Liyumba

Haina ubishi kwamba macho na masikio yataelekezwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwenye kesi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa BoT, Bw. Liyumba ambaye anatakiwa apande kizimbani leo.

Kuna wanaomamini kwamba Bw. Liyumba keshaingia mitini na kuna wanaotarajia kwamba atajitokeza kiaina mahakamani baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya hati za mali za sh bilioni 55.

Mshitakiwa mwenza wa Liyumba, aliyekuwa Meneja Mradi wa BoT, Deogratius Kweka, ambaye hadi sasa bado yuko rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Majuzi TAKUKURU ilitangaza kutoa donge nono kwa atakayetoa taarifa za kumpata Liyumba, kufuatia juhudi za vyombo vya dola kuanzia Alhamisi ya wiki iliyopita hadi sasa kushindwa kumkamata na kumfikisha katika mahakamani baada ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa hati ya dharura ya kukamatwa mshitakiwa huyo na wadhamini wake wawili.

Wakili wa Serikali, Mwangamilia, ambaye alikuwa akisaidiana na Tabu Mzee kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), alidai mahakamani Ijumaa iliyopita kuwa hawajafanikiwa kumkamata Liyumba kama walivyoamriwa na mahakama hiyo.

Wakili wa mshitakiwa Liyumba, Majura Magafu, ambaye alijiunga rasmi mwishoni mwa wiki iliyopita kumtetea mshitakiwa huyo akisaidiana na Wakili Hudson Ndusyepo, aliiambia mahakama kuwa mteja wake hajafika mahakamani, lakini wadhamini wake ambao ni Otto Agatoni, na Benjamin Ngulugunu walikuwapo mahakamani hapo.

Hakimu Hadija Msongo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema kesi hiyo itatajwa leo Februari 24 mwaka huu kama ilivyopangwa awali na kwamba wadhamini hao wanatakiwa kufika siku hiyo pamoja na mshitakiwa.

Redio mbao zinasema kuwa Liyumba hajatoroka, bali yupo nchini, tena jijini Dar ambako amejificha ili kuhakikisha anakamilisha masharti ya dhamana ambapo leo atakapofika mahakamani aweze kutimiza masharti hayo.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, taratibu zilizotumika kumpatia dhamana ya awali zitafutwa na atatakiwa aenze upya, hali itakayosababisha kurudishwa tena rumande.

Redio mbao zingine zinadai kwamba hiyo ndiyo imetoka, ikirudi pancha baada ya uvumi kuwa Liyumba ameingia gizani, na kuifanya mahakama kutoa hati ya kukamatwa kutokana na mazingira ya utata wa dhamana yake.

Liyumba alikuwa amedhaminiwa kwa hati ya mali ya sh milioni 882, badala ya mali yenye thamani ya sh bilioni 55.

Liyumba na Kweka wanakabiliwa na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuidhinisha ujenzi wa minara pacha ya BoT, maarufu kama ‘Twin Towers’ na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221.

Mwamuzi ni dakika 90 kwani gemu bado halijaisha. Sie yetu ni macho na masikio kusubiri kitachojiri hii leo hapo mahakamani Kisutu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Changa la Macho hilo,watu wanahakili

    ReplyDelete
  2. Maanake hata akitoa billion 55 hizo hela atakuwa amezipata wapi? Maanake kwa mtumishi wa benki tu haiwezekani kuwa na mali ya kiasi kikubwa namna hiyo.

    ReplyDelete
  3. Michuzi naona unielimishe kidogo kwani nimejiuliza nimeshindwa kupata jibu. Kwani ujenzi wa majengo ni moja kati ya kazi za afisha utawala?
    Inakuwaje mkurugenzi wa utumishi na utawala akahusika kwenye ujenzi wa majengo? Tafadhali nifahamishe.

    ReplyDelete
  4. We anon wa pili (7.38 am) fahamu kwamba mali anayotumia mtuhumiwa kujidhamini siyo lazima iwe yake binafsi. Anaweza kuunganisha mali yake binafsi na za watu wengine ambao wapo tayari kutoa mali yao itumike kama dhamana. Ndivyo Mramba alivyofanya, ukiachia Yona ambaye mali yote alotumia inasemekana ni yake binafsi.Kwa hiyo kutoa dhamana ya bilioni 50 ni kitu kinachowezekana kwa mtu kama liyumba ambaye profiler yake, na network yake, lazima ni kubwa sana na yenye watu wazito kiuchumi; hata kama uzito huo umnaweza kuwa umepatikana kiufisadi.

    ReplyDelete
  5. WEE ANONY WA LaMBEGU MBONA INAONYESHA HUJAELEWA CONCEPT YA FLEXIBILITY, MKURUGENZI WA UTUMISHI NA UTAWALA ANAWEZA AKAINGIA KAMA KUNA FURSA NZURI KIMASLAHI. WEWE HUKUMBUKI ILE ISHU YA PRESIDENT MMOJA ALIPOIONA FURSA YA UWEKEZAJI KULE SONGWE MGODINI HAKUSITA KUFANYA HIVYO KWA HIYO AKAWA NI RAIS NA WAKATI HUOHUO NI MJASIRIA MALI. IDUMU TANZANIA YETU NA AMANI TULIYO NAYO WATANZANIA

    ReplyDelete
  6. kweli hiyo ni redio mbao,betri papai,antenna mnazi

    ReplyDelete
  7. hahah naona atazuka mtu kavaa mask ya mr liyumba na hakimu hatajua ndo mwenyewe hio ndo Bongoland bwana si unajua tena kama mtu kapewa dhamana ki makosa pia hakimu anaweza kukosea sura au vp mdau stellenbosch

    ReplyDelete
  8. Yupo hapo Geneva anakula kuku kwa mrija na beer kwa umma.

