ukumbi mpya a mlimani city conference center kwa nje. hapa ndipo miss universe tz 2009 imefanyikia
iluminata james miss universe tz 2009
tano bora
iluminata james akiwa na majaji baada ya mchuano. toka shoto ni rosie motene mtangazaji wa tv ya channel 53 ya sauzi, masudi kipanya na mbunge wa viti maalumu mh. al sharyamaa kwegyabir.
wadau wa kenya airways na mrembo iluminata
meza ya mabosi wa sumsung tanzania, wafadhili wakuu wa miss universe tz
gwaride la warembo
kumi bora
mwandaaji maria sarungi-tsehai akielekeza jambo kwa majaji

maria akieleza jambo majaji. kulia ni mzee mzima john kitime ambaye naye alikuwa jaji. cheki alivyotoka pina!
msanii wahuu toka kenya akitumbuiza

ambwene yesaya a.k.a ay alikuwepo kuwapa watu raha
kikundi cha ngoma cha albino kilitia fora katika shoo hiyo
sindimba toka mang'aka lilimwaga na wasanii albino

sebene lilimwagwa na diamon musica
mwandaaji wa miss universe tz maria sarungi-tsehai akimzawadia tuzo mshindi wa miss universe tz 2009 iluminata james baada ya kuibuka kidedea usiku huu kwenye mchuano uliofanyika ukumbi mpya wa mlimani city conference centre hapa dar. iluminata ana umri wa miaka 23 na anatokea mwanza
miss universe tz 2009 iluminata james (kati) akipozi na mshindi wa pili evelyn almasi (kulia) na hidaya maeda ambaye ni mshindi wa tatu

iluminata akiwa na mshindi wa pili evelyn (kulia) na mshindi wa tatu hidaya baada ya matokeo
wadau wa precision air ambao ni moja ya wadhamini wakipozi na miss universe 2009 iluminata james baada ya kutangwanza matokeo usiku huu.
Habari Kamili
Mlimbwende Iluminata James kutoka mkoani Mwanza leo usiku ametwaa taji la Miss Universe Tanzania kwa mwaka 2009 na kujikatia tiketi ya kuliwakilisha taifa katika michuano ya dunia itakayofanyika baadaye mwaka huu katika visiwa vya Bahamas.
Iluminata ambaye anampokea taji hiyo mwanadada nyota katika fani ya mitindo nchini Miriam Odemba alifanikiwa kutwaa taji hilo baada ya kuwashinda walimbwende wenzake 19 ambao nao walikuwa wakichuana vikali kuwania taji hilo.
Shindano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam , mbali ya mashabiki wa masuala ya ulimbwende kupata burudani ya kuonyeshwa mavazi na miondoko ya ‘catwalk’ kutoka kwa washiriki 20 pia walikongwa nyoyo zao na burudani safi ya muziki kutoka kwa msanii nyota wa Bongofleva , Ambwene Yesaya ‘Mzee wa Comercial’ , mwanadada Wahuu kutoka Kenya anayetamba na wimbo wa ‘Sweet love’.
K abla ya hapo bendi ya Diamond Musica chini ya Allaine Mulumba ilikuja na wimbo wao maarufu wa ‘Mapenzi kitu gani’ na kufuatiwa na sebene la uhakika na burudani hiyo ilihitimishwa na ngoma za utamaduni kutoka kikundi cha Albino Revolution Cultural Troope.
Mbali na Iluminata washindi wengine katika fainali hizo za Miss Universe Tanzania ambazo zilihusisha warembo kutoka mikoa mitano ya Tanzania , Arusha , Mwanza , Dodoma , Morogoro na Dar es Salaam walikuwa ni Evelyne Almasi ambaye alichukua nafasi ya pili na hivyo kujipatia nafasi ya kushiriki kwenye shindano la Miss Earth.
Mwanadada Hidaya Maeda ambaye alishinda nafasi ya tatu katika kinyang’anyiro hicho, yeye ataliwakilisha taifa katika shindano la Miss International baadaye mwaka huu, na nafasi ya nne ilikwenda kwenye Zeinab Kianda na Gisela Tarimo alinyakua nafasi ya tano.
Miss Universe Tanzania 2009 mbali ya kujipatia tiketi ya kushiriki kwenye shindano la dunia pia alizawadiwa Sh milioni tatu , nafasi ya kusoma kozi ya lugha ya kifaransa kwa mwaka mmoja katika kituo cha Alliance Francaise pamoja na kupatiwa vipodozi vyenye thamani ya Sh 500,000 na duka la Shear Illusion .
Majaji wa shindano hilo walikuwa ni pamoja na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Al Sharyamaa Kwegyabir , mwanamuziki John Kitime,Masoud Kipanya , Mbunifu wa mavazi Ally Rhemtullah, Maria Sarungi Tsehai , Amit Patel kutoka kwa wadhamini wa shindano hilo kampuni ya Samsung ambao waliongozwa na jaji mkuu Rosie Motene kutoka Afrika Kusini ambaye ni Muigizaji nyota na Mtangazaji wa kituo cha Studio 53.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

 1. AnonymousMay 31, 2009

  jamani mishel obama ndiye anayetoa zawadi au ni macho yangu.


  madau!!

