kama kawaida yao Kilimanjaro Band maarufu kama Wana-Njenje (pichani) watauaga mwaka 2008 na kuukaribisha 2009 pale pale pa kawaida yao, yaani viwanja vya karimjee hall jijini Dar KESHO JUMATANO kuanzia saa tatu unusu usiku hadi kokoliko.

kiongozi wa njenje, waziri ally, kaiambia globu ya jamii sasa hivi kwa ung'eng'e kwamba wao huwa hawa tale advantage ya sikukuu kwa kupandisha kiingilio na kwamba dau lao mlangoni ni lile lile la miaka nenda miaka rudi la kiasi cha mboga yaani sh. 5,000/- tu!

waziri kasema pamoja na burudani kibao na kuduarika pia kutakuwa na big screen ambayo itachezwa dvd za njenje tokea miaka ya 80 na pia atayependa atauziwa. ila kasema ziko chache kwa hiyo mdau ukifika tu toa oda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. sasa wewqe Michuzi mbona hujatuambia ni lini yaani tarehe ngapi?

    Kwani kuuaga mwaka mpya hakuna sheria inayosema lazima tarehe 31 Disemba. wako wengine wanaouga kabla ya tarehe 31 kama vile tarehe 30.

    We vipi wewe? Usi tek fo granted bwana!

    ReplyDelete
  2. Digital age haiongopi mkuu,post ya Michuzi ina tarehe....30.12.08 na yeye kasema KESHO JUMATANO yaani kesho ya tarehe 30.12.08 ni tarehe 31.12.08! mdau umechemsha na umeumbuka!!Kuna watu huwa wanasoma posts kutafuta makosa tu..sasa badala yake makosa wanayafanya wenyewe!!Kaka michuzi uko right

    ReplyDelete
  3. we mdau wa kwanza mbona unapenda kujifanya mjinga? alivyosema michuzi sawa sawa na hapo mtu unajua kabisa kwamba sherehe ya kuuaga mwaka mpya inafanyika tarehe 31 popote pale hata mwendawazimu anajua,ingekuwa tarehe tofauti na hio ndio ungewekewa tarehe sasa ambayo ni tofauti na siku ya mkesha wa mwaka mpya.
    mie swali langu kwanini wanamuziki wa tanzania wanapenda kutengeneza copy chache za cd au kama njenje hapo dvd zao kwenye maonyesho kama hayo wakati wanajua ukumbi unaweza kubeba idadi ya watu wa ngapi na kama copy zitabaki watauza tu kwenye maonesho zingine kulikoni wapenzi wao kuambiwa zimeisha kwani ni hasara kwao na pia uzuni kwa washabiki wao.
    haya na watakia kila la kheri kusherekea mwaka mpya popte pale mlipo mungu hawa bariki.
    by mzawa.

    ReplyDelete
  4. Naam waungwana, wakati sisi wengine tukiungulika roho huku mbali hatusiti kuwatakia kila lililo jema katika shoo yenu ya kesho natumaini itakuwa maridadi kama ilivyokuwa ya mwaka jana.
    Moddy, Keppy,Mebbu,Nyota,Juma, John,Ustadh na swahiba uzi ule ule, mduara kwa kwenda mbele! Nawe Balozi mteule tuletee picha nyingi tujione kama tupo pamoja.
    Much love!
    Babu Boko!

    ReplyDelete
  5. hasheeeem thabit
    http://msn.foxsports.com/cbk/story/9004848/No.-11-Hoyas-expose-No.-2-UConn-in-road-win?MSNHPHMA

    ReplyDelete
  6. .....Kilio cha baba sikulia,kilio cha mama sikulia cha mpenzi wangu nimelia...............Lia mtoto lia............lia mwanangu lia,jamani hii ni nyimbo ya lia moja ya myimbo zao mpya.Mmmmh Michuzi,yani ukiskia mtu anamiss home ndio mimi japokuwa ntaenda time square lakini badonatamani niruke nije kwenye huo mkesha,yani njenje wananikosha ile mbaya hasa nyimbo ile ya hatuonani,boko,kinyaunyau,gere.Naomba tuwekee snepu za kutosha michuzi hata na kajivideo.Naomba wambie akina babu njenje watengeneze website.Warumba cheeeeee......warumba henya......warumba mpooooo!!!!!!!!????Lete vitu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...