THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Archive for April 2008

njenje kuduarika a-taun mkutano wa sullivan

habari zilizoingia sasa hivi ni kwamba kilimanjaro band 'wana njenje' (pichani) watatua a-taun jumapili ijayo tayari kutumbuiza wakati wa mkutano wa siku nne wa sullivan jijini hapo.
kiongozi wa njenje waziri ally ameiambia globu hii usiku huu kwamba watatua a-taun jumapili na kufanya onesho lao la kwanza siku ya ufunguzi wa mkuatno huo juni 2, 2008 na pia wakati wa ufungaji june 6, 2008.
na mambo yakienda mswano huenda wakatia timu matongee pub & nightclub wikiendi itayofuata. waziri kasema usiku huu kwamna wakazi wa a-taun wakae mkao wa kuduarika na vibao vya vipya kibao.


kicheni mwisho wa reli

hii ndio kicheni katika hoteli ambamo mdau john kitime alifikia huko kigoma


fasheni

wakwe kwa fasheni tu hawajambo...


msaada tutani

Habari za kazi kaka michuzi,
mimi nipo fine kabisa,
napenda kwanza kutoa pongezi zangu kwako kwa kazi nzuri unayoifanya katika hii blog yako.Mimi nipo huku ughaibuni, nilikua naomba msaada tutani,ninamtafuta rafiki yangu mpenzi ambae nimepotezana nae kwa muda mrefu kwa jina anaitwa SELEMANI H KISESA.
mara ya mwisho niliwasiliana nae mwaka 1999 akiwa Canada,na baada ya hapo tukapotezana ki mawasiliano mpaka leo hii,ila nilisikia yupo Tanzania,sasa nilikua naomba popote alipo au kama kuna mtu yeyote ambae ana contact zake awasiliane na mimi kupitia Mail yangu revovinny@yahoo.co.uk.
Asante.


miss tz shengen yakaribia


Welcome to "Miss Tanzania Europe 2008"


The mission of the Miss Tanzania Europe Pageant is to promote Tanzania and its people in the rest of the World: Tourism, culture, the beauty of this East African Nation.


We aim to further raise awareness on issues pertinent to Tanzaniaa and most of all empower the Tanzania Queen to educate and enlighten communities as a goodwill ambassador for Tanzania.


The winner of Miss Tanzania Europe 2008, chosen on June 28th in Essen, Germany, and first runner up will represent Tanzania Europe* at the Miss Tanzania pageant to be held in Dar es Salaam in August 2008.


If you want to apply, please go on the Application-Page


If you wish to apply for running in the Miss Tanzania Europe Pageant, you must be at least 18 years of age, of Tanzanian origin and residing in any State of the European Union wich is a Member of the so called "Schengen-Agreement".
habari ndiyo hiyo


Habari hiyo hapo chini inapatikana pia www.nukta77.com sehemu ya "Ukumbini"


Ad-Aware ambayo ni toleo la Lavasoft's la anti-spyware/anti-adware
linapatikana bure kwa sasa. Katika toleo hili, UI na anti-virus vimeboreshwa na kuwezesha kutambua nyendo mbovu za virusi, spyware na trojan wanaojipanga kuvamia kompyuta yako.
Orodha ya yaliyoboreshwa katika Ad-Aware 2008 ni pamoja na:
Improved Threat Detection
Enhanced Rootkit removal system
Faster Updates & Faster Scans
Less Resource Usage for optimal computer performance
Easy to Download, Install and Use
Lavasoft ThreatWork submission tool
Ipakue Ad-Aware 2008 Free hapa
Toleo jingine la bure la anti-virus lililotolewa miezi kadhaa iliyopita ni:
Spyware Doctor 5.5
Type: full commercial application
Platform: Windows 2000, Windows XP, Windows Vista
Manufacturer:
PC Tools
Size: 25.3MB
Price:Free full commercial download
Download


libeneke jipya munich


Haya tena wadau wa Munich na Vitongoji vyake mnakaribishwa katika Sherehe ya Ufunguzi wa Club yetu mpya iitwayo Hakuna Matata


Ufunguzi utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 31.05.08 kuanzia saa 12 jioni.


Klabu hii sasa imehamia katika makao yake mapya

Bayer strasse

103 München.


Mdau Malumbo

Munich


jumuiya yazinduliwa uswisiHabari za leo kaka Michuzi,ninayo furaha kuwaletea habari kuwa hatimaye Umoja wa watanzania waishio nchini switzerland yaanzishwa rasmi leo siku ya jumapili tarehe 25 mwezi wa 5.


Mkutano huu uliohudhuriwa na watanzania wengi tu waishio Geneva pamoja na miji mengine ya karibu uliweza kujadili na kupitia katiba ambayo ilipitishwa na kukubalika kuwa muongozo wa jumuiya hiyo.


Umoja huo utajulikana kama Tanzanians Association in Switzerland kwa kifupi TAS.


Kwakweli mimi binafsi kaka michuzi nimefurahishwa sana kuanzishwa kwa umoja huu maana ni jambo lililokuwa wazi kuwa wengi wa watanzania waishio nchini humu walikuwa na hamu ya kuwa na jumuiya itakayoweza kuwakutanisha wakati wa raha na hata wakati wa shida.


Pamoja na mambo mengine mengi Umoja huu pia umelenga kuwawezesha watanzania waishio nchini humu kuweza kuunda mikakati itakayo wasaidia katika nyanja mbalimbali hasa ya elimu kwa vijana na watoto wao na hata maendeleo ya kiuchumi wakiwamo nchini hapa na kwingineko.


Mheshimiwa Balozi Marten Lumbanga ambaye ndiye Balozi wa Tanzania kwa Umoja wa Mataifa hapa Switzerland ameteuliwa kuwa Patron wa jumuiya hio.
Pamoja naye viongozi wa jumuiya hio ni kama ifuatavyo:

Mlezi-----------------------Balozi Mh. Marten Lumbanga
Mwenyekiti-----------Dr.B. Nyenzi
Makamu M/kiti---------------Mrs. Mpatwa,
Katibu----------------------Mr.S.M. Sillayo
Katibu Msaidizi------------Mr. B. Luvanda
Mhasibu-----------------Mr.I. Lupatu


Kwa niaba ya watanzania wote waishio hapa napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza sana na kuwatakia kila la heri katika nafasi zao ili waeze kuiongoza vema jumuiya hii.
mdau,

geneva.


maandalizi miss universe tz 2008

Maandalizi ya fainali ya mashindano ya Miss Universe Tanzania 2008 yaanza rasmi ikiwa ni harakati za kutafuta mrithi wa mrembo wa kimataifa – Flaviana Matata (Miss Universe Tanzania 2007), ambaye mwaka jana aliipeperusha bendera ya taifa na kufanikiwa kuingia katika kumi bora ulimwenguni.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yanaandaliwa na Compass Communications chini ya mkurugenzi wao Maria Sarungi Tsehai.

