Halow Michu…
Leo nimekuletea yaliyojiri wakati wa vekesheni yangu mkoani morogoro mji kasoro bahari na kukuletea ya pande hizo. Pichani utaona kivuko cha Mto kilombero na bei za uvushaji. Picha zingine ni moja ya pahala pataaamu na murua pa kujiburudisha panaitwa Mbega resort, huwezi amini ipo ifakara na mpk ukumbi wa mikutano ndani.
Nakutakia siku njema kaka, endeleza libeneke.
Rgards,
John Mnamba.

feri ya ifakara
mbega resort ifakara



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Duh hizi picha zimenigusa.Asante Mr John.

    ReplyDelete
  2. Mlongo! Ukaya pa maa,Ifoza kumekucha siku hizi. Hapo kivukoni pananikumbusha ngalangi na mlamu kaliandili.

    ReplyDelete
  3. Tunamshukuru mdau kwa kutuletea picha hizi za Ifakara na kuelekea Mahenge.Hii ni sehemu nzuri sana katika nchi yetu na ni sehemu ambayo haijatambuliwa kabisa!
    Nimepita huko mwaka jana nikielekea Mahenge, the roof of centrally located "Tanganyika".
    Ni sehemu nzuri sana.
    Ila tu, hako kakivuko ni HATARI!!!
    Ile milango ilikuwa inachota maji nilipouliza nikaambiwa wanafanya hivyo siku zote na hakuna matatizo!!!

    ReplyDelete
  4. Aisee safi sana umenikumbusha nyumbani ifakara, kijiji cha Lipangalala jirani na kwa njichichi ndio njia hiyo hiyo iendayo mto kilombero. sasa ebu tutumie namba ya simu ya hiyo mbega. Safi saaaaana.

    ReplyDelete
  5. Du hizi picha zimenikumbusha mbali sana balozi, huyu jamaa alipitaje mpaka huko amesahau picha za Mikumi,Kilombero na Ruaha?

    ReplyDelete
  6. Awije bambo,Ifakara bomba ila hapavumi. sasa samaki wako wapi? Jamani si nilisikia kivuko kipya kimeletwa sa ndo icho au kile cha kuvutwa na kamba tena ah jamani Mhe.wa miundo mbinu mbinu yenyewe ndo hii au? jamani tya tulema ton?

    Bint wa Kindamba

    ReplyDelete
  7. Watu wazima 200! maiti bure au?

    ReplyDelete
  8. Kwa nini Mikokoteni hakuchanganywa ktk kundi la magari(saloon)
    Watu wazima shi'ngi 200.Swali-Mimi ni kiwete nitatozwa shi'ngi ngapi?

    ReplyDelete
  9. DAH PAMENIKUMBUSHA HOME CHILOMBORA SI MCHEZO ILA KIVUKO NI SOO NA TULIANDIKAGA VOCHA YA KUNUNUA KIVUKO ENZI ZA WIZARA YA UJENZI MWAKA 2002 WEKENI KIPYA JAMANI

    MDAU UKEREWE

    ReplyDelete
  10. nimeoona, inapendeza sana

    ReplyDelete
  11. Nimeiona hiyo Mtua huu mto ifakara unanikumbusha wakati nikielekea katika wilaya yetu ya (majuu) Mahenge ambapo huwezi kufika huko mpaka uupite mlima mmoja uitwao Ndololo nikipita hapo naelekea kwa bibi yangu Nawenge mpaka Epanko wei tu go !!!! balozi michuzi
    Mdau Canada

    ReplyDelete
  12. anny wa 2:49 maiti bila shaka itakuwa kwenye gari hivyo inajumuishwa na vitu vingine vinavyolipiwa na gari. La sivyo kama maiti yenyewe imebebwa kawa machela waliobeba ndio watalipia/
    anony uliyeulizia kivuko nakuunga mkono tuliambiwa kivuko kipya kimekuja na sikumbuki vema lakini nadhani Mkwere alienda kukifungua. Kama ndio hicho kipya huo ni ufisadi ulio kubuhu.

    ReplyDelete
  13. nilipita Ifakara nikitoroka jeshi kambi la chita. nilikula vitumbua na mandazi makubwa sana. hivi ile depot ya breweries bado ipo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...