Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Ruth Mollel (kulia) na Katibu Mkuu Afisi ya Waziri Kiongozi Zanzibar Bw. Ali Rajab wakiongoza kikao cha Makatibu wakuu wa pande mbili za Muungano kujadili kero za Muungano leo, katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.(Picha na Ali Meja)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Vikao vya kero za muungano ni geresha na usanii wa kisiasa tu. Hakuna kero itakayoondoka.Hasa ukizingatia kuwa hizo kero baada ya kupungua zinaongezeka.

    Kwa bahati mbaya wenzetu wa Tanganyika ndio waliozitengeneza hizo kero kwa makusudi ya kutubana Wazanzibari. Sasa iweje leo wawe na moyo thabit wa kuzitatua kero walizozifanya kwa maksudi.

    Hivi ni vikao vya kuwapatia pesa hao wanaohudhiria tu kwa maoni yangu.Mnasemaje wadau wengine?

    Mdau

    ReplyDelete
  2. Hapo kinaochoonekana ni kama mdau hapo juu alivyosema ni kupata posho ya kikao tu. Hao wote waliohudhuria hapo hawana ubavu wa kufanya lolote kwani kila mmoja amekuja na mapendekezo toka kwa mkubwa wake na akienda kinyume ni kukosa kazi.

    Kero zijadiliwe na bunge la muungano kwani ndilo lenye wawakilishi wa wananchi toka bara na visawani ni hawa watendaji ambao hawana constitutional power ya kubadili katiba. Kwani kero za muungano ni za kikatiba, kama katiba inakuwa ni ya wananchi na wao wanaikubali hakuna kero tena hapo.

    Ila haya mambo ya ku- impose mambo kwa wananchi yenye mlengo wa kulifanya kundi fulani kuendelea kupata ulaji ndiyo yanayozua kero tena kwa wao wenyewe si kwa sisi kwani wao ndiyo wanagombania nani anakula sana wala si wananchi wa Nungwi au Tandahimba

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha sana kuona mtu anakuwa ni wakulaumu tu bila hata kujua linalozungumziwa. Hata hivi karibuni ktk mkutano ulioitwa na MUWAZA wanaojidai kujaribu kujenga umoja wa Wazanzibari hamkuhudhuria. Sasa wewe unataka nini? Unakalia kulaumu tuuuu. Shame!!! Jifunze kukubali kuwa serikali haina sababu ya kufanya geresha kwa kuwa ni kwa manuafaa yake kutataua matatizo ya muungano na yale yote yanayorudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu. Kwanza jivunie muungano halafu ukubali kutoa ushauri wa kujenga si kubomoa. Naona siku hizi serikali irejeshe jeshi la kujenga taifa. Vijana wetu hawana uzalendo kabisa kwa sababu wengi hawajui tulikotoka ndiyo maana wengine wamediriki kusheherekea sikukuu ya uhuru bandia wa Zanzibar. Kweli kijana anayejua maana ya uhuru atasheherekea siku ambayo Mkoloni alithubutu tena mbele ya halaiki ya watu wakiwepo wazee wentu viongozi wazalendo kumkabidhi sultani hati ya uhuru?? Ujinga ni kitu kibaya na kwa kweli badala ya kumwita mtu mjinga kwanza mwonyeshe elimu ili aweze mwenyewe kujitambua na ndiyo maana tunahitaji Natinal Service irudi. Vijana wetu wanapotea.!!!

    ReplyDelete
  4. vikao vyote hivi ni kupoteza pesa na wakati hakuna jipya litakalotokea, sote tunajua outcome haitokuja kuwa muungano sio halali au muungano na uvunjike.

    ReplyDelete
  5. Born Again Pagan anasema:

    Wa-Zanzibari wameishawaambia wa-Tanganyika, sisi ni nchi kama yenu. Tunataka Zanzibar yetu. Kwani serikali ya Tanganyika imegeuzwa kuwa sasa ndio Muungano!

