WATUKUFU WADAU WA GLOBU HII YA JAMII,
ASALAAM ALEIKHUM!
BWANA APEWE SIFA!
SHALOM!
WAAMA BAADA YA SALAMU, NAOMBA KWA IDHINI YENU, NA KWA KUWEKA TASWIRA HIYO YA DELTA YA MTO RUVU, NITOE SALAMU ZA UPENDO ZA HERI YA MWAKA MPYA KWENU NYIE WADAU WOTE POPOTE PALE MLIPO.
SEKUNDE, DAKIKA, SAA, SIKU, MAJUMA NA MIEZI IMEKATIKA KAMA MCHEZO VILE NA LEO TUNAUAGA 2008 NA TUKIJAALIWA MUDA MFUPI UJAO TUTAUANZA MWAKA 2009. NAWATAKIA MAISHA MEMA NA UTEKELEZAJI KWA VITENDO YALE YOTE AMBAYO WADAU MTANUIA KUYAFANYA MWAKA MPYA UJAO. KUMBUKA, YALIYOPITA SI NDWELE NA KUTELEZA SI KUANGUKA.
NI MENGI YAMEPITA, IKIWA NI YA FURAHA, HUZUNI NA KUCHEKESHA, BILA KUSAHAU UOSHAJI WA VINYWA, YOTE IKIWA NI KATIKA KUENDELEZA LIBENEKE LA GLOBU HII YA JAMII.
KAMA ALIVYO BINADAMU YEYOTE HAKUNA ALIYE KAMILI. KUNA WADAU AMBAO HAWAKURIDHIKA KWA HUDUMA ILIYOTOLEWA NA GLOBU YA JAMII, NA KUNA WALIORIDHIKA NA KUNA WALE AMBAO HAWAJALI, BORA SIKU IMEPITA NA AMEPATA JIPYA LA SIKU HIYO. NAMI DAIMA NAAMINI ULE USEMI WA 'KILICHO KIZURI KWA KUKU, NI KIBAYA KWA BATA MZINGA', HIVYO SIWEZI KUJIPA MOYO KWAMNA NINA UWEZO WA KURIDHISHA KILA MMOJA WA WADAU.
HIVYO NAOMBA RADHI PALE NILIPOTELEZA NA KWA UNYENYEKEVU MKUBWA WOTE NAWASHUKURU KWA USHIRIKIANO MKUBWA MLIOUONESHA NA AMBAO BADO MNAENDELEA KUONESHA.
NI HIVI MAJUZI TU GLOBU YA JAMII ILISHUHUDIA MDAU WA MILIONI 5 NA LEO TUNAKARIBIA HESABU YA MDAU WA MILIONI 5 NA ALFU 50, IKIONESHA NI JINSI GANI USHIRIKIANO HUO ULIVYO IMARA. NAWASHUKURU SANA KWA KUENDELEA KUTEMBELEA GLOBU HII PAMOJA NA KUCHANGIA.
MIAKA INAVYOKWENDA MBIO NI VIGUMU KUKUBALI KWAMBA SASA YAPATA MWAKA WA NNE NA USHEE TOKA GLOBU YA JAMII IZALIWE KULE HELSINKI, FINLAND, SIKU YA SEPTEMBA 8, 2005. ILIANZA KAMA GLOBU YA KUWEKA HEWANI KASHIKASHI ZANGU BINAFI LAKINI KADRI SIKU ZILIVYOZIDI KWENDA GEMU LIKAGEUKA, GLOBU IKAWA SIO YANGU TENA BALI NI YA JAMII NZIMA, NAMI NIMEBAKI TU KAMA MTUMISHI WA WADAU POPOTE DUNIANI, JUKUMU AMBALO NALITEKELEZA KWA FURAHA NA FAHARI.
NA WAKATI TUKIUAGA 2008 NA KUUKARIBISHA 2009 NAWEKA NADHIRI YA KUENDELEZA LIBENEKE KWA KADRI MOLA ATAVYONIJAALIA, HUKU NIKIENDELEA KUWEKA MASLHAI YA WADU MBELE KWA KILA JAMBO.
HERI NA FANAKA YA MWAKA MPYA WADAU WOTE!
-MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Asante sana kwa salamu za kumaliza mwaka 2008 na kuanza mwaka 2009!

    Mambo mawili:

    Umeandika, "TASWIRA HIYO YA DELTA YA MTO RUVU."

    Hiyo si delta; utakumbuka tuliwahi kuizungumzia hapa bloguni kwamba ni "ox-bow lake" lilio mithili ya "horse shoe."

