Bendi ya African Stars maarufu kwa jina la Twanga Pepeta International, inaondoka leo kuelekea mjini Nairobi, Kenya kwa ajili ya onyesho maalum la kuuaga mwaka 2008 na kuukaribisha mwaka 2009.

Jumla ya wanamuziki 25 na viongozi watandoka kwa basi maalum la kukodi (SHUTTLE) tayari kwa onyesho hilo la funga mwaka lililoandaliwa na Safari Park Hotel ya mjini Nairobi.
Mwaliko hu unatokana na jinsi Twanga Pepeta ilivyoweza kujikusanyia wapenzi wengi mjini Nairobi na vitongoji vyake na kuwa bendi ya kwanza kupata mialiko mingi nchini Kenya kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya tano kwa Twanga Pepeta kutumbuiza Kenya ambapo mara ya kwanza ilikua wakati wa uzinduzi maalum wa vituo vya huduma ya tiba, mara ya pili ilikua kwa ajli ya kusheherekea sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, mara ya tatu ilikuwa ya kuadhimisha miaka ishirini ya “AERC” Taasisi ya Kimataifa inayoo jishughulisha na tafiti za Uchumi na mara ya nne kwa ajili ya uzinduzi wa mtandao wa simu wa Orange.

Kutokana na hilo, Twanga imejijengea umaarufu mkubwa nchin KENYA. Wanamuziki wamejiandaa vilivyo na nyimbo mbali mbali mpya kama “Sumu ya Mapenzi, Nazi Haivunji Jiwe na Mwana Dar es Salaam ambazo zitawekwa hadharani kwa mashabiki wao wa huko Nairobi siku hiyo ya Desemba 31.

Pia nyimbo za zamani kama Safari 2005, Kuolewa, Fainali Uzeeni, Aminata na nyinginezo nyingi zitapigwa siku hiyo kuwapa wapenzi wa burudani ya funga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya.

Pia rap mpya kama za Obama, Wizi Mtupu, Kisigino na Kutapika zitatambulishwa kwa mara ya kwanza katika onyeshonyesho hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake.

Baada ya onyesho hilo katika mkesha wa mwaka mpya mjini Nairobi Januari Mosi 2009, Twanga itafana nyesho lingine kwenye ukumbi wa Triple A mjini Arusha watakapokuwa wanarejea nchini na siku nayofuata Ijumaa tarehe mbili watatumbuiza Meeda Garden ya Sinza, Mori na Jumamosi Januari 3 watarejea kwenye ngome yao, Mango Garden, Kinondoni na Jumapili mchana watakuwa Leaders Club na usiku, TCC, Chang’ombe.
Hassan Rehani
Meneja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...