    Kuna wakati Mwalimu Nyerere alitetea ya kutopendelea serikali ya Tanganyika, serikali ya Zanzibar na serikali ya Muungano!

    Nyerere alikosea aliposema kuwa "moja ongeza moja ni mbili na wala si tatu".

    Kwahiyo, Nyerere kakataa ya serikali tatu!

    Nyerere kakosea kweli! Zanzibar na Tanganyika sio solid matters, ni mithili ya liquids au fluids!

    Ukichukua tone moja kubwa la Tanganyika na ukaongeza tone dogo la Zanzibar, huwezi kupata matone mawili; utapata tone moja tu, tena kubwa zaidi (volume, weight, size, mass) !

    Na wala hayakumwingia akilini Mwalimu Nyerere wakati anachanganya mchanga wa vibuyu vya Tanganyika na Zanzibar, pale Mnazi Mmoja na kuuweka ndani ya bakuli!

    Hakupata mabakuli mawili; alipata bakuli imoja!

    Nchi mbili zikiungana zinafanya nchi moja kubwa na wala sio nchi mbili!

    Hata hiyo Biblia imetafsiriwa ikitaja kuwa kuna Mungu mmoja tu - ingawa kuna Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu - na kukiita Utatu Mtakatifu! Ni sawa na kusema moja ongeza moja ongeza moja ni moja!

    Hata ndoa ya ki-Kristu (Biblia) inasema moja ongeza moja ni moja! Mke na mme wataunganika na kuwa mwili mmoja!

    La sivyo, kama wakiendelea kujifikiria kuwa moja ongeza moja ni mbili, basi mafarakano yataanza kuelekea kutengana na hatimaye ndoa kuvunjika na kubaki moja ongeza moja ni mbili!

    Hata katika hali ya kawaida ya urafiki, kama kuna marafiki wawili, basi urafiki huo ni moja ongeza moja ni moja! La sivyo, mmoja akianza kumsengenya mwenzake, basi huo si urafiki ni moja ongeza moja ni mbili!


    Timu ya soka ya upande mmoja ni wachezaji 11 ambao huchangia kucheza, kama timu moja !

    Are you getting it ?

    Tamati, kama Muungano wetu una maana yeyote, basi Zanzibar iingie kikamilifu na Tanganyika iingie kikamilifu bila kujali idadi ya watu au ukubwa wa eneo kwa kila nchi!

    La sivyo, vunja huo Muungano!

    ReplyDelete
  6. halafu ukiona mtu kuanza kukandia mambo ya usultani ujue kanyweshwa siasa za ufisadi.
    kuna ishu nyingi tu zimefanyika wakati wa mapinduzi na kwa hakika waliofanya dhambi hizo wengi wao tayari wameshafariki wanalipwa kwa walioyafanya na mola mtukufu...bora nyamaza brother..mtu huwezi kumwambia aenzi mapinduzi sijui uhuru wakati mzee wake ameuliwa bila sababu wakati wa mapinduzi na kumuacha akitaabika kukosa huduma muhimu kama uwezo wa kusoma wakati mzee ameuliwa..halafu kwa vile hana qualification ya kumuingiza kazi nzuri unamlaumu kwa kukosa elimu..
    tunawaona waliofaidika na mapinduzi saivi wako wapi(mfano mzuri ni amani karume na washkaji zake)wametengezewa maisha bora na sasa ndio viongozi..watakubali vipi kua muungano una kasoro hao wakati kupitia huo huo muungano ndo siku za uchaguzi huwa wanapewa jeshi na SIRI KALI ya ufisadi TANGANYIKA kuja kulindwa wasitolewe madarakani hata wakishindwa michaguzi hata ikibidi kwa kuuwa raia?
    kwa hakika kama mchangiaji mmoja hapo juu alivosema hizi kero za muungano huwa zinaongezeka kila siku na si kupungua..hivo vikao ni vya kujipatia marupurupu tu..shame!!
    logically tulitakiwa tuwaone maraisi wawili hapo pia wapo kuonyesha umuhimu wa topic yenyewe lakini kwa vile wanazarau na kutolipa umuhimu jambo lenyewe ndio ukaona hao makatibu wameekwa hapo si ajabu ukakuta wanajadili kupandishiwa mishahara na mafao baada ya kustaafu!
    huu muungano wa tanganyika na zbar ni usanii tu na ni changa la macho kabisa kabisa..
    na kama kitu hakina faida kina kero tu kwa nini kisiondoshwe???

