Msuluhishi wa mgogoro wa Darfur na Katibu mkuu mstaafu wa AU Dk. Salim Ahmed Salim akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kutoa mhadhara kuhusu hali ya jimbo la Darfur kwa kikosi cha JWTZ kinachoelekea Darfur-Sudan leo katika kambi ya Jeshi iliyoko Msata ,Pwani. Kulia ni Mnadhimu mkuu wa JWTZ Luteni Generali Abdulrahman Shimbo 
  

Msuluhishi wa mgogoro wa darfur na Katibu mkuu mstaafu wa AU na  Dk. Salim Ahmed Salim akiagana na mkuu wa kikosi cha JWTZ kinachoelekea Darfur nchini Sudan Luteni Ally Katimbe leo katika kambi ya Jeshi hilo iliyoko Msata ,Pwani baada ya kutoa mhadhara kwa kikosi hicho kuhusu hali ya jimbo la Darfur. 

Kundi la wanajeshi wanawake wa JWTZ watakaoshiriki katika ulinzi wa amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan wanaotarajia kuondoka nchini mwezi huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. WARWANDA NA WAGANDA WAMEULIWA HUKO SO BE VIGILANT PLEASE, WE DON'T WANNA SEE BODY BAGS COMING BACK.

    ReplyDelete
  2. leo april moja,
    Warembo hawa hawaendi popote,au mnataka warabu wa JanJAweed wapete ze utamu wa dezo from tz
    Mzee michuzi leo siamini chochote utakachoweka ktk blog yako,kama unakitu sio cha April fools day,plse weka kesho
    thanx
    mdau Mzalendo

    ReplyDelete
  3. jamani tanzani kuna watoto wazuri,angalia watoto wakike hao walivyopendeza hata ndani ya magwanda. ama kweli bizimana alisema kila nguo huwapendeza.
    angalieni vimwana,kule hakuna ngoma ,msije rudi na vimimba vichanga,kwani wale wasudani kusini walivyo,nyie ndo mtakuwa mamiss kule.

    ReplyDelete
  4. Karibuni jamani Darfur. Tupo tunapeta na maisha yaliyoghali kuliko sehemu yoyote ile duniani. Karibuni Desert kwenye maraha na mapesa mengi!

    Kwanza kwa warembo kwenye picha-nyie bwana jiandaeni na saluni items huku hamna kabisa mambo ya kisaluni kama rollers, weaves, dawa,pedicure n.k ila creams za kujichibua ziko kibao. In fact inashangaza wanawake wa Darfur wanavyopenda wawe weupe kama waarabu kwa kutumia krimu za kujichibua. Mtakuta macream yaliyopigwa marufuku Tanzania zinauzwa madukani huko Nyala.

    Pili, msihofu maisha huku ni kama kawa zaidi zaidi nyuzi joto zinachanganya hadi 55c na kuna Haboob. Kuna kila kitu mnachohitaji in terms of food, clean water[kuliko hata Dar], maisha. Ila tu mfahamu kwamba mkifika huko Muhajeria na Khor Abeche marebel group lazima watawajaribu nguvu zenu za kivita wakati mwafanya patrol-AMBUSH. UN inasisitiza kwamba matumizi ya weapons iwe last solution lakini msiwe watoto wa theory-kuweni makini hakikisheni mnajilinda kwanza. Maisha yenu kwanza. wafundisheni adabu marebel watakaowajaribu. Kwa kufanya hivyo mara moja na ya kwanza hawatarudia kuwachokoza na mtatengeneza jina. Watanzania wanasifika kwa vita but here you gotta prove it. Mwaka jana Wanyarwanda kumi waliuwawa kwenye ambush huko Shangil Tobai. Isingekuwa kujitetea wote wangekwisha. They fough back japo wengi walijeruhiwa. Nyie mkija mkifuata vya UN per see yaani asilimia 100 mtashangaa.

    Tatu Marebel ni hatari bwana-acha Janjaweed. Wapo JEM, SLA branches kibao na wengine wengi tu na wana watoto wengi wanaofanya kazi miongoni mwao na wasomi wengi tu. KUWENi MAKINI na matranslator-wengine ni mainfiltrator kwa hiyo kama mna watanzania miongoni mwenu wanaoongea kiarabu ni bora kuwaengage itawasaidia sana sana sana.

    Mkifika Nyala mwaweza kujishirikisha na masuala ya kuendeleza jamii iliyopo pale kwa mfano katika kuwasaisia kupanda miti, kilimo cha mifugo, matibabu na kwa kufanya hivi mtapunguza maadui na kuwafanya watu waone nyie ni marafiki na siyo tu wanajeshi-wahindi, wabangladeshi, waegypt, wakenya wanatumia sana mbinu hizi.

    Mkija na vifaa vya vita mtalipwa hela nyingi zaidi na UN-hela ambayo inaweza kulipa wanajeshi wengi tu Tanzania-yaani kuonegezea kipato cha wanajeshi.

    Kwa kifupi nafurahia sana mwamko wa Tanzania -JWTZ kujiunga na peacekeeping-hakika hamtajuta kufanya hivi.

    ni mimi mdau wa habari.

    ReplyDelete
  5. general wetu salim unatuwakilisha wazenji keep it up

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...