Warembo wamechaguliwa kupitia mahojiano na msako wa kitaifa na warembo 20 wamepata nafasi ya kushiriki katika fainali itakayofanyika tarehe 29 Mei 2008, katika hoteli ya Moevenpick Royal Palm.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yatawapa nafasi warembo hawa kunolewa na wataalam mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupewa mafunzo ya urembo, mazoezi ya viungo, ngoma za asili na kadhalika.

“Tunaweza kuona ya kuwa viwango vya warembo wetu mwaka huu vimezidi kuwa juu na tunategemea kuona mchuano mkali kwa ajili ya taji hili kubwa,” alieleza Maria Sarungi Tsehai. “Warembo wetu wanawakilisha tamaduni na asili mbalimbali za nchi yetu pana. Fainali itakuwa ni ya kusisimua.”

Warembo wa Miss Universe Tanzania 2008 ni: Catherine Mungure, Joanfaith John, Jamillah Nyangasa, Lucy Tilaha, Lilian Michael, Alicia George, Namrata Mandania, Grace Mumburi, Happy Kimbe, Eline Maronga, Happiness Kisanga, Clara Wekwe, Adeline Kapinga, Fransisca Mushi, Asia Said, MaryStella Swai, Fatma Banka, Zakhia Sheamdoe, Eva Evance na Zubeda Sakuru.

Warembo watakaa kambini katika hoteli ya Belinda Ocean Resort na wamesindikizwa na matron wao Jamilla Munisi na Sarah Martin wa Compass Communications.

Mashindano ya Miss Universe yamedhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Coke Light, SeaCliff Casino, Clouds FM, TBC, Prime Times Promotions, Smoove, Chuo cha uandishi cha TIME, Shear Illusions na Golden Touch Saloon.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Compass Communications:
Tel: 2182405/2182596
au 0784 305122


tujadili mkataba wa maximo

zimebakia takriban siku 90 kabla mkataba wa kocha mbrazil marcio maximo wa kukochi taifa stars umalizike. mkataba huo wa miaka miwili ulibarikiwa na serikali ambayo ndio inamgharamia kila kitu. je, mkataba huu ukiisha aongezewe mwingine?


nyundo a-taun

mtaa wa goliondoi leo. sio dar pekee ambako nyundo zinatembea kila kona katika harakati za kubomoa majumba makuukuu na kujenga mapya. a-taun nako ni nyundo mtindo mmoja. ila, kama ilivyo dar, nyundo hizo haziendi sambamba na uboreshaji ama upanuaji wa miundombinu hasa ya maji safi na machafu pamoja na maegesho ya magari ambayo ni ile ile ya miaka ya 47


ali kiba kutua norway piataifa stars sare na malawi

pambano kati ya taifa stars na malawi 'the flames' limemalizika sasa hivi na matokeo ni 1-1


TENDA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA YATOKA

SERIKALI IMETANGAZA TENDA KWA AJILI YA UTENGENEZAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA NA DOLA 152 AMA SHILINGI BILIONI 180 ZA MADAFU ZIMETENGWA KWA SHUGHULI HIYO. HABARI KAMILI BOFYA HAPA


taifa stars yasawazisha

salum swedi anaisawazishia stars kwa kichwa baada ya fred mbuna kurusha kama kona dakika ya 35 na sasa ngoma ni 1-1 dhidi ya timu ya taifa ya malawi


malawi yaongoza 1-0

taifa stars imetumguliwa bao moja na malawa dakika 9 baada ya kipindi cha pili kuanza, goli lililofungwa na na mchezaji wa kulipwa anayecheza urusi, essau kayenga, kwa uzembe wa mabeki wa stars.
malawi wanashambulia sana na hadi sasa ni nusu uwanja, ambapo wamalawi wako kwenye 18 ya stars muda mwingi.
dakika ya 18 wamalawi wanakosa bao baada ya mpira kugonga besela, kipa ivo mapunda akiwa kapelekwa sokoni.


taifa stars vs malawi

hivi sasa ni mapumziko katika uwanja mpya wa neshno na si taifa stars wala malawi walioona lango la mwenziwe, yaani hadi sasa ngoma ni 0-0 na malawi wanashambulia ile mbaya


mama pinda

Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (mwenye kitenge) akitazama vyakula vilivyosindikwa na Fablonia Kalongoti (kusoto) wa Chama cha Kitume cha Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) katika hafla fupi iliyotnguliwa na ibada ya shukurani ya WAWATA iliyofanyika kwenye kanisa hilo leo


tx akiwa nanihii-moto...

mdau TX (kulia) ambaye ni memba wa kijiwe cha empress kwa fundi mussa akiwa na wafadhili wake wa kampuni ya East Africa Automobile Services wakipozi katika mji wa nanihii-moto huko japan.
hii ndiyo kampuni inayokagua magari yanayokuja ist afrika mashariki na asia.
Mdau Prosper
Kanagawa,Japan


jk aenda japani leo


Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka nchini leo jioni (25 Mei, 08) kuelekea Japan kuhudhuria mkutano wa nne unaohusu maendeleo ya Afrika, ujulikanao kama Tokyo International Conference on African Development (TICAD) utakaofanyika katika jiji la Yokohama.

Kabla ya kuhudhuria mkutano huo, Rais Kikwete atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Yasuo Fukuda, tarehe 27 Mei, 08 kuzungumzia mahusiano na ushirikiano wa nchi mbili hizi katika maswala ya kiuchumi na kidiplomasia na pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Kikwete anatarajiwa kumweleza mwenyeji wake juu ya maendeleo na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika na kujadili utatuzi wake.

Japan ni mshirika mkubwa wa maendeleo ya Tanzania ambapo Japan ni moja ya nchi zinazoisaidia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuchangia katika bajeti na pia imechangia katika misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula, barabara na maji

Mkutano wa nne wa TICAD utaanza tarehe 28-30 Mei, ambapo viongozi wote wa bara la Afrika wamealikwa kuhudhuria pamoja na viongozi wa Japan, wakuu wa mashirika mbalimbali ya kimataifa duniani kama vile Umoja wa Mataifa, mashirika ya fedha duniani, taasisi sizizo za kiserikali kutoka bara la Asia na Afrika, nchi rafiki na wenza katika maendeleo duniani.

