GHALA LA SILAHA LA JESHI LIMELIPUKA NA KUSHIKA MOTO KWENYE KAMBI YA JESHI ILIYOKO MBAGALA KIZUIANI NA KUSABABISHA MILIPUKO MIKUBWA YA MABOMU NA KULETA KIZAAZAA JIJI ZIMA.
GLOBU YA JAMII ILIYO KATIKA ENEO LA TUKIO IMESHUHUDIA ASKARI WA JESHI LA ULINZIM POLISI NA ZIMAMOTO WAKIWA WAMEJAZANA NJIA PANDA KUELEKEA KAMBINI HUKO AMBAKO MOSHI MZITO NA MILIPUKO IMEKUWA IKISIKIKA TOKA ASUBUHI.
KUNA HABARI KWAMBA BAADHI YA MABOMU YANARUKA MAZIMA MAZIMA NA KUTUA KILOMETA KADHAA TOKA MBAGALA NA KULIPUKA. KATIKATI YA JIJI TAYARI WATU WAMETANGAZIWA WASHUKE MAGHOROFANI.
HABARI ZINASEMA KWAMBA MOTO HUO WA AINA YAKE UNAWEZA KUZIMIKA KWA UTAALAMU WA HALI YA JUU ILA USALAMA DHIDI YA MLIPUKO WA MABOMU NI MDOGO. WAKAZI WENGI WA MBAGALA WAMESHAONOLEWA SEHEMU HIYO WAKATI JUHUDI ZA KUTHIBITI MOTO NA MILIPUKO IKENDELEA.
GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUWA ENEO LA TUKIO NA INAAHIDI PICHA NA HABARI KEDEKEDE BAADAYE KIDOOOOO....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Mungu wangu,ina maana leo hatuendi nyumbani, manake kwenda kwenyewe ni vita,kugombea usafiri, sasa tena wanatuleta janga la mabomu.

    ReplyDelete
  2. Eeeh Mola waondolee balaa hili ndugu jamaa na marafiki walio karibu na eneola tukio. Aaameen

    ReplyDelete
  3. poleni sana wote mlio kubwa na janga hili. let be responsible so it won't happen again.

    ReplyDelete
  4. Hatimaye umetuhabarisha!!!!

    ReplyDelete
  5. Duh sasa huo utaalam si unaweza patikana wakati kila kitu kimeteketea na impact kuwa kubwa, well poleni sana wananchi/ wakazi wa maeneo jirani..

    ReplyDelete
  6. Poleni sana. Sasa watu watakuwa wamechanganyikiwa na watasababisha ajali nyingi mno. Janga juu ya janga. Mungu atunusuru kwakweli.

    ReplyDelete
  7. kweli nashindwa kuamini kilichotokea mana mimi nipo mikocheni ila nimesikia icho kisanga jamani inatia huruma sana dah!ila Mungu atawanusuru tuzidi kuombeana

    ReplyDelete
  8. inasikitisha sana! sasa shule kujengwa karibu na ghala la kuhifadhia silaha mbona wasichukue tahadhari mapema?. serikali na iwahamishe waliojenga karibu na maghala ya silaha ni hatari kwa maisha ya watu. Kwa ufahamu wangu ghala la silaha linalindwa, Je waliokua zamu wakoje? kaka tunaomba ufuatilie ujue chanzo cha moto huo. poleni sana Mungu yu pamoja nanyi.

    ReplyDelete
  9. ahasante kwa kutuhabarisha.. atimaye tunapata picha kulivyo huko

    ReplyDelete
  10. Mungu tunaomba uwasaidie watu wote walioko katika jiji la Dar es Salaam wanusuru Bwana na janga hili kubwa la moto wapate kupona.

    ReplyDelete
  11. Mungu tuepushe na janga hili. Mungu waokoe wote walio katika tukio na watie nguvu wote walio katika harakati za kuepusha janga hili.

    ReplyDelete
  12. Wabongo kwa kutopenda kazi! Mlipuko umetokea Mbagala lakini asilimia kubwa ya Wafanyakazi katikati ya Jiji wamekimbilia majumbani mwao. Saa 8 tayari kuna foleni barabarani.

    ReplyDelete
  13. Je kuna usalama kwa wananchi baada ya huo moto kuzimwa?

    ReplyDelete
  14. my prayers, fot Tz safety.
    Mungu atulinde.
    Koku

    ReplyDelete
  15. PEPE-WA-KALEApril 29, 2009

    Uvumi ulioenea sehemu nyeti ni kwamba hii ni hujuma na inahusishwa na matukio ya hivi karibuni ya kisiasa hususan mambo ya muungano. Stay tuned!!!!

