Michuzi, 
Hivi  ni kwa nini watanzania wengi wanazichanganya hizi herufi mbili 'R' na 'L'? Ninajua kuwa watoto ndio wana tatizo la kubadilisha 'R' na kutamka 'L' kwa mfano 'langi' badala ya 'rangi'. Lakini kuna watu wengi wazima ambao wana tatizo hilo. 

In fact, hata waandishi wa habari wanazichanganya hizi herufi...kila siku nikisoma magazeti naona 'msululu' wa magari badala ya 'msururu' wa magari au 'kombola' badala ya 'kombora'.

Je kuna njia ya kuibadilisha lafudhi hiyo?
Mdau Murad

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Mie Binafsi naweza Kuunga Mkono na Kupinga.

    1. Shuleni Lazima kujuwa kuweka Herufi sawa za Misemo au Msemo sababu unaweza ukawekewa makosa.

    Ila Kiswahili chakuongea Sehemu si tatizo ni kuelewana tu kwani ni Lugha na Tanzania ina makabila mengi kwahiyo mtu akiongea mchukulie kwa kuelewa.

    Katika kuandika ndio lazima tujuwe tunaandika inavyotakiwa Salama sio Sarama au Hatari sio Hatali.

    Sawa na Wenzetu Marekani hukosea mengi Accent za West na East ni tofauti au hata wakiandika utaona mpaka imewakaa watu wenzetu weusi You ataandika U, au tukiwacha hiyo Tarehe wao Marekani wanavyoweka Tofauti na Sie sababu wana Rules za za American/English utakuta Herufi nyingi wanakosea. Yote ni Lugha tu. Kwani siku hizi Mtu Akikwambia naona Umekatwa Upara unaweza kupigana unachukulia Vengine. John.

    ReplyDelete
  2. Ubongo wa binadamu unahifadhi yale unayojifunza kwa kupitia sensory organs ikiwa ni pamoja na kuona au kusikia. Kwa maana hiyo, tatizo la kuchanganya R na L ni tatizo la spelling ambalo limo katika lugha zote - sijui Kichina ambacho naambiwa hakina herufi - na ni matokeo ya kutoyaona au kutoyasikia maneno yaliyoandikwa au kutamkwa kisahihi mara kwa mara. Kama umezaliwa Tabora(la) basi utakuwa umezoea kuwasikia watu wote wakipaita Tabola (ra) na kama unatoka Sirari "tulale" itakupa tabu unless uwe unasoma nyaraka za Kiswahili zilizo na neno hilo. Si hivyo tu, bali pia mazingira yana uwezo juu ya tabia zetu ikiwa ni pamoja na tunavyozungumza. Ukizaliwa na kukulia Mombasa basi kiberiti utaita kiribiti hata kama unaona imeandikwa vinginevyo.

    Siamini katika Origins of the Species ya Darwin lakini wakati mwingine huona kuna ukweli kidogo ndani yake kwamba evolution inatokea kidogo kidogo - wataalamu wa lugha wanaweza kukuambia jinsi lugha zinavyobadilika kadiri miaka inavyokwenda.

    ReplyDelete
  3. Hii yote inatokana na asili ya mtu. Kwa mfano kule Mara (Musoma) na maeneo mengi ya kanda ya ziwa herufi 'L' ni almost haitumiki. Pia ukiangalia watu wa pwani, herufi 'R'hawapendi kuitumia. Ndio maana mara nyingi unakuta watu wanachangana wakati wa kuandika.

    ReplyDelete
  4. Wanaokosea kutamka hizo herufi kwenye maneno ya kiswahili mara nyingi ni watu wa kuja (kutoka Bara) Wengi ya hawa wenzetu wametokea vijijini kama Musoma, Bukoba, Mwanza na wamekua wakiongea lugha zao za asili kiasi kwamba zimesababisha hata lafudhi zao za kiswahili kuathirika. Kiswahili kitamu na halisi kinazungumzwa ukanda wa Pwani na maeneo ya karibu.