Mbali na mkutano wa TICAD Rais pia atashiriki mikutano na makongamano mbalimbali yanayohusu uchumi, miundo mbinu, maendeleo na maswala mbalimbali yanayohusu utunzaji wa mazingira barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Aidha Rais Kikwete ataongoza mkutano utakaojadili tatizo la chakula duniani ambapo atazungumzia swala hili kwa kina hususan katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo barani Afrika na hatimaye atashiriki katika kupitisha azimio la Yokohama.

Rais pia anatarajia kutumia nafasi hiyo kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Afrika watakaohudhuria mkutano huo.

Rais atafuatana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Benard Membe, Waziri wa Fedha - Mhe. Mustapha Mkulo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zanzibar - Mhe. Haroun Suleiman, Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko - Mhe. Cyril Chami na Mbunge wa Muleba Kusini na Mwenyekiti wa Kamati Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama - Mhe. Wilson Masilingi.

Rais anatarajiwa kurejea Dar-es-Salaam tarehe 31 Mei, 2008.Imetolewa na Ikulu-Dar-es-salaam
25.05.08


nick pub yaungua

leo nimeshushuka. nimekwenda nick pub sehemu za njiro na kukuta kiota hicho maarufu kwa kilaji na nyama chima na samaki kimefungwa. kuuliza nikaambiwa kiliteketea kwa moto hivi karibuni. nusu nilie. yaani ukiwa a-taun bila kutembelea hapo unakuwa hujatembelea wadau na machalii kabisa. pole sana kaka nick kwa mkasa huo, Mola akujaalie katika kukifufua upya kiota


misa ya marehemu balali washington dc

HAPA MWILI WA MAREHEMU DAUDI BALALI UKIWA KANISANI. SAMAHANI SIKUWEZA KUCHUKUA PICHA VIZURI NDANI YA KANISA. LAKINI KAMA UNAVYOONA KWA MBALI KUNA JENEZA .

PICHA NA MDAU WASHINGTON DC


jk apokea ripoti ya madini leo

JK na (kutoka shoto) Mhe. John Cheyo, Jaji Mark Bomani, Mhe Iddi Simba na Mhe. Zitto Kabwe wakiwa katika mazungumzo ya kukabidhi ripoti ya madini leo huko ikulu, dar. chini JK akiwa katika picha ya pamoja na kamati teuli ya madini ikulu
ilala mabingwa taifa cup

timu ya mkoa maalumu wa kisoka ya ilala leo imeshinda mkoa wa kinondoni kwa mabao 5-0 katika fainali za safari lager taifa cup neshno na mpir umeisha dakika mbili zilizopita.
ilala, inayofundishwa na kocha machachari jamhuri kihwelo 'julio', itapewa kombe na kitita cha shilingi milioni 30 zilizotolewa na wadhamini ambao ni kampuni ya bia ama tbl.
mshindi wa tatu ni mbeya ambao wameifunga arusha 4-3 katika mchezo uliochezwa awali katika mtanange huu wa wiki tatu uliojumuisha timu kutoka mikoa yote 23 ya bara.


pemba kuzuri jamani....

mdau bernard rwebangira katuletea hii picha kuonesha sehmu ya kisiwa cha pemba ambacho kwa jinsi kilivyojaaliwa rutuba unaweza kusema uko tukuyu ama bukoba. bofya jina la bernard utembelee globu yake ambayo imesheheni picha za matukio mbalimbali


kwa wanaopenda ku-mingo


ukipenda kumingo nenda http://eastafricamingleclub.com/ kwenye klabu ya ku-mingo ya ist afrika mashariki.


jk atoa rambirambi kwa kifo cha balali

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA FAMILIA YA MAREHEMU DAUDI BALALI

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Ndugu Daudi Balali kilichotokea tarehe 16 Mei, 2008 huko Boston, Marekani.
Wakati huu mkijiandaa kwa mazishi yake baadaye leo, napenda kutumia nafasi hii kutoa mkono wa rambirambi kwenu na kwa ndugu zenu wote.

Naungana nanyi katika wakati wenu huu mgumu na wa majonzi makubwa kutokana na msiba mkubwa uliowakuta. Tunaelewa machungu mliyonayo kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu na kiongozi wa familia.
Ni kazi ya Mungu haina makosa.

Tunawatakia mazishi mema.
Tuzidi kumuombea marehemu apate mapumziko mema.
Amin.

IMETOLEWA NA OFISI YA MAWASILIANO, IKULU
TAREHE 23 MEI, 2008


libeneke miss tz eu 2008 lanukia

Cinderella"," Nakshi nakshi" na Miss Schengen 2008 ndani ya Germany kufanyika tarehe 28.06.08, Essen
Katika shindano la kumsaka mrembo wa Schengen 2008 , burudani itatolewa na msanii Ali Kiba ambaye ameahidi kurusha nyoyo za wapenzi wake usiku huo wa raha. Katika sakata hilo Mgeni rasmi atakua ni Balozi wa Tanzania nchini Germany Balozi A.R. Ngemera.
Wageni wengine maalum ni mratibu wa Kitengo cha kiswahili radio Deutsche Welle bi Andrea Schimdt, Mratibu wa Beautiful tanzania Agency bi Irene Kiwia na Miss World Africa Nancy Sumari.
Akifafanua zaidi Mratibu wa Shindano la Miss Tanzania Schengen bi Nashe Mvungi ameelezea kuwa kwa mara ya kwanza Miss Tanzania kushirikisha mrembo kutoka Schengen 2008, Ambapo mwaka jana UK ilikuwa ya kwanza kushirikisha mrembo kutoka nje ya bara la Afrika.
Nia ni kutaka kupanua utamaduni na mila ya mtanzania ulimwenguni, kushirikisha watanzania walio masomoni au wanaoishi ughaibuni katika kuchangia maendeleo ya tanzania kiutalii na elimu na kuweka uhusinao katika ya jamii iliyoko nyumbani na Ulaya.
Pia alipenda kufafanua kuwa shindano hili limepitishwa na kupewa baraka zote na Uncle Hashim Lundenga wa LINO International agency waandaaji wa miss Tanzania.
Mshindi wa shindano hili atajipatia zawadi ya ticket na nafasi ya kushiriki shindano la kitaifa mwezi August 2008 Dar es salaam.

info@misstanzania.eu
+49 1520 588 0863


jk atoa rambirambi kwa kifo cha balali

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA FAMILIA YA MAREHEMU DAUDI BALALI

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Ndugu Daudi Balali kilichotokea tarehe 16 Mei, 2008 huko Boston, Marekani.
Wakati huu mkijiandaa kwa mazishi yake baadaye leo, napenda kutumia nafasi hii kutoa mkono wa rambirambi kwenu na kwa ndugu zenu wote.

