JEETU Patel (pichani katikati) anayetajwa kuwa kinara wa ufisadi katika wizi wa Sh bilioni 133 kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) pamoja na wenzake tisa, jana walifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kuiibia benki hiyo.
Wengine waliofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam ni Devendra Vinodbhai Patel na Amit Nandy, Ketan Chohan, Johnson Lukaza, Bahati Mahenge, Davies Kamungu, Godfrey Mosha na Manase Mwakale anayeshitakiwa na mkewe, Eddah Mwakale, ambaye ndiye mwanamke pekee katika kesi hiyo ya kifisadi.
Jeetu, ambaye jina lake halisi ni Jayantkumar Chandubahi Patel, katika moja ya kesi anazokabiliwa nazo, anashitakiwa kwa pamoja na Devendra Vinodbhai Patel na Amit Nandy.
Kwenye shitaka hilo, washitakiwa wanatuhumiwa kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, kuiba na kujipatia Sh bilioni 2.6 kwa kutumia kampuni yao ya Bencon ya Dar es Salaam. Wanadaiwa waliiba fedha hizo baada ya kudanganya kuwa Kampuni ya Matsushita Electric Trading Company iliwapa jukumu la kulipwa fedha hizo kupitia kampuni yao ya Bencon International Ltd.
Washitakiwa hao pia kwa pamoja wanashitakiwa kula njama, kughushi, kuiba na kujipatia tena Sh bilioni 7.9 kwa kutumia kampuni hiyo ya Bencon International Ltd. Katika wizi huo, washitakiwa hao wanadaiwa kudanganya kuwa walipewa jukumu la kulipwa fedha hizo na Kampuni ya Maruben Corporation ya Japan wakati wanajua kuwa si kweli.
Hakimu Euphamia Mingi alisema dhamana kwa washitakiwa ziko wazi, ila kila mshitakiwa anatakiwa kuweka mahakamani nusu ya fedha anazodaiwa kuiba, wadhamini wawili na mmoja kati yao awe ndugu wa karibu na wote watasaini hati ya dhamana.

Washitakiwa hao pia wanatakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiria mahakamani, wanatakiwa wasisafiri nje ya mkoa hadi kwa ruhusa ya mahakama. Sharti jingine ni kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi wataripoti kwa mwendesha mashitaka na pale wanapokuwa na matatizo, wadhamini wao watalazimika kwenda kutoa taarifa mahakamani.
Jeetu pia anashitakiwa katika kesi nyingine na Ketan Chohan na Amit Nandy ambao wanadaiwa kuiba Sh bilioni 3.3 kwa kutumia Kampuni ya Navy Cut Tobacco Tanzania Limited. Walidanganya kuwa wameruhusiwa na Kampuni ya Matsushita Electric Trading Company ya Japan walipwe fedha hizo. Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Neema Chusi na uamuzi wa dhamana yao utatolewa leo.
Kinara huyo wa ufisadi, pia anashitakiwa kwa wizi wa Sh bilioni 3.9 ambazo aliiba kwa kutumia kampuni ya Bina Rosorts Ltd kwa kudanganya kuwa walipewa mamlaka ya kulipwa fedha hizo na Kampuni ya C. Itoh & Company Ltd ya Japan. Katika shitaka hilo anashitakiwa kwa pamoja na wenzake Devenra Vinodbhai Patel na Nandy na kesi hiyo iko mbele ya Hakimu Mkazi Richard Kabate. Katika shitaka jingine, Jeetu anashitakiwa kwa wizi wa Sh bilioni 4.9 kwa kushirikiana na Devenra na Nandy.
Wote wanatuhumiwa kufanya wizi huo kwa kutumia Kampuni ya Maltan Mining Company Ltd wakidanganya kuwa wameruhusiwa na Kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan walipwe fedha hizo na BoT.
Mtuhumiwa mwingine aliyefikishwa mahakamani jana ni Johnson Lukaza ambaye naye anatuhumiwa kula njama, kughushi, kuwasilisha hati ya uongo, kuiba na kujipatia Sh bilioni 6.3. Mtuhumiwa huyo na mwenzake aliyetajwa kwa jina la Mwesiga Lukaza ambaye hakuwapo mahakamani, wanadaiwa kufanya wizi huo Desemba 2005.
Dhamana kwa mshitakiwa iko wazi ila mshitakiwa anatakiwa kuweka mahakamani nusu ya fedha anazodaiwa kuiba na wadhamini wawili na mmoja kati yao awe ndugu wa karibu, wote watasaini hati ya dhamana. Mshitakiwa pia anatakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani, anatakiwa asisafiri nje ya mkoa hadi kwa ruhusa ya mahakama.
Sharti jingine ni kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ataripoti kwa mwendesha mashitaka na pale anapokuwa na matatizo wadhamini wao atalazimika kwenda kutoa taarifa mahakamani. Wengine waliopanda kizimbani ni Bahati Mahenge, Davies Kamungu, Godfrey Mosha na Manase Mwakale anayeshitakiwa na mkewe, Eddah ambaye ni mwanamke pekee katika kesi hiyo ya kifisadi.
Washitakiwa wanatuhumiwa kuiba Sh milioni 855.4 ambazo waliiba kwa kutumia Kampuni ya Changanyikeni Residential Complex Ltd baada ya kuwasilisha nyaraka za kughushi BoT wakionyesha kuwa kampuni hiyo, mkurugenzi wake Samson Mapunda ndiye aliyetoa idhini ya kulipwa fedha hizo.
Watu hao pia walishitakiwa kwa wizi wa Sh bilioni 1.2, mali ya BoT baada ya kutumia kampuni ya Changanyikeni Residential Complex Ltd wakidai wamepewa mamlaka ya kulipwa fedha hizo na kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan. Uamuzi wa dhamana yao utatolewa kesho na Hakimu Victoria Nongwa.
Akihutubia Taifa Ijumaa iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alisema Sh bilioni 69.3 ambazo ni sawa na asilimia 76.7 ya Sh bilioni 90.3 zilizochotwa kutoka EPA, zilikuwa zimerejeshwa kufikia Oktoba 31. Hata hivyo, aliagiza kuwa wote ambao kufikia siku hiyo, watakuwa hawajatekeleza agizo la kurejesha fedha hizo, hatua za kisheria zichukuliwe.
Alitoa maelekezo kamili kwa ambao hawakutimiza malipo, majalada yao yakabidhiwe kwa Mkurugenzi wa Mashitaka mara moja, kwa hatua zipasazo za kisheria. Kampuni 23 zinadaiwa kuchota fedha, Sh bilioni 133 katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya BoT, na iligundulika baada ya ukaguzi wa hesabu uliofanywa na Kampuni ya kigeni ya Ernst & Young katika mwaka 2005/2006 ambayo ilipewa kazi iliyoachwa na Deloitte & Touche ya Afrika Kusini.
kachelo koba kimanga 'assossa' (shoto) akimuelekeza jeethu patel pa kwenda wakati watuhumiwa wa EPA walipotinga mahakama ya kisutu sasa hivi kujibu tuhuma hizo
baadhi ya watuhumiwa wakiwa wamechuchumaa kusubiri kuingizwa mahakamani
baadhi ya watuhumiwa wa EPA wakisubiri kupanda kizimbani mchana huu katika mahakama ya hakimu mkazi wa kisutu, dar

