Kaka Michuzi,
Nimeona hii habari kwenye Daily News kwamba Tanzania imepata hasara ya SHS TRILLIONI 4, (4,000,000,000,000.00). kutokana na BIDHAA FEKI - Link
http://dailynews.habarileo.co.tz/columnist/index.php?id=9185
Jamani kwanini TUENDELEE KUFA NA TUZIDI KUWA MASKINI KWA BIDHAA FEKI?

Kwanini serikali inashindwa kutoa adhabu kali ya kifungo, kufunga biashara permanently na faini kwa wafanyabiashara wanaokutwa na hizi bidhaa? Kuna nchi nyingine wanajadili hukumu ya kifo kwa watu kama hawa.

Hawa ni wauaji kwa sababu,
1) mtu anaumwa malaria yupo hoi halafu anapata dawa feki ya malaria anakufa
2) kuunguza moto nyumba kwa bidhaa feki za umeme na kuua watu na watoto,
3) watu kuumwa magonjwa kutokana na madawa makali na material fake yanayotumika kwa vitu kama rangi za nyumba, malighafi kwa vitu kama redio, maziwa ya watoto, vyakula etc.
4) gari kupata ajali kwa brake pad feki au spare feki. na kuua.

Cha kushangaza bei hazipishani sana kati ya genuine na fake na athari za fake ni kubwa sana.
Serikali ikikamata wafanyabiashara 20 tu na wakapata miaka 20 jela, kila mfanyabiashara aliyekuwa anauza bidhaa feki atafikiria mara mbili kabla ya kuuza, naomba bunge lipitishe muswada wa sheria ya adhabu kali haraka iwezekanavyo na PCB, polisi kwa kushirikiana na Confederation of Tanzania Industries (CTI) vifanye zoezi la kimya kimya, mitaa ya hawa wafanyabiashara inajulikana, uhuru, mnazi mmoja, clock tower etc.

Kuna mambo yanayohitaji misaada na know how kutoka nje lakini hili halihitaji tuna uwezo nalo, kamata bidhaa, tuma sample kwa kampuni mama au mwakilishi wake tanzania fake au siyo feki habari imekwisha.

Mafisadi hawataifurahia hii habari kwa kuwa itawaumiza mirija yao.
WADAU HII MNAIONA IMEKAAJE?
MDAU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Michuzi wakati mwingine una akili sana, huu ni mmoja wa wakati huo. Lakini nyakati zingine huwa unachemsha sana .Eti siku ile unapanda ndege unaenda wapi sijui ukapiga picha ndege za ATC eti "tazama midege yetu yote leo ipo uwanjani" !!! HAYA SHIRIKA LIMEFUNGWA SASA, utasema nini?
    lakini kwa topiki ya leo, HONGERA SANA.

    ReplyDelete
  2. hayo ni mawazo mazuri sana, ila ufisadi. hao wauzaji wana fedha sana hasa kutokana na bidhaa feki. kukamatwa hao inahitajika nguvu halisi ya wananchi. wananchi wanapaswa kuishinikiza serikali izuie.

    hao nao ni mafisadi tu. wauaji wakubwa.

    ReplyDelete
  3. Welcome to Tanzania, the land of stupidity....
    Sipendi kusema maneno hayo juu, ila imefika sehemu sisi watanzania tumekuwa kama kondoo au nyani (not sure with exact wording) ambao unamuua mmoja wao badala ya kukaa kidete na kukukimbiza, wanakimbia baada ya muda wanarudi pale pale mwenzao alipouawa wanaendelea kula majani kama vile hakuna kilichotokea.
    Kwa ufupi ukiehesabu watu waliopoteza maisha just because of the fake medicines being provided in our country you wont sleep for rest of ur life.
    Ngojea niachie hapo make machozi yashaanza kunitoka, this is is sick.

    ReplyDelete
  4. Mapambano yaliyoanza ya ukombozi wa Tanzania ili kuokoa maisha ya watu dhidi ya mafisadi na wababaishaji wengine yanapaswa kugusa nyanja hii ya BIDHAA FEKI.
    Adhari za bidhaa feki hazipimiki na wala hazina fidia kwani nyibgi hugharimu maisha ya watu na kutia hasara ya uchumi wa nchi. Hebu fikiria hasara tupatayo pindi maradhi kama malaria yajengapo usugu kwa dawa kutokana na mgonjwa kutumia dawa feki??
    Biashara hii kwa kiasi kikubwa inashamirishwa nna uwepo wa RUSHWA na KUTOWAJIBIKA miongoni mwa watu waliokabidhiwa dhamana ya kulinda ubora wa bidhaa ziingiazo nchini.
    Hakika Tanzania changamoto ni nyingi ili kuyafikia maisha bora, tusiangalie upande wa kipato tu, hebu na tuboreshe taratibu na kkanuni zetu zitakazotuhakikishia ustaarabu miongoni mwetu kama taifa.
    Hebu 2009 uwe mwaka wa kuboresha ufahamu na uelewa mpana wa WATANZANIA juu ya mambo yenye manufaa na adhari mbaya kwa Jamii.