Naungana nanyi katika wakati wenu huu mgumu na wa majonzi makubwa kutokana na msiba mkubwa uliowakuta. Tunaelewa machungu mliyonayo kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu na kiongozi wa familia. Ni kazi ya Mungu haina makosa.

Tunawatakia mazishi mema. Tuzidi kumuombea marehemu apate mapumziko mema.
Amin.

IMETOLEWA NA OFISI YA MAWASILIANO, IKULU
TAREHE 23 MEI, 2008


old trafford ya kigoma

mdau john kitime a.k.a jfk katembelea mwisho wa reli na kutulete hii kitu.anasema hapo ndipo maarufu kwa kuonesha gemu zote za ughaibuni pamoja na sinema zingine na pia pana disko


karume afunga mkutano wa utalii


rais wa zanzibar mh. amani karume akiagwa na wazirir wa maliasili na mazingira mh. shamsa mwangunga baada ya kufunga rasmi mkutano wa 33 wa africal travel association katika kituo cha mikutano cha kimataifa aicc. nyuma ya waziri ni bosi wa kituo hicho mh. kaaya


wafanyakazi wa wizara ya utalii na mazingira

hawa ni baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya utalii na mazingira waliofanikisha mkutano wa 33 wa africa travel association kwa kazi mbalimbali za sekretarieti ya waandaaji


kubemenda

Shikamoo anko Michuzi!
Nimesikia hili neno 'Kubemenda mtoto' nikashindwa kujuha maana yake, naomba msaada tutani kwa wadau wanisaidie - ikiwezekana hata kwa kimombo naomba nifahamu ni nini...
Mdau wako mpenzi
Esta,
Lindi


fulanazzz....

wadau poleni na kazi za ujenzi wa taifa. bado niko porini nawinda. na kuhusu libeneke msikonde wala nini. japo niko porini lakini mambo kama kawa....


mambo ya ngorongoro

nala mkono nusu na wadau wa ngorongoro na chini ni mdau ambaye kahama mjini na sasa anaendeleza libeneke ngorongoro crater lodge. kabla ya hapo alikuwa sopa


tangazo rasmi la msiba wa balalinondozzz uchina

WELCOME TO STUDY IN CHINA

Universities:
Weifang Medical University, Taishan Medical University, Shangdong University of Science & Technology

Fields of Study:
Clinical Medicine, Nursing, Medical Image, Biomedicine Engineering, Laboratory Medicine, Pharmaceutical Engineering, Pharmacy, Parmacy (Clinical Oriental), Chinese Traditional Medicine, Biotechnology, Kinesiology, Environment Engineer, Chemistry Technology, Statistics, Marketing Management, Public Health, Engineering, Science, Management, Humanities, Law, Education, Art, Chinese Language etc

Level:
Bachelor and Masters

Teaching Language:
English

Tuition Fee:
Bachelor: USD$ 2,000 per year
Masters: USD$ 3,000 per year

Financial Support:
Financial awards are available every year for registered students who exhibit excellent academic performance.

For further information contact:
Masozi Nyirenda
or 0754 304 181,
I will connect you to Mr. Song Tan,
the Chinese representative of these Universities, who is in Dar now.


haya, msintoe macho bure

wachezaji wa mani yuu wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa nanihii juzi huko moscow


pamba high school

junior katembelea mwanza hivi karibuni na kuvutiwa na neno lililoandikwa ukutani kulia. mandhari zingine pamoja na mapicha kibao kama hizi bofya hapa


kiluvya pub yazindua globu
Killuvya Pub, baada ya kuwachengua Wapenzi wake kwa Burudani ya Nguvu ya mwaka Mpya 2008, mara hii inakuletea Burudani ya aina yake.

Huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Miaka ya 1960 na 1980 kumekuwepo Wanamuziki Magwiji wawili waliotamba sana Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati.
Hao ni Luambo Lwanzo Makiadi (Franco) na TPOK Jazz na Tabu Ley Rochereau na Afrisa International.

Katika kuwakumbuka na kuwaenzi Wanamuziki hawa, Kiluvya Pub inaandaa Tamasha kwa Wapenzi kumtafuta Nani zaidi kati yao. Historia za Wanamuziki hawa zimeandaliwa na Miziki yao iliyotamba pia imeshakusanywa.

Wapenzi wa Burudani Kaeni Mkao wa kula ili mtakapojulishwa tarehe ya kuanza Mpambano huo usikose kushiriki. Tembelea Globu hii kila wakati upate taarifa kamili.

Mkurugenzi.
NACHUKUA NAFASI HII KUMPONGEZA MKURUGENZI WA KILUVYA PUB KWA HATUA HII YA KIMAENDELEO YA KUZINDUA GLOBU KWA AJILI YA WADAU WAKO. HII INAONESHA KWAMBA TARATIBU TEKNOHAMA INAINGIA NDANI YA DAMU ZA WABONGO NA ITAKUWA RAHA ZAIDI KILA FANI IKAFUNGUA YAKE. KWA HABARI ZAIDI ZA PUB HIYO BOFYA HAPO CHINI


jk aelezea kuundwa serikali ya umoja wa afrika


Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete (Pichani akiwa na Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zinawi na Rais Yoweri Museveni wa Uganda) leo amesema kuwa, kimsingi, nchi za Afrika zinakubaliana kuhusu umuhimu wa kuanzishwa kwa Serikali ya Umoja wa Afrika, isipokuwa zinatofautiana kuhusu namna ya kufikia Serikali hiyo.

Amesema kuwawapo wanaotaka Serikali hiyo kuundwa mara moja, na wapo wanaotaka Serikali hiyo kufikiwa hatua kwa hatua.

Akifungua Mkutano wa Siku Mbili wa Kamati Maalum ya Wakuu wa Nchi 12 za AU (Committee of 12) kuhusu uundwaji wa Serikali hiyo leo katika Hoteli ya Ngurdoto, Arusha, Rais Kikwete amesema kuwa mwenendo mzima wa mjadala kuhusu Serikali hiyo unaonyesha kuwa kuna makubaliano ya jumla.

“Tunakubaliana kuhusu lengo kuu la kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Afrika. Tofauti pekee ya msingi ni kati ya wale wanaotaka kuundwa mara moja kwa Serikali hiyo na wala wanaotaka uundwaji wa Serikali hiyo uje hatua kwa hatua,” amesema Rais Kikwete.