    ReplyDelete
  5. Tatizo kubwa la watu wengi ni kutokuwa makini na wanachoongea, wamezoea kiasi cha kutotambua kwamba wanafanya makosa. Inahitaji jitihada Binafsi za hali ya juu sana kuweza kutumia lugha fasaha.
    Kwa kuwasaidia wenye matatizo hayo, unaweza kuwa unawakumbusha kwa upole na unyenyekevu wanapotumia herufi hizo kimakosa. Usimcheke na wala usimkaripie,usimkosoe kama mtoto mdogo, na mueleze kwa moyo mkunjufu kabisa kwamba Si hivyo ni hivi. Nina uhakika kama watu wataamua kubadilika na kusaidiana halitokuwa tatizo kubwa.

    Mdauz

    ReplyDelete
  6. John umechemka wanapoandika U badala ya you sio kwa sababu hawajui ni kufupisha tokana na verbal ni staili tu hakuna chochote.
    Kwa watanzania wengi ni sababu ya "MOTHER TONGUE" au lugha zetu za asili(kabila).Kwa mfano:-Sisi wahangaza tunachanganya R na L.Katika R tunaweka L,ingawaje huwa tunamaanisha R.
    Wahaya hawawezi sema ku"fa" wanasema Ku"fwa".Pia wanaongeza "H" katika maneno yanayoanzia na (A,E,I,O,U).Ua wanasema Hua nk.Anyway hata Wajamaica wako hivi hivi ka wahaya.
    Wachagga wanasema Msee badala ya Mzee.
    Hata wazungu unaweza kusikia tofauti Wajerumani na wafaransa wakiongea english "w" wanasema "v" sababu kwao ndivyo inavyoitwa.
    Hii yote ni Mother-tongue effect.

    ReplyDelete
  7. Tukifanya mambo mawili tu tatizo linapungua kama sio kuisha. Mosi ni kuimarisha elimu yetu ya msingi kwa kuwa na walimu stadi, vitendea kazi na maslahi ya kuridhisha. Pili ni kujenga utamaduni wa kujisomea. Watanzania wanapenda kujisomea, shida wanapenda kujisomea magazeti ya udaku. Kwenye magazeti ya udaku haya matatizo ya 'reoreo' yapo pale pale. Kuna uhaba wa vitabu vilivyoandikwa vema kama vya marehemu Shaban Robert au walau hata vitabu vya kuburudisha +tu kama vya Willy Gamba.

    ReplyDelete
  8. Naungana nawe ulosema kuwa lugha ya awali (mother tongue)ndio huweka msingi wa matamshi yako katika lugha nyingine kama hayo matumizi ya R na L ktk Kiswahili. Inahitaji juhudi binafsi ili kuzingatia matumizi sahihi ya herufi katika matamshi na kuandika pia. Ni rahisi kukosea kutamka kuliko kuandika, makosa ktk kuandika yaweza kuwa ni UZEMBE wa kutozingatia mafundisho ya SARUFI shuleni.
    Adhaniaye kuwa watu wa Mwambao hawakosei matumizi ya hizi herufi, namwomba awasikilize atakuta ni "L" kila mahali, kwa sababu ya mazoea wanadhani ni sahihi. Hukosea pia kwa kusema "Chengine" badala ya "pengine" , "Hichi" badala ya "hiki".

    Watanzania tunaelekea kuwa jamii ya MACHOTARA wa lugha. Tunababaisha Kiswahili, Kiingereza na lugha za makabila yetu au wazazi wetu. Ukikosa kumudu lugha yoyote basi unapoteza nguvu ya mawasiliano na utamaduni pia, unakuwa kama mkimbizi au mtu asiye na makao ktk jamii husika.

    ReplyDelete
  9. Tunaawambia kila siku wale "urojo" wanabisha wameng'ang'ania "hot chair" ona sasa!