    Heri ya Mwaka Mpya kwa Watanzania wote popote walipo Duniani.

    Mdau, Oslo Norway

    ReplyDelete
  5. guys!!! where is the purchasing power? bidha feki. That's ita zinaletwa fake simply majority can't afford genuine goods. Kwa nini magari ya kijapani yamejaa tz na sio ma-cadillac au GMC?

    Ni lazima tukubari ukweli, wenye uwezo wa genuine wache wanunue, walala hoi kama mimi mzee ngwengwesa niachieni

    ReplyDelete
  6. Kazi yetu ni kutoa lawama lakni wafnay bisahra wengi wa Tanzania kwa mfano Pharmacy wanakuuliza unataka ya dawa fualni ta India bei yake shilling 500 au tunayo ya UK shillingi 2000. Halafu uansema lete hiyo ya 500 sasa wakulaumiwa ni nani?
    India street wanuza siwtich wanakwambia hii hapa ya China bei poa 250/ na hii hapa orginoooo shillingi 1200/. fundi wako ananua ya 250.

    Kwani kila mtu anajua kuwa bidhaa fulani ya Taiwan bei yake ni karanga na ile ya Ujerumani inauzwa mara sita. Inakuwaje wakiwa wawazi namna hii bado mnataka kuwashupalia badala ya kujilaumu wenyewe?
    Watu wengi wanotaka vitu origino wanahiyari kununua mtumba Congo kwa bei ya juu kuliko mpya ya kifala. Chingaz wote wanajua rahisi ni ghali, utanunuaje fungu la RADO kwa shillingi elfu?

    ReplyDelete
  7. Halmashauri yauza eneo la makazi Dar

    2008-12-28 13:09:18
    Na Muhibu Said


    Wakati serikali ikiwafikisha mahakamani wanaodaiwa kulitia taifa hasara ya mabilioni ya fedha kwa njia za kifisadi, ufisadi mwingine umeibuliwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam, baada ya uongozi wa manispaa hiyo kudaiwa kuwauzia wafanyabiashara wawili eneo lenye makazi ya watu kwa nyakati tofauti na kwa siri.

    Wafanyabiashara waliouziwa eneo hilo, lililoko kwenye Kiwanja namba 109 Kitalu `C`, Eneo la Viwanda, Chang`ombe `A` Unubini, jijini Dar es Salaam, ni Kampuni ya Africariers Limited na Kampuni ya Faiz Enterprises Limited.

    Manispaa inadaiwa kuwauzia wafanyabiashara hao eneo hilo na kufuta umiliki kwa wamiliki wake halali (wakazi hao) kimya kimya.

    Kutokana na kitendo hicho, zaidi ya kaya 200 zinazoishi katika nyumba 16 katika eneo hilo, zinahofiwa kupoteza makazi na fidia kutokana na nyumba wanazoishi kuingizwa katika mpango wa kubomolewa baada ya kuwekewa alama ya X, kwa njia ambazo hazitambuliki kisheria.

    Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Luteni Mstaafu Abdallah Kihato, ambaye amelithibitishia Nipashe Jumapili kuwa eneo hilo limemilikishwa watu wawili, hadi sasa ndiye kiongozi pekee wa serikali, jijini Dar es Salaam aliyejitokeza hadharani kupinga kitendo hicho cha manispaa kupitia barua zake tofauti alizouandikia uongozi wa manispaa hiyo. Nipashe inazo nakala zote za barua hizo za Luteni Kihato.

    Siri ya uuzwaji wa eneo hilo imefichuka, baada ya wafanyabiashara hao kufikishana mahakamani kwa nyakati tofauti, huku kila mmoja akimtuhumu mwenzake kwa madai kwamba, amevamia `eneo la mwingine`.

    Kumbukumbu za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa, zinaonyesha kuwa awali, Kampuni ya Faiz Enterprises Limited, ilifungua kesi mahakamani na kudai kuwa ndiye mmiliki halali wa eneo hilo na kuituhumu Kampuni ya Africariers Limited kuwa ni mvamizi.