Kwa sababu hiyo, amesema Rais Kikwete, ndiyo maana Kamati hiyo inayokutana Arusha inayo kazi kubwa ya kupata mwafaka wa jinsi ya kuwashauri wakuu wengine wa Afrika kuhusu jinsi ya kufikiwa kwa Serikali hiyo.

Mkutano huo unajadili ripoti ya Baraza la Utendaji la Mawaziri wa AU kuhusu uundwaji wa Serikali ya Afrika na kuhusu ripoti ya tathmini iliyofanywa kuhusu shughuli za AU ukiwamo muundo wa umoja huo.

Baraza hilo lilifanya kikao chake hivi karibuni mjini Arusha chini ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuandaa kikao kilichoanza leo.

Amesema Rais Kikwete: “Kazi iliyofanywa na Baraza la Utendaji itatusaidia, kwa njia nyingi, katika kufikia mapendekezo ambayo, ni matumaini yangu, kuwa yataunganisha mawazo ya pande hizo mbili na hivyo kupatikana kwa njia zitazouvusha Umoja wa Afrika kuwa Serikali ya Umoja endelevu na imara.”

Mbali na Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa mkutano huo, viongozi wengine wanaohudhuria ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Umaru Yarâ Adua wa Nigeria, Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi.

Nchi zinazowakilishwa na mawaziri wa nchi za nje ni Misri , Libya, Cameroun, Senegal, Botswana na Gabon. Ghana inawakilishwa na Mshauri Maalum wa Rais John Kuffour.

Mapema, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika, Jean Ping amesema kuwa ni muhimu kwa baadhi ya mapendekezo Baraza la Utendaji na kamati nyingine kukubaliwa na kikao cha sasa, ili kuweza kuiimarisha AU na hatimaye kuweza kufikia Serikali ya Afrika.


ombaomba matonya afungwa kwa kuomba

Na John Nditi, Morogoro

MAHAKAMA ya Mwanzo ya Nunge ya Manispaa ya Morogoro, imemhukumu omba omba maarufu Matonya Mazengo, kutumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka amri iliyomzuia kuendelea kufanya kazi ya kuomba mitaani.

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu, amethibitisha kuhukumiwa kwa Matonya baada ya kufikishwa Mahakamani na Idara hiyo Mei 19, mwaka huu baada ya kukiuka masharti aliyopewa ya kumtaka asiendelee na shughuli za kuomba omba katika mitaani ya Manispaa ya Morogoro.

“ Ni kweli alikamatwa na askari wa Mgambo wa Manispaa ya Morogoro na kuletwa kwetu sisi wa Idara ya Ustawi wa Jamii ili kupata ushauri wetu kwa kusudio la kumfikisha Mahakamani” alisema Ofisa huyo wa Mkoa wa Ustawi wa Jamii

Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro, Matoya awali alikamatwa na Askari wa Mgambo wa Manispaa mwishino mwa mwaka jana katika zoezi la kuwaondoa ombaomba mitaani na kutakiwa kujaza fomu ya kula kiapo cha kuacha kuomba mitaani na kubalia Kambi ya Wazee wasiojiweza ya Fungafunga ya Mjini hapa.

“ Matoya alikula kiapo cha kuacha kuomba na kurudishwa Mkoani Dodoma pia aliahidi endapo akirudi Morogoro ataishi katika Kambi ya Wazee wasiojiweza na iwapo atajihusisha na kuomba basi apelekwe Mahakamani afungwe jela” aliongeza kusema Ofisa huyo.

Kwa mujibu wa Ofisa huyo , Matonya aliamua kurudi tena Mkoani Morogoro mwanzoni mwa Mei mwaka huu na kuendelea kukaa eneo la daraja la Shani Cinema na kufanya shughuli za kuomba omba kwa staili ya kulala chali chini katika eneo hilo la Daraja.

Alisema kufuatia kuwepo kwake katika eneo hilo na kuendelea na kazi hiyo , alikamatwa na Askari wa Mgambo na kufikishwa katika Ofisi za Ustawi wa Jamii na baadaye kufikishwa Mahakamani.

Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa Idara ya Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Matoya amepelekwa katika Kambi ya Wazee wasiojiweza ya Funga Funga akisubili fedha za kumsafirisha kurudi makwao.

“ Hiki kifungo cha nje cha mwaka mmoja ni kuachakutembeea mitaani kwa kazi ya kuomba…tukizipata fedha kutoka Halmashauri ya Manispaa sisi Idara ya Ustawi wa Jamii kutamsafirisha kurudi nyumbani kwao Mkoani Dodoma” alisema Ngungamtitu

Kwa mujibu wa Ofisa huyo, ombaomba wengi waliorudishwa makwao wamerudi tena na kubadili mfumo wa uombaji wa kukaa barabarani ambapo kwa sasa wanapita katika maeneo ya Mahoteli, Baa na Migahawa wakiongozana kwa zamu kwa ajili ya kuwaomba wateja.

Hivyo kutokana na kushamiri kwa hali hiyo, Ofisa huyo ameushauri Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuchukua hatua kwa kuwaelekeza Askari wa Mgambo kuendesha msako katika maeneo hayo.


ali kiba in da house!!


AFTER A SUCCESSFUL WINTER SPLASH TOUR '08 FEATURING T.I.D.


BONGO FAMILY UK PRESENTS......


SPRING BREAK TOUR '08 (A BIG BANK HOLIDAY WEEKEND) FEATURING ALI KIBA (PICTURED ARRIVING IN LONDON TODAY) PERFORMING HIS HIT SINGLES SUCH AS CINDERELLA, NAKSHI NAKSHI, MREMBO


AND MANY MORE.....


THIS TIME WE ARE KICKING OFF FROM


SCOTLAND ON FRIDAY 23RD @ TIGER TIGER CLUB, GLASGOW


MANCHESTER SATURDAY 24TH @ AQUA BAR


BIRMINGHAM SUNDAY 25TH,


AND FINISHING UP


IN LONDON ON FRIDAY 30TH @ CLUB AFRIQUE


MORE INFO
WWW.BONGOUK.COM


kero ya usafiri gogolamboto


Ndugu michuzi, mimi ni miongoni mwa wapenzi wa blog hii. Tunaipenda kwasababu ni moja ya chombo kinachosaidia wanyonge, kwa kupata habari , na kutoa habari zao pia. Nami nimeona nitumie uwanja huu kutoa dukuduku letu sisi wananchi wa Gongolamboto na vitongoji vyake kuhusiana na swala zima la Usafiri.