    ReplyDelete
  10. Wahaya na wanyalukolo wengine wabara wengi tu... ndio wana huo mchezo! Hawajui tofauti ya "L" na "R", wala "a e i o u" na "H"!!!!
    Inachefua kweli kama mswahili!!! Kisha tukisema tunaambiwa "wapwani hao wanajifanya wanajua sana kiswahili". Na walimu nao ni mambumbu vile vile!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 01, 2009

    wee unayeongea eti watu bara, wanatatizo hilo, na kusema eti Mwanza na Musoma na Bukoba ni kijijini ushawahi kufika huko au unaongea tu.si ajabu mkoa uliotoka ni kijijini ndo maana unaongea pumba, ungesema ni kwa sababu ya matumizi ya lugha tungekuelewa na si swal la kijiji, wacha upuuzi mshamba mkubwa ala.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 01, 2009

    Nampinga kabisaaaaaa mtoa maoni APRIL 30,2009 @ 6:48PM. Ushindwe kabisa. Nimeona watu wengi sana kutoka Pwani Kiswahili chao ni sawa tu na watu wengine. Tukianza kukosoana hapa tutakusona mpaka mwisho wa dunia. Kwa mfano pale mwandishi anapotakiwa kutumia "H na A, ZA na DHA, SA na THA, R na L." Nimekuwa nikisoma hizi comments za watu watu wengi tunakosea sana katika FASIHI SIMULIZI na FASIHI ANDISHI. Wote tukubaliane.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 01, 2009

    kiswahili kigumu kwa hiyo ruksa kubofoa kidhungu pia.

    ni kama wazungu lugha yao lakini nao wabovu kwa maneno haya their and they, here and hear, to and too na kubwa ni wanavyoandika than kila siku utaona badala yake wameandika then halafu hawa watu wana masters but still

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 01, 2009

    Mbigiri nakupa tano. Umegonga hapo. Wapo wasemao 'hakili' wakimaanisha 'akili'. Wapo pia wanaosema 'umeshahona?' wakimaanisha 'umeshaona?'. Hilo ni tatizo litokanalo na 'dozi kali ya lugha mwitu' yaani lugha msitu au pori nukipenda. Yaani vernacular languages ukipenda. Lakini pia ni uzembe mwepesi yaani kutokuwa waangalifu au kutojali kwa wahusika.
    Ingawa uwezekano wa kuelewana upo, kuna sababu gani ya kuongea lugha ugoko? Kwa nini mtu asiongee lugha fasaha moja kwa moja? Huu ni uzembe ambao hutufanya wabongo tuharibikiwe si kaytika lugha tu bali kwa mambo mengi ya kitaifa pamoja na maslahi kwa/ya waTanzania*

    Binka

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 01, 2009

    DUUUUUUUUUUU!! KWELI HII KALI! KUNA VIJIJI VINAITWA MUSOMA, MWANZA BUKOBA???????????!!!! DA! KAZI IPO KWA WATANZANIA!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 01, 2009

    Hii yote ni kutojua lugha. Swala hili nishawahi kuliuliza kwenye blog ya fotobaraza. Watanzania wengi walioenda na wasioenda shule,cha kushangaza ni kuwa wala hawawezi kuongea lugha yao kiswahili kwa ufasaha, hawawezi kuongea kizungu kwa ufasaha hata lugha za kikwao kwa ufasaha AIBU TUPU. Inaishia kuongea kwa kuchanganyachanganya kiswahili kibovu kizungu kibovu matamshi ya kusikitisha TABU TUPU. Waalimu, watangazaji hata bungeni.

    KILI, BG

    ReplyDelete
  17. Mdau wa GhubaMay 01, 2009

    Wewe usiejua hata Mwanza, Musoma na Bukoba kuwa si vijiji unaweza kutuambia nini wewe? si kweli kwamba watu wanaotoka bara kama unavyodai mwenyewe ndio wanaoharibu lugha, kwani hata haoa wazaramo wako pwani mbona wao ndio wanaofurunda L na R?

