Mkuu wa Wilaya ya Morogoro , Said Mwambungu akizungumza na  wanafunzi wa shule ya Sekondari Lupanga ya Mjini Morogoro  leo  mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na walimu wa shule hiyo kuhusiana na mgomo wa wanafunzi na kuwataka warejee madarasani wakati uchunguzi wa kina dhidi ya walimu walioongoza kupigiwa  kura za maoni  dhidi ya tuhuma za unyanyasaji wa ngono ukiendelea kwa ajili ya kuchukua hatua za kinidhamau na za kisheria. Picha na mdau wa mji kasoro bahari John Nditi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. No mjadala, walimu wanaojihusisha na matendo ya ngono lwa wanafunzi wafukuzwe mara moja. Wafutiwe leseni zao za uoalimu na wandikwe majona katika kila bango la tangazo la wilaya , na mikoa kwamba hawa walimu ni pedophilia.
    wanafunzi wako sahihi kugoma juu ya walimu wahuni.
    iwe fundisho kubwa kwa walimu wasiopenda kufundisha bali wanaotaka dogo dogo. Tukianza hapo basi hata wengineo kama maafisa wa serikali, makapuni, wafanyabiashara na walevi wataacha hiyo biashara ya kutongoza watoto wa shule za msingi, na sekondari.

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wanafunzi kwa usumbufu wa kufanyishwa mchezo mbaya na watu waliokabidhiwa dhamana ya kuawapa maarifa!

    Serikali isituzuge hapo, ilipopeleka walimu wa voda fasta wasio na taaluma ya ualimu ilitarajia nini kama sio kutongozana mashuleni!! Ualimu ni taaluma ihusishayo mambo mengi siyo kusomesha tu! Taifa limepoteza mwelekeo wa elimu kila mahali kwa sababu ya ubabaishaji wa wanasiasa na ufisadi wao.

    Nchi ilipokuwa maskini tuliweza kuwalipa walimu vizuri na kuwa na shule nzuri za umma!! Leo tunachimba dhahabu, gesi, tanzanite, rubi, almas na maliasili kibao, elimu ya umma inauawa ili kuzalisha manamba wa kuwafanyia kazi watoto wa vigogo maana wao wana shule zao maalum ziwahakikishao elimu bora, kazi bora na maarifa ya kifisadi!

    Nchi za Scandinavia hakuna shule binafsi maana za umma zinakidhi haja ya mahitaji ya taifa husika. Tanzania elimu imebaki kwenye takwimu tu kama mradi wa kuombea pesa kwa wafadhili. Wizara ya Elimu inasema uandikishaji ni asilimia 95, huku tafiti zinaonyesha asilimia 20 ni hewa maana hawajawahi kufika shule, tunadanganya tupate pesa kwa gharama ya ustawi wa Taifa kwa kuwa na watu mbumbumbu!

    vIJANA MSIFE MOYO MAANA MAFISADI SIKU ZAO ZINAHESABIKA kama zilivyohesabika za MAKABURU wa Afrika Kusini amabao hawakuamini kuwa mtu mweusi ataongoza SA. Ushindi unakaribia 2015!!
    Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  3. Sasa kunafanywa uchunguzi gani? What kind of non sense jamani.,....

    ReplyDelete
  4. Wewe DC..unataka warudi darasani wakawasikilize hao hao waalimu wanaowatuhumu? Kwanza ilibidi hao waalimu wasimamishwe kazi, wawe nje ya shule ili wasi-contaminate ushahidi..!! Hao watoto hawawezi kufundishwa na waalimu ambao wandhaniwa kuwa wanawanajisi watoto wadogo..wasimamishwe kazi kwanza waruhusu uchunguzi ufanyike..!!

    ReplyDelete
  5. Apelekwe DC Mnali hapo awachape walimu wote wanaofanya ngono na wanafunzi.

    ReplyDelete
  6. Cheer up ma home people.
    Ukombozi wa wanafunzi wanaochafuliwa na walimu washenzi unaanzia Morogoro.

    So great. Ni ugonjwa bongo nzima na kwakuwa kila kigogo ni fisadi wa ngono hakuna anayesikiliza. So teribo. Ukiona mataifa yaliyoendelea hiyo ni kesi mbaya sana. Bongo inaonekana kama kamgomo ka watoto na DC anatumwa. Vyombo vya nchi viamke na president atoe tamko. Yatima na uchumi mbovu unatokana ni matokeo ya walimu kuwafundisha watoto ngono utotoni.

    Waziri wa elimu tamka. Waziri wa sheria soma vifungu. President say some.
    Ndomana wasomi haturudi bongo. Kunatisha. Hasa baada ya kuona wenzetu wanavyoheshimu mambo ya msingi.

    Ona ngono makazini-Office rape. Sheria ya bosi kuto-sex na mtumishi wa chini yake ipo. Ila mabosi ndio wana uhuru wa kulala na waliochini kutokana na dhiki na mwisho kuvunja ndoa za watu na watoto wasio baba.

    TAMWA wanakula misaada wamelala-Niliwahi kuwatumia tuhuma nzito ya kweli hakuna aliyejibu email.
    Ofisi ya waziri mkuu haisilikilizi vilio vya watu

    Bongo bongo tubadilike.
    Hongera watoto wa kiluguru-Tunapelemba sheria.

    Lukwangule weka neno wape nguvu watoto wa home

    ReplyDelete
  7. Stinking bongo.
    Hakuna sheria wala utaratibu. Kilio cha watoto kiwe cha kitaifa. Ni kweli. Ni kweli kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu

    ReplyDelete
  8. no mjadala.madenti hakuna kuingia class wala nini? yaani hao hao ndio wakawafundishe tena?haiwezekani.kila siku tumechoka kusikia maredioni wadogo zetu wanakatiza masomo kwa kupewa mimba tena ikiwezekana wa chapwe viboko hadharani.HIVI MWANAFUNZI WAKO SI SAWA NA MWANAO?

    ReplyDelete
  9. disgusting!
    DC anawarudisha wanafunzi kwa walimu wale wale. lakini tusimlaumu public governance tanzania yote imevunda na hawa viongozi wa chini wanajifunza kutoka kwa mabosi wao. we kama mafisadi wapo wanatanua na serikali kuu inawaangalia na kuendelea kula na kunywa nao,unategema nini watajifunza ma-DC?
    wizzzzzi mtttupu!!!!

    ReplyDelete
  10. Watu wa mbagalla enzi zile mnakumbuka lile jibaba linene mwalimu lilimrape msichana mmoja wa form one akapata asma attack. Lile jimwalimu lilikimbia na hamna aliyemtafuta kabisa. Mtoto wa watu nusu afe. Na wala masabo hakufuatilia ile ishu. Tanzania bwana by the timu uchunguzi unaisha hao walimu wameshapata kazi mahali pengine kimya kimya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...