    ReplyDelete
  9. Mshikaji alikuwa hapa Geneva ameondoka jana jioni kurudi bongo.

    ReplyDelete
  10. utawala ni kila kitu wee "mbegu" cut-across all departments,na pesa kwa sana tu.
    mafaili yote lazima yapitie kwa mtawala ata confidentil files,UPO?
    so anahusika saaaaaana tu,kafara uyo
    tutafika tu,Muumba ataingilia ktk aya yote

    ReplyDelete
  11. Jamani Watanzania wenzangu,kwa sisi tulio kwenda shule,tunatambua kwamba Kina Liyumba na Kweka ni watu wadogo sana pale Benki Kuu kimaamuzi!Maamuzi mazito kama yale ya kujenga TWIN TOWERS au Minara Miwili ya Benki Kuu lazima yafanywe na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu waliokuwepo wakati huo.Maaadamu Mtendaji Mkuu wa Benki Kuu,aliyekuwepo wakati huo Bw.Balali alisha "fariki" japo mwili wake haukuonyeshwa hadharani kwasababu za "usalama wa taifa" lakini Wajumbe wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi wao si wapo?Au nao pia walishakufa?Kina Liyumba na Kweka wapate wapi Ubavu wa kupitisha maamuzi mazito kama hayo bila ya Ridhaa ya Bodi ya Wakurugenzi?Hata hiyo Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu hufukia mahali haiwezi kupitisha maamuzi yenye maslahi makubwa ya kitaifa bila Ridhaa ya Waziri wa Fedha akishauriwa na Katibu Mkuu wake?Kina Liyumba na Kweka watapata wapi Ubavu huo wa "Kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 221 kwa kuidhinisha ujenzi wa minara pacha ya benki kuu?na eti kwa matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuidhinisha ujenzi huo".Anybody in his right senses should tell me,how does one justify the lawsuit against Liyumba and Kweka in their very peripheral rolesa and jurisdiction in this context?Jamani Mkitaka kuiba shurti mkomae kwelikweli lakini siyo kuanza kusingizia small fishes namna hiyo!This is yet another stageplay of Usanii Bongo!Mmechemsha tena Wajomba zangu,pity isn't it!Be a lot more Smart next time!Bodi ya Wakurugenzi ya BOT itashitakiwa lini kwa ubadhirifu huo na wakina Liyumba na Kweka waachiwe zao?-spies---

    ReplyDelete
  12. Jamani Watanzania wenzangu,kwa sisi tulio kwenda shule,tunatambua kwamba Kina Liyumba na Kweka ni watu wadogo sana pale Benki Kuu kimaamuzi!Maamuzi mazito kama yale ya kujenga TWIN TOWERS au Minara Miwili ya Benki Kuu lazima yafanywe na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu waliokuwepo wakati huo.Maaadamu Mtendaji Mkuu wa Benki Kuu,aliyekuwepo wakati huo Bw.Balali alisha "fariki" japo mwili wake haukuonyeshwa hadharani kwasababu za "usalama wa taifa" lakini Wajumbe wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi wao si wapo?Au nao pia walishakufa?Kina Liyumba na Kweka wapate wapi Ubavu wa kupitisha maamuzi mazito kama hayo bila ya Ridhaa ya Bodi ya Wakurugenzi?Hata hiyo Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu hufukia mahali haiwezi kupitisha maamuzi yenye maslahi makubwa ya kitaifa bila Ridhaa ya Waziri wa Fedha akishauriwa na Katibu Mkuu wake?Kina Liyumba na Kweka watapata wapi Ubavu huo wa "Kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 221 kwa kuidhinisha ujenzi wa minara pacha ya benki kuu?na eti kwa matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuidhinisha ujenzi huo".Anybody in his right senses should tell me,how does one justify the lawsuit against Liyumba and Kweka in their very peripheral rolesa and jurisdiction in this context?Jamani Mkitaka kuiba shurti mkomae kwelikweli lakini siyo kuanza kusingizia small fishes namna hiyo!This is yet another stageplay of Usanii Bongo!Mmechemsha tena Wajomba zangu,pity isn't it!Be a lot more Smart next time!Bodi ya Wakurugenzi ya BOT itashitakiwa lini kwa ubadhirifu huo na wakina Liyumba na Kweka waachiwe zao?-spies---

    ReplyDelete
  13. HAWACHELEWAGI KWENDA KWA WAGANGA WA KIENYEJI, AKAMZINGUE KIASI KWAMBA HAKIMU AKIMUONA ANAMUONA HANA HATIA, ALIPOTEA ALIPOTELEA WAPI? KAMA SIO KUZINGUANA HUKU!!!

    ReplyDelete
  14. WE `Usiyejulikana' wa February 24, 2009 12:47 PM. Wataenda kwa waganga gani wakati wote wamefungiwa leseni? Labda kwa `vigagula'
    M3

    ReplyDelete
  15. He looks like Sir Allen Stanford at worst...

    ReplyDelete
  16. ...or Balali at best...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...