THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

katuni ya nathan mpangala, maoni ya shayo

www.nathankatuni.wordpress.com
-----------------------------------------

My eye on 2009, G20 height in London

By Hildebrand Shayo

In pursuance of current global economic crisis governments of the developed capitalist countries and the major international economic institutions, such as the World Bank, the International Monetary Fund (IMF) and the World Trade Organization (WTO), have been straining developing countries to desist from economic intervention and allow global markets to determine their national policies.

International trade is one main policy area in which this pressure for re-engineering economic recovery has been persistent. In my view, governments of the developed countries and the leading economic institutions, in the spirit of neoclassical trade theories, have been demanding African and other developing nations to open or open their domestic markets to the products of the former. 

Since the 1980s, such demands have become institutionalized in the form of IMF/World Bank stabilisation and adjustment lending programs linked to trade liberalization policy conditionalities. Even the new and stylized demand for “good governance” or global governance being made of the less developed countries is now broadly interpreted as including market liberalization.

It is hypocritical on the part of the world’s economic powers to try to impose on the weak countries a free trade doctrine that they themselves cannot practice. Pre-meeting held yesterday between British Prime Minister Mr. Gordon Brown and Presidents of leading powers centred among other issues protectionism. 

The fine predictions of the neoclassical comparative advantage and free trade theories have never been achieved in real life, because governments of nation-states have always had important internal economic and political reasons for not playing by the neoclassical assumptions. 

Just as the British, on the way to establishing their industrial predominance in the nineteenth century, not only protected their own industries from foreign competition but also destroyed those of other countries, most of today’s advanced capitalist economies benefited from protectionist polices.

 Even, as I write, I hope there will be serious trade battles brewing between the United States and its European, North American and other major trading partners, over issue of protectionism. France and Germany have shown their own way. What African countries position going to be is still unidentified! The above point underlines the difficulty, ineffectiveness and double standards of enforcing an ideal-typical global free trade system. Every nation-state has its own domestic economic and political priorities that will always weigh heavily in its public policy decisions.

Given the impossibility of achieving an ideal-typical global free trade order, it is an ultimate hypocrisy for the world’s economic powers to seek inject fiscal economic stimulus packages help their economies that in a way in my view will entail such an ideal system on the less developed economies, when they-the advanced countries-are not able to practice it among themselves.

 Instead of pressuring these countries to adhere to such an unrealistic ideal-typical policy regime, through adjustment lending and other financial aid conditionalities, and bailout incentives to meet this global dispute, perhaps it would be better for all trade issues and problems to be negotiated with these countries, without the specter of financing conditionalities hanging over their heads.Kuna Maoni 13 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Napenda mijadala ya globu ya jamii kama hii ila sasa kwa kuwa inawalenga watanzania woote kama mjuavyo internet ipo mpaka vijijini siku hizi NAWASHAURI mkiandika makala kama hizi mTUMIE KISWAHILI iwafikie wote.

 2. Anonymous Anasema:

  We Shayo inaelekea uwezo wako ni kulalamikia kitu kimoja tu, kwamba Tanzania haifanyi kitu au Afrika haifanyi kitu. Cha ajabu hufuatilii jambo lolote kwa karibu. Maarifa hayaendi hivyo baba. Siku chache zilizopita Afrika imewasilisha mawazo yake London, wewe hukusikia? Tatizo tu ni kwamba mawazo hayo hayakuwa kama baadhi yetu tulivyopenda iwe. Sasa haya maneno yako ya nini:

  What African countries position going to be is still unidentified!

  Hebu tumia akili ndugu yangu, siyo kujaza blgu tu.

 3. Anonymous Anasema:

  Shayo kama hujui position ya Afrika soma hapa, tuondolee Kiingereza cha Kichagga.

  Hii ni sehemu ya hotuba ya Rais Kikwete akielezea mikakati ya Afrika. Hata kama huipendi, lakini kubali kwamba ipo, usidhani kwamba watu wengine ni wajinga kiasi hicho.

