MAREHEMU PROFESA HAROUB OTHMAN
PROFESA HAROUB OTHMAN, MMOJA WA WAHADHIRI WAANDAMIZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, AMEFARIKI DUNIA ASUBUHI HII HUKO UNGUJA AKIWA USINGIZINI.

MWANA WA MAREHEMU, TAHIR OTHMA, AKITHIBITISHA HABARI HII AKIWA NJIANI KUELEKEA MSIBANI AKITOKEA DAR, AMEIAMBIA GLOBU YA JAMII KWAMBA MAREHEMU AMEKUTWA AMEFARIKI ASUBUHI HII AMBAPO JANA ALILALA AKIWA BUHERI WA AFYA.

HABARI TOKA UNGUJA ZINASEMA MAREHEMU PROFESA HAROUB OTHMAN USIKU WA KUAMKIA LEO ALIHUDHURIA UZINDUZI WA TAMASHA LA MAJAHAZI (ZIFF) KATIKA NGOME KONGWE NA HAKUONEKANA NA MATATIZO YOYOTE KIAFYA.

MSIBA UKO NYUMBANI KWAKE SEHEMU ZA MICHENZANI ENEO LA BARASTE, NA HAIJAJULIKANA KAMA ATAZIKWA LINI. HABARI ZA MAZISHI YAKE TUTAWALETE MARA ZITAPOPATIKANA.
PROFESA OTHMAN, ALIYEKUWA MHADHIRI WA DEVELOPMENT STUDIES HAPO UDSM, AMEANDIKA SANA MASUALA YA MAENDELEO YA AFRIKA NA ALIKUWA MSEMAJI ANAYEHESHIMIKA KUHUSU MASUALA YA BARA LA AFRIKA NA AGHALABU VYOMBO VYA HABARI VYA NYUMBANI NA VYA KIMATAIFA VILIKUWA KILA MARA VIKIMHOJI KILA LITOKEAPO JAMBO KUBWA LINALOHUSU BARA HILI.
ATAKUMBUKWA PIA KWA UCHAMBUZI WAKE WA MAMBO YA HALI YA KISIASA SEHEMU MBALIMBALI BARANI AFRIKA NA ULIMWENGU KWA JUMLA, MOJAWAPO IKIWA NI MADA NYETI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR PAMOJA NA MIGOGORO YA SOMALIA NA DARFUR. SOMA BAADHI YA MAANDIKO YAKE KUHUSU MUUNGANO:
GLOBU YA JAMII INATOA POLE KWA WAFIWA NA KUMUOMBA MOLA AILAZE ROHO YA MAREHEMU PAHALA PEMA PEPONI
-AMIN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. its so sad who will be slightly like him?? lets try

    ReplyDelete
  2. My uncle,my hero, my guardian, my role model, my Prof..

    The family is at lost,
    Tanzania is at lost,
    ZANZIBAR is at lost,
    Africa is at lost,
    Palestine is at lost,
    The left is at lost,
    U should not leave us now prof Othman...

    Not now when we need ur wisdom,
    Not now when we need your patience,
    Not now when we need ideals,
    Not now when we need ur values,
    Not now when we need ur integrity,
    Not now when u need u most...

    Yes u have done ur share,
    Yes u have given us the most,
    Yes u have stand for us during the worst,
    Yes u have taught the greatest,
    Yes u have inspired the best,
    But u shouldn't leave us the earliest.....

    Ur the best,
    Ur the greatest,
    Ur the LEFT,
    Ur the THA PANAFRICANIST,
    Ur the teacher, ur the wisdom, ur the hope, ur the role model, ur THA comrade, ur the friend in the struggle...

    Omarilyas

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2009

    IL. wa IL. R.

    Wiki hili Balaa tupu!! Vipenzi vya watu vinaondoka kimzaha mzaha hivi!

    RIP Prof.

    ReplyDelete
  4. We should honour him by doing things he always preached to the world. R.I.P. Prof. Othman.
    E.Sozigwa,
    Espoo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 28, 2009

    Mambo kama haya mtu unachoka tu. Unakunywa maji una tafakari bila majibu
    RIP Prof, RIP Baba, RIP kijana wa Afrika

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 28, 2009

    Mwanaharakati wa Ki-Marx na mwanaharakati wa Ki-Pan Africa Prof.Haroub Othman.Tungependa Glob ya jamii ikatuwekea wasifu wa Hayati(Marehemu?)Prof.H.Othman ili tufaidike na iwe njia ya kutufanya tuige mfanowe kama zilivyowekwa wasifu za Mikail Jackson.Huyu ni mwanaharakati wa Kiafrika na Kitanzania.TYupeni wasifu wake ili akumbukwe vyema
    J.J Masiga

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 28, 2009

    hakika sote tunatoka kwa allah na kwa allah sote tutarudi, mola amlaze mahali pema peponi na amsameh makosa yake na ya waislamu wote waliotangulia amin

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 28, 2009

    Poleni wafiwa wote
    RIP Prof.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 28, 2009

    RIP Professor Haroub Othman.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 28, 2009

    whats palestine got to do with him? is he from palestine?
    Im at the right and I mourn his death.