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 01, 2009

    wewe Binka, unayesema kuongea namna hiyo ni uzembe, kweli nimeamini wewe ni mjinga, kama ni uzembe umeonyesha ulivyo mzembe. Utatamkaje neno ug'oko uliite ugoko. Hapo ndipo unajidhalilisha mwenyewe na kujitusi. Cha muhimu hapa sio kuongea cha muhimu je watu wamekuelewa. Huwezi kunibadilisha kama natoka Kagera nisiongee R badala ya L ulimi hajazoea, au nitamke H badala ya a, e, i, o, u. Siliza hata wazungu wanapoongea kingereza msikilize Mdachi au mjerumani atakapotamka neno W atalitamka V, V ataitamka F, J, Y etc. Hakuna kabila hapa Tz lisilokuwa na laaja (lahaja, or Rahaja, or raaja?) yake angalia watu wa pwani wanatamka HICHi badala ya iki, je ni sawa?, mamake, babake, mjombake badala ya yake, wanatumia ngei badala ya nipe, kiswahili hicho? Mkurya hana L, Mnyambo hana L, Mhaya hana R, 'ng', h, Mhehe atakwambia nimefulahi, mmakonde atakwambia ntu yule, mchagga atakwambia nji hii, msee wangu. Cha muhimu ni je mwongeaji ameeleweka kile alichowakilisha mbele ya watu na wala si kuchambua vitu vidogo, kumbuka kiswahili ni mchanganyiko wa lahaja (laaja) mbali za lugha za makabila na lugha za kigeni kama kiarabu, (kiharabu?) kiingereza, kireno, kijerumani etc

    ReplyDelete
  19. MchunguziMay 01, 2009

    Hata mdogo wake Michuzi anajiita Michuzi Junia ana tatizo hilo.
    Kila siku tunamsahihisha lakini bado hasikii tu.
    Nendeni kule kwenye Bulogi yake ya "JIACHIE" mutaona kile ninachokisema.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 01, 2009

    Hahahahaaaaaaa
    Burudani kweli kweli maana mimi kila siku nagombana na mume wangu juu ya swala hili. Yeye ni mtu wa Shinyanga..na inanikera sana tunapokuwa na marafiki anaweka L badala ya R...ni balaa na disaster pia. Ila nishaona kuwa hakuna jinsi atabadilika..it traces its way back into anakotoka. Lakini I must admit inaboa sana na inatia kinyaa pia.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 01, 2009

    nimefurahi sana kuona swali hili limeletwa hapa na wengi mmejitahidi kulichambua kulingana na uelewa wenu.
    sababu nyingi mlizozitoa zinaweza kuchangia kiasi fulani lakini sio sana. hasa hii ya watu kutofahamu utamkwaji sasa ni upi,lakini kwa wale ambao wanafundishwa lakini inashindikana kutamka kwa usahihi inakuwa ni tatizo KTK UBONGO, UBONGO WA BINADAMU umegawanyika ktk nusuduara mbili kubwa [two hemispheres],na ndani ya hizo nusuduara kuna centers zinazohusika na mambo mbalimbali.kuna mishipa ya fahamu inayotoka ktk center ya matamshi[speech]ikiwa ktk fungu moja inalekea ktk ulimi lakini inapitia ktk nuclei tofauti tofauti, hii njia inaitwa tractus corticonuclearis, sasa ikitokea ikapata madhara kwa pandezote mbili za ubongo kwa namna yoyote ile, mhusika anapata tatizo la matamshi=dysathria, R ataitamka L n,k. HII INANIPA CHANGAMOTO YA KUJA KUFANYA RESEARCH YA KINA HUKO ILIKUJUWA UHUSIANO ULIOPO KATI YA MATAMSHI YA WAHUSIKA NA UZIMA WA sehemu hizo nilizo kwisha zitaja hapo juu.inawezekana kuna uhusiano wa kuathirika ktk maeneo hayo bila watu kufahamu,ama ikawa ni kutokufahamu usahihi wa maneno.shukrani kwa michango yenu.

    *****xxx*****

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 01, 2009

    hahaha wadau asante kwa kibuludisho hiki. Mi naona laha ndani ya loho. Nimefalijika sana!

    Mdau Lehema ;)

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 02, 2009

    oooh this is so fantastic!!

    nimeanza siku njema sana!!

    habalini wadau wote??amjambo?mie safi tu

    L na R

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 02, 2009

    Mbona hata wewe mtoa mada umekosea,sio "msururu" neno sahihi ni "MSULULU"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...