Kwa habari kamili nenda:
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=13538
na
http://dailynews.habarileo.co.tz/home/?id=8254
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 57 mpaka sasa

 1. Keko na Segerea leo kutakuwa na pati. Vimwana wapya halafu wazuriii! Kudadeki wauaji, majambazi, vibaka, wamachinga na watemi wa ngomeni watawagombania kama mpira wa kona.

  "..Keko Swahili iko gombania k..du kama yake.."

  ReplyDelete
 2. Tunaomba usiwe mchezo wa kuigiza...sheria ifuate mkondo wake kwelikweli!!

  ReplyDelete
 3. Hawa jamaa mbona wanaonekana kama wanakondoo.

  ReplyDelete
 4. Jamani mnaowajua hawa watu waliokaa hapo mahakamani tusaidieni majina yao tafadhali,

  ReplyDelete
 5. JK na serikali yake wasanii sana, wamesubiri wakati kuna big news "obama's victory" ndio wameamua kuwakamata hawa 'watuhumiwa' wa EPA!

  Hili ni changa tu na namna janja ya JK ktk kusherehekea ushindi wa Obama

  ReplyDelete
 6. Muhidin,

  Blog haongopi. Nakuomba uirejeshe au uipandishe tena hiyo thread hapo chini na maoni yake. Ili wasomaji wengine wapate kuona ina nini.

  http://issamichuzi.blogspot.com/search?q=johnson+lukaza

  ReplyDelete
 7. I personally congratulate the EPA probe team, DPP & his Excellence Mr. President for this good job but my worry is that are these people get jailed? na mali zao kufilisiwa au tunaleteana sanaa tu kama picha ya kihindi steling anapiga watu huku anakula karanga enzi zile za Disco dansa Mituni Chaklaboth

  ReplyDelete
 8. Huyo Mwanamke mwanye kitenge ni nani? au na yeye ni mmoja wa watuhumiwa?

  Mlio bongo tupeni nyuzi.

  Mdau #2

  ReplyDelete
 9. aaaaahh wapi? mmmh mmmmh hapana

  ReplyDelete
 10. mbona hamna ffu na hawajapigwa tanganyika jeki kama wale wazee waloandamana kuomba wapewe hela zao za EAC walozitolea jasho?

  ReplyDelete
 11. mbona wana twaja wawili tu..wengine ni akina nani au bado siri?!!!!!

  ReplyDelete
 12. hadi huyo mwanamke alievaa kitenge jambazi?kweli siku za mwisho zimewadia! asalamaleko walahii!