    ReplyDelete
  16. Hii ni ajali mungu atunusuru na majanga mengine lakini inasikitisha sana ugumu wa vichwa vyetu wa TZ tumeshakatazwa kujenga maeneo karibu na kambi za jeshi na mabondeni na maeneo mengine ya hatari kama vile airport lakini bado tuko ignorant tunakufa na our own ignorance na ubishi,

    ReplyDelete
  17. Tume ya kuchunguza hiyooo naiona ipo njiani na bajeti ya bilioni kadhaa!

    ReplyDelete
  18. huku swine flu nyumbani mlipuko wa mabomu sasa tutakimbilia wapi???
    MIMI NAMUACHIA YOTE MWENYEZI MUNGU SITAPANIC KIASI HICHO ILA YEYE TU
    poleni sana watu mlio karibu na tukio naelewa njisi gani mlivyokosa amani

    ReplyDelete
  19. Presha michuzi! kuna MAAFA ZAIDI?

    ReplyDelete
  20. jaman pole sana watu wa mbagala na walioathirika. Mungu awalinde. Wahusika waangalie sana jambo hili,limeathiri watu na mali zao. Nasema tena polen sana.

    ReplyDelete
  21. Jamani poleni sana watanzania wenzangu mliokumbwa na hili janga tumuombe mwenyenzi Mungu huu moto uweze kuzimwa bila kuleta madhara zaidi.Asante uncle Michuzi kwa kutuhabarisha.

    ReplyDelete
  22. poleni sana ndugu,jamaa,marafiki na wote kwa ujumla kilichobaki tumuombe mungu awaepushe na janga hilo la kitaifa,ingawa tupo mbali na upeo wa macho yenu ila nahakika tupo pamoja katika hilo,aaaaamen!!!!!!

    ReplyDelete
  23. mabomu feki toka uchina. Tanzania tumekwisha

    ReplyDelete
  24. ohoo, masikini poleni jamani, lakini jamani mnawekaje hayo mabomu karibu na maeneo ya watu wanapoishi? mimi nilifikiri mambo kama hayo ya kijeshi yanatakiwa yawepo mbali kabisa na sehemu ambazo watu wanaishi au wanafanya biashara?!!!! jeshi linatakiwa lisogee mbali sasa, huo mji ushapanuka jamani ahaa.

    ReplyDelete
  25. we anon wa hapo juu unataka jeshi lisogee mbali mpaka wapi???
    Look,ni kweli jeshi halitakiwi kuwa karibu na makazi ya raia,jaribu kufukiri jeshi mmelisogeza mpaka songea labda halafu Dar inavamiwa,utaikomboa namna gani.
    Lazima kuwe na kikosi karibu kila eneo la muhimu ili once adui anapojipendekeza tu,anapewa huduma ya dose ya kwanza wakati heavy artilary zinaletwa kutoka huko nje ya mji.
    Dar es salaam ndyo kuna almost kila kitu(capital city),unawezaje kuiacha hivihivi bila kinga?Think!!

    MKulima-Kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  26. Jamani poleni sana ndg wote wa mbagala yaani nuluposikia wala sikuamini!!! Hiyo ni mizinga na kwanini ilipuke jamani!! Huo ni uzembe lazima serikali iwe makini sana katika kuwalinda wananchi wake.

    ReplyDelete
  27. GHALA HALIKAGULIWI???? YANI APO KM SII JOTO/MSUGUANO ULIOKUWEPO KTK MABOMU AYO!! JAMANI
    basi kama annon apo juu alosema hatuwez fikiri mbali na ugaidi/hujuma mana tulishalizwa na magaidi.
    kama una utu mbona kazi hutafanya?ata uku mbali tuliko tulivoangaika kuwatafuta ndugu apo mbagala,God knows!!
    NA IVO VIPANDE VYA MABOMU VILIVYODONDOKA URAIANI YAWEJE,ASKARI WAMELALA APO KUKAGUA ENEO ZIMA NA KUYATOA??TZ HATUJAZOEA AYA MASWALA,MTU ATAOKOTA AKALIPELEKE HOME WASHANGAE VIZURI THEN WHAT NEXT!!!
    Yesu utaokoe
    ASKARI WETU WAMEPONA UWIIIII

    ReplyDelete
  28. mabomu ya uchina??

    uwiii hahahahahaahahahaaa,wee annon

    inawezekana!!

    1.usafiri kero/vita
    2.vumbi
    3.msongamano wa watu hakuna mfano
    4.environment ziro
    5.wizi/vibaka
    6.walalahoi/no kazi
    7.kiwanda cha nguo kinachochafua mto unaotumiwa na wakazi
    8.mipango miji holela
    9.foleni
    10.MABOMU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...