Taswira ya kwanza
Taswira ya pili

Wakati kidonda cha ajali hiyo hakijapona, kuna taswira mbili ambazo zimekuwa zikisambazwa mtandaoni duniani kote kuonesha hali ilivyokuwa muda mchache kabla ya ndege hiyo kuanguka.

Habari zinazoambatana na picha hizo zinasema dege hilo liligongana angani na ndege ndogo aina ya Embraer Legacy ikiwa futi 35,000 toka usawa wa bahar, na kwamba hiyo ndege ndogo iliweza kutua salama katika uwanja kwenye msitu wa Amazon, wakati dege la A330 likidondoka baharini na kuua kila aliyekuwamo. Ati abiria na wafanyakazi katika ndege ndogo hawakujua kilichotokea.

Stori hiyo inasema taswira hizo mbili bila shaka zilichukuliwa na mmoja wa abiria katika dege kubwa mara tuu baada ya kugongwa na kabla ya kudondoka, na kwamba picha hizo ziliopatikana kwenye kijiti cha kumbukumbu (memory stick) cha kamera ya digito ambayo pamoja na kamera kuharibika kijiti hicho kilisalimika.

Katika picha ya kwanza inaonesha tundu kubwa sehemu za nyuma ya ndege likionesha sehemu ya mkia, na ingine ilionesha abiria mmoja akivutwa nje kwa upepo mkali kupitia kwenye tundu hilo huku abiria wengine wakihaha.

Globu ya Jamii, baada ya kuchimba sana imeibuka na ugunduzi kwamba stori hiyo pamoja na picha ni kanyaboya, yaani si ya kweli, na chanzo chake inasemekana ni jamaa mmoja aitwaye Carlos Cardoso wa Brazil, mdau ambaye aliiweka stori hiyo kwenge globu yake Oktoba 26, 2006.

Bw. Cardoso anasema aliiweka stori hiyo feki ili kudhihirisha jinsi gani watu walivyoa na tabia ya kusoma paragraph ya kwanza to ya stori na kuamini kuwa ni stori ya kweli pamoja na kwamba kuna ushahidi tosha kwamba si ya kweli.

Ukweli ni kwamba taswira hizo zimechukuliwa kutoka katika tamthilia maarufu ya 'Lost' na kwa ushuhuda
BOFYA HAPA
ila soma habari yote hadi mwisho ndio uelewe. Pia kuna video ya filamu hiyo ya sehemu zilikochukuliwa hizo picha


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2009

    Hizi ajali za ndege ukianza kuzifikiria hamu yote ya vekesheni inaisha manake huwa ikitokea ajali moja ya ndege we sikilizia tu nyingine zinafata lazima zifike 4 sasa tunasubiria tu mnh bora ziishe kabla sijaruka bongo December
    from zee la stbosch

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2009

    Any reason kwanini huwa kuna mapachuti na hakuna anaeyatumia? Yaani hapo ni kusubiri kifo tu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 12, 2009

    stbosch,

    Do you have brain? What kind of comment is that?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 12, 2009

    Michuzi don't publish these kind of stupid hoax...to play with people's mind on something else is ok but when death is involved is completely out of line.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 12, 2009

    Wewe anonymous wa 4:52pm; hakuna parashuti kwenye ndege za abiria! ni life jackets tu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 12, 2009

    Na mara nyimgi ajali ikitokea,hakuna anaepona.kwa kweli inasikitisha.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 13, 2009

    sasa si ushasema ni ya uongo hii newz??

    cha kuturusha roho nini asa?

    msitake tusipande ndege wala meli jameni,wengine ndo usafiri uliopo ufike utakako!!

    yan ajali ya air france sitaisahau kabisa,imenifanya imani ipungue kabisa.

    bora km si kweli izi picha.

    wee annon life jackets ndo nini,na parachute nini???unataka kusema life jacket ukivaa uruke hewani utatua mzima-mzima tu?si utavunjika?bora yasiwepo tu maana sijawai ona watu wanaweza yavaa kipindi cha ajali,na sijawai sikia labda Hollywood movizzz

    khaaaaaaaaaaa

    Mwenyezi awatunuku waanga wote wa ajali ile,i can imagine wavokuwa wanahaha!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...