Mgeni Mh. Balozi Elly E. Mtango akitoa nasaha zake wakati wa hafla hiyo
Hellow Mr Michuzi ,
Hivi majuzi tulikuwa na sherehe ndogo ya kuitangaza Tanzania katika jiji letu la Osaka , shughuli hii iliandaliwa na Ubalozi wetu mdogo wa hapa Osaka kwa mara ya sita mfululizo . Mgeni rasmi alikuwa Mh. E .E.E Mtango ambaye alikaribishwa na President Konoike of Konoike Construction Company kutoa nasaha chache.

Wageni mbali mbali walikuwepo , Mabalozi waliowahi kufanya kazi Africa , wawakilishi toka Osaka City council , viongozi wa Kyocera Comp. , wawekezaji ,wafanyabiashara mbali mbali na fans of Tanzania walikuwepo pia.
Shughuli hii ilifana sana kwa kutumbuizwa na kikundi cha ngoma toka Osaka University na vyakula vya kitanzania kutoka kule nyumbani.

Mengi mazuri yalisemwa , Kyocera waliweza kutoa ahadi ya Solar Panel System 5 kwa ajili ya shule za sekondari , baadhi ya NGOs waliahidi kujenga madarasa ya shule huko nyumbani.
Mark Mrutu
Osaka , Japan
Rais Konoike wa Konoike Construction Company akihtubia
vijana wa kijepu waliowahi kufanya kazi bongo wakitumbuiza kwa nyimbo za kiasili za kibongo

mkwaju ngoma ukirindima

wageni wakitosti kwa furaha

Mh. Balozi Elly Mtango akiwa na wadau







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hongereni wadau wa Japan. Mdau Mark Mrutu naifagilia sana kazi yako. Kazeni buti ili kusaidia nchi yetu

    Ni mimi yearmate wako wa Mzumbe (1996- 1998)

    ReplyDelete
  2. Nice move Mark Mrutu and the rest! Kudoz to ya'll! Na wengine tuige mfano huu sio kazi kukalia kunywa mapombe tu!!!!!! We need to change our views of life. I wish you all luck in the coming new year 2009. May God lead each and every one of you towards your new resolutions!
    Peace be with you!

    ReplyDelete
  3. haya wapelekeeni wajanja ridhki yao hio kisha tuzugwe wamepandishana vizimbani wako nje kwa dhamana hadi baada ya uchaguzi ujao 2010 ndipo kesi yao itatajwa tena

    ReplyDelete
  4. Haya nyie lalani usingizi tu, mwenu Juma Pinto wa London alinza kama nyie, sasa mwenzenu yuko mbali kwakazi hiyo ya kuitangaza tanzania.Nadhani mtakubalika tu ongereni sana

    ReplyDelete
  5. Wizi wa kutisha wagundulika NDC

    2008-12-29 13:31:15
    Na Mwandishi Wetu


    Ufisadi mkubwa umetokea katika benki ya Barclays London ambapo dola za Kimarekani milioni 1.5 zilizokuwa zitumike kwa ajili ya upembuzi wa miradi ya makaa ya mawe Mchuchuma na chuma Liganga, hazijulikani matumizi yake.

    Kufuatia hali hiyo, Serikali imeliagiza Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), kuchunguza jinsi amana ya kiasi hicho cha fedha ambazo ni karibu sawa na Shilingi bilioni mbili zilizowekwa katika benki ya Barclays London, Uingereza zilivyotumika.

    Ufisadi mwingine, uligundulika mapema mwaka huu, baada ya uchunguzi wa kampuni ya Ernst & Young kugundua kuwa zaidi ya Sh. bilioni 133 za Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zimechotwa na makampuni kadhaa kwa matumizi binafsi.

    Baadhi ya watuhumiwa hao wa EPA tayari wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

    Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na menejimenti ya NDC jijini Dar es Salaam jana, maagizo hayo yanafuatia taarifa za ukaguzi wa ndani ya NDC.

    Taarifa hiyo inaonyesha kuwa mnamo mwaka 2000, Shirika lilipata mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 1.5 kutoka Benki ya Barclays na kuziweka katika tawi la London, Uingereza.

    ``Fedha hiyo ilikuwa itumike kwa ajili ya upembuzi wa Miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma na chuma Liganga,`` ilisema taarifa hiyo.

    Menejimenti hiyo ilisema nyaraka ambazo shirika limezipata zimebainisha kuwa fedha hiyo ilitumika mwaka 2002 kudhamini mkopo uliotolewa na Benki ya Investec Mauritius kwa kampuni moja ya Singapore iitwayo Uhuru Capital Management PTE Ltd.

    ``Kwa vile Bodi ya Shirika haijawahi kuruhusu dhamana hiyo, Serikali imeona ipo haja ya kuchunguza kwa kina matumizi ya fedha hiyo na iwapo umetokea uvunjaji wowote wa sheria, hatua mwafaka zichukuliwe haraka kwa watakaobainika kuhusika,`` ilisema.

    Ilianisha kuwa uchunguzi huo unalenga katika kubaini walioidhinisha kutolewa kwa dhamana hiyo, kubaini wamiliki wa kampuni iliyodhaminiwa, kubaini uhusiano wa kampuni iliyodhaminiwa na NDC na kwamba uchunguzi utakapokamilika utawezesha mamlaka husika kuamua hatua zifaazo kuchukuliwa.

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  6. Ongereni kwa kuitangaza nchi yetu Tanzania, lkn hizo picha zinaonyesha wajapan wakicheza ngoma, je walikuwa walikcheza ngoma za asili ya kwetu au za kijapan? Kama ni za kijapan basi bado hatujafanya kitu

    ReplyDelete
  7. Anony wa Dec 30 2:45pm, soma caption zilizopo chini ya picha vizuri, mbona vitu vinajieleza. Au wapenda kuuliza tu ?!

    ReplyDelete
  8. hongera sana kwa kutangaa nchi yetu lakini mie naonba kutoa ushauri kidogo, naomba ndugu zetu wajitangaze kisayansi kidogo. mfano mzuri ni majirani zetu tu, ambao wao hutumia mpaka power point kuitangaza nchi yao na matokeo ni unaona kuwa hupata wateja wengi zaidi. ni hilo tu, naomba vijana hawa wajifunze mbinu mpya kidogo.

    ReplyDelete
  9. hongera sana Mark Mrutu, kazi nzuri sana, na sisi wadau wa China tutafata mfano wenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...