  ReplyDelete
 13. Mr Issa ,tunashukru kuona watuhumiwa wa EPA wakikamatwa ,ila swali ni moja mbona Kikwete hajakamatwa?na viongozi wengine?au ni shinikizo la USA?JK na yeye ni mhusika mkuu katika

  ReplyDelete
 14. jamani eeeh hapa kuna danganya toto watanzania tunachezewa akili mjue hapa kuna watu ndio wezi na waliofanya sio mazurti lakini kwa tunaowafahamu ni binadamu na walipa kodi na trust me kuwekwa kwao jela ama kufilisiwa hakutatusaidia lolote kwani hata hizo mali zao hatutaziona zitahamia mikono mingine tuu. hiyo moja mbili kuna watu kibao hapa hawajaonekana wameshakula madili na serikali ndio tusahau hawa ni wale chambo ama sacrifice , kwani nyie mna habari hizo pesa asilimia kubwa ndio iliendesha uchaguzi wa mwaka 2005 (ingawa inadaiwa JK alikuwa hayajui haya so msimshutumu yeye alikuwa anajione tuu watu wanamsupporti na kumchangia mapesa kumbe ndio hivyo ) sasa wale vigogo wahusika wako wapi ? Mimi naona hawa wasifungwe adhabu yao waaambiwe kutoa asilimia 75% ya uzalishaji mali wao kwa miaka kumi ijayo kwenye VAT, na community services , walazimishwe kujenga mahospitali na mashule na wapewe targets. watujengee nchi kwani wakikaa huko lupango sisi tumelosti, nchi yetu imepoteza VAT zao, na wao juu wamepoteza maisha, haina faida ni wezi na sio wauaji so na tutake tusitake huo utajiri hawajaupata kupitia tuu hiyo pesa ya EPA ya mwaka 1996 labda kina bwana mdogo kama Lukaza lakini hao wazee wazima kina Jitu ni wafanyabiashara na wana mkono wa biashara miak kibao so bora tuwatumie hizo resourse kujiendeleza kuliko kuwamalizia lupango! anyway ni mawazo yangu tuu haya. Na hii listi itoke yooote sio watu kuchagua wa kuwakandamiza hapa wengine wamesharoooga mpaka wamekuwa invisible !!

  ReplyDelete
 15. Huyo demu naye anashukiwa kwa ufisadi? Duu! You can't judge a good book by its cover.

  ReplyDelete
 16. mbona inaonekana hawa kama sio.hii ni kafara bwana hata siamni.kuna mchezo mchafu hapo.

  ReplyDelete
 17. Asalaam aleykum? cha kushangaza hapo ni kuwa ni lini tuliona watu wanaiba na kusamehehewa wakirudisha hasa pesa ya serikali? huko kukaa tu na hiyo pesa kumesababisha raia wema wanaotegemea pesa hiyo kufa kwa kukosa dawa na mahitaji mengine. Pia sina imani na hao jamaa walioonekana ktk picha kama wezi cha kushangaza ni kuwa ni imani yangu kuwa wametumika kama kipoza roho wazungu wanasema (scapegot). Mimi nina imani rais na serikali kuna ukweli wanauficha hapo au kuna watu wanaogopewa je hao waliorudisha hizo pesa wamezipata wapi za kurudisha na kwa nini hao washindwe nafikili hapa kuna watu wanaogopewa na mkono wa sheria haujafanya kazi na kama kikwete atatetea hao watu ajue msalaba wake atakuja beba yeye mwenyewe maana history itatuhukumu na huwezi kufikili au kuhisi viongozi wote wajao watakumbatia fikra na sera zako wapo watakaotaka kukujaribu mahakamani vile vile maana ukimaliza muda wako unakuwa mtu wa kawaida na si rais tena. Tukiangalia watu wengi waliotoa maoni hawawajui hao jamaa hata kidogo? na kama kuna waliolipa kwa nini wasiwalipie wezi wenzao na kusahau ili kwa mtazamo wangu suala zima kwenda mahakamani ni kuwa halijaisha na kufanya raia/wazalendo wahoji zaidi. Sidhani kama kuna busara hapo kwani kama kuna waliolipa na wasiolipa wote ni wezi maana walipokea pesa na kujua zimetoka wapi! Jamani kama kuna yoyote mwenye kumbukumbu au mfano halisi ya watu kuliibia taifa lolote na kulipa pesa kusamehewa atuambie? maana naona giza hapo! na nia au dhamira ya kulipa na kusamehewa ipo wapi kama kuna waliolipa na kusahaulika na wengine wapo mahakani. Hapo kuna umuhim gani wa kuficha waliokula pesa za serikali cha kushangaza ni kuwa hizo Dirty Laundry zenu fulieni ktk mashine za serikali na sio kutumia mashine za public sasa nini maana ya kusema atakayelipa anasamehewa nafikili kuna makubwa yanakuja na ukweli utaanikwa hadharani muda si mrefu. Je washikaji mnaonaje hapo?
  Tizama wahindi walivyowajanja wamekubali kutolipa pesa ya nchi na kwenda jela wakitoka poa, au wanaweza hata wasifungwe je hao jamaa wana uchungu na nchi au ni kuchuma na kuondoka. Kwa kweli mimi sio mbaguzi wala nini lakini waarabu na wahindi wanakuwa wanaume Tanzania kuliko wazawa Je tutafika?

