MABAHARIA WA BOTI YA RUBANI YA SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR WAKISHUSHA MIILI YA MAREHEMU WATATU WA AJALIM YA MELI HIYO AKIWEMO MTOTO WA KIUME NA WATU WAZIMA MMOJA WA KIUME NA WA KIKE
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA AJALI YA MELI YA FATIH IKIWA IMEBIRUKA KATIKA BANDARI YA ZANZIBAR IKITOKEA DAR-ES-SALAAM IKIWA NA ABIRIA NA MIZIGO MPAKA SASA TAYARI MAITI TATU ZIMESHAPATIKANA WAFANYAKAZI WA MSARABA MWEKUNDU WAKIONDOA MWILI WA MMOJA WA MATI WA AJALI YA MELI YA FATIH WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WA KAMATI YA UJENZI NA MAWASILIANO WAKIFUATILIA UTARATIBU WA UOKOAJI WA ABIRIA WA MELI YA MV FATIH USIKU WA 29-5-2009, KUTOKA KULIA ZAKIA OMAR JUMA CUF, MZEE ALI USSI CCM,MAKAMO MWENYEKITI HAMADI MASUOD HAMADI CUF, RAMADHANI NYONGE CCM NA MWENYEKITI WA KAMATI HIYO KAMAL BASHA CCM.
WANANCHI WALIOFIKA LEO ASUBUHI KUSHUHUDIA AJALI YA MELI YA FATIH WAKIWA NJE YA BANDARI YA MALINDI KUTAKA KUJUWA WATU WALIOPATA AJALI HIYO YA MELI
WANUSURIKA KATILA AJALI YA MELI YA FATIH WAKIJIPATIA MSOSI KATIKA KITUO CHA POLISI
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KWA VIJANA WA MSALABA MWEKUNDU KUTOA HUDUMA KWA MAITI WA AJALI YA MELI
BAADHI YA MALI ZILIZOOKOLEWA KATIKA MELI ILIOZAMA KATIKA BANDARI YA ZANZIBAR IKITOKEA DAR-ES-SALAAM YAKIWA KATIKA BANDARI HIYO BAADA YA KUOKOLEWA. MAJINA YA WALIOPOTEZA MAISHA BADO KUPATIKANA NA IDADI KAMILI BADO KUJULIKANA KWANI LAZIMA NDUGU WA MAREHEMU WAJULISHWE MWANZO, NA JUHUDI ZA KUOPOA MAITI ZINAENDELEA.
Picha zote na mdau Othman Maulid Mapara
HABARI KAMILIFU

MELI ya mizigo ya inayomilikiwa na Kampuni ya Seagul, Mv Fatih, imepinduka na kuzama katika Bandari ya Malindi Zanzibar usiku wa kuamkia jana huku maiti za watu watatu zikiwa zimepatikana zikielea na watu wengine 27 wamejiokoa katika ajali hiyo ambapo mamilioni ya mali yanasadikiwa kupotea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Bakari Khatib Shaaban amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, na kusema kwamba Meli hiyo ilikuwa tayari imeshafunga gati katika Bandari ya Malindi majira ya saa 4.00 kamili uski juzi usiku na abiria waliokuwemo walikuwa wanataka kushuka lakini ghafla ilipinduka na kuzama baharini.
Kamanda Shaaban alisema hadi jana mchana ni maiti za watu watatu tu ndizo zilizoonekana ikiwemo ya mtoto mdogo wa kiume, na watu wazima mwanamke na mwanaume ambao hawakuweza kufahamika majina yao kamili kutokana na hakna jamaa waliozitambua maiti hizo.
Waliookolewa katika ajali hiyo ni pamoja na Machano Mkinai Mkaazi wa Mkwajuni na Kitiba Mussa Kitiba, wa Gamba Mkoa wa Kaskazini 'A' Unguja, Halima Mussa wa Arusha, Hassan
Omar, Maulid Abdalla, wote wa Kisiju Mkoa wa Pwani.