    Kesi hiyo namba 307/ 1987 iliyofunguliwa Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam Februari 3, mwaka 1987, iliisha Machi 27, mwaka 2006, ambapo Kampuni ya Faiz Enterprises Limited ilishinda kesi hiyo. Uamuzi wa kesi hiyo ulitolewa na Jaji wa Mahakama Kuu, Stephen Ihema.

    Hata hivyo, Aprili 6, mwaka huo, Kampuni ya Africariers Limited, ilikata rufaa namba 60/2006 katika Mahakama ya Rufaa kupinga ushindi wa Kampuni ya Faizen Enterprises Limited. Hata hivyo, rufaa hiyo ilitupwa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo, Januari Msoffe, Suleiman Mbarouk na Bernard Luanda.

    Nipashe inazo nakala za mwenendo na hukumu zote za kesi hizo pamoja na nakala za nyaraka za malalamiko na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wakazi wa eneo hilo.

    Nakala za barua za wamiliki hao, zimepelekwa Ofisi ya Rais, Ikulu na kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, jijini Dar es Salaam.

    Wakizungumza na Nipashe hivi karibuni, wakazi hao walisema baada ya kuliuza eneo hilo kwa wafanyabiashara hao, maofisa wa manispaa walikwenda na kufanya uthamini na kisha wakawazuia kukarabati na kuendeleza majengo yao na kuyawekea alama ya X.

    ``Baada ya kipindi kirefu kupita na majengo yetu kuchakaa, alitokea tajiri mmoja aitwaye Muna. Huyu alitaka kutusaidia kununua eneo letu ili awekeze biashara zake,`` alisema Chabo Shamte, ambaye ni mmoja wa wamiliki wa nyumba katika eneo hilo.

    Hata hivyo, Shamte, ambaye alizungumza na Nipashe akiwa pamoja na mmiliki mwenzake wa nyumba katika eneo hilo, Ahmed Mbondo, alisema baada ya mazungumzo ya awali na kuagana, siku nyingine Muna aliwafuata na kuwadokeza kuwa ameshindwa kununua, kwani amegundua kuwa eneo hilo limeuzwa mara mbili kwa wafanyabiashara hao na kila mmoja amepewa hati ya kulimiliki.

    ``Ndipo tukaanza kufuatilia manispaa, ambako walitueleza kuwa ni kweli eneo lina kesi Mahakama Kuu,`` alisema Shamte.

    Baadhi ya nyaraka zinaonyesha kuwa, Septemba 5, mwaka 2007, wakazi hao kupitia Mwenyekiti wao, Hamisi Kiliza, waliwasiliana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa barua, wakiomba mwekezaji, Kampuni ya Tanzania Sports House kama mnunuzi aliyeshinda zabuni yao (wamiliki) apatiwe hatimiliki ya eneo hilo.

    Hata hivyo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupitia barua yake yenye kumbukumbu namba MD/L.30/2 VOL/41 ya Oktoba 30, mwaka 2007, iliyosainiwa na Michael Ole-Mungaya kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa, iliwataka wasubiri hadi rufaa iliyokatwa na Kampuni ya Africarriers mahakamani iamuliwe.

    Wakazi hao pia, katika tarehe tofauti Julai na Agosti, mwaka 2007, waliiandikia manispaa barua kuomba suala hilo, lakini katika barua yake yenye kumbukumbu namba LD/TM/CH/109/79/GN ya Julai 31, mwaka huo, iliyosainiwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Iddi Nyundo, ilitupa ombi lao kwa maelezo kwamba, eneo hilo linamilikiwa na Kampuni ya Faiz Enterprises Limited tangu mwaka 1986.

    ``Kufuatana na sheria ya ardhi Na. 4 ya 1999, G.N. 72 ya 2001 hatuwezi kutoa milki ya kiwanja hicho kwa mwombaji uliyempendekeza kabla ya kusitishwa milki ya awali,`` ilieleza sehemu ya barua hiyo ya Nyundo kwenda wakazi hao.

    Nyundo kwa sasa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

    Shamte alisema baada ya kesi kati ya Faiz Enterprises na Africarriers kuisha, walifuatilia tena manispaa suala lao, lakini juhudi zao zikagonga mwamba baada ya maofisa wa manispaa kuwajibu jeuri.

    Alisema kutokana na hali hiyo, waliwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Luteni Kihato, ambaye aliwaahidi kulimaliza tatizo hilo baada ya kukiri kwamba, manispaa imefanya makosa.