Kipindi cha nyuma tulikuwa tukiwacheka `Mbagala’ kwa jinsi walivyokuwa wakisota kwa usafiri. Lakini kwao sasa hivi mabasi yapo mengi ila tu foleni ndio kikwazo kwao. Adha hii sasa hivi imeelekea kwetu wakazi wa Gongolamboto na vitongoji vyake.
Adha hizi zimezidi kwasababu eneo hili la Gongolamboto na vitongoji vyake limekuwa haraka sana. Wakazi wengi wamejenga huko, hivyo idadi ya wananchi ambao wengi wao ni wafanyabiashara, wafanyakazi na wanafunzi imekuwa kubwa kuliko huduma kama za usafiri.

Tatizo letu kubwa ni usafiri. Tunaamuka saa kumi ili tuweze kufika makazini kwetu, lakini cha ajabu unaweza ukasota ukajikuta unafika ofisini saa tatu, na unarejea nyumbani saa tatu za usiku (unaacha watoto wamelala unawakuta wamelala).

Magari mengi yaliyopangiwa huko hayakamilishi `ruti’ zao, mengi yanakatisha njia. Mfano, wengi wetu ambao tunaishi Kipunguni, au vijiji vya karibu inabidi tupande magari matatu au manne hadi makazini kwa wale wanaofanyia kazi maeneo kama Msasani, Mikocheni, na nauli zake ni shilingi 350, kwa kichwa. Baya zaidi ili upate gari inabidi upande kwa mtindo uitwao `geuza nalo’ yaani ulipe nauli mara mbili, kwa kwenda nalo, angalao mwendo kiasi halafu ugeuze nalo, hapo unalipa mara mbili ya nauli hiyo.

Jaribu kufikiria mwenyewe mishahara ilivyo, halafu kwa siku kwa wale tunaofanyia kazi Mikocheni tunatumia shilingi zaidi ya shilingi elifu mbili kwa usafiri tu, je watoto watakula nini, utalipia nini ada zao, je utapata wapi hela yao ya matibabu ! Mwajiri hajui wala hajali kuhusu matatizo haya.

Tunaomba vyombo vinavyohusika waangaze eneo hili, watusaidie na sisi.
Barabara ziendazo vitongojini ni mbovu ajabu (Pitia Mombasa kwenda Kipunguni utaona mwenyewe, na kwingineko). Wale waliojisajili kusafirisha abiria maeneo haya kama hawawezi waseme, wapewe watu wengine. Yawepo magari ya moja kwa moja kutoka vitongojini hadi mijini, Kariakoo, Posta, Mwenge na kwingineko, kuliko kupanda magari mengi tofauti. Asubuhi na jioni matrafiki waangalie sana hawa madereva wanaokatisha njia.

Tunategemea mabadiliko ya haraka ili na sisi tufike ofisini tukiwa hatujachoka kwa sababu ya usafiri, kwani ni heri ya kwenda Morogoro unaweza ukafika mapema ukiwa na nguvu zako kuliko usafiri wa Gongolamboto.

Mimi Mdau wa Kipinguni.


Nyota wanaowania tuzo za filamu bongo


Msemaji wa One Game Promotion, Khadija Kalili, akionyesha moja ya tuzo zitakazokadhiwa kwa washindi wa 'Tuzo za Vinara wa Filamu' nchini, zinazotarajiwa kufanyika Mei 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Kulia ni moja wa majaji wa tuzo hizo, Beda Msimbe.
Na Anastazia Anyimike


WASANII nyota kwenye fani ya filamu wameshindwa kuchaguliwa kwenye kinyang'aniro cha tuzo za Vinara huku msanii Single Mtambalike akionekana kutajwa katika vipengele vitatu.

Mtambalike ambaye anajulikana kama Richie amependekezwa kuwania tuzo za mwigizaji bora wa kiume kutokana na filamu ya Agano la Urithi, mtunzi bora msaidizi na mwigizaji bora msaidizi kutokana na filamu ya The Stranger.

Akitangaza majina na filamu hizo, Makamu Mwenyekiti wa jopo la majaji, Cuthbert Kabunga alisema kuwa filamu 20 kati za 70 zilizoshiriki kwenye tuzo hizo zimechagukuliwa kuwa bora.

Alizitaja filamu hizo kuwa ni Agano la Urithi, Behind the Scene, Copy, Crying silently, Diversion of Love, Fake Pastors, Fungu la Kukosa, Karibu Paradiso, Mzimu wa Kolelo, Macho Mekundu, Malipo ya Usaliti, Miss Bongo2, Misukosuko 2, May Sister, Sengito, Silent Killer na Simu ya kifo.

Wanaowania tuzo ya Mwigizaji bora wa kike na filamu zao walizoigiza zikiwa kwenye mabano ni Lucy Komba (Diversion Of Love), Grace Michael (Malipo ya Usaliti), Halima Yahya (The Stranger), Elizabeth Chijumba (Copy), Riyama Ally 'Serena'(Fungu la Kukosa) wakati kwa wanaume ni Mtambalike (Agano la Urithi), Nurdin Mohamed "Chekibudi' (Utata), Jacob Steven (Copy), Haji Adam 'baba Haji' (Miss Bongo) na Yussuf Mlela (Diversion Of Love).

Muigizaji chipukizi wa kike ni Irene James (Miss Bongo II), Irene Uwoya (Diversion Of Love), Fatuma Makame (Karibu Paradiso), Jennifer Mwaipaja 'Shumileta' (Silent Killer), Grace Michael (Malipo ya Usaliti) wakati kwa upande wa wanaume ni Emmanuel Muyamba (Fake Pastors), Laurent Anthony (Karibu Paradiso), Hassan Nguleni (Body Guard), Yussuf Mlela (Diversion Of Love) na Uswege (Malipo ya Usaliti).

Muigizaji msaidizi wa kike ni Irene Uwoya (Diversion Of Love), Mama Frank (Yolanda), Irene James (Miss Bongo II), Susan Lewis 'Natasha' (Behind the Scene) na Tecla Mjata 'mama bishanga'(Macho Mekundu) wakati kwa wanaume ni Aliko Tshmwala (Segito), Mtambalike (The Stranger), Adam Kuambiana (Fake Pastors), Halfan Ahmed (Copy) na Emmanuel Muyamba (Fake Pastors)

Wanaowania tuzo ya mwongozaji bora ni Gervas Kasiga (Fake Pastors), Jimmy Mponda (Misukosuko II), Kulwa Kikumba 'Dude' (Macho Mekundu), Haji Adam (The Stranger), Halfan Ahmed (Copy) wakati Mtunza Sauti Bora ni Adam Waziri (Fungu la Kukosa), Cleophance Ng'atingwa (Kolelo), David Sagala (Copy), Camillius Kanuli (Fake Pastors), Swalehe Juma (Fungu la Kukosa).


