benki ya NBC imeshaonesha mfano mzuri  kwa kujitolea kuitunza bustani ya posta ya zamani hapa dar. kuna habari makampuni kibao yanatamani kusaidia ila sijui kuna jinamizi gani linalozuia juhudi zao ambazo zitasaidia kupendezesha jiji na pia kuwapa raha walipa kodi
wadau wakitamani kusogelea bahari ya hindi lakini senyenge iliyowekwa hapo kuzuia walipa kodi wasiguse ufukwe inaweka kigingi. redio mbao zinasema mamlaka ya bandari ndio walioweka uzio huo unaoudhi kwa sababu za kiusalama...
haiingii akilini kuona ufukwe wa posta ya zamani unaachwa bila matunzo kwa kisingizio gani sijui
choo na bafu cha kulipia pamoja na genge la mama lishe kwa mbele ndio ubinifu pekee unaoonekana  kufanyika sehemu hiyo. lakini hadhi yake ina utata ukizingatia hapo ni kati ya jiji
uzio wenyewe umeshaoza na kuendeleza taswira ya uchafu sehemu hii.

Zamani  eneo hili lilikuwa linatoa burudani pamoja na ajira kwa wadau kwenda kula kacholi na rambaramba huku wakifurahia upepo mwanana wa bahari ya hindi. bila shaka anasubiriwa JK apaone na kutoa mwongozo. tatizo akipita sehemu hii anapita mkuku hivyo mpaka aje asimame na kujionea mwenyewe aibu hii ya mtindio wa ubunifu wa wazee wa jiji  inaweza kuwa mwaka 2025. wadau naomba tulijadili hili na mengine mengi kama hayo na pia tutoe maoni ya nini kifanyike ili kuwaamsha wazee wa jiji ambao inaonesha wamelala fo fo fo fo fo......

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Aibu, hiyo fence ni kielelezo cha mamlaka husika hazijali wananchi.

    Katika karne hii ya leo usalama wa bandari hauwezi kulindwa na hako ka-fence, sana sana huenda yalikuwa mawazo finyu ya watu wachache.

    Huo uzio uondolewa mara moja kwani hatuko Guantanamo.

    Bandari hawaihitaji kuweka uzio mji mzima kwa sababu za kiusalama. Hivi kilataasisi ikianza kuweka uzio kama hao bandari huo utapitika kweli?

    ReplyDelete
  2. mimi naona huo ufukwe tuwauzie wachina tu. maana kama kila kitu tumebinafsisha bahari tunashindwa nini? JK mwenzio alianzisha ubinafsishaji na wewe malizia kwa kuuza bahari na Ikulu

    ReplyDelete
  3. tatizo viongozi wetu wengi hawana creativity kabisaaa! Nakumbuka kuna daktari mmoja aliulizwa na mh. naibu waziri wa afya ni kwa nini wagonjwa wanalala bila vyandarua na hali wamepokea vyandarua vya msaada karibuni? daktari bila aibu akajibu hajampata fundi wa kuvitundika vyandarua hivyo! huyo ni daktari mkuu wa wilaya, tutafika kweli????

    ReplyDelete
  4. Ushauri upi na wazee wa jiji hata choo kwake hana!

    ReplyDelete
  5. Michuzi, unanikumbusha "BOMBAY", ice cream na viazi vya machalee!
    Wakatuona tunafaidi kila wikiendi wakaweka uzio. pumbaf zao!

    ReplyDelete
  6. Ndugu Michuzi unafanya kazi nzuri ambayo hata magazeti yetu ya kila siku hayafanyi. Kweli kuna haja ya wahusika (serikali ya jiji au ya JK) kuchukua hatua. Ushauri: kwa vile JK anaelekea kuelewa na watu wake wana vichwa vya mbuzi, tengeneza ka-album kadogo ka picha hizi kaambatishe na maelezo/maoni yako au ya wadau wengine kama hayana mitusi, kafungashe vizuri kwenye bahasha na mwombe katibu mkuu wa ikulu amkabidhi mheshimiwa. Ninakuhakikishia JK ni msikivu na atachukua hatua!!

    ReplyDelete
  7. kwani nyie wazee wa mji mkipita hapo hamuoni kuwa pamekuwa neglected. kwanza hapo ni karibu sana na down town, pili kuna beach hamuoni kuwa hapo mungeweza kupafanya papendeze. amkeni mu crack your heads mpate ideas ya vitu vya kufanya hapo. ni aibu sana kuona mahali kama hapo pana acwa kuonekane hivyo. pesa za kodi zinaenda wapi. kama hakuna pesa kodishenieni watu. hata hizo choo zinaweza kujengwa vizuri halafu watu wakalipa kuzitumia. men come up with ideas to utilize the place. don't just sit and let the place bexome vibaka garden.