    Pili, ili kurahisisha usomaji, ni vizuri sana kama baadhi yetu tutaachana na kuandika kwa kutumia herufi kubwa!

    Tuuanze kwa upendo na "productive contributions"!

    ReplyDelete
  2. Kunradhini, zaidi, niongezee la tatu, umeandika, "NI HIVI MAJUZI TU GLOBU YA JAMII ILISHUHUDIA MDAU WA MILIONI 5 NA LEO TUNAKARIBIA HESABU YA MDAU WA MILIONI 5 NA ALFU 50, IKIONESHA NI JINSI GANI USHIRIKIANO HUO ULIVYO IMARA."

    Idadi hiyo inaonesha tu ni mara ngapi ukurasa wako umefunguliwa; sio idadi ya watu!

    ReplyDelete
  3. Mh Balozi na Mkuu wa Wilaya ya Nanihii....nami nakupongeza sana kwa kuwa na blog ya jamii iliyosimama.Naamini 2009 Fulanaz zimeshaongezeka, Bwawa la Maini ndio hilo linagawa dozi, si nyumbani si ugenini, breaking news tunazikubali.Binafsi nakuombea kwa Mola akupe nguvu zaidi ya kuendeleza libeneke kaka Michuzi.

    HERI YA MWAKA MPYA 2009
    MAKULILO Jr,

    ReplyDelete
  4. Mh Balozi na Mkuu wa Wilaya ya Nanihii....nami nakupongeza sana kwa kuwa na blog ya jamii iliyosimama.Naamini 2009 Fulanaz zimeshaongezeka, Bwawa la Maini ndio hilo linagawa dozi, si nyumbani si ugenini, breaking news tunazikubali.Binafsi nakuombea kwa Mola akupe nguvu zaidi ya kuendeleza libeneke kaka Michuzi.

    HERI YA MWAKA MPYA 2009
    MAKULILO Jr,

    ReplyDelete
  5. thats very good mr michuzi,mwaka umeisha salama kabisa.

    ReplyDelete
  6. Mzee Misupu aka Mdau # one!! Kwa heshima zoote Na mimi ningependa kukutakia kila lenye kheri kwenye mwaka 2009!! Naona nyie mmesha uona Mwaka Mpya huko... sisi bado masaa kama sita hivi!! Mungu aendeleeze kipaji chako mzee...

    Ni mimi Mdau ulie Mpiga Makange pale BreakPoint July....nitakupigia!

    ReplyDelete
  7. Ee bwana kaka Michuzi au balozi michuzi. Heri ya mwaka mpya nawe pia. Tunakushukuru kwakuweza kutuunganishia haya mawasiliano ya kujengana japokuwa penye pazuri apakosi pabaya hiyo nia hali ya kawaida, Ila Brother michuzi wewe ni NO 1. There is no body to stop you, Katika kuwaunganisha watanzania kwenye kutoa maoni, na hasa katika kuitumia hii lugha yetu ya kiswahili kwenye kutoa maoni inapendeza sana. MUNGU AKUBARIKI WEWE NA FAMILIA YAKO, Mwaka mpya Mwema!!!! Mdau kutoka canada!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. DELTA NI MTO UNAPOINGIA BAHARINI, HIYO NI MEANDERING. JUST AS SIMPLE AS FORM ONE GEOGRAPHY. MTO UNAPOPINDAPINDA HIVYO NI MEANDERING, NA HIYO HUTOKANA NA UGUMU WA ARIDHI, MAJI UFUATA SEHEMU NYORORO KUBOMOA NJIA YAKE. MTU AKIKUAMBIA RUFIJI DELTA ANAMAANISHA PALE MTO RUFIJI UNAPOINGIA BAHARINI

    ReplyDelete
  9. Happy New year to you too. Thanks for all that you do everyday.

    This New Year, may your right hand always be stretched out in friendship, never in want.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  10. kila la kheri na afya njema michu.

    tupo pamoja tutafika tu

    ReplyDelete
  11. dah, huyo kaka anonymous wa kwanza kabisa anajua jiografia, utafikiri kazaliwa huko huko jiografia.....................

    ....sifa za kijinga!!!!!!!!!.........

    ReplyDelete
  12. NEW YEAR...NEW VISION. TOGETHER AS ONE.
    Happy and prosperous 2009 to you all.

    Mdau Cardiff

    ReplyDelete
  13. happy new year kaka michuzi na wadau wote.

