitia picha hii nimemkumbuka Br. Polykarp GAMA (Polikalipi) wa kitengo cha uchapishaji bila kuwasahau marehemu Pd. Clemens na Michael OSB. Hapo palikuwa na bado pataendelea kuwa ni kimbilio la walio wengi wetu, maana hapo tunapata huduma za hospital (chini ya uongozi wa Br. Ansgar OSB na wasaidizi wake). Du, kuna mengi ya kuongelea kuhusu Peramiho lakini kwa leo naishia hapo.
ReplyDeleteMtoto wa Mngongoma kule Nakahuga.
mdau hapa ndo nyumbani, ni sehemu ya historia si tu ya kanisa bali hata kuwa kwamua watu katika ujinga, kwa vile ni sehemu ya kwanza kanda ya kusini kutoa kozi ya uwalimu na ufundi na hivi tunaweza kusema ni sehemu kati ya sehemu muhimu kusini mwa Tanzania.
ReplyDeleteDuh...mswahili bado anamuabudu mungu wa kizungu!!!
ReplyDeleteDu! Penye apa! bomba hii nyumba hii.
ReplyDeleteMdau Lizaboni.
hawa jamaa hawana lolote nasikia wezi sana hapo chini ya hiyo tower naambiwa kuna MADINI KIBAO sisi wajinga tunasali hapo juu yake na kuimba kwaya wenyewe wanadokoa kiulaini.Kwa hiyo kina tower hapo TZ tujaribu kuichunguza wao wanaona raha gani kujenga Africa? Kila kwenye kanisa (PAROKIA)KULIJENGWA STRATEGICALLY KUWAONYESHA WAJUKUU ZAO KUNA CHOCHOTE ENEO HILO HIVYO MNAKARISHA UWEKEZAJI WENZENU WANAJUA WAPI KWA KWENDA.
ReplyDeleteKalaga bao!
MWONILE BAMBO KAPINGA!!!!
Karibuni Sana Wadau Ndani ya mji wa Peramiho.Ni Mji ambao umejengeka una majengo mengi ya zamani ambayo yanavutia,Una vitu Vingi sana ambavyo vinavutia...karibia ujionee mwenyewe...
ReplyDeletePALI-PALI PENYEE PALI BWANA. UMEPATIA KABISA. HII NI ILI ILI TWIN TAWA YETU BWANA.
ReplyDeleteImenikumbusha tulipokuwa tukienda kununua mitumba, na kusafisha picha zetu (black and white), tukitokea Songea Boys' miaka ya 79-82.
Nawakumbuka rafiki zangu kina
Adoh,
Aaron,
Chacha Mwita,
Ussi,
Cuthbert,
Apolinary,
Marehemu Shilatu,
Na wengineo.
Nawatakia Christmas njema.
Siamini kuwa ni miaka karibu 30 sasa imepita tangu tulipokuwa Box 2.
Mdau,
London-Paris-Tokyo (ommi_r@hotmail.com)
Duuh!mdau amenikumbusha mbali sana.Nilibatizwa na kupokea komunio ya kwanza na kipaimara katika hili kanisa.Shukrani mdau
ReplyDeletenadhani na huu msamiati wa kikwangua anga itabidi pia nao tuambiwe maana hwenda mwengine akaleta kichuguu cha mchwa kilichoongoka nacho kikawa kikwangua anga!!!
ReplyDeleteWe mtoa maoni wa novemba 28, 10.26pm una uwezo mdogo sana wa kufikiri! Unapowashangaa waswahili ambao bado wanaabudu Mungu wa kizungu, jishangae kwanza wewe kwa kutumia mashine na teknolojia ya kizungu kutoa maoni yako. Suala la kuabudu Mungu wa Kiarabu, Kizungu, Kiafrika, nk ni uamuzi wa mtu binafsi. Uwe na heshima kwa uhuru na utashi wa wenzako!
ReplyDeleteHii picha imenikumbusha my 4 years spent at Peramiho Girls school in early 90's tulikua tunasali hapo kila siku asubuhi.
ReplyDeleteTukuoni bambo,
ReplyDeletemmmhh Bwana mimi hapo ndio kwetu hospitali hii ilikuwa na huduma bomba kuliko zote tanzania at 1990's. Kuna hoteli ilikuwa inaitwa kwa deo moka alikuwa anatengeneza mikate si mchezo na chai ya maziwa. Hawa jamaa wa peramiho ni mabingwa wa kutengeneza soseji na mikate hakuna tena tanzania. Ansagar alikuwa ni rafiki sana wa baba angu mkubwa alikuwa anagawa sana mitumba na vitu mbali mbali vya msaada. Bila kuisahau Trade school ambao ndio mabingwa wa kufundisha ushonaji wa suti Tanzania nzima. Wazee suti ya peramiho si mchezo
Tunashukuru sana kwa picha hiyo nzuri ya Minara Pacha ya Peramiho. Kwa yule aliyetoa maneno ya kashfa kuhusu majengo hayo tunamsamehe kwa kuwa hata hajui chochote. Wale wazungu wemetumia nguvu zao zote na hata wanafia peramiho na wanazikwa pale pale. Europe to them is nothing than proclaiming the good news to the poor.
ReplyDelete