  ReplyDelete
 2. AnonymousMay 31, 2009

  huyo miss sarungi simjui. lakini nampongeza kwa kufanikisha hii miss universe tz...well done next time get some big names from africa 'n outside africa as judges. well done again.

  ReplyDelete
 3. AnonymousMay 31, 2009

  Sasa huyu Maria ana hangaika nini nyuma ya ma jaji au alikua anataka kuhakikisha mtu wake ana chaguliwa?

  Ai leti picha nzuri bibibie , maana kama umeandaa mashindano kwa level ya kimataifa unatakiwa kuwaachia majaji wawe huru ,bila kupita pita kuongea nao , maana tuna kua na uhakika wamesha pewa semina kabla ya show , so hawaitaji msaada wowote siku ya show wa kuelekezwa .

  Siwezi piga picha eti Donald Trump ana pita pita nyuma ya ma jaji na kuongea nao siku ya show.

  ReplyDelete
 4. AnonymousMay 31, 2009

  IBRA BUKENYA aka KYAKALONGO NAKUONA IN WHITE BIG UP MWANA

  ReplyDelete
 5. AnonymousMay 31, 2009

  am agreed with da guy hapo juu..haipendezi kuingilia kazi ya majaji..next tym maria jifunze kutulia kitini or uwe jaji mwenyewe kama unashindwa kutulia.othrwz kitu kipo bomba

  ReplyDelete
 6. AnonymousJune 01, 2009

  labda anataka kujua wamefikia wapi, atoe updates, kwa wageni, IM JUST SAYING......Maana nimeona kama alikuwa na mikrofoni pia, I dnt know....labda kuna sababu ya msingi yuko hapo nyuma kwa majaji ...

  ReplyDelete
 7. AnonymousJune 01, 2009

  Naomba kuuliza huyu MARY SARUNGI, ndie yule aliesoma Zanaki miaka ya 90, SHOMBE hivi, au majina tu, baba ake nadhani alikuwa Profesa, au majina tu yanafanana?.

  ReplyDelete
 8. AnonymousJune 01, 2009

  Vinywaji vilikuwa bure nini...Maana huyo mkorea yupo BWAAAAAAAAAAXXXX!!!!

  ReplyDelete
 9. Zanaki productJune 01, 2009

  Mdau, 8:11am

  Yea, Maria went to Zanaki in late 80's I think, that's her, Mzee Sarungi used to be Waziri wa afya pia, if you remember well. Maria has changed a lot, she looks even more pretty.

  ReplyDelete
 10. AnonymousJune 02, 2009

  acha kubania hoja za watu zenye maana hawa mamisss nao wamezidi kwa tabia mbaya watu tunaandika halafu unatubania poa

  ReplyDelete
 11. AnonymousJune 02, 2009

  Asante Mdau-Zanaki Product, kwa info, kwa kweli amebadilika sana ndo maana nilikuwa sielewi vizuri,kama ni yeye au macho yangu,asante.nakumbuka wakati anamaliza shulemi ndo nilikuwa naanza form one.thanks.She is cool.

  ReplyDelete
 12. AnonymousJune 02, 2009

  Kwa wadau wa Zanaki kapo juu. mnacho zungumza ndio nilikuwa nakiwaza .
  Ninapenda kusema katika watu wano zeeka vizuri mmoja wapo ni huyu Maria Sarungi

  Kwakweli mtakubaliana na mimi haswa kwa wanao mjua hapo zamani ni tofauti na sasa ,tena ka kiasi kukibwa sana , yani ni amekuwa mdada na amependeza zaidi kupita zamani.
  Na nani naweza hisi siku moja Maria ata shughulika na urembo na kuweza kufanikisha vizuri ?

  Maria nimesoma naye Oysterbay Primary school ,alikwua madarasa matatu mbele yangu na alikwua na Siter wake anaitwa Verocica ambaye ndio tulikuwa tuna muona mzuri kupita maelezo .

  Hongera sana Maria ,kazi nzuri na unazidi kuwa mrembo .

  ReplyDelete
 13. AnonymousJune 02, 2009

  JAMANI KWA TAARIFA YENU WOTE HUYO MSHINDI WA PILI ANAITWA EVERLYNE AMASI NA SIO ALMASI,

  KAKA MICHUZI REKEBISHA HILO KAMA UTAWEZA.

  ReplyDelete
 14. AnonymousJune 02, 2009

  huyu maria sarungi yuko na mwenzie wamefanana sana, alafu mmoja ndio alikuwa pale zanaki tena alikuwa dada mkuu, waliosoma naye wanasema alikuwa mnoko sana na walidhani atakuja kufanya kazi wizara ya mambo ya ndani kumbe yuko kwenye fani ya urembo.


  keep it up mrembo!

  ReplyDelete
 15. AnonymousJune 02, 2009

  jamani natafuta mchumba sasa huyu dada mwana wa sarungi vipi!!

  ReplyDelete
 16. zanaki productJune 03, 2009

  Mdau wa 8:16pm

  Kama sijakosea, I think ameolewa but, she's very pretty.

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...