    ReplyDelete
  7. NAUNGANA NA MCHANGIAJI WA TATU KWAMBA ZAMANI WATU WALIKUWA NA UDUGU, UKOMREDI, UZALENDO NA KUPENDANA, NA KUJIVUNIA UTANZANIA, MIMI NIMEKULIA NYAKATI HIZO NAWEZA KUSEMA KATIKATI NA MWISHONI MWISHONI WA NYAKATI HIZO, NILISOMA HADI FORM SIX BURE TENA MIKOA YA MBALI NA KWETU TUKICHANGANYIKANA NA MAKABILA MBALIMBALI NA WATU TUSIOJUANA TUKAJENGA UJAMAA NA URAFIKI, TUKAOELEA. TUKIFUNDISHWA SIASA MASHULENI, NILIAJIRIWA NA KUSOMESHWA NA MWAJIRI WANGU BURE, AMBAYE ALIKUWA NI MTOTO WA SERIKALI. TULIENDA JKT KUJITOLEA NA KUJIFUNZA MAISHA YA KAWAIDA YA WATANZANIA WOTE TUKICHANGANYIKANA NA WATU WALIOSOMA NA WASIOSOMA TUKIWA KAMA KITU KIMOJA TUKIJIFUNZA MAMBO YA NCHI YETU NA TUKIJIVUNIA MUUNGANO KWELI KWELI. KWA KWELI HALI ILIKUWA SAFI NA NZURI. MAMBO YAMEBADILIKA HIVI KARIBUNI BAADA TU YA MWALIMU KUACHIA UONGOZIWATU WATU WAKAANZA KULIMBIKIZA MALI, UBINAFSI NA UDINI KWA KASI KUBWA SANA NA KUWAACHA MASIKINI NA WASIO NA WATU SERIKALINI KUTESEKA NA HAPO NDIPO UKAWA MWANZO WA WATU KUKOSA UZALENDO KWA VILE HAWAFAIDIKI NA NCHI YAO WAKIISHI KWA SHIDA NA WAKIKODOLEA MACHO WACHACHE WANAOFAIDIKA, AMBAO NI WAKUBWA SERIKALINI. HAWA WATU WANAJUWA JINSI YA KUSAIDIA WATU NA KUWAUNGANISHA KIMAENDELEO LAKINI HAWATAKI KWA MAKUSUDI MAZIMA ILI KUTANUA UFA ULIOPO WA UTAJIRI NA UMASIKINI ILI WAENDELEE KUABUDIWA KWANI TUKIWA SAWA HAWATA-ENJOY, WANAFURAHI SANA WANAPOONA WANAABUDIWA NA MASIKINI AMBAO KILA KUKICHA HAWAJUWI WATAKULA NINI NEXT SECOND, NOT NEXT DAY NA WAO WAKIISHI KAMA WAKO PEPONI. KUNA NCHI KIBAO ZINATOA MISAADA KWA WATANZANIA YA KIELIMU KUPITIA SERIKALINI AMA KWENYE MASHIRIKA YA DINI LAKINI WANOKWENDA HUKU NI WATOTO WA WAKUBWA SERIKALINI HUWA VITU KAMAHIVYO HAVIWEKWI WAZI, NENDA CHINA, MALAYSIA, USA, CANADA NAKWINGENEKO UTAWAKUTA WATOTO WA WAKUBWA HUKO KIBAO WAKISOMA KWA SCHOLARSHIPS. ILI TUJENGE NCHI NA UMOJA NA UPENDA TUNATAKIWA KUSAIDIANA KUUPIGA VITA UMASIKINI KWA KILE KIDOGO TUPATACHO, TUAMBIZANI MBINU ZA KUPATA ELIMU ILI TUUANGAMIZA UMASIKINI. TUNATAKIWA KUJENGA UZALENDO WOTE KWA PAMOJA SI WALALAHOI TU NDIO WATAKIWE KUJENGA UZALENDO.