Tuzo zingine zinazowaniwa ni Mpiga picha bora wa Filamu, Adui bora wa Filamu, Mhariri bora wa Filamu, Mwandishi bora wa Filamu, Mapambo na Maleba bora, Mtunzi bora wa Filamu wakati filamu zinazowania tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka ni Behind the Scene, The Stranger, Diversion Of Love, Macho Mekundu, Misukosuko II, Simu ya Kifo, Copy, My Sister, Silent Killer, Miss Bongo I, Agano la Urithi, Malipo ya Usaliti, Utata, Kilio Moyoni (Crying Silently) na Fake Pastors.


layan ngorongoro crater leo

katika pitapita zetu ngorongoro crater leo tumekutana na jamaa huyu wa mtaa wa msimbazi...


ngorongoro

wadau msione kwikwi ya libeneke kuwa nyingi. niko nanihii nikinanihii. hawa wadau wanatoka nigeria, niko nao huku sehemu sehemu. wenyewe wamebrooo. wanasema bongo noma kwa vivutio!


KLH Exclusive: Safari ya Mwisho ya Balali

Mwili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Daud Timoth Said Ballali (65) aliyefariki Ijumaa iliyopita umehifadhiwa katika Nyumba ya Maziko ya De Vol iliyoko mjini Washington DC, nchini Marekani ambako inasubiri mazishi siku ya Ijumaa.

Taratibu za ibada na mazishi ambazo KLHN imepata nafasi ya kuziona inaonesha kuwa Gavana Balali alifariki tarehe 16 hapo Washington DC na atazikwa hapo hapo siku ya Ijumaa. Misa ya kumwombea Marehemu itafanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Stephen Shahidi mjini Washington DC anuani yake ni ST. STEPHEN MARTYR CHURCH 2436 Pennsylvania Ave, NW Washington, DC 20037.

Ibada hiyo ya mazishi itaenda sambamba na kuuona mwili wa Marehemu kuanzia saa nne asubuhi. Hata hivyo shughuli hiyo nzima ni kwa ndugu, jamaa, na marafiki wa karibu na si kwa hadhara ya kila mtu atakaye kushiriki. Marehemu atalazwa katika makaburi ya Wakatoliki ya Gate of Heaven eneo la Silver Spring, MD.

Hata hivyo haijajulikana kwa uhakika kama mwili wa marehemu utazikwa ardhini kama ilivyo desturi ya kiafrika au utateketezwa kwa moto kwani makaburi hayo yanatoa huduma hiyo pia. Kama ulikuwa ni usia wake kuteketezwa basi kwa kanuni za Kanisa Katoliki basi itafanyika mara tu baada ya ibada.
Kwa kanuni za Kanisa Katoliki mwili uliolazwa kwa njia ya kuteketezwa kwa moto mabaki yake (majivu) hawapewi familia, kusambazwa au kugawanywa katika mafungu madogomadogo na badala yake ni lazima viwekwe ardhini au kwenye sehemu maalumu inayotumika kwa maziko ya namna hiyo.

Dr. Ballali ambaye amefariki akiwa amezungukwa na wingu kubwa la kashfa dhidi yake na dhidi ya taasisi aliyoingoza inasemakana aliacha usia uliotaka atakapofariki basi azikwe Marekani. Hata hivyo pamoja na kashfa nyingi zilizoandikwa na vyombo mbalimbali vya magazeti na kutangazwa majukwaani Bw. Ballali hakuwa mtuhumiwa yeyote na hakukuwa na kesi yoyote ile ya kihalifu dhidi yake na hivyo amekufa kama raia na mtu huru.

Hata hivyo Dr. Balali ilidaiwa kuwa aliandika barua ya kutaka kujiuzulu kutokana na hali mbaya ya kiafya uamuzi ambao haukujibiwa hadi pale taarifa ya uchunguzi wa EPA ilipotoka na Rais Kikwete kutengua uteuzi wake kama Gavana wa Benki Kuu.
Hata hivyo, taarifa ya Rais iliyosomwa na Katibu Mkuu kiongozi haikusema kama Gov. Ballali ni mhalifu, anatafutwa, au kwa namna yoyote ile amefanya makosa ya kisheria. Hilo lilithibitishwa siku chache zilizopita ambapo Ikulu walitangaza kuwa walikuwa hawamtafuti Ballali na ya kuwa kokote alikokuweko alikuwa ni “mtu huru”.

Ni kwa sababu hiyo basi ibada ya mazishi inatarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiongozwa na Balozi wa Tanzani nchini Marekani Bw. Ombeni Sefue, watumishi wa idara mbalimbali alizowahi kuzitumikia ikiwemo IMF, ndugu zake ambao wamewasili siku chache zilizopita, na baadhi ya Watanzania kadhaa waishio maeneo ya Washington DC. Gavana Ballali ameacha mke na familia.

Raha ya milele umpe ee Bwana
Na mwanga wa milele umuangazie
Apumzike kwa amani.
Amina.


wabongo watamba mysore

Vijana wa Kitanzania wameonyesha uwezo wa juu kisoka hapa Mysore kiasi cha kwamba hawana mpinzani kabisa.

kukiwa na baadhi ambao wamesajiliwa kwenye timu chache za hapa,vijana hao wameweza kuwafunga Wasudan jumla ya mabao 5-2 katika mechi iliyochezwa tar 18/5/2008,wafungaji nia Abdilah Amour pia alikuwa nyota wa mchezo na alifunga magoli mawili,Wilbard Mkoba goli moja,Walter Joseph Mbwiliza alifunga goli moja na Hamad Changale.


wanyiramba kukutana dar jumamosi

Kutakuwa na kikao cha Wanyiramba wote waishio Dar Es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 24.05.2008 saa 9.00 mchana Msimbazi Centre.
Aonaye tangazo hili amtaarifu na mwenzake.
Tafadhali tuwahi bila kukosa.
Adam
Katibu wa UKWAMI


nyama choma a-taun

ukisikia mdau kahamia a-taun kimoja usishangae...


ndio gemu hiyo...

keki maalumu iliyotengenezwa na wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa africa travel association unaomalizika ijumaa hapa a-taun katika kudhimisha siku ya gemu. mliobenjuliwa poleni na mlioshinda hongera zenu. ila dah! nyie mlioshinda fundi wenu noma... besela mara tatu???? mani yuuu mnatisha!