  Mkutano wa G-20
  Ndugu Wananchi;
  Jambo la mwisho ambalo ningependa kuliongelea leo hii ni kuhusu msukusuko wa uchumi wa dunia na hasa mkutano wa Kundi la Nchi Ishirini Tajiri Duniani (G-20) ambao unategemewa kufanyika kesho tarehe 2 Aprili na kumazika tarehe 3 Aprili, 2009 mjini London, Uingereza. Mkutano huu umeitishwa kutafuta njia za pamoja za kukabili kudorora kwa uchumi duniani.

  Mataifa haya tajiri ishirini, ambayo yanamiliki asilimia 85 ya uchumi wa dunia ni pamoja na Marekani, Uingereza, China, Japan, Ujerumani, Ufaransa, Afrika ya Kusini, Australia, Uturuki, Brazil, Canada, Argentina, Mexico, Indonesia, India, Italy, Urusi, Korea Kusini, Umoja wa Nchi za Ulaya na Saudi Arabia.

  Ndugu Wananchi;
  Uchumi wa dunia sasa hivi unapita kwenye kipindi kigumu kuliko wakati wowote katika historia ya dunia. Hali hii isipodhibitiwa kwa haraka na kwa umakini itakuwa na athari kubwa ya kushusha viwango vya hali ya maisha ya watu katika nchi zote duniani tajiri na maskini. Matajiri watakuwa maskini na maskini watakuwa fukara zaidi.

  Kama nilivyosema katika hotuba zangu zilizopita, kiini cha kudorora huku kwa uchumi wa dunia ni machafuko na kuanguka kwa mfumo wa fedha wa kimataifa. Tatizo lilianzia nchini Marekani na kuenea katika mataifa tajiri ya Ulaya na Asia. Mabenki makubwa na madogo yameanguka na kufilisika. Viwanda vikubwa na vidogo pamoja makampuni makubwa na madogo yamefilisika na kufungwa. Mamilioni ya watu wamepoteza ajira na wanaendelea kupoteza ajira. Maelfu kwa maelfu ya watu wamepoteza nyumba zao za kuishi. Kwa ujumla, mamilioni ya watu katika mataifa tajiri wanaishi maisha ya mashaka. Wengi maisha yao yameanza kuporomoka.

  Nchi zetu hazihusiki na kuzuka mwa matatizo haya lakini, athari za kudorora kwa uchumi wa dunia zinatukumba sote. Tayari tunashuhudia kupungua kwa bei na mahitaji ya bidhaa za nchi zetu kwenye soko la dunia, kupungua kwa idadi ya watalii na kupungua kwa uwekezaji na vitega uchumi kutoka nje. Aidha, mapato ya fedha za kigeni na mapato ya Serikali nayo yanapungua. Mambo haya hatimaye yatasababisha kushuka kwa uchumi wa nchi zetu, watu kupoteza ajira na kipato na hali za maisha za watu katika nchi zetu kuporomoka.

  Kunahitajika hatua thabiti zichukuliwe na hatua hizo ziwahusishe na kunufaisha wadau wote. Nchi tajiri duniani zinao wajibu mkubwa zaidi. Kwanza, zina wajibu wa kuhakikisha kuwa wanadhibiti hali ili uchumi wa nchi zao usiendelee kudorora. Pia zinao wajibu wa kuzisaidia nchi kama zetu ziweze kukabiliana na athari za kudorora kwa uchumi wa dunia. Nchi tajiri zimekuwa zinachukua hatua za kunusuru uchumi wa nchi zao na bado wanaendelea. Bahati mbaya nchi zetu maskini ambazo hazina uwezo wa kuwa na mipango kama hiyo, pamoja na ukweli kwamba nazo pia zinaihitaji sana, bado hazijasaidiwa.