    ReplyDelete
  8. Mdau wa 3 hapo juu...umemalizia vizuri ila hiyo hoja yako uliyoanza nayo ya kuunda umoja wa Wazanzibaria ilisha anza kunichefua. Sijui upo nchi gani lakini hapa UK kuna hizo "Umoja" za Wazanzibari tatu au zaidi wote hakuna wanachofanya zaidi ya kusubiri mialika ya kwenda kula wali na mabalozi au kukaa meza kubwa wakija viongozi wa kitaifa.

    Been there done that, watanzania hasa UK ni wazito na wavivu wa kufikiri kupita kiasi hawawezi kuwa na umoja wowote wenye akili....Balozi Maajar alijaribu.

    ReplyDelete
  9. Ndugu yangu Kipili. Ili bunge liweze kujadili jambo ni lazima litayarishwe na watendaji. Wewe unakalia kulaumu kuwa ni watu wanatafuta posho na ni watu wanataka kuendeleza ulaji wa kundi moja. Ni dhambi kutoa shutuma ambazo ni za hisia tu. Kweli zipo kero za muungano na kweli ni muhimu kabisa zijadiliwe na wahusika. Hapa ndugu yetu Issa Michuzi katupa mahala pa kutoa maoni. Basi tutoe maoni yenye nguvu ya hoja si hoja ya nguvu au shutuma zisizo za msingi. Muungano wowte unaweza kuwa na matatizo na si jambo la ajabu. Muhimu ni kuwa kwanza na mtizamo wa kuujenga muungano na tuangalie jinsi ya kufanya hivyo kwa kuondoa kero. Lakini ukianza na lawama kuwa yule kala zaidi, oooh yule anatafuna nchi, oooh yule Mtanganyika, yule Mzanzibari au Mzanzibara, oooh yule Mpemba... hatufiki ndugu yangu.

    ReplyDelete
  10. Hivi hawa wazee kweli hawajatimiza miaka 60? inaelekea ndiyo sababu tunashindwa kufikia muafaka

    ReplyDelete
  11. KWA TANZANIA BARA:
    Kero za muungano hazitomaliza, wazanzibar wataendelea kupiga zogo maadamu wanaiona vipi serikali ya muungano inaibana serikali ya zanzibar, kampuni ya zantel ilikataliwa kufunguliwa bara au ilibidi ihamie uko. mwaka 2001 pemba waliuliwa watu zaidi ya 1oo (ingawa serikali ilidai 40) na jeshi kutoka bara, nambie mtu gani atakaefurahi akiona watu wake wanauliwa km kuku kama si kibaraka huyo, (amani karume).

    KWA WAZANZIBAR
    ikiwa wazanzibar wenyewe kwa wenyewe wanasema yule mpemba yule muunguja, hususan waunguja kuwaita wenzao wapemba na wao wazanzibar wa kweli, sasa mtu mwengine asiyekua mzanzibar watasemaje?, mwaka jana wapemba walitaka kuwa na nchi yao kwasababu washachoshwa na viongozi wa kizanzibar, wanasahau kabisa kama pemba ni sehemu ya zanzibar ingawa mapato yao makubwa yanatokea hukohuko pemba, karafuu, na saivi waunguja wanasema karafuu ishapitwa na wakati hatutegemei tena karafuu, tujaalie ni kweli, na huo muda wote serikali ilipokua inatumia pesa za karafuu wamesahau!, zanzibar ilikua inazalisha 45% ya karafuu duniani kipindi hicho wanachosema kulikua na mkoloni ambae hana jema alilolifanya (kwa fikira za wazanzibar wa sasa baada ya kujazwa sumu), sasa nchi iko mikononi mwa tunawaona wazalendo zanzibar inazalisha 7% tu. jambo jengine hao zanzibar wakijitoa kwenye muungano wataweza kujiongoza?, viongozi wenyewe wamemaliza form 4.