    God bless you prof.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 28, 2009

    Inalillah wainaillah rajiun.Mweneyezimungu akuweke mahali pema peponi.Dunia,Taifa na sisi walalahoi tumepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mpigania haki zabinadamu.Uchambuzi wako uliokuwa ukiutoa ktk BBC au DW ulikuwa ulikuwa ni wakueleweka kwa kila msikilizaji.Israili ungebalance wiki hii maana watu muhimu na mashuhuri wamekuwa wakitutoka kimzahamzaha tu.Anglia sasa unatupunguzia vichwa muhimu unatubakizia wababaishaji tuu.
    RIP Haroub Othman.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 28, 2009

    R.I.P Prof.. tutaendelea kuzienzi kazi zako milele.
    Mungu ailaze roho ya marehemu Haroub Othman mahali pema peponi.
    Amen

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 28, 2009

    Kweli kifo hakina huruma (Remmy Ongala). Naona wiki hii imewachukua watu wengi wapenzi wa watu bila taarifa yeyote. Tutamkosa sana Profesa Othman. Mungu aiwweke Roho yake mahala pema peponi. Napenda kuchukua fursa hii kuwatakia watanzania wote, familia yake na watu wote wa karibu wa mwalimu huyu kinara wa africa.
    Nawasilisha

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 28, 2009

    Inalilahi wainailahi rajiun, kwa kweli nimeshtushwa na taarifa hii sana, Prof. alikuwa mwalimu wangu, muumini mzuri wa dini yake, real african, Alijitahidi sana kusema ukweli bila chembe ya unafiki kama wasomi wengine! nilikuwa nahudhuria debate zake zote. I will miss him dearly. Allah Bless you. Wiki hii tumekumbushwa wanajamii umauti, tujitahidi inshallah.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 28, 2009

    Bye bye Profesa Othman.
    Bye bye Michael Jackson.
    Bye bye Farrah Fawcett.
    Bye bye Ndugu Nanihii.
    Bye bye Mrs Nanihii.
    Bye bye Comrade Nanihii.
    Bye bye everybody
    That went to be with the
    Lord this week

    Its a tough week for us all
    We will miss you all
    And God willing
    Will see each on the other side.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 28, 2009

    Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Raajiun.

    Profesa Othman alikuwa mwalimu si tu kwa wale waliokuwa darasani kwake bali hata kwa wale waliokuwa wanafuatilia maswala mbalimbali ya maendeleo ya Taifa.

    Professa Othman ni miongoni mwa wasomi niliowaheshimu na kuwapenda sana. He was extremely knowledgeable yet very humble.

    Wana familia poleni sana na Mwenyezi Mungu awajaaliye subra.

    R.I.P profesa.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 28, 2009

    R.I.P Prof. Tutakukumbuka sana kwakutetea wanyonge. Mungu hakulaze mahala pema Amina.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 28, 2009

    R.I.P pro wewe ni mfano wa kuigwa,mpiganaji wa kweli,kuanzia enzi za mwalimu mpaka now umekuwa mstari wa mbele kusema ukweli kwa pande zote.ulikuwa si mnafiki kama wengi wa ma pro wa africa,umekuwa ukisifia serikali ikifanya mazuri,na kuikosoa ikikosea,umekuwa ukisuport upinzani na chama tawala,as long hoja inasimama kwenze kuendeleza taifa.wewe ni mfano wa kuigwa,bado na wasiwasi sana kama mpiganaji kama wewe atatokea tena tz katika kipindi hichi cha uroho wa madaraka na ufisadi.rest in peace
    mwanafunzi wako

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 28, 2009

    Nilibahatika kufundishwa pale mlimani (development studies). Aliamini katika haki. Dunia imempoteza mtu muhimu. Mungu ampe raha ya milele. Amin

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 29, 2009

    innaalillahi wainnaa ilayhi raajiuun. Bila shaka huu ndio mwisho wetu sisi binadamu na mwenye kufaidika na siku hii ni yule mwenye imani na mpenda haki na aliyetanguliza mema ya bayana kama alivyokuwa al marhoum proffesor haroob inshl. mwenyezimungu amjaalie raha za milele zisizokuwa na kifani. Kwa wale mafisadi na wenye uroho wa madaraka jueni kama hamtofaidika na udhalim wenu na mbele ya haki tutarejeshewa tu! RIP pro. haroob u did the best man!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 29, 2009

    mdau #2

    palestina??ndo nini

    ndo nyie wenye mawazo eti nchi ifutwe kutoka uso wa dunia,afu mnasema haki

    aisee prof haroub,poleni jamaa zake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...