Wengine ni Fatma Ali Salum, wa Kinyasini Wete kisiwani Pemba, Hawa Juma Saleh wa Rukwa Tanzania Bara, Zainab Ali Kitiba, Tandale Dar es Salaam, Sharifa Hamad wa
Wingwi Pemba, Ramadhan Juma Mohammed Tandale na Omar Khamis Mohammed wa Vinguguti Dar es Salaam.
Amesema baada ya kutokea tukio hilo polisi walitaka maelezo ya Nahodha wa Meli hiyo, Ussi Ali ambaye wanamshikilia kwa maelezo zaidi lakini lakini maelezo yake yanaonesha wasi wasi kwa jeshi la polisi kutokana na kuwepo utatanishi mwingi katika maelezo ya Nahodha huyo.
Kamanda Shaaban alisema kwamba awali Nahodha alisema katika meli yake
kulikuwa na abiria 25 na wafanyakazi 13, lakini Polisi inatilia shaka taarifa hizo kwani yawezekana Meli hiyo ilibeba abiria wengi na mizigo hivyo wanaendelea kumhoji
Nahodha huyo hadi hapo maelezo jeshi la polisi litakapopata maelezo ya kuridhisha kutoka kwa Nahodha huo.
"Jeshi la polisi halijaridhishwa na maelezo ya Nahodha bado hasa katika idadi za abiria alizozitoa lakini bado tunaendelea kumuhoji kwani hatujaridhika na taarifa yake" Alisema Kamanda huyo.
Kamanda Shaaban alisema jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi wa kina ili kujua chanzo cha ajali hiyo na haitosita kuwachukulia hatua wanaohusika na kuwataka wananchi kutulia na kuacha vyombo vya sheria kufanya kazi zao kwa wazi.
Hali katika Bandari ya Zanzibar baada ya ajali hiyo kutokea ilikuwa kitahanani kwa wananchi wakiwemo wafanyabiashara waliokuwa eneo hilo wakisubiri mizigo yao na jamaa zao jambo ambalo lilisababisha msongomano mkubwa kiasi cha kuwafanya Polisi kuwatawamya kwa kurusha risasi hewani.

Kutokana na hali hiyo Jeshi la Polisi lililazimika kuweka doria kali katika maeneo yote huku
wakishirikiana na baadhi ya askari wa vikosi vyengine kutokana na baadhi ya vibaka kujipenyeza na kuanza kuvuna mali zilizokuwemo katika Meli hiyo.

Kazi za utafutaji wa maiti nyengine iliendelea kwa siku nzima ya jana baada ya
wazamiaji zaidi ya 30 wa KMKM kuifanya kazi hiyo baada ya kuwasili saa 8.00 za usiku wa juzi.

Kazi hiyo, baada ya kupatikana kwa maiti tatu ilisita kwa usiku huo, iliendelea tena jana asubuhi kuanzia saa nne ambapo waokoaji hao waliamua kutumia mbinu mbalimbali za kuwawezesha kuingia ndani ya meli hiyo lakini hadi saa saba mchana walikuwa bado hawajafanikiwa kuingia ndani ya meli hiyo

Akisimulia mkasa wa ajali hiyo kepteni aliyekuwa akiendesha meli hiyo Ussi Ali Ussi, alisema wakati akiingia Bandarini ghafla aliona meli hiyo ikijaa maji na kulala upande wa
kushoto.
Alisema alianza safari yake saa 10.00 jioni kutoka Dar es Salaam na kuja Unguja ambapo aliwasili saa 3.30 usiku lakini akiwa njiani alipata tatizo la usukuni kutoenda vizuri akiwa karibu na kufika Bandarini hapo.
Akiendelea alifahamisha ndani ya meli hiyo alibeba mizigo yenye uzito watani 40, abiria 25 na wafanyakazi wake walikuwa ni 13 ambapo watatu aliwaona baada ya meli hiyo kuzama lakini kwa wakati huo wa usiku hakujua wapi walipo.
Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ni miongoni mwa viongozi waliofika katika eneo la bandari na Zanzibar kuonana na abiria waliookolewa na kushuhudia ajali hiyo.