    kwa kumalizia mimi naona uo muungano ue basi,ni kheri kwa nchi zote mbili, lakni hata kama itatokea hivo basi ni vizuri kuwa na uhusiano mzuri tu

    ReplyDelete
  12. Wachangiaji, baadhi wameonyesha mashaka juu ya vikao kama hivi na kusema kuwa ni va kula tu fedha. Kuna sababu ya kusema hivo; wameshaona sehemu nyingi jinsi watendaji wetu wanavyojipa tu posho na hamna kinachofanikiwa.

    Lakini, kwa tunaowaona kwenye picha hapo juu, naomba nami nichangie kuwa si tu wala posho. Kama alivosema mjumbe mmoja, kabla swala halijaenda Bunge huwa wapo walioshauri liende huko. Nakubali kabisa, na wadau waliokaa hapo juu ni watendaji wa serikali, wanaokaa kabla hatujatupiwa sisi wananchi au wabunge wetu.

    Niwape imani, kwa waliosoma UDSM, au wanaoishi Tanzania, mmepata kumsikia distinguished profesa Haroub Othman, kama miongoni mwa wana harakati wazuri sana nchini mwetu hasa kwenye taaluma ya Uraia pale Mlimani, ukiacha akina prof. Issa Shivji wa sheria. Basi, hapo juu wamekaa Prof. Othman na prof. Saida-Othman (ke wake) kama wataalamu (naamini) kusaidia mjadala wa makatibu wakuu. Prof Othman na mke wake ni wa asili ya Zanzibar, na wameshirikishwa sana kwenye mijadala mikubwa kama hii sababu ya uzoefu wao. Mwaka 2001 au 2002 nakumbuka huyo mwanamama aliongoza kikao cha "HALI YA SIASA NCHINI TZ" akikaimu kiti baada ya rais Mkapa (wakati huo) kufungua. Aliendesha mjadala akiwa na akina Tendwa, Lipumba, Mrema, nk, nk, unawataja wote waliobobea kwenye mambo ya siasa, uongozi, na taaluma ya siasa kwa jumla.

    Pia, Othmans wamekuwa na uzoefu mkubwa kwenye shirika la UN. Mzee Othman alikuwa mshauri kwenye mambo ya amani nchini Liberia au Siera Leone kwa muda mrefu, kama wajibu wa UN, kabla ya kuja kufundisha UDSM.

    Finally, I really miss waalimu wa UDSM hasa waliotufunua macho kwenye DEVELOPMENT STUDIES. Hakuna kkozi kama ile. Nimesoma baadaye huku nje sijasikia kozi kama ile inayotolewa kwa wanachuo wote bila kujali wanasomea nini. Ni nzuri sana. Ninafkiri hata nje huku wakijifunza wataona uzuri wa Development Studies (the content), names don't really matter. You can call it anything, afterall.

    NOTE:
    Watu wa mtazamo kama wa BAP ni hatari sana kwenye mazingira ya sasa, hasa kwa wanaofikiria positively kuwaweka Watz kuwa kitu kimoja. Anasema Wazanzibar walisema hawataki muungano, ni utafiti au sensa ipi hiyo ilionyesha? Au tunasikiliza wenye power in the media kama viongozi wao wa Siasa Zanzibar?

    Mdau,

    USA

    ReplyDelete
  13. Kutoka kwa Born Again Pagan kwa “NOTE” ya Mdau , USA:

    Moja, Mdau anaaandika, “Watu wa mtazamo kama wa BAP ni hatari sana kwenye mazingira ya sasa, hasa kwa wanaofikiria positively kuwaweka Watz kuwa kitu kimoja.”