kaburi la bandaHellow Mr. Michuzi,


nadhani u mzima. Ingawa siyo mdau wa Blog yako ila ni mfuatiliaji , msomaji na mpenzi mzuri sana wa blog hii. Sielewi sifa za kuwa mdau lakini tuyaache hayo ila nakutumia picha alipozikwa Rais wa Malawi Kamuzu Banda. Sijui ni kiasi gani cha fedha kilitumika kujenga kaburi hilo ila kweli wamalawi wameamua kumuenzi kiongozi wao huyo. Pamoja na yote sehemu hiyo ya kaburi imekuwa ni kivutio kikubwa kwa watalii wengi wafikapo huko malawi. Nami nilibahatika kufika huko kama mtalii wa kibongo. Sijui Baba yetu wa taifa alizikwa vipi ila naomba kama itawezekana tuwekee picha ya sehemu alipozikwa na kama ilishawahi kuwekwa tafadhali nijuze ni tarehe gani uliweka. Maana wengine hatujawahi fika butihama.

Kazi njema.


BALALI KUZIKWA IJUMAA MAREKANI


ALIYEKUWA GAVANA WA BENKI KUU DAUDI BALALI (PICHANI) AMBAYE ALIFARIKI DUNIA SIKU MBILI ZILIZOPITA HUKO BOSTON, MAREKANI, ANATARAJIWA KUZIKWA SIKU YA IJUMAA HUKO HUKO BOSTON.


HABARI ZA UHAKIKA KUTOKA MAREKANI NA NDANI YA BENKI KUU AMBAKO TAYARI MSIBA HUU MZITO UMETANGAZWA RASMI SASA HIVI, ZINASEMA HAYATI BALALI ALIFARIKI BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MREFU.

MUDA NA MAHALI ATAPOZIKWA TUTAJULISHANA BAADAYE KIDOGO....


msaada tutani

Hello Kaka Michuzi,
Habari yako. Naomba msaada. Naomba unitangazie kwa blog yako huyu mtu anaitwa Aston Kabeta (Tonny Kabeta).
Nina ujumbe wake muhimu sana. Number ya simu aliyotoa ni +1 267- 230 - 3999. Tumejaribu kupiga hiyo simu na anayepokea simu katika number hii hamjui huyu Tonny au Aston Naomba tafadhali uniwekee jamani hii ili kama kuna mtu anamfahamu au yeye mwenyewe akiona basi awasiliane na mimi. Nina ujumbe wake muhimu sana.
Asante sana na Mungu akuengezee kwa kazi hii unayofanya
Sara


balali

wadau kunradhi,

habari za aliyekuwa gavana wa benki kuu mh. balali nimezipata toka jana, ila bado sijazithibitisha, ingawa vyombo kadhaa vimerusha. tutapashana mara mambo yatapokuwa tayari.


kinga

nimefurahi kukuta mambo haya kwenye vyoo vingi vya ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa aicc, kuonesha kuwa wanaafiki kwamba kinga ni bora kuliko tiba. na hii siyo kwa nanihii tu bali pia hata fegi. huu ni mfano wa kuigwa, mnasemaje wadau - hala hala waosha vinywa msianze... huo mkono si wangu.....


rugimbana na mfugale

wadau rugimbana (shoto) na mfugale wakiwa a-taun kwenye mkutano wa utalii. rugimbana ni mmoja wa wadau wakubwa wa sekta ya utalii na pia alikuwa kiongozi wa mchezo wa lawn tennis kwa miaka kibao wakati mfugale ndiye bosi wa hoteli za peacock


MKOMBOZI WA NAMBA ZA SIMU

NATUMAINI KILA MTU ANAFAHAMU ADHA ANAYOIPATA PALE ANAPO POTEZA SIMU UKWELI KIKUBWA KINACHOUMANI NAMBA ZAKO ZA SIMU ZINAKUWA NYINGI ZIMEPOTEA.
LEO HII KUNA VIFAA AMBAVYO UNAWEZA KUWEKA NAMBA ZAKO ZA SIMU 1000 NA KUKIHIFADHI NYUMBANI. CHOMBO HIKI KINA UWEZO WA KUCOPY NAMBA ZAKO ZILIZOKO KWENYE SIM CARD YAKO NAKUZIHIFADHI.
PIA KUKUONYESHA JINA NA NAMBA WAKATI UNAPOHITAJI KWA HARAKA.NIKITU AMBACHO KILA MMOJA WETU NAFIKIRI ANAKIHITAJI.
WASILIANA NASI KATIKA NO ZILIZOTAJWA HAPO JUU BEI NI NAFUU SANAAA PIA UNAWEZA KUPIGA NO 0712404044 KWA MAELEZO.
MDAU MKOMBOZI


uso-kwa-uso na maprofesa

leo nimepata bahati ya kugongana uso-bin-uso na profesa pius z. yanda ambaye ni mmoja wa wasomi waliokuwa kwenye jopo la utafiti wa athari za mazingira duniani liliopelekea makamu wa rais wa marekani al gore kupokea tuzo ya nobel. profesa yanda, pamoja na kuwa pia mkurugenzi wa taasisi ya institute of resource assessment (www.ira.udsn.tz) ya udsm pia ni mkurugenzi wa afrika wa the pan african start secretariat (http://pass-africa.org)

niko na profesa wa uchumi, yaw nyarko, wa chuo kikuu cha new york university (http://www.nyarko.com/) cha marekani ambaye pia yupo a-taun kumwaga pepa katika mkutano wa kimataifa wa africa travel association juu ya hali ya uchumi katika sekta ya utalii na safari duniani
jk alipotembelea afrika sana

jk akiangalia nguo za kitamaduni katika banda la maonyesho la afrika sana siku alipofungua mkutano wa kimataifa wa utalii na safari wa africa travel association (ata) a-taun jana. mkurugenzi wa afrika sana mwafrika merinyo yuko pembeni akifurahia ugeni huo


kumbukumbu ya mv bukoba

mnara wa kumbukumbu ya ajali ya mv bukoba uliojengwa maeneo ya bwiru, mwanza
mdau miriam makalla wa chuo kikuu mtakatifu agostino huko nyegezai mwanza katutumia picha hizi kutukumbusha waliopoteza maisha katika ajali ya mv bukoba iliyotokea miaka takriban 12 iliyopita


vazi la taifa

hili ni vazi la kitaifa kwa kinamama


wapi hapa

kwa kukusaidia hii sehemu ipo dar, na sio a-taun...


simba


kwenye ukumbi wa simba katika aicc kuna bonge la simba mlangoni. halafu wala haumi...