  Ndugu Wananchi;
  Mkutano wa kesho wa Mataifa 20 Tajiri Duniani umeitishwa kujadili hatua zaidi za kuchukua kuzuia mambo yasiwe mabaya zaidi na kufanya uchumi ukue. Pia wanakusudia kuzungumzia njia za kuepuka maatizo kama haya yasitokee tena duniani. Katika mkutano wa kesho pia watazungumzia namna ya kuzisaidia nchi maskini za Afrika na zile zinazoendelea ziweze kujihami na kukabiliana na athari za matatizo ya uchumi wa dunia.

  Katika mkutano wao wa kwanza, uliofanyika Washington, Marekani, jambo hili halikufanyika. Wakati ule nikiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), nilimwandikia Rais George Bush wa Marekani, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano ule, kumuomba wayaangalie maslahi ya Afrika, lakini hatukufanikiwa. Tulipata ahadi kuwa katika mkutano utakaofuata jambo hilo litazingatiwa.

  Tunamshukuru Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Gordon Brown kwa kutimiza ahadi yake aliyonipatia kuhusu kujali maslahi ya Afrika pamoja na kutoa fursa ya ushiriki na sauti ya Afrika kuwepo katika mkutano huu wa pili. Kwa nia ya kupata maoni ya Waafrika hasa kuhusu matakwa na matarajio ya Afrika katika mkutano wa G-20, Waziri Mkuu wa Uingereza, tarehe 16 Machi, 2009 aliitisha mkutano maalum baina yake na viongozi kadhaa wa Afrika mjini London, Uingereza. Mkutano huo uliohusisha viongozi wa nchi za Tanzania, Liberia, Afrika Kusini, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Botswana, Misri, na Cape Verde ulikuwa na manufaa makubwa.

  Ndugu Wananchi,
  Nilitumia nafasi hiyo kuwasilisha maoni na mapendekezo ya mkutano wa pamoja wa Mawaziri wa Fedha, Magavana wa Benki Kuu za Afrika na Shirika la Fedha Duniani (IMF) uliofanyika hapa Dar es Salaam kuanzia tarehe 10 hadi 11 Machi, 2009. Mapendekezo hayo yalikuwa msingi wa mazungumzo yetu katika mkutano wetu na Bw. Gordon Brown.

  Kwa muhtasari, matarajio ya Afrika katika mkutano wa G-20 ni kwa Afrika kusaidiwa kujikinga na kukabili madhara ya kudorora kwa uchumi wa dunia. Miongoni mwa mambo ambayo tuliyasisitiza ni haja ya kuanzishwa mfuko maalum ambapo fedha zake zitatumika kuzisaidia nchi za Afrika kuchukua hatua za kunusuru uchumi wao kama wafanyavyo mataifa tajiri.

  Kwa maneno mengine tuliunga mkono pendekezo la Benki ya Dunia na kutaka Mkutano wa G-20 ukubali kwamba asilimia 0.7 ya fedha walizotumia kugharamia mipango yao ya kuchochea uchumi wao (stimulus packages) zitengwe kwa ajili ya kusaidia kuchochea kukua kwa uchumi kwa nchi za Afrika. Pili, tulisitiza kuwa nchi tajiri zisipunguze misaada ya maendeleo kwa nchi maskini. Badala yake misaada hiyo iongezwe kama walivyoahidi kwenye mikutano ya Monterrey, Gleneagles na kwingineko.

  Tatu, tulisema kwamba tunatarajia pia misaada kwa Afrika, na uwekezaji kutoka nje vitaelekezwa katika kujenga na kuboresha miundombinu, kuleta mapinduzi katika kilimo, kukuza biashara miongoni mwa nchi za Kiafrika na baina yake na nchi nyingine za dunia na kusaidia zaidi makundi katika jamii ambayo yanahitaji msaada zaidi (vulnerable groups).