    Nasikitika mimi si “hatari sana kwenye mazingira ya sasa, hasa kwa wanaofikiria positively kuwaweka Watz kuwa kitu kimoja.” Labda wengine unaowajua. Ningependa sana kupata orodha ya watu hao “hatari”.

    Nilizingatia, ki-nadharia, kwamba katika mikitadha ya kuuunganisha nchi mbili, moja ongeza moja ni moja, kamwe haiwezi kuwa mbili, kama Mwalimu Nyerere alivyotamati, ki-mantiki.

    Hatuna budi kutafuta njia nyingine mbadala ua kuwaunganisha watu wa “Tanganyika” na “Zanzibar” kuliko haya ya Muungano wa kuweka viraka!

    Naunga mkono ya Muungano, si kwa Tanzania tu bali pia kwa Afrika Mashariki na Afrika! Naunga mkono Muungano wa Tanzania; lakini si kwa “ariticles” zilizouzalisha mwaka 1964! Lakini kama tutaingia “muungano”, kama ulivyo hivi sasa, kasoro zake ni sumu!

    Hata sababu za kuungana nazo ni za utata utata: Moja, tulitekeleza “Afrika ni moja”, kwahiyo kwa nini tusiungane? Lakini hoja ya namna hii ilishindikana japo tulitaka kuchelewesha uhuru wetu hadi hapo Kenya, Uganda na Zanzibar zitakapojitawala!

    Mbili, Zanzibar ilikuwa dhaifu wakati huo (kuogopa kuvamiwa na marafiki wa Sultani)!

    Tatu, wakati mwingine kuna wenye kuamini kuwa ilikuwa ni janja ya wakubwa kuogopa u-komunisti kuingia Afrika “via” Zanzibar, ikiwa ni pamoja na kulinda kituo chao cha mambo ya anga Zanzibar!

    Hii ya moja ongeza moja ni moja itakujaingilia pia umoja wetu wa Afrika Mashariki: Burundi (moja) ongeza Rwanda (moja), ongeza Uganda (moja), ongeza Kenya (moja) na ongeza Tanzania (moja) = moja!

    Umoja wa namna hiyo unaimarika tu bila kujali ukubwa, utajiri, maliasili, idadi ya watu wa kila nchi!

    Mfano mzuri ni makoloni 13 ya Amerika. Yaliungana vizuri na kuwa nchi moja bila kujali sana tofauti zilizokuwepo, ingawa tofauti za wingi wa watu zinajitokeza katika kumchagua Rais (electoral college votes).

    Mbili, Mdau anatamka, (BAP) (a)nasema Wazanzibar walisema hawataki muungano, ni utafiti au sensa ipi hiyo ilionyesha? Au tunasikiliza wenye power in the media kama viongozi wao wa Siasa Zanzibar?

    Mdau, penda usipende, kuna “a general concern” hiyo ya wa-Zanzibari kujiona hivyo! Kama utafanywa “utafiti au sensa” yeyote kamwe kujitoa nje ya kipengere hicho ni ku-“confound” ukweli wa kile nikiitacho, “the Zanzibari Factor” kuhusu Muungano wetu!

    Ni matumaini ynagu kwamba kuwepo kwa “a general concern” ni mwanzo mzuri sana wa utafiti! Ni kutokana na kitu kama hicho ambapo tunaweza tukapata “a researchable question” na kulitaja wazi.

    Incidentally, nina msimamo kama huo wa baadhi ya watu unaowataja: Issa Shivji na Saida Yahya (Mrs. Saida Yahya-Othman)!

    Incidentally, nilianza nao mwaka wa kwanza hapo Mlimani na huyo Saida alikuwa darasa langu. Issa alikuwa akichukua masomo ya sheria.

    Kwa bahati Saida katutangulia na kumaliza mwaka 1969; na Issa na mimi, mwaka 1970 – tulipoteza mwaka mmoja shauri ya mgomo wa 1966!

    BAP

    USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...