Rais Karume aliwataka mafundi wanafanyakazi ya uokozi kuona kuwa wanajitahidi kuhakikisha kuitafuta miili zaidi kama bado imo ndani ya meli hiyo.
Katika bandari hiyo umati kubwa ulikuwa umesheheni huku mamia ya watu wakiwa wamekaa nje ya geti la gati wakitaka kuingia ndani kushuhudia jamaa zao na ajali hiyo ambayo jambo ambalo limesababisha msongamano mkubwa bandarni hapo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar, Mustafa Aboud Jumbe alimweleza Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, kwamba juhudi za uokoaji inaendelea kwa kushirikiana na Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Polisi na wadau wengine wanaojitolea kusaidia uokozi huo.
Jumbe alisema bado ni mapema kuielezea serikali juu ya hatua za kuweza kuchukuliwa zaidi kwa vile wameanza kuifanya kazi hiyo ambapo imekuwa ngumu kutokanana na meli hiyo kuwa na mzigo mkubwa kiasi ambacho kimekuwa kikiwapa usumbufu waokowaji.
Kutokana na kuwepo kwa umma wa wananchi katika eneo la bandari Shirika la Bandari liliamua kufunga milango yake yote ya Bandari hiyo kwa usalama wa watu huku waandishi wa habari wakipata kazi kubwa katika ufanyaji kazi zake kutokana na vikwazo walivyokuwa wakiwekewa katika eneo hilo.
Jumbe alisema kwamba baadae watajaza upepo Meli hiyo iliyozama kwa kutumia kifaa maalum ili mizigo na watu waliokuwepo waweze kuja juu ambapo kazi hiyo itafanywa baada ya maji kujaa kwani kwa wakati huo maji yalikuwa yanakupwa na kazi hiyo ingeshindikana kufanyika.
Waziri Kiongozi aliwataka Viongozi wa Bandari kuieleza Serikali ni msaada gani wanaohitaji ili kuweza kufanikisha uokoaji wa mizigo, watu na meli hiyo ambapo Shirika la Bandari lilisema limejipanga vyema kukabiliana na janga hilo.
Wakati shirika la bandari likitoa ahadi hiyo hadi sasa hakuna msaada uliopatikana wa kutoa maiti zilizokuwa ndani ya meli hiyo huku Rais wa Zanzibar akilitaka shirika hilo kuomba msaada shirika la bandari la dare s salaam kuja kusaidia kuwaokoa watu waliomo ndani ya meli hiyo.
Habari zaidi kutoka kwa abiria walionusurika katika ajali hiyo wamedai kuwa ndani kulikuwa na watu wengi wanaokisiwa kufikia 100, lakini Nahodha wa Meli hiyo anapingana na idadi hiyo na kusisitiza kwamba meli yake ilikuwa na idadi ndogo ya abiria.
Halima Mussa mkazi wa Arusha ambaye amenusurika katika ajali hiyo alisema kwamba wakati tukio hilo linatokea alikuwa tayati ameanza kushuka ndani ya Meli hiyo, lakini ghafla aliona ikipinduka wakati ikiwa imefunga gati na baadae akiwa katika maji alijikuta ameshikilia kitu.
"Mimi namshukuru Mungu kwa sababu nilikuwa nashuka lakini ghafla nikajikuta nimo katika maji lakini baadae nikakamata kitu bila kukijua ni kitu gani nilichoshikilia na nikaaza kupiga
mayowe ya kutaka msaada na huku nyuma yangu nasikia sauti nyengine watu wakiomba msaada.
"Kuna watu waliokuwepo katika maji ndio wakanisaidia kwa kunambia shikilia hivyo hivyo hicho kitu na kunitaka ninyooshe mikono ndio waliponiokoa na kunileta juu" alisema Halima Mussa huku akihema.
Watu waliofika katika bandari ya Malindi yameilaumu serikali kwa kushindwa kuchukua hatua za dharura za kuweza kukabiliana na shughuli hiyo ambapo ajali imetokea majira ya saa 4 usiku lakini hadi saa tisa ndipo waokoaji waliopofika huku wakiwa hawana vifaa vya uokoaji.
"Ni dharau za hali ya mwisho hii maana ajali tokea saa 4 usiku lakini hawa watu wa KMKM wanakuja sa 9 hawana chochote cha kuweza kuwasaidia kuokoa abiria matokeo yake wamekuja na kuondoka kwa kisingizio cha kuongojea maji yakupwe" amesema Ali Haji Mkaazi wa Jangombe ambaye ana jamaa yake katika meli hiyo.
Naye Kepteni Juma wa meli ya Sea Bus amesema ipo haja ya kuwa na timu nzuri ya waokoaji na diver ili waeze kuwaokoa watu pindipo inapotokea ajali kama hiyo kwani.
"Lazima tuwe na timu nzuri ya divers wasaidie kuokoa lakini pia tax force ni muhimu kuwepo kwa ajili ya maafa kama haya na kufuata madili ya kazi ni kitu cha lazima kwa sisi manahodha ili kunusuru maisha ya watu" alisema Kepteni huyo.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad aliwaambia waandishi kwamba
wakati umefika hivi sasa kuhakikisha serikali inalifanyia kazi tatizo hilo ambalo linaweza kuathiri wananchi wengi kwa kuziwajibisha taasisi husika kwa vile meli hiyo tayari hapo
awali ilipata hitilafu na kulazimika kushusha abiria katika Bandari ya Mkokotoni baada kupata maharibiko ikitokea Pemba.