  ReplyDelete
 18. Mkuu wa nanihii ya Nanihii, salam zangu kwa mahakimu wa kei ya hawa wezi wa EPA nifikishie tafadhali tena kama posti usibanie.
  Wazo langu ni kwamba hapa hamna kesi ya kujibu mana wote tunajua ni wezi na isitoshe naona sio wote wapo hapa wengine wako wapi ? Sasa ni kwamba huku nchi zilizoendelea kuna Adhabu wanaiita "Community Service" yaani ni kuwadhalilisha watu warudishe mchango katika jamii , waitumikie jamii. Sasa hawa wezi wangepewa adhabu ya badala ya kuwapeleka jela miaka sijui thelathini , wakamalize maharage yetu huko , mahakama ingewaamuru wabaki uraiani lakini kwa kuitumikia jamii, na hivi wana mapesa yetu ya wizi basi baada ya kurudisha pesa na wapewe miaka si chini ya kumi waendelee na maisha yao kama kawa isipokuwa tuu serikali ihakikishe inaratibu vitabu vyao kwa huo muda na kiuwazi na kila wanachochuma basi asilimia 85% irudishe kuendeleza miradi ya jamii.

  ReplyDelete
 19. Mtashangaa kesi itavyokwisha,oooh hakuna ushahidi wakutosha, kwa maana hiyo watuumiwa hawana hatia. Ndio maana mpaka leo hii hatuna maji, hatuna umeme, hatuna elimu ya kutosha kwa kuwa watu kama hao hawachuliwi hatua zozote kisheria, huyo jaji wa hiyo kesi tayali amesha tajirika.Bush Queen.

  ReplyDelete
 20. anon 7:51 kuwa na soni mpuuzi wewe, JK akamatwe,na wakati yeye ndio kashinikiza watu warudishe mamilioni ya pesa! mi ningependa wewe ukamatwe,kwa kuropoka ropoka ovyo

  ReplyDelete
 21. This is great finally the EPA scandal is coming to an end but we all know, end of the day that all of these guys will never be jailed, they are probably spending their night at a 5 star hotel under police security. remember in Tanzania money and corruption is king

  ReplyDelete
 22. UONEVU MTUPU, MI NILIDHANI WA KWANZA KUFIKISHWA MAHAKAMANI WANGEKUWA BIG FISHES, SASA HAWA NI KINA NANI??? UKIWAANGALIA TU UNAONA HAKUNA HATA MWENYE MAMILIONI HAPO!!! UONEVU TU

  ReplyDelete
 23. Hii ndio picha halisi au ni tela tu..
  jumla ya pesa ambazo hao mafisadi kumi waliiba ni chache hazifikii bilioni 133 ambazo tunawadai..wapo wapi wengine>?? au ndizo ambazo uchunguzi bado unaendelea wa wale wa nje za inzi.

  ReplyDelete
 24. Mmmm uh!!! Mbona atuhumiwa wenyewe hata hawana wasi wasi. Mpiga box nimechoka na box la leo, ila hii habari imenitoa uchovu wote, mh!! Ipo namna. bado natafakari nipeni siku mbili tatu afu ntawapa jibu.Hataaa, hata kidogo!!!

  Mpiga Box

  ReplyDelete
 25. HAWA WAHINDI WALITUIBIA MDA MREFU NA HII KESI LAZIMA WA TZ TUIFUATILIE kwa karibu sana, wakitufanyia kiini macho/mahakama wakiwatema tuwasuburi mitaani tuwachome mote kama wezi wengine

  ReplyDelete
 26. LEO DUNIA NZIMA WATU WANASHEREKEA USHINDI WA OBAMA..{http://news.yahoo.com/s/ap/us_elections_world_view}
  NASI HATUNA BUDI KUUNGANA NAO KWA KUSHEREKEA KUPELEKWA KEKO WEZI WA EPA ..

  KWANI KWA WAMAREKANI NA DUNIA NZIMA NI USHINDI WA WATU AMBAO WAMENYONYWA KWA MUDA MREFU..

  KWETU tANZANIA...

  RAISI KASIKIA KILIO CHETU.

  ...WATU 10 WACHUKUE BILIONI133 WAKATI PESA HIZO ZINGETUMIKA KUZUIA VIFO VYA WATOTO,MAMA, BABA ZETU..

  TENA MIYE NADHANI HAO NI KUWANYONGA KAMA WAUAJI WA ALBINO..
  MNASEMAJE wana blogu ya jamii?????

  ReplyDelete
 27. Jamani mnakumbuka mlivyomtetea Johnson Lukaza kwenye hii post hapo chini?

  http://issamichuzi.blogspot.com/2006/09/nyu_20.html

  miaka miwili na zaidi iliopita tena hapahapa kwa michuzi, mlileta blah blah blah kuwa dogo ame win leo mnaona majibu yake.

  ReplyDelete
 28. Mbona Jamaa Wamechoka namna Hii?? Hivi Kweli Hawa Wanaweza Kua na Mabillions ya helaa?? Isije Jamaa wametolewa Kafara Tu Tutiwe Changa halafu Watu Wametulia..Mie Bado Hainipi

  ReplyDelete
 29. Cinema ya Kihindi hii.