    ReplyDelete
  8. Bwana michuzi mi naona kujadiliana hapa ktk blog peke yake haitoshi,mi naona kama kuna njia yeyote ya kuweza kumfikishia JK post hizi pamoja na maoni ya wachangiaji basi usaidie hilo kwani utamsaidia kwa kiasi kikubwa sana ktk kuyaona haya na mengine mengi tu yanayojiri ktk kona mbalimbali za nchii hii.

    mdau TLS,FR

    ReplyDelete
  9. ......JUST IMAGINE JIJI LINA WAKURUGENZI,MADIWANI,MAMEYA,WAKUU WA WLAYA,MKUU WA MKOA,WABUNGE,WIZARA HUSIKA[WAZIRI,NAIBU WAZIRI]LAKINI BADO MNASUBIRI RAISI AJE,BONGO KWELI KAZI IPO,YAANI INAKERA MPAKA BASI,MIMI NASUBIRI WEEKEND HAPA WASHINGTON DC NIKAFAIDI KODI YANGU KWENYE BEACH ZENYE KILA SIFA,NYIE ENDELEENI KUPIGA DOMO NA VIONGOZI WENU WANAOTANUA NA MASHANGINGI.

    ReplyDelete
  10. Na vipi kuhusu vibanda vya mabasi,kujikinga na jua la dsm. Ni jiji nao wanahusika? Watu wanachukua mabati kama chuma chakavu.

    Pamoja na kwamba ni kazi ya jiji, kutunza mazingira ya bustani za dsm. Ustaarabu watanzania ulishatushinda. Tunajua sana kutoa maoni, lakini hatutendi yale tunayoyasema.

    Ingekuwa vp kama Tz kungekuwa na benefits kama UK?

    ReplyDelete
  11. HAWA WATU HAWANA AJA YA KURUDI CLASS WANGEKUA WANAPITIA BLOG YAKO NI DARASA TOSHA.

    ReplyDelete
  12. 1.Vunjilia mbali Halmashauri zote za jiji na weka Dar City Commission kama wakati ule wa Keenja.

    2. Anzisha nafasi ya City Planning Czar atayesimamia ukuzaji wa jiji na concept nzima endelevu ya "Urbarn Rejuvenation" (siyo lazima awe Mtanzania). Unajua ukienda jiji kama Sandton, London, NY, kila siku jiji linaonekana kama jipya, siyo tu kutokana na usafi, bali pia kutokana na Urban rejuvenaton. Hapa Dar, tangu mwingereza atuachie Askari Monument, hakuna monument nyingine ya maana tuliyoweka.

    3. Majengo mapya yote yalazimishwe kufuata Zoning laws. Siku hizi watu wanajenga majengo ambayo hayafuati mtiririko wa mitaa na hivyo kufanya mji uonekane kama Kijiji kikubwa. Mfano hai ni hili jengo la Uhuru Heights. Lingine ni lile kwenye makutano ya Morogoro/ Bibi Titi, linalotazamana na NSSF Towers - lile jengo lingetakiwa kukumbatia curve ya barabara badala ya kuwa kama box. NSSF wamepatia lakini hawa wameharibu Jiji.

    4. Beach Plots wasipewe watu binafsi. Angalia hata Ikulu haina Beach Plot. Ilitokeaje Dar tukagawa Beach plots kwa watu hali tukijua kufanya hivyo ni kuwanyima wananchi raha ya kuishi katika jiji lenye Bahari?

    ReplyDelete
  13. Issa

    Nakubaliana na wadau hapo juu, tusiishie kwenye Blog tu katika hii vita dhidi ya viongozi wa halmashauri kutowajibika katika kutunza mazingira ya jiji letu. Hii vita inatakiwa isikike nje ya blog maana sio viongozi wote wana ufahamu juu ya mambo ya blog na mtandao kwa ujumla. Wadau tufanyaje?

    Aluta Continua

    ReplyDelete
  14. Mimi nishasema muda mrefu, dawa ya nchi hii ni kubadilisha system, wawekeni watu wenye elimu na kuwajali wananchi, suala dogo la usafi na kuboresha mazingira mpaka asubiriwe Rais wa nchi, kwani viongozi wa jiji wanafanya nini na wafanya kazi wao?
    Watanzania tunapaswa kufanya mageuzi, hatuwezi kufanikiwa mpaka kwanza waje watu wanaojali wananchi na sio matumbo yao kama hao walioko sasa hivi, Chama cha Matumbo!

    ReplyDelete
  15. Mr. Michuzi ningependa kukushauri utumie kiswahili fasaha, unapotumia neno kama kweshenei unamaana gani... mimi naishi india na hilo neno hapo halilandani kabisa na unachojaribu kusema... watanzania tusiwe wepesi sana kukumbatia lugha za watu wengine na kuzarau kiswahili chetu ambacho pia kiliharibiwa kwa kuingiza maneno ya kiarabu humohumo... watukuu wetu watakuta kuswahili kinakuwa kihindi na watanzania tunaoneka ka watu wasio na utamaduni wao tunadharaulika... tafadhali.