    Luteni Kihato, alimwandikia Mkurugenzi wa Manispaa, Nyundo (wakati huo) barua yenye kumbukumbu namba B.40/9/95 ya Desemba 29, mwaka 2006, inayoeleza kama ifuatavyo:
    ``Rejea barua ya Afisa Ardhi mteule Bwana Maiba M.1 ya tarehe 10 Novemba, 2006 Kumb. Na. LD/TM/CH/109/50. Kwenye barua hiyo nimefahamishwa kwamba umiliki wa kiwanja hicho una utata na shauri hilo lipo mahakamani. Ili ifahamike mmiliki halali kati ya Faiz Enterprises Ltd na Africarriers Ltd.``

    ``Suala hili lina zaidi ya miaka 28 tangu wakazi wa eneo hilo walipojulishwa kuwa watahamishwa lakini hadi sasa hawajalipwa fidia wanazostahili na wala hawajaonyeshwa pa kwenda.

    Hii imesimamisha shughuli za maendeleo ya wakazi wa hapo kwa makazi yao kuendeleza mtaa wao na vilevile kulitumia eneo lao katika kujiondolea umaskini.``

    ``Kwa sababu hakuna yeyote aliyewalipa fidia wakazi wa eneo hilo, sioni sababu ya mtu kudai uhalali wa milki ya eneo hilo.

    Nionavyo mimi bado kiwanja Na. 109 ni mali ya wakazi wa eneo hilo na wanayo haki ya kufanya wanachopenda. Sina hakika jinsi wao wanavyohusishwa na kesi iliyopo mahakamani. Iweje watu wagombee umiliki wakati eneo lenyewe lina watu wa asili na hawajaondolewa.``

    ``Nimetembelea eneo lenyewe na hali niliyoikuta si nzuri kwa kuishi watu na hii inatokana na kushindwa kutekeleza maamuzi ya kuwahamisha na wao wakawa wanangoja kwa miaka zaidi ya 28 bila kufanya lolote la maendeleo.

    Ili watendewe haki wananchi hawa ikubalike kwamba hawahusiki na shauri lililopo mahakamani na kwamba wameteseka kwa muda wote huo bila sababu za msingi.``

    ``Nashauri yafuatayo:-Iwapo dhamira ya kuwahamisha wakazi wa eneo hilo bado ipo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke au Halmashauri ya Jiji iwalipe fidia na kuwaonyesha maeneo ya kwenda.

    Kwa sababu muda waliosubiri ni mwingi sana malipo ya fidia yafanyike katika kipindi kisichozidi miezi mitatu kuanzia tarehe 1 Januari 2007.``

    ``Endapo itakubalika kufidiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke au Halmashauri ya Jiji lazima tathmini ifanywe upya.

    Isiwe iliyofanyika mwaka 1978 na iliyofanyika 2000. Kama haya yanakubalika, (wewe au Mkurugenzi wa Jiji) uitishwe mkutano wa wananchi kuthibitisha utekelezaji wa ushauri huu na kuweka taratibu za kushughulikia.

    Hadi ifikapo tarehe 15 Januari, 2007 hapatakuwa na mkutano nilioutaja hapo juu nitawaruhusu wananchi waamue la kufanya kwa sababu ni mali yao.``

    Nakala ya barua hiyo ya Luteni Kihato ilipelekwa kwa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa Jiji na Ahmed Mbondo, ambaye ni mmoja wa wamiliki wa eneo hilo.

    Hata hivyo, pamoja na barua hiyo ya Luteni Kihato, hadi sasa hatima ya wakazi hao bado haijajulikana na habari zilizolifikia Nipashe Jumapili jana zinaeleza kuwa mmoja wa wafanyabiashara aliyeshinda kesi, amewafungulia kesi mahakamani wakazi hao akiiomba mahakama iwaamuru kuondoka katika eneo hilo.

    Kwa mujibu Shamte, tayari wamekwishapelekewa hati ya kuitwa mahakamani kwenda kujibu madai ya mfanyabiashara huyo.

    Luteni Kihato alipoulizwa jana na Nipashe Jumapili, alikiri barua hiyo kuwa ndiye aliyeiandika na kusema kuwa suala hilo kwa sasa limefikishwa kwa Kamishna wa Ardhi, katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

    ``Ni kweli hizo barua nimeziandika mimi na suala hilo lipo kwa Kamishna wa Ardhi. Pale kuna tatizo la hati mbili za umiliki na wahusika walifikishana mahakamani, sijui kesi iliishaje ila suala hilo tumelifikisha kwa Kamishna wa Ardhi,`` alisema Lutenio Kihato.