  ReplyDelete
 30. Duh, dada yangu Eda Mwakale. Maskini, tulikuwa mbali sasa wanataka kutumaliza hivi hivi. Uwiiii! Lakini ni maji ya moto. Yatapoa au ku-evaporate tu. Vumilia siku hizi za mpito ndugu yangu

  ReplyDelete
 31. Mahakama yenyewe mbona kama imechokachoka hivi! Wakikamatwa ma-bouncer si wanaweza vunja vunja na kusababisha maafa?!

  ReplyDelete
 32. Kwa harakaharaka nilidhani ni wawekezaji wa TRL...

  ReplyDelete
 33. Tafadhalini ndugu zangutusiwahukumu kabla.Tusisahau usemi wa 'Innocent till proven guilty' Haki sawa kwa wote awe muhindi au mbantu
  Mdau, UK

  ReplyDelete
 34. Wadau mimi simuelewi huyu mnayemuita JK, hivi anatumia sheria gani kusema kuwa waliorudisha hawashitakiwi? Kwa hiyo kosa la hawa jamaa ni kushindwa kurudisha na siyo kuiba?!! Kama hivyo ndivyo mbona wezi wengine hawapewi hiyo nafasi ya kurudisha ili waepuke kifungo? Mimi nafikiri ametumia fursa hii kuwaokoa some of his friends who were in the scam.
  Sidhani kama anastahili pongezi yoyote!

  ReplyDelete
 35. HAPA HAKIELEWEKI KITU, SISI TUNATAKA CHIPS WEWE UNATUPA CHAMA! HATULI CHAMA HAYO NI MABUA YALIYOTIWA FLAVA YA CHPIS.

  ReplyDelete
 36. Unafikiri kipindi cha mwaka mzima hiyo ngija ngija ya makachero kila siku mlangoni watakuwa na afya gani tena, hela yote inakuwa chungu! Na huyo Jitu Patel mnamtetea nini na anajulikana kwa kupata hela za ujanja ujanja kila siku? Mimi kilichonifurahisha zaidi ni hayo masharti ya dhamana! Kwahiyo acheni wacheke tu hapo Mahakamani kama wana nusu ya hizo hela wazitoe wapewe dhamana!

  ReplyDelete
 37. Yaani hawa watu ndio waliokua wameiba mabillioni na wamerudisha billion sijui 19 au nakosea habari hizi

  Mbona hawa hata hawaonyeshi kuwa walikua wankula kuku kwenye mrija. Hizo hela waliiba kweli aua wanatumiwa kama scapegoat tu hao....sijui wahindi manake kupauka kwao ni jambo la kawaida hata ukiwa na hela lakini hao weusi basi wangependeza kidogo kama kweli waliiba mahela yote yale

  ReplyDelete
 38. HAWA JAMAA WANAONEKANA WAMECHOKA KWA SABABU WAMEANZA KUPATA PRESSURE TANGU UCHUNGUZI ULIPOANZA KWA SABABU WALISHAJIJUA HATMA YAO SI NZURI HIVYO WAKAWA HAWANA RAHA TENA ZAIDI YA TENSION.

  KWA HALI HIYO HALI ZAO ZIKAWA HIVI TUNAVYOWAONA LEO.

  HAYA NI MATOKEO YA KUKOSA USINGIZI KUTOKULA VIZURI UKIFIKIRIA WHAT WILL HAPPEN TO ME?

  HOPE I ANSWER THE QUESTIONS.

  ReplyDelete
 39. JAMANI EH...! HAPA NI CHANGA LA MACHO NA UNAFIKI WA VIONGOZI TULIONAO:
  JIULIZE WALIKUWA WAPI KUTOA MAJINA YA WEZI WOTE (WALIORUDISHA NA WASIORUDISHA) HADI MATOKEO YA MAREKANI? NINI HOFU YAO SASA? MABADILIKO EH..! KIKWETE HATA UKIFANYA NINI UMESHACHELEWA NA DHAMBI YA UBAGUZI, VISASI NA UONEVU ITAKUTAFUNA 2010 TENA UKILAZIMISHA UTAFANANA NA HAO ULIOWATAJA MAJINA YAO NA KUWAPANDISHA KIZIMBANI.
  SISI WANAJAMII TUNAWAFAHAMU MAFISADI WAKUBWA NA MASWAIBA WAKO WA KARIBU, UMEWABEBA KWA VILE WALIKUBEBA. KUMBUKA ULIMBEBA SANA MAREHEMU DITOPILE, AKAWA NA JEURI MPAKA AKAWA ANAPITISHIWA MILANGO YA MAJAJI, PAMOJA NA HAYO YOTE MWENYEZI MUNGU AKAKUONYA, HUKUJIULIZA AU HUKULIONA?
  SASA HAWA HAWA UNAOWATOA KAFARA ETI WALIKUWA KAMBI YA AKINA SUMAYI NA WENGINE, ACHA HIZO BWANA!! EBHOO...!!