Maalim Seif alisema ipo haja kwa serikali hivi sasa kuvifanyia ukaguzi vyombo vya usafiri kwa kuona inatenganisha huduma kati ya vile vinavyotoa huduma baharini.
Meli hiyo ambayo inamilikiwa na Said Mbuzi imeelezwa kuwa ilibeba mizigo mbali mbali ikiwemo Trekta, gari mbili, magunia ya unga wa ngano, sukari, mchele, magunia ya viazi, ya nyanya, mifuko ya saruji, magodoro na bidhaa nyengine ambazo zote zimezama huku wajanja wakitumia nafasi hiyo kuopoa bagodoro na bidhaa nyengine na kukimbia nazo nchi kavu.
Tukio za kuzama kwa Meli hiyo ambayo uzamaji wake unafanana sana na ule wa
MV Bukoba linatokea wiki moja tu katika kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba mwezi Mei mwaka 1999 ambapo watu kadhaa walifariki dunia na kweka historia ya Tanzania katika ajali mbaya za meli zilizowahi kutokea nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Wananchi "waliofika kushuhudia ajali" walikuwa wametaarifiwa mapema kwamba kutatokea ajali waje kushuhudia?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2009

    Huyu anayeandika si Michuzi, kuchapia kwa kwenda mbele yaani. Vipi Mzee wa vekesheni uko vekesheni au siku hizi una msadizi?

    Mungu awalaze pema waliotutoka.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2009

    Pole wafiwa inasikitisha ila kamati itaundwa tujue nini chanzo cha ajali. Ushauri wangu tu wewe Misupu usiwe unaweka mambo ya vyama sijui kafu mara sisiem si wakati wake.
    Asante.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2009

    poleni sana wafiwa na wahanga mlionusurika kwenye ajali hii.

    ReplyDelete
  5. NYEPESI NYEPESI ZINASEMA MELI ILIKUWA OVERLOADED, WAHUSIKA WA USAFIRISHAJI MAJINI WAWAJIBISHWE KWA HILI. POLENI SANA WAFIWA WOTE. HUU NI MSIBA WA WATANZANIA WOTE

    ReplyDelete
  6. huyo ambaye alikuwa akiwazuia watu wasitoke wakati meli imejaa,alitumwa auwe watuu!muwaji mkubwan huyo.mimi ninge kuwepo na angesubutu kunizuia wakat meli iko oveload ninge mtoa koromeo.nataarifa 2 tutafanya dua special ya kuwalaani wote walihusika katka kusababisha vifo vya ndugu zetu.nadhani fika mnawafahamu wapemba vizuri hakuna neno,tutawazika mmoja mmoja mpaka waishe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...