JUMLA ya vyuo 17 vinatarajia kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini. 
  
Kongamano hilo litakalofanyika Mei Mosi hadi  2  mwaka huu katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, linatarajia kuwakutanisha wanafunzi hao na waajiri mbalimbali wakubwa. 
  
Kongamano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Trinity Media Limited limelenga katika kuboresha myenendo ya vijana hususani katika kukuza vipaji,elimu na ujasiriamali. 
  
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa  Idara ya Habari (MAELEZO) jana mratibu wa kongamano hilo Austin Makani  alisema  wanavyuo watapata fursa ya  kubadilishana mawazo kati yao na waajiri ili kuweza kuwasaidia  wanaohitimu katika soko la ajira. 
  
“Wanavyuo wengi hupata shida ya kutafuta ajira, wengi wao wanatafuta kazi kwa muda mrefu hii ni kutokana na ukweli kwamba  wanauelewa mdogo wa soko la ajira nchini. Kuwakutanisha na waajiri itawasaidia katika kufikiri kwao na pia kujua wapi pa  kuanzia katika kutafuta ajira.” alisema Makani. 
  
Pia mratibu huyo alieleza kuwakutanisha wanavyuo hao si tu kusaidia  kusikiliza mada ila pia watapata fursa ya kujichanganya na kuwauliza maswali waajiri yaani networking. 
  
Baadhi ya mada zinazotarajiwa kujadiliwa katika siku hiyo ni pamoja na mada ya ujasiliamali itakayotolewa na kitengo cha ujasiliamali cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam,jinsi ya kujiajiri kwa njia ya mikopo mada itakayotolewa na Tanzania Gatsby Trust inayoshughulika na masuala ya mikopo.Pamoja na masuala mbalimbali yausuyo ajira kwa vijana. 
    
Waziri wa Kazi,Ajira  na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma anatarajiwa kutuma muwakilishi atakayefungua kongamano hilo. 
  
Kongamano hilo linalofanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini litakuwa linafanyika kila mwaka kwa lengo la kuwasaidia wanavyuo kote nchini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Inafurahisha kuona vijana wanahusishwa kuandaa vitu kama hivi ambavyo vitawanufaisha.Hongera Austin Makani na organization yenu

    ReplyDelete
  2. Thats what am Talking about brother....ohooo JK alisema ajira kwa vijana mmmekaa tuu hamsumbui brain zenu..mnataka mteremko mtaendela kutoa macho...keep the spirit Austin and the others...I beleive million of people will find it intresting and valuable as i think.

    Qr

    ReplyDelete
  3. Mchuziiiiiiiiii Unaona mambo hayo tunataka vichwa kama hivyo.

    Nimeipnda hiyo nitashirikije?

    Na je itakuwa kila wakati! na mara ngapi?
    Duh duh sio mchezo huyu jamaa anaitwa i mean Makani nimekukubali sana.

    Mjasiriamali

    ReplyDelete
  4. "Baadhi ya mada zinazotarajiwa kujadiliwa katika siku hiyo ni pamoja na mada ya ujasiliamali itakayotolewa na kitengo cha ujasiliamali cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam,jinsi ya kujiajiri kwa njia ya mikopo mada itakayotolewa na Tanzania Gatsby Trust inayoshughulika na masuala ya mikopo.Pamoja na masuala mbalimbali yausuyo ajira kwa vijana."

    Hizi taasisi zisizo za kibenki kama Gatsby, DECI nk ni moja ya vyanzo vya mtikisiko wa uchumi unaoendelea sasa.

    ReplyDelete
  5. Anonymous 4:17pm... we need to change, sio kila kitu ni DECI au kama upatu, unakopa na kukatwa riba inayokubalika dunia nzima sio 300% uje usikilize usaidiwe. Kubali wito kataa neno ndio neno la busara. Nijuavyo mimi si mratibu mwenyewe annony 3:58pm uje tuu Karimjee upate ufafanuzi zaidi kuanzia saa 2 asubuhi. Sisi ambao tumepata nafasi ya kusoma nje ya nchi hii, mada kama hizi hutolewa kwa wanafunzi vyuoni.. big ups brother kuanzisha jambo zuri kama hili nchi mwetu Tanzania... where brain ndio mahala pake

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2009

    Well done Austin. You have my full support and prayers on this. I am really proud of you. Keep Up the spirit.
    Lots of Love, BIG SIS
    Cleo Reena

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...