  ReplyDelete
 40. Mandata A.K.A manjagu wamekomaa utfikiri wao siyo EPA. tena wao ndiyo wanaongoza kuwaEPA raia wema. Yaani wanatamani wawaweke rokapu.

  ReplyDelete
 41. Watanzania Zindukeni!Hil ni Changa La Macho!Kikwete hapa anajaribu kujifanya ameanza kujisafisha.Kumbukeni kauli yake ya mwanzo.Kwamba wale Wezi wastaarabu na wenye huruma ambao walifanikiwa kurejesha Fedha za EPA wao hawatapelekwa Mahakamani kwa sababu lengo la serikali yake lilikuwa ni kuzipata pesa zilizoibiwa lakini siyo wale walioziiba.Lakini kwa wale Wezi ambao wameshindwa kuzirejesha Fedha za EPA katika muda waliowekewa basi majalada yao yamefikishwa kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu ili waweze kufikishwa kizimbani na wakipatikana na hatia sheria ichukue mkondo wake!Sasa kwa mtazamo huo tu inatosha kabisa kuelewa nini kinacho kusudiwa kufanyika hapa.Huu ni Usanii mtupu wa kutaka kuwalaghai Wadanganyika ili wafikirie kwamba kweli Rais wao yuko pamoja nao.Makampuni yaliyohusika katika wizi huo hayapungui 22.Yapo yale ya DEEP GREEN FINANCE;KAGODA AGRICULTURE;MEREMETA GOLD;etc;ambayo yanahusisha VIGOGO ambao hapo hawaonekani na hawakuhusishwa katika mkumbo huo wa kupelekwa mahakamani!Hii ni DanganyaToto tu ndugu zangu.Usiri huu unatoka wapi katika uhalifu mkubwa wa kiwango hichi?Lets be serious.Hatutafuti Kichwa cha Mtu hapa bali Sheria itende Haki kwa wote na pasiwepo na mtu yeyote ambaye atakuwa juu ya Sheria HATA KWA RAIS MWENYEWE akibainika kwamba amehusika katika sakata hili!Hao wanao onekana hapo katika picha mahakamani ni DAGAA WATUPU HAO.MAPAPA BADO YAMEPEWA KINGA NA HIFADHI YA KISIASA!If Justice is to be done,then It must be seen to be done!Nobody is above the Constitutional Law!Kama wengine hawastahili kufikishwa mahakamani basi wote wasifikishwe mahakamani,waachiwe huru!Watanzania tumezoea kuibiwa na viongozi toka siku nyingi sanaaa!Lakini hatutaki Hadaa na kutugeuza sisi sote Mapunguani!Hapa kuna mawili yanayofanyika.Kwanza ni kuja kwa Rais Mteule wa Marekani Obama.Kuja kwake kutawapa wakati mgumu sana viongozi wengi wa kiafrika ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakivunja Katiba za nchi zao na kutawala kwa mabavu bila kuheshimu misingi ya Demokrasia.Sote tunwajua viongozi hao.Muda wao wa kuendelea kubakia madarakani katika Utawala wa Obama Marekani umekaribia ukingoni.Hapa Kikwete anajaribu kupeleka ujumbe kwa Obama kwamba ameanza kwa vitendo kukabiliana na Ufisadi hapa nchini hata atakapo jaliwa kwenda Marekani atakuwa na jibu tayari iwapo akiulizwa swali hilo!Pili,tukumbuke muda uliobakia kabla ya uchaguzi mkuu ujao ni mdogo sana chini ya miaka miwili.Watanzania wengi wamejawa na ghadhabu kuhusu Ufisadi huo ambao umekuwa ukifumbiwa macho na serikali ya Kikwete!Ili kurejesha matumaini tena kwa wapiga kura wake aweze kuchagulika tena katika uchaguzi ujao,vituko hivi vya kuanza kuwapeleka DAGAAA WA UFISADI MAHAKAMANI ili Watanzania waamini kwamba suala la EPA sasa limefikia ukingoni na Wahusika wote wako Kizimbani!Lakini ukweli sio huo.HILI NI CHANGALAMACHO!Why did the EPA issue have to take so long?Why the cover-ups?Who is telling the Truth?Do we still need to give our President Kikwete an extra Benefit of Doubt?How many Times should we do that?How much is the Price of Irresponsible Government Behaviour?Who should ultimately pay that PRICE?

  ReplyDelete
 42. jeetu patel (jitu patel) kavaa hirizi mkononi.Walokole vunjeni nguvu za giza jamaa asije akaruka na ungo kutoroka baada ya kupata dhamana.