  Nne, kwamba nchi tajiri duniani pamoja na Taasisi za Kimataifa za Fedha Duniani zilegeze masharti na kupunguza urasimu wa kupata fedha za misaada na mikopo kwa kutambua kwamba hiki ni kipindi kugumu na cha dharura. Aidha, masharti ya kukopa kutoka vyombo vingine vya fedha yalegezwe pia.

  Tano, kwamba nchi tajiri zisaidie nchi za Afrika kujenga mitaji ya vyombo vya fedha vya kikanda kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika. Na, la sita, kwamba, nchi tajiri zitakubaliana kuruhusu uwazi katika mabenki yao na taasisi zao za fedha ili kuwezesha nchi za Kiafrika kufuatilia na kurudishiwa fedha, majumba na rasilimali zilizoporwa kutoka katika bara letu na kuhifadhiwa kisirisiri katika mabenki ya nchi tajiri.

  Ndugu Wananchi,
  Tunamshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu Gordon Brown kwa kuyapokea mapendekezo haya ya Afrika kwa moyo mkunjufu na kuahidi kuyafikisha na kusaidia kuyatetea katika kikao hicho. Pia tunamshukuru amepokea rai ya Afrika ya kuwakilishwa kwenye mkutano huo kwa kumwalika Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Meles Zenawi, ambaye atatuwakilisha kwa kofia yake ya Uenyekiti wa NEPAD.

  Ndugu Wananchi;
  Mkutano huu wa G-20 ni muhimu sana kwani unalo jukumu la kihistoria la kuuokoa uchumi wa dunia. Kwa msemo wa Kiswahili tungeweza kusema kuwa kazi ya mkutano huu ni ya kufa na kupona. Mkutano ukifanikiwa, sote tumenusurika. Ukishindwa sote tutakuwa mashakani na tunaweza kuangamia. Tuwatakie viongozi wa G-20 heri na fanaka tele katika mazungumzo yao. Hatima ya maisha na ustawi wa dunia na watu wake uko mikononi mwao.

 4. G.shayo Anasema:

  Brother michuzi habari za asubuhi,asubuhi nimepokea msg kutoka kwa mdau wa blog yako,sasa baada ya kusoma msg,ilikuwa inasema leo umechangia mada kwenye blog ya Michuzi?kuna watu wanakukandia huko,mimi nikamwambia siyo mimi,kwahyo bro Michuzi Shayo wanayemtaja kwenye blog yako siyo mimi Shayo wa blog ya Ujasiri Amali.asanteni sana,BARIKIWENI.

 5. Anonymous Anasema:

  Shayo,thanx for the Rhetoric!Je,Afrika yenyewe imeungana au kushikamana kiasi gani katika kukabiliana na Global Recession?Je,imesha bainisha ukubwa na uzito wa Tatizo lenyewe?Na,imejizatiti kwa kiasi gani katika kukabiliana na Tatizo hilo la Mkanganyiko wa Uchumi "japo kutatua asilimia ngapi" ya tatizo zima?Does Africa really know what she should be doing?Shayo anasema bado msimamo wa Afrika haujatambulika!Nani atakayeutambulisha kama si Afrika yenyewe?Mimi nafikiri Maprofesa wetu wajitahidi wanapoelezea kitu wawe na ujasiri wa "kupendekeza Afrika ifanye nini" ili kujikwamua kutoka hapo ilipokwama" Our own learned experts should have the audacity to propose tenable and feasible solutions to our own brand of economic problems rather than simply ending up "merely Theorising!"on what already exists in the Domains of Global Economic Literature!Hata hivyo nakupongeza Shayo for showing us that atleast you've gone to school!Keep it up,I know you can do better than that!That is ,Showing Africa the way!Still remember scholars like Walter Rodney?Justinian Rweyemamu?Clive Thomas?Rene Dumont?Rostow?and so many others,just to mention a few!So,walk in their footsteps,I know you can!