    ReplyDelete
  16. Ndugu Issa
    Hongera sana tena sana kwa kazi nzuri,Raisi keshatoa maelekezo kwa Halmashauri siku hiyo walikuwepo Mkuu wa mkoa,wakuu wa wilaya, Meya na mameya wake, madiwani wote na baadhi ya mawaziri tengezeni mabustani na fukwe za bahari na pia alitoa maelekezo ya watu watumie fukwe kwa kupumzikia na starehe hata sherehe na akakemea tabia ya kuwazuia watu wasitumie fukwe hata kukiwa na sherehe za Arusi, ila watendaji ni wabovu wakishapata uongozi basi hawana tena ubunifu wapox2 tu. Kwa ukweli Jiji linanuka, kusema jamaa JK atapita spidi haoni si kweli anayajuwa sana mazingira hayo ni miaka 3 tu ndio kawa Raisi lakini miaka zaidi ya 10 ofisi yakle ni hapox2 Wizara ya Nje anajuwa sana
    Watendaji ndio wa kuwajibika

    Mohammed

    ReplyDelete
  17. kwa nini tangazo la udhamini limeandikwa kwa kiingilishi?

    ReplyDelete
  18. JK
    Utaweza kila kufuatilia kila kitu?
    It is Terrible
    I`m Mr Terrible

    ReplyDelete
  19. TAFADHALI YEYOTE ALIYE NA E-MAIL ADDRESSES ZA WAKUBWA KANDORO NA MEYA WA JIJI WAZITOE HAPA ILI TUWATUMIE HIZI COMMENTS. PENGINE, NA NASISITIZA PENGINE ITASAIDIA KUWAAMSHA/// AAAnnghghhrrhhhhhhshh!

    ReplyDelete
  20. hivi watu wa mipango miji mnapokuja huku ulaya kwa safari za kiofisi mnafanyaga nini mida yenu ya ziada?

    maana kama huwezi buni kitu mwenyewe unacopy na kupaste.miji na fukwe za ulaya zimejengwa vizuri sana. badilikeni kidogo ...muwe na mawazo ya kuona mbele.

    hicho chooo hata ukimpa babu yangu kijijini hatumii bora ajimbe shimo

    mdau netherlands

    ReplyDelete
  21. issue ni kwamba siyo viongozi hawako creative...wapo ambao ni creative ila walioko juu yao kivyeo ni maconcervative wanaona kujenga vizuri ufukwe ni kuchezeea hela wakati mafisadi wanamaliza

    Kuongea hapa ni very easy ila ingia kwenye ofisi za serikali ujionee.....utakuwa na focus nzuri kabla hujaingia lakini ukishaingia kuapply idea zako itakuwa ngumu sana.

    sanasana maseniour watakwambia tulia we kijana hujui kitu.inabidi utulie kwa sababu unamind mshahara wako tuuuuuuu. thats all

    madau netherlands

    ReplyDelete
  22. Kuhusu hili swala la mazingira mfano ufukwe kuwa msafi, jiji lote kwa ujumla kuwa msafi nakubaliana nanyi wadau wenzangu mliochangia lakini mkumbuke pia kuwa hao hao wadau wengine ndio waharibifu wakuu na wachafuzi. Tusilaumu viongozi peke yake pia sisi wenyewe tujitume katika kulipenda jiji letu na nchi kwa ujumla. Hiyo fence ya ufukwe sio kama itakuwa imeanguka yenyewe, ni wananchi wenzetu ndio watakuwa wamesababisha ikaanguka wale wanaofanya biashara kule na kukaa kaa.

    Suala la usafi tulilinde pia sisi ndipo viongozi nao watakapo pata moyo wa kuboresha. Watanzania ni waharibifu mfano mitaro ya maji machafu tunatupa vitu hata vingine vinachangia kuziba. Tusitupe taka ovyo, tusi zibue vyoo wakati wa mvua. Tuimarishe usafi wa mazingira, si huko mbali hata mazingira yanayotuzunguka tu ingetosha kuleta tasiwra ya jiji. Tupande miti karibu na majumbani kwetu, maua tusipende mazingira yanayotuzunguka kuwa machafu na yenye ukame. Pia tuepuke majumbani mwetu kuwapa taka mateja kwa bei rahisi, wale hawapeleki panapostahili zaidi ya kutupa mabarabarani. Tembeleeni wachaga vijijini Moshi, Arusha muone mazingira. Tuige wenzetu Arusha, Moshi mbona wanaweza iweje sisi tushindwe?
    Tuweni wasafi jamani. Ubaya wa wabongo wengi ni madada du na makaka du hawataki kufanya usafi lakini ni wachafua ovyo, hawatupi taka sehemu zitakiwazo. Usafi wa nguo tu lakini ndani fu fu fu fu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...