  ReplyDelete
 43. Jamani wadau msianze kudakia tu ooh wamechoka, oooh mahakama imechoka, kwanza kabisa lazima ujue hapo ni africa, na pili hao watu believe me hawajachoka. Kwa msiowajua mtasema wachovu lakini mali walizonazo si mchezo. Nilipokuwa Tanzania nilibahatika kukutana na huyo Johnson Lukaza, kampuni yake ya Karnel iko pale regent, jamani si mchezo, yani ukiwa pale ndani ya kampuni huwezi jua kama uko bongo jinsi ilivyo bomba, na hapo mnamuona kachoka, kwanza quality ya picha sio nzuri, pili matajiri wengi kama hutaambiwa huyu ni tajiri huwezi mjua, kuna matajiri dar huwezi wajua mpaka uonyeshwe, so achani ushamba wa kusema wamechoka hao watu wanaishi maisha luxury sio kawaida. Johnson ana bonge la jumba pale masaki nyie bakini kusema wamechoka tu. Huyo Jeetu ndio litajiri kupita wote hao. Yani ukitaka kujua hao watu wanishije dar, utatamani uache kubeba maboksi uwaulize wamatajirikaje ili na wewe uwe na maisha kama yao na magari wanayoendesha wao na wake zao. Wacheni bwana

  ReplyDelete
 44. Jamani someni hi comment hapa chini, huyu jamaa alitoa maoni kuhusu Johnson Lukasa mwaka 2006


  http://issamichuzi.blogspot.com/2006/09/nyu_20.html


  Kumbe kuna watu waliona hii soo mapema na waka ishubiri tuu na huyu jama alitoa hii commnet mwaka 2006
  "[b]Tarehe September 21, 2006 2:07 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Wezi wa mabenk nao mnawaita wana Feza? Mpeni muda huyo millioner wenu kwani za mwizi ni arobaini ndo mtaelewa namaanisha nini "wezi wa fedha za bank". Siri yake tunaijua na wameshamshtukia bado kumtia kizimbani kama wale wenzake japokuwa yeye wizi wake ni wa kimataifa na bongo ndo kaanza kuufanya yeye na wajanja wachache. mabank kaeni chonjo mtu huyu hatari.[/b]"

  Huyu jama alikua amesha jua nini kitawatokea na wao nadhani pia walisha jua kuna kasheshe inakuja na labda walijiandaa.

  ReplyDelete
 45. We anon wa November 06, 2008 11:26 AM, wewe ni nyang'au kabisa,
  huna hata chembe moja ya uchungu wa nchi yako. Unatufundisha na sisi tuwe mafisadi??? hiyo sio system ya dunia ya leo ku-win. Angalia Marekani matajiri wameanguka vibaya na chama chao kinachowakumbatia Republican.
  Huu ni wakati wa uzalendo. Walalahoi wawezeshwe na serikali zao. Obama si ndio Rais wa Marekani sasa (aka Dunia) subiri uone, watalia mafisadi. Kwa taarifa yako balozi za Uingereza na Marekani kupitia FBI, CIA na vyanzo vyake vingi vya upepelelezi wanayo list ya mafisadi wote. hata kama serikali ikitudangaya. Marekani au Uingereza mafisadi, watoto, na ndugu zaohawaingiii ngoooooooooooo.
  Pumbavu zaoooooooooo.

  ReplyDelete
 46. Kama tunasubiri hayo mapapa ndiyo yaonekane hapo we might die of old age waiting, mkumbuke wapo wale ambao makampuni waliyotumia kuchukulia pesa hayana majina yao binafsi, kwa hiyo kuwadaka moja kwa moja nina imani kuna ugumu wake. Kumbukeni kuna kampuni moja wapo ambapo address yake ilipofuatiliwa maeneo ya nyerere rd, haikuonekana in short hai-exist! Inawezekana kabisa wapo wliokamatwa ambao 'kosa' kubwa walilolifanya ni kujitolea kuji-register kama wao ndio wakurugenzi wa hizo kampuni, wakaishia kupewa 5% kama kamishen (10% watambe?).

  Tuendelee kuwasikilizia hao akina Mwanyika kama wana jipya kwa huo uchunguzi wanaoendelea nao! Huchelewi kukuta uchunguzi miaka mingine mitano.

  ReplyDelete
 47. Halo kaka Michu!
  Tunashukuru kwa taharifa za watuhumiwa/washukiwa, sasa tunaomba kama ingewezekana mdau yeyote atupatiye majina kutokana na picha ili tujue Jitu patel ni nani, na nani ni nani
  Msaada kwenye tuta kaka

  ReplyDelete
 48. Unayesema makampuni yalikuwa hewa hawapati mtu akina Mwanyika hujui ulisemalo.

  Akaunti za mabenki ya hayo makampuni unadhani nazo zilikuwa hewa? Kuna watu wenye picha zao waliofungua.

  Na unadhani mikataba ya kusaini kwenye makaratasi ili wakwapue hela benki kuu zilisainiwa na majini? Walisaini watu kwa mikono yao na mbele ya mawakili na sio majini.

  Kuwajua ni kazi kuwa ndio wahusika wa hayo makampuni ni rahisi mno ningekueleza zaidi lakini niachie hapo usije ukawa unahaha kutafuta namna ya kujitetea mahakamani nisikupe faida bure.