 6. Amani Paul Anasema:

  Dear wasomaji
  mtu anapowakilisha mada humu siyo kuwa analalamika.
  Ni uwanja wa kujaribu kuona ni kitu gani kinachoendelea na ni uwanja wa ku debate kwa hoja. Mimi sioni kama shayo analalamika, yeye anasema kama nilimwelewa vizuri nchi masikini ziwe makini na kujipanga katika kuelewa kuwa mtiririko wa unyonyaji uko pale pale

  mkutano uliofanyika dar na kuhudhuriwa ulikuwa na mambo mazuri sana, ila namna baadhi ya viongozi walivyokuwa wana jieleza kuhusiana na hili tatizo la kiuchumi ilikuwa inasikitisha.

  niliangalia kwa makini debate ilivyokuwa inaendeshawa pale ndani na kwa kweli it is sad. rejea video clip zilizopo kwa mtandaoni na utajionea wewe mwenyewe.

  Cocopy na kupesti hutuba ya rais ili kuonyesha kuna kitu kinachofanyika haisaidii,

  suala hapa ambalo shayo analizungumzia ni kuwa huu unafiki wa hawa mataifa matajiri tutakabiliana nao vipi?

  Hivi katika mkutano wa dar ulimsikiliza yule mwakilishii wa South Africa?

  Iko kazi kweli kweli

 7. Anonymous Anasema:

  Africa we have perpetual recession! Sasa sijui huo muarobaini wa G20 utasaidia vipi.

  Hivi kweli nyinyi wasomi hebu tusaidieni... Yaani all of the sudden Africa tumeathirika na financial crisis? kwa uchumi upi? ..sana sana sema watakaoumia ni viongozi wetu ambao wamezoea kuomba omba..na kurudisha hizo hela huko huko ulaya in form of "vijisent".

  Kwa hiyo wakaoathirika ni mafisadi waliozoea hela za bure akina Chenge and co. Mwananchi wa kawaida ambaye anaishi kwa Jembe la mkono..sioni matatizo ya Wall Street au Lehman brothers yatamuathiri vipi!....financial crisis iwepo isiwepo..haoni tofauti!

  To be honest, mwananchi wa kawaida wa Tanzania, Malawi au Cameroon..haoni impact yoyote..maana hali yake imekuwa duni miaka nenda rudi...Sana sana...mwananchi wa kawaida angepata ahueni kama tungesweka mafisadi wa pesa ya umma..kule gerezani Keko...the impact of that could be great than mgao wa Stimulus package ya akina Obama na wenzake..! Kwa hiyo ni unafiki kuja kumwambia mtu huyu huyu eti hali yako imekuwa duni kwa sababu ya uchumi wa dunia..Je huo uchumi ulivyokuwa safi mbona hakupata auheni ya maisha bora?

  Hii G20 business ni ya hao hao wazungu huko na washirika wao wachache humu kwetu akina Chenge na Lowassa. Sisi tunaweza kuathirika perhaps kutokana na utalii au wanaotuma remmitences..otherwise..this is a perfect opportunity kwa mafisadi kuiba na kuhamishia hela yote Dubai na kutwambia ni "mtikisiko wa uchumi wa dunia" ndo maana hatuoni chochote cha maana.....Wadanganyika kazi tunayo jamani...

  Hao akina Shayo and co..ni wale wale wasomi wetu..ambao wanaamini kwamba Africa to solve its problems we need to negotiate as equals with the west. I agree with this assumptions. But kama waswahili wasemavyo..huwezi tembea kabla hujatambaa!

  Africa kabla hatujapiga kelele za kudai mgao wa stimulus package we need to adress the basics of governance..TUJUE NAMNA YA KUJITAWALA KWANZA. So far hatujui! Kusudi tukipewa huo mgao uweze kufanya kazi yake..for now hata G20 wangetupa Millions and millions..zitaishia kwenye matumbo ya wachache na sisi tutaendelea kugawana umasikini.