    ReplyDelete
  14. Na wewe pia Sir Michuzi.2008 ulikuwa mwaka mzuri kwa serikali ya Kikwete.Keep it up JK

    ReplyDelete
  15. tetetetete mdau number 1 na 2 umeanza mwaka vibaya nini?

    hasira za nini hivyo? Ikiwa ni umefunguliwa mara million 5 au ni watu tofauti wamefungua mara million 5 lakini ukumbuke amehit number 5 that is a big accomplishment no matter how you view it...the way you judge it is up to you....HNY

    Happy new year our beloved brother. usikate tamaa kutupa story na mapicha ya bongo wanaotaka kuelimika waambie warudi darasani hapa twafarijika wengine siye tuko mbali na nyumbani...Kama ni delta au ox bow lake who care.....

    ReplyDelete
  16. NAKUTAKIA KILA LA KHERI NA BLOG HII IENDELEE INAFURAHISHA SANA KWA HABARI ZA NYUMBANI MOTOMOTO,MIMI MDAU WA KAMPALA MWANA WA TZ NAIPENDA NA SITASAHAU MJADALA WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI KWA KWELI NILIFALIJIKA SANA NA MAONI YA WANATANZANIA,WENGI WAO HAWAUPENDI NA JANA TUMEONA WAGANDA NAO WAKISEMA SUALA LA ARDHI KILA MOJA ASIINGILIWE KWELI HATUTAKIWI KUPAPATIKIA HILI SHIRIKISHO TUNAHITAJI MUDA NAWATAKIA KILA LA HERI WACHANGIAJI WOTE NA BLOG IENDELEE KUELIMISHA JAMII MICHIZI KILA LA KHERI KAZA BOOT....."YOU WILL NOT WALK ALONE".....................ISMA KABENGO-KAMPALA

    ReplyDelete
  17. Kaka Michuzi!
    HERI YA MWAKA MPYA
    Natambua kuwa wewe huwa haukasiriki unapokosolewa na mimi naomba nianze mwaka huu kwa kukukosoa na kama hutabandika post yangu hii basi najua ujumbe utakuwa umeupata kama ulivyoupata ule wa Liverpool(email)

    Binafsi sikufurahishwa na kitendo chako cha kutuita ''WATUKUFU'' kwa kweli neno TUKUFU limebeba maana kubwa sana ambayo kwangu mimi naona si sahihi kuitumia kwa kutuita watukufu, Kumbuka hata Raisi wa awamu ya tatu mh Benjamin W. Mkapa alipoingia madarakani akakataa kuendelea kutumia neno MTUKUFU yaani MTUKUFU RAISI, kwa maoni yangu naomba ubadilishe na ni vyema ukawa muungwana kwa kufanya hivyo maana utakuwa umewafanyia kitu muhimu sana wadau wako wote walikwazika na matumizi ya hilo neno.
    Asante na nakutakia libeneke jema

    ReplyDelete
  18. Wewe, ewe wa tarehe January 01, 2009 9:23 AM, tunataka kuanza mwaka Mpya na some sense of serioussness! Tuwe focused! Tusichukue majambo na kuyakumbatia hivi hivi tu!

    Ama sio?

    Uongo, uongo wa danganya, danganya toto tuutupilie mbali! Hauna nafasi miongoni mwa watu wengine!

    Ila kwa mambo ya ads, unaleta fedha!

    Wewe kaukumbatie ana kuubusu, in the name of Mwaka Mpya!


    a

    ReplyDelete
  19. Michuzi na wewe bwana Speech ndeeeeeefu kwani wewe umekuwa JK? Wewe tutakiane tuu hiyo HAPPY NEW YEAR na tuombeane afya njema ya
    Kuendeleza libeneke. Sawa basi
    We love you tooooooooooooo ! Mdau Ukerewe

    ReplyDelete
  20. Wewe mdau wa 2:27am kama mtu huna mkono wa kulia itakuwaje?

    ReplyDelete
  21. It is probably the best photo of 2008.
    Kwanza samahani najua hii ni blog yako na unaweka chochote unachotaka.

    Naomba uwe unaweka picha kama hizi na za maendeleo kwa wingi na upunguze picha zako wewe na watu wanaokutembelea kwa mwaka 2009.

    ReplyDelete
  22. Asante Michu na heri ya mwaka mpya to you too. Asante sana kwa kazi nzuri ya kutuunganisha especially kwa sisi tuliokuwa mbali na nchi, tunapata habari zote za nyumbani.