  ReplyDelete
 49. Johnson Lukaza has owned the following to mention a few
  Mu-teck (T)Ltd supplie of computers equipment etc
  Proin Limited dealing in Real estate, which has several apartments in UAE
  Johnson Equipment hire,
  KERNEL Limited,
  etc etc
  Shida ninini wabongo wengi walianza kuwa wasanii enzi hizo kumbe ni ufisadi tu.
  Ukimwangalia kortini anasmaili tu!!
  TANZANIA Kaa chonjo hao watu wenye majumba na magari ya kushangaza waangalie mara mbili!
  Mbaya zaidi wote ni ma-sponsa wa CCM, anagalia kwenye maharambee wanavyomwaga mapesa na kukumbatiwa na Pres JK, wengine wanaandama nae kwa miamvuli ya ufanyabiashara katika tripu zake zisizoisha ughaibuni.
  THIS CRAP IS STINKING LIKE HELL!!!
  TANZANIA SHOULD WAKE UP NOW THAN LATER

  ReplyDelete
 50. EEE mola angalia hili,,,
  aisee yan haiingii akilini kabisa awa ndo wameiba izo billions,yan kuna list ya wazito kibao nyuma yao.wee ngoja yoote aya yana mwisho tuu mali ya dhurma itawatokea puani na familia zao milele,,yan nchi haina ARVs simply no funds to supply uku wengine wala mipesa iyo afu wanatuletea izi mtu apo???WATU HAWAOGOPI JEHANAMU

  ReplyDelete
 51. MBONA MAWAZIRI HAWAMO?

  ReplyDelete
 52. Anon wa 12:58 wewe ni pweka, nimejaribu kusoma comments zote na sioni sababu ya kumtukana huyo wa 11:26 kwani anajaribu kusema watu wasidhani kuwa jamaa wamechoka, kwani kuna watu wanadhania wamesingiziwa huko juu, rudi juu usome comments kabla ya kutukana watu, pumbavu kabisa

  ReplyDelete
 53. Hii, haina maana. watumuhiwa hawana pingu kabisa mikononi, wamechuchumaa tu bila pingu. Hii maanake ni kwamba wakubwa huwa wanasindikizwa mahakamani bila pingu ila mwizi wa kuku ndio huwekwa pingu.
  najua ndani mahakamani hawatakiwi kuwa na pingu, ila nje ya chumba cha mahakama muda wote wanatakiwa kuwa na pingu.
  Pia mwanamama mshtakiwa alitakiwa kuwa na askari wa kike pembeni yake.
  hili la dhamana nalo naona ni ujinga tu, kwani watakuwa nje na kutakuwa hakuna ushahidi wa kuwafunga.
  Hii kesi itaamishwa mahakama kuu, maana hiyo mhakama ya kisutu haina sauti juu ya kesi za namna hiyo.
  Kesho utasikia hao wanaishtaki serikali na kupewa fedha kibao.

  ReplyDelete
 54. Huyo Giantkumar Patel si yumo na kwenye dili la rada?

  ReplyDelete
 55. Hee wallah anon wa 4:18 ushaniona na mie fisadi....mie nimetoa mtazamo wangu wala usinitafutie namna ya kujitetea kesini, uchungu nilio nao kama wako....labda nikukumbushe kitu kimoja kuwa hao waliochukua pesa wanajulikana na hata kamati ya mwanyika inawafahamu fika (hasa huyo big fish ambae watu wengi tungependa kuona anaadhibiwa kwa hilo), na ameshiriki kwenye shughuli nyingi 'chafu' ambazo karibu kila mtu anazijua. Pesa zilipitia benki yetu wenyewe (kumbuka details za ufunguaji benki source yake ni documents from the registrar, so garbage in garbage out!), labda unisaidie tu kama huyo mheshimiwa alisimama kwenye foleni kudraw hizo pesa.....ningependa sana kukupa mfano wa bwana mmoja akipita mbele yako utamuona sijui muungwana wa wapi maskini, chini na makubazi yake sura kaiinamisha chini.....lakini kuna vijikampuni fulani ambavyo yeye anaonekana kama ni mkurugenzi kwenye makabrasha, tafuta sasa nani ni mmiliki halali....utashika kichwa..

  Mungu ibariki TZ..

  ReplyDelete
 56. KAKA MICHUZI WATU TULISHUHUDIA RANGE ROVER NEW MODEL ZINASHUSHWA AIRPORT KUTOKEA UK,MBILI KWA MPIGOOO!IMAGINE KUZIPAKIZAA TUU ZILIGARIMU PESA NGAPIII!YANI MBRITISH MWENYEWE ALISHANGAA KUWA HIZO GARI ZIMENUNULIWA NA KIJANA MTANZANIAA NA KWA JEURII ZIMEPAKIZWA NDANI YA BRITISH AIRWAY CARGO!WE ARE TALKING ABOUT POUNDS,NOT DOLLAS AU SHILLINGS,WATUU WAMEKULA BINGOO!WANASHAANGAA WATANZANIAA WANALIA NJAAA,LAKINI HAOHAO WATANZANIAA WANAPAKIZA MA-RANGE KWENYE NDEGE WAKATI HAKUNA MBRITISH ALIYEWAHI KUFANYA UJINGAA HUOO HATA SIKU MOJAA!!!!!

  ReplyDelete
 57. Hata siwezi kukubali ili changa.Yani kama sio picha jipya la james bond basi litakuwa picha la kihindi,akianani tena!

  Potz.

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...