  Hivi ..jiulizeni..juzi juzi tuliambiwa kwamba soko la mafuta limeathirika kwa kupanda bei..mpaka kiranja wetu mkuu Kikwete akasema kwamba tufunge mikanda...ni tatizo la kidunia..leo mafuta yameshuka kwa asilimia kubwa sana..hebu piga picha bei ya mafuta Africa especially bongo..imeshuka kiasi gani?

  Sasa sijui huo uchumi wa dunia ukipona..sisi tutapona vipi! My motherland Africa..never ceases to amaze me!

  "Ni mipango ya Mungu" so Kikwete will say.

  Masanja,

 8. Anonymous Anasema:

  Nadhani wengi mliochangia maoni ya Shayo mmesahau kuwa Gavan wa Benki ya Tanzania, alisema kweney mkutano LOndon kuwa Credi Crunch haiweze kuathiri Africa. aibu sasa..maana watoa misaada na wanunuzi mazao yetu ni hawa walioathirika, na kama hawanunui tena au kutoa misaada tena na sisi tunaathirika, ndio kelele sasa zinaanza.
  Mkutano ulikwa wa watananzania waishio nje(Diaspora)

 9. Juma Al-barik Anasema:

  Wandugu, naungana na Masanja wa hapo juu, na Shayo aliyotoa hii mada.
  ukiangalia kwa makini huu mkutano wa G20 utagundua kuwa Africa ambayo ndiyo wazalishaji wakuu, na ambao wanatarajiwa kuwa next destination ya kitu wanachokiita trade credit ili kuzisaidia kukua na kujenga uwezo hazijawasilishwa ipasavyo. hivyo kwenye hiyo communique hawa mabwana watakayosign huko excel leo africa ni kama iko excluded

  Kualikwa kwa ethiopia kunawakilisha PAN, Gadafi AU. South Africa ni hao hao tu.

  Unajua usijidanganye,
  Africa tungetumia productivity capability zetu
  tukatumia intellectual capability zetu
  tukawa na nguvu na msimamo mmoja, then tutaweza kusema tunahitaji hiki au hatutaki kile

  Kwa sasa, hawa mabwana wanatumia divide and rule na kujaribu kutulinganisha kama maembe kwenye kapu wanapotaka kuchukua rasilimali zetu.

  Huu ndiyo unafiki kama nimemuelewa vizuri shayo anaozungumzia.

  nakuambieni wachanche wenye mianya hu ndiyo wakati wataweka rehani nchi zao bila kujali kizazi cha mbeleni

  Kweli wewe unafikiria "tax heaven" zinazozungumziwa zitajulikana kwa public?
  Leo wanazungumza kwenye G20 ati wablack list nchi ambazo viongozi wake wanafilisi nchi zao, unaona kweli hapa kuna kitu?

  Hiyo financial regulation na transparent wanaozungunzia ni kwa nini viongozi wa kiafrica wasihusishwe? na badala yake waletewe model ya kutumiwa?

  Leo ukiwauliza kwa nia na uthibitisho ni kitu gani wamefanya toka G20 iliyopita, utasikia kisingizio tuangalie kwanza hii credit cruch

  Anyway yapo mengi ambayo tunatakiwa tuyaelewe, na siyo kukubali kila tu wanchoamua hawa mabwana. Tuna rasilimali, na hawa mabwana wanatuhitaji sana kuliko sisi tunavyowahitaji

  mchango kama wa shayo, au mashaka, au masanja na wengineo siyo kwa manufaa ya tanzania tu, ni kwa ajili ya nchi zote zile ambazo wanadhirika na huu unafiki wa hawa mabwana.

  Tusimsingizie mungu, we need to put our house in order na kujaribu kufanya mambo yenye matunda kwa vizazi vijavyo.

