Ndugu Wajumuia,
Kwa niaba ya mwenyekiti wa muda ndugu Simon Nkanda, napenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha kuwepo kwa mkutano mkuu utakaofanyika Jumamosi ya tarehe 28, Februari 2009, kwenye ukumbi wa 12727 Hillcrest Dallas TX 75230.
Mkutano huu utaanza saa kumi na moja jioni mpaka saa nne usiku. Tukio hili kubwa na la kihistoria lina nia na madhumuni ya kuimarisha jumuia ya Watanzania waishio jijini Dallas na vitongoji vyake. Katika harakati zake za kuunda jumuia hii mwenyekiti, katibu, na viongozi wa kamati mbalimbali wa muda walichaguliwa.
Vilevile hatua nyingine ya kihistoria iliyochukuliwa ni kuundwa kwa katiba ambayo jumuia hii itafuata mwenendo, taratibu na muelekeo wa kimaendeleo. Mkutano huu utachukua fursa ya kutambulisha jumuia ya Watanzania hapa Dallas na vitongoji vyake umuhimu wa kuwa na amani, upendo, ushirikiano, umoja na kufuata tararatibu ambazo zitaimarisha jumuia hii.
Katika mkutano huu, mwenyekiti, katibu, na viongozi wa kamati mbalimbali watatambulishwa.
Vile vile katika jitihada za kuimarisha jumuia hii, hatua zimechukuliwa za kusajili jumuia hii, kuanzishwa mfuko wa dharura, kuanzishwa mtandao mpya, kutumia njia ya teknohama ili kuimarisha mawasiliano na kuutaarifu ubalozi wa Tanzania hapa Marekani tukio hili la kihistoria.
Kiongozi wa ubalozi wa Tanzania huko Washington D.C. , Dr Mkama atahudhuria mkutano huu. Kijiweni restaurant wanafadhili mkutano huu na watatoa huduma ya chakula..
Kutakuwa na wageni kuoma miji mingine hapa Marekani ambao watahudhuria mkutano huu. Tunaomba Watanzania wote mliopo Dallas na vitongoji vyake mjitokeze kwa wingi ili tukamilishe jitihada hizi.
Tukumbuke tena,
“Our real values are expressed in our actions, in what we do and how we do it”.

Kwa maelezo zaidi tunaomba muwasiliane na:

Ndugu Simon Nkanda
Phone: 469-585-8476
(Mwenyekiti wa muda)
au
Ndugu Abdul Amiri
Phone: 214-535-6329
(Katibu wa muda)
www.Tanzaniadallas.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Nchi za watu inabidi tuungane na kusaidiana katika maisha yetu. Jumuiya kama hizi ni muhimu kuimarishwa katika kila state kwani kuna idadi kubwa ya watanzania sasa USA. Pamoja na majukumu yetu mengi ya kila siku ni vizuri kushiriki katika kutoa michango na kushiriki katika vikao kukutana na wenzetu kila tupatapo nafasi. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu

    ReplyDelete
  2. safi sana? hongereni mliotoa hii mada. cha msingi kuwa na clear defined goals kwamba ni kwanini kitu kama ichi kinaanzishwa na pili kila mwanachama ajue wajibu wake kwa kikundi na 3 watu wawe tayari kutoa michango nne ni watu wawe waaaminifu na upendo! otherwise is a very good idea

    ReplyDelete
  3. habari hii nzuri sana...ila swali langu ni kwamba hiyo katiba ilivotungwa wanajumuiya walishirikishwa au?

    ReplyDelete
  4. Naomba kumjibu anonymous wa tarehe February 24, 2009, 9:38. Nashukuru kwa kuelewa kuwa kuna umuhimu wa kuwa na jumuia kama hizi hapa Marekani. "Defined goals" za jumuia hii zimeandikwa kwenye katiba. Katiba hii ina vipengele kama 32. Kama wewe unaishi Dallas unakaribishwa ufike kwenye mkutano ili uweze kujibiwa masuali yako na vile vile utoe mchango wako. Katika katiba kuna kamati mbali mbali ambazo zimepewa majukumu ya utendeji wake wa kazi na viongozi wa kamati hizi wako tayari kutoa huduma kwenye jumuia yetu bila ya kuwa na riba. Napenda kukutaarifu kuwa wakazi wengi wa Dallas wamependezewa na jitihada hizi, nasi tunaomba Mungu atusaidie ili tufanikishe na kuimarisha harakati hizi.

    ReplyDelete
  5. Napenda kumjibu anonymous wa tarehe February 25, 2009, 6:00 AM. Swali lako ni zuri. Hii katiba iliundwa kutokana na mawazo ya wachache walioona kuwa kuna umuhimu wa kuwa na jumuia yenye umoja, ushirikiano, uwezo na muelekeo ambao utafuata taratibu za kimaendeleo. Kama vile "American constitution" ilivyoundwa na watu wachache, hivi ndivyo hii katiba ilivyoundwa. Kwenye hii katiba kuna vipengele vizuri ambavyo vina manufaa kwa jamii yetu. Vile vile uongozi unakaribisha mawazo mbalimbali kutoka kwa wajumuia ili kufanya mabadiliko kwenye hii katiba. Wenzetu wamarekani wanaita "amendments" kwenye katiba yao. Kwa mfano, katiba inazungumzia mfuko wa dharura ambao ni kwa ajili ya manufaa ya jumuia au kutokuwa na tifauti za ukabila, udini, jinsia au matabaka ambayo ni muhimu katika maendeleo ya jamii. Nashukuru kwa swali lako na unakaribishwa kwenye makutano tarehe 02/28/09 ili tusaidiane kimawazo kujenga jumuia yetu.

    ReplyDelete
  6. Tunawatakia heri katika mkutano wenu. Tunaomba pia mtupe matokeo yake ili kuweza kuhamasisha vikao vya namna hii katika states nyingine. We need each other katika raha na shida zetu. Fikiria misiba inapotokea gharama za kusafirisha, you can not do it by yourself. Ndio hivyo inabidi account inafunguliwa na michango kutolewa. Kukiwepo na umoja na uongozi mzuri this is a big help.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...