    Nipashe ilipowasiliana na Nyundo hivi karibuni kutaka atoe ufafanuzi kuhusiana na madai hayo, alimtaka mwandishi awasiliane na Mkurugenzi wa sasa wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Stephen Kongwa, kwa maelezo kwamba hivi sasa yeye (Nyundo) si mkurugenzi wa manispaa hiyo.

    Hata hivyo, Kongwa alipotafutwa na Nipashe Jumapili, hakupatikana na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi jana, ilikuwa imezimwa.

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  8. MZALENDO MENGI AMEONGELEA SANA SANA KUHUSU JAMBO HILI, HAKUNA HATA MUONGOZO WA KUKABILIANA NA BIDHAA "FEKI".

    SERIKALI INAPAMBANA NA WAMACHINGA NA SIO WANAOINGIZA BIDHAA FEKI.

    BIDHAA ZINA KUJA NA MAJAHAZI NA MITUMBWIPAMOJA NA MELI.

    TANZANIA INAONGOZA KWA 4TH CLASS YA BIDHAA/MBOVU NA FEKI WATU WANAKUFA NA KUPOTEZA FEDHA NYINGI SANA BILA KUJUA.

    ReplyDelete
  9. Anon wa 30 dec 12:26

    Swala la msingi ni madhara ya bidhaa feki kwa watanzania na kisheria haziruhusiwi, hivyo ni kosa la jinai kuuza hizi bidhaa.

    Swala la watu kununua ni 'ignorance' ya kutoelewa madhara yake kwa baadhi ya watu. Ugonjwa huu umeingia kwa nguvu na kuambukiza wengi akiwemo anon wa dec 29, 10.41 pm eti wenye uwezo wanunue kwasababu ni bei ghali. ameshindwa kuelewa kuwa huyu anayenunua fake kwa bei rahisi mwisho wa siku atalipia kushinda huyu wa kwanza kutokana na msiba, ajali etc- kuendeleza umasikini - mfano halisi ni mwaka 1995 huko nigeria ambako watu 2500 walikufa kwa kupata chanjo feki ya meningitis.Mifano ni mingi watu kufa kwa umeme moto, maziwa, vipodozi, magari, etc.

    Pili Serikali ina wajibu wa kulinda afya za wananchi wake na hii haitakiwi kuangalia sababu za biashara etc afya kwanza.Hii inatakiwa kufanyika mara moja bila kungoja ukiritimba.

    Tatu serikali ielimishe watu dhidi ya huu ugonjwa, (mindset, ignorance) madhara yake kiafya na kibiashara kwa kila mtanzania, i.e kutuzidishia umasikini kwa kupungua kwa pato la taifa, magonjwa, vifo kutokana na uongo wa wazi kwamba feki ni bei rahisi.Bidhaa feki nyingi hazijatengenezwa kwenye viwango kwa hiyo huwa havifanyi kazi inavyopaswa na hivyo kuleta madhara. Wanunuzi wengi wanadanganywa kwamba imetengenezwa kwenye viwango, si kweli.

    Mwisho inabidi serikali iungane na ngo na makampuni kwenye kampeni dhidi ya bidhaa feki.

    Jibu kwa anon wa 30 dec 12.26 ni anatakiwa kuelewa kwamba switched socket outlet ya shs 250 itaharibika chini ya mwaka mmoja wakati socket outlet ya shs 1200 na kuhakikiwa na kiwango cha BS 1363-5:2008 itafanya kazi si chini ya miaka 20.

    Hesabu ya haraka ni inabidi huyu jamaa kwa miaka 20 anunue kila mwaka hivyo miaka 20 x shs 250 ni shs 5000 bado athari za kuwaka moto, kubadilisha wiring kwa kuungua na gharama ya fundi kila mwaka.Sasa yupi amenunua bei rahisi? Anon naomba uwe na upeo mpana na siyo kuangalia jioni utakula nini angalia na mwaka kesho utakula nini!

    ReplyDelete
  10. wadau tusichanganye rahisi (cheap) na fake (feki). Kitu kinaweza kuwa rahisi lakini kinafikia ubora. Mfano, Landcruiser Standard na Landcruiser VX zote zinaweza kuwa original na zina ubora wa hali ya juu lakini bei zinatofautiana kukidhi uwezo wa kifedha wa wateja mbalimbali.

    Kwa upande mwingine unaweza kwenda mtaa wa Samora ukanunua mountainbike feki kwa 300,000/- wakati mountainbike feki hiyohiyo Kariakoo inauzwa 50,000/-.

    Ufeki na bei ni vitu viwili tofauti kabisa. Cha msingi TBS na serikali inabidi wahakikishe bidhaa zote zinazoingia nchini, ghali au rahisi, zinafikia viwango vya juu vya ubora.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...