 10. Anonymous Anasema:

  Inafurahisha na kufundisha unaposoma hoja za waafrika kuhusu masuala ya kidunia. mara nyingi sisi ni kulalamika tu. kama alivyosema mchangiaji mmoja, akina shayo ni wengi sana Afrika, kazi yao ni kulalamika na kuwaita wengine wanyinyaji, makabaila nk. yaani tunaowaona makabaila na mabepari wa ulaya tu bila kujua kwamba makabaila na mabepari wabaya zaidi ni wale ambao tunawatengeneza hapa hapa Afrika!
  kama tunatafuta ni nani anayelifanya bara la Afrika kuwa masikini zaidi, hatuwezi kuvuka kwanza bahari na kwenda ulaya au Marekani! ni kuangalia hapa hapa karibu yetu, tunaona nini??
  Ninakubaliana kabisa na maoni ya mchangiaji mmoja kwamba mtanzania wa kawaida anayeishi vijijini na anayetegemea kilimo cha jembe la mkono anaguswa kwa kiasi kidogo sana na athari hizo. kwani ni nini cha ajabu ambacho kitatokea ambacho hakijawahi kumpata? tayari economic crisis anaishi nayo katika maisha yake yake yote!
  lakini cha muhimu sisi kama waafrika tujadili na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu wenyewe. mfumo wa kidunia hauna cha ujomba kama sisi tunavyofikiri, kwa hiyo ni kupoteza muda kuanza kuilaumu ncho moja kwa sababu ya matatizo yetu. Hizi dozi tulizopatiw ana maprofesa wa chuo kikuu cha Dar es salaam ambao wengi wao ni wafuasi wa falsafa ya Maxism haitusadii lolote. ni mawazo yaliyopitwa na wakati na hayatusaidii sisi kama tanzania au afrika kuondokana na matatizo yetu.

 11. Anonymous Anasema:

  Dr Shayo kwanini usiandike mada zako kwa kiswahili? tulio wengi tunapenda kujadili ila hatuna utajiri wa maneno ya kiingereza, nadhani huku ni kutafuta hits za kirahisi juu ya jina lako mtandaoni.hili ndio tatizo la wasomi wa bongo.mbona kuna makala nyingi nzuri za kiswahili? michuzi piga marufuku kiingereza kwenye blog yako.

 12. Anonymous Anasema:

  Shayo ni anapenda kusema kila mara .watanzania tunataka vitendo.mara ooh Tanzania haiukuchangamkia fursa ya kombe la dunia.yeye yuko UK kama alijua kuna hilo kwanini hakwenda ubalozini au kuwasiliana na wizara?
  au hana contact za wahusika zaidi ya kuleta maandishi yake kwa michuzi?
  huyu bwana anataka sifa tu kwa wana blog.hana cha maana.
  ukitaka kujua limbukeni blog hii ni ya watanzania ambao kwa asilimia kubwa tunaongea kiswahili.yeye na mwenzake mashaka wanatukoga kwa kiingereza.sasa kama kiswahili mmesahau na mnataka mje kutuongoza jee mtakuwa mkitumia kiswahili bungeni na kwenye mikutano?
  shayo na mashaka hawana miaka 13 nje na wamekwenda wakubwa.kweli wamesahau kiswahili?

  mzungu akija Tz Akakaa miaka 12 anaweza kusahau kizungu na akawa anatuma maoni kwa ndugu zake wa ulaya kwa kiswahili?

  shayo acha kujionesha na kizungu chako cha Daily News kwa michuzi.

 13. suzan kimaro Anasema:

  Wadau wasomi wetu jamani andikeni kwenye lugha ambayo sote tutafaidika.

  Wewe Dr shayo kama voice of Ameica wanaweza kukuhoji kwa kiswahili na nilivyokuzikiliza jana saa moja jioni ulikuwa unaelekea kukifahamu kiswahili vizuri, basi kijana wetu tuandikie kwa kiswahili nasi tufaidi utaalamu wako.

  aksante.