wadau katika foleni ya luku kwenye sheli ya bp express mchana huu
foleni ndefu juu na chini
KWA MUJIBU WA MSEMAJI WA TANESKO ANTI BADRA MASOUD NI KWAMBA MASHINE ZA LUKU ZITAKUWA ZINAFANYA KAZI KWA MUDA WOTE ISIPOKUWA KUANZIA SAA NNE USIKU AMBAPO ZITAZIMWA ILI KUFANYIWA MATENGENEZO YA KAWAIDA.
BADRA KASEMA SI KWELI KWAMBA LUKU ITAKUWA HAMNA KWA MUDA WA SIKU KIBAO KAMA AMBAVYO REDIO MBAO ZINASEMA NA KWAMBA HATA HILI ZOEZI LA KUKARABATI MIUNDOMBINU YA LUKU JIJINI DAR ITAKAMILIKA BAADA YA SIKU NNE TOKA LEO. BAADA YA HAPO LIBENEKE KAMA KAWA...

ANGALIA FOLENI YA VIDEO HII KWA

KUBOFYA HAPA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. HIVI JAMANI HAWA CCM MIAKA YOTE WANASHINDWA KÜSOLVE TATIZO LA UMEME JAMANI?SASA UMBUMBU HUU MPAKA LINI JAMANI?NA MNATARAJİA CCM ILETE MAENDELEO?SIJUI......

    ReplyDelete
  2. TANZANIA BIASHARA NI KULAZIMISHA,SERIKARI KUKATAA KUNUNUA MITAMBO MIBOVU NDIO WANALAZIMISHA HIVI.HII NCHI NI LAZIMA IPATE UTAWALA WA KIJESHI ATA KWA MWAKA MMOJA LABDA UTASAIDIA KUONDOA UPUMBAVU

    ReplyDelete
  3. huu sio uwanja wa siasa. wee anon hapo juu

    ReplyDelete
  4. I dont think kama siasa inatakiwa ichukue nafasi hapa, ingekuwa vyema kama comment zingekuwa za kuilaumu serikali ambayo ndani yake hata viongozi wa upinzani wamo.

    ReplyDelete
  5. Mimi naona tatizo siyo chama ila ni viongozi wetu waliopo kwenye taasisi zetu. Tatizo la uongozi usio na maslahi kwa wananchi haupo Tanesco pekee bali katika taasisi nyingi za umma. Wafanyakazi wengi hawafanyi kazi zao ipasavyo pamoja na kuendekeza sana rushwa. Maoni yangu kwa wananchi wenzangu ni kwamba tuache kutoa lawama kila siku bali sisi wenyewe tuwe mfano wa kuacha kula rushwa pamoja na kufichua wala rushwa ili tusonge mbele. Kulamika huku tunaficha wahalifu haisaidii, jichunguze wewe mwenyewe kwanza kama unatimiza wajibu wako kwa jamii na ukimaliza waangalie wenzako kwani mabadiliko yananzia kwako binafsi. Hatutaweza kuendelea mpaka hapo tutakapoacha kushabikia na kuwasifu wala rushwa

    ReplyDelete
  6. poleni watanzania wenzangu! maendeleo yanahitaji elimu kujituma uvumilivu na muda hata kama msipopata huduma nzuri nyinyi leo basi watapata hata wajukuu au vilembwe. poleni sana

    mdau U.S. AAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  7. Ushauri wa bure kwa TANESCO. ongezeni vioski vya kununua umee jamani, ikiwezekana hata Maburo de chanji pelekeni mtoe pasenti zao muwape, sisi tutaenda kufata huko msitupe hesabu za kuwa na A/C NMB mambo ni yaleyele ya mchezo wa karata nyeusi nyekundu hakuna jipya, ukienda huko pia msururu kama siafu wanaenda kushambulia, jamani tuhurumieni kuokoa mida yetu ili tupate mda wa kujenga taifa letu, sio kubung'aa kwenye foleni kuanzia saa moja mpaka saa nne eti umeenda kuteka maji ayaaa kunradhi ni kuteka umeeme, kadhia ni nyingi mpaka ulimi unaenda songombingo songopare wajemenii!

    ReplyDelete
  8. ni aibu...Da tuna teswa na Viongozi wetu...

    ReplyDelete
  9. nna hasira ya kutetemeka!!

    ReplyDelete
  10. hi nchi iko siku lazima damu imwajike maana hakuna haki sasa cheki mambo kama haya ivi mnafikiri wanadamu hawachoki siombei mabaya lakini yetu macho watu watachoka siku moja tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...