    Ombi langu kwa mwaka huu, ingawa najua kuwa wewe ni mshikaji wa JK naomba usibinye sana comments zinazohusiana na mafisadi. Jaribu kubalance as much huku unajaribu kutetea kazi yako. Hii nchi ni watu kama wewe tunaowategemea kuleta mabadiliko. Tafadhali see aslo the side of mwananchi asiye kuwa na uwezo.
    Nilifurahia sana kusikia mheshimiwa speaker anapinga ufisadi. Wanajaribu kumtoa katika jimbo lake na tupo tayari kusimama kwa nguvu zote kumsaidia. Michu, you don't have to go that distance lakini please uwe upande wa wananchi watanzania.

    Mungu atubariki for us to celebrate 2010 again. Happy New Year

    ReplyDelete
  23. HAPPY NEW YEAR michuzi. ninakuombea MWENYEZI MUNGU akupe kila la kheri mwaka huu wa 2009 uzidi kutuburudisha na hii blog yako. Mr. Michuzi you are the best. ningeomba wale wengine wenye blogs zisizo na kichwa wala miguu na ambazo huwezi hata kupeleka maoni wajifunze kutoka kwako

    ReplyDelete
  24. Bw. Michuzi shukrani nyingi kwa salamu za mwaka mpya na kutuhakikishia kuwa libeneke ni kama kawa!!!
    Nimerejea kutoka kavakesheni ka wiki mbili za mwishoni mwa disemba hapo Bongo. Nilijaribu kukutafuta katika vijiwe kama vitatu hivi, lakini kwa bahati mbaya kila nilipofika nikaambiwa kuwa ndo ulikuwa umeondoka dakika chache. Mara nyingine nitatafuta simu yako na kukufahamisha kabla ya kuanza kukusaka!! Kweli hakuna ubishi bongo inazidi kuwa tambarare, lakini pia haikosi vituko vya kumbakiza mtu ametumbua mimacho!! Kwa mfano, nilifarijika kukuta barabara ya Sam Nujoma imekamilika na kuwekwa taa za kisasa za kuongozea magari. Lakini kilichonifanya kubakia nimepigwa bumbuazi ni kwamba madreva hawasimami wakati taa zikiwa ni nyekundu. Kila niliposimama nilipigiwa honi na siku moja alimanusura shangingi la STJ linikwangue!!! Afande wa kikosi cha trafiki hana budi apatupie macho hapo ili kutokomeza huu 'utamaduni' mbaya.
    Lakini lililonitoa jasho zaidi ya yote ni utamaduni wa noti za dola mia za Marekani. Hii ilikuwa mara ya pili. Mara ya kwanza ilikuwa ni 2007. Kutokana na ushamba wangu huwa ninabeba vijisenti kidogo (katika maana halisi ya neno vijisenti)ili kuepukana na kupanga mistari mirefu katika ATMs. Mwaka 2007 noti zipatazo tano nilizokuwa nazo zilikataliwa na kila duka la kubadilisha fedha kwa madai kuwa zilikuwa na vichwa vidogo (ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kusikia hadithi ya vichwa vidogo na vikubwa). Nililazimika kurejea nazo US. Katika kavakesheni ka juzi nilihakikisha ninabeba noti zenye vichwa vikubwa. Basi nilifika katika duka la kwanza nikiwa na moyo wa kujiamini kuwa mara hii hanibabaishi mtu!!! Kwa mshangao niliona mhudumu akinirejeshea noti kama sita hivi! kulikoni? "tunapokea noti za kuanzia mwaka 2000 na kwenda juu tu." Nilipitia maduka mengine mawili matatu hivi na hadithi ilikuwa ni hiyo hiyo. Nilipohoji huo utamaduni unaanzia wapi, nikaambiwa kuwa ni watu wa Benki Kuu. Sijui kama kuna mdau anayeweza kunielimisha kwa nini Benki Kuu ya Tanzania bado inafanya kazi kana kwamba tunaishi karne ya 19!!! Bongo tambarare, lakini .....

    mdau
    USA

    ReplyDelete
  25. Mdau hapo juu uliyesumbuliwa na $100 zako. Net time ukitaka kufaidi nunua American express travelers checks. So cool

    Happy new year kwako michuzi na wana blog wote.

    ReplyDelete
  26. ni delta wee annon,Tz hatuna ox-bow lake,,,
    afu nawe michu hotuba ndeeefu khaaa
    tunachokaga kusoma,,shule tusoma na bloguni pia???aaagh
    HERI YA MWAKA MPYA MICHUZI NA FAMILIA NA WADAU WOTE
    nakufagilia saaana yan michu dah!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...