January Makama akimwaga mada katika moja ya vikao vya vijana wa CCM
Mh. Lawrence Masha akiongea kwenye kikao hicho
Wazee wa busara wa CCM hawako mbali na vijana wao. Hapa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akitega sikio mada za vijana
Mh. Mahmuod Thabit Kombo ni mmoja wa vijana wakereketwa wa CCM visiwani

Mh. Peter Sherukamba akiongea

Mzee Thabo Mbeki alikuwepo kwenye moja ya mikutano hiyo ya vijana wa CCM
Mdau Aidan akimwaga sera
Mh. Mohamed Dewji, Heri Bomani (kulia) na Peter Mwanyika wakisikiliza kwa makini
pamoja na kuondekana mpole na mkimya January Makamba ni muongeaji mzuri mbele ya kadamnasi
Fatma karume akielezea jambo kwa hisia
Deo Mwanyika akifafanua jambo












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2009

    E bwana huyo sio Peter Mwanyika ni Deo Mwanyika wa Barrick Tanzania. Umekumbusha mbali lakini...yuko wapi yule nyanda?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2009

    Michuzi Na wewe Ulikuwepo kama Mwandishi,Mpiga Picha hapo au na wewe CCM? tunataka kujuwa tu kama Ni Mtu wa Siasa Je wewe Ni Chama Gani?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 12, 2009

    kweli CCM Vijana iko juu! na hakika kama vijana tukiwa pamoja,basi tunaweza kujenga chama na Tanzania iliyo nzuri.
    Ushauri wangu kwa vijana wezangu ni wajaribu kuzingatia maadili mazuri ya kutojiusisha na vitendo vya ubinafsi nikamaanisha corruption,na vile vile tujaribu kutoa fikiria za kila mtu atako kuwa kiongozi lazima ale,nadhani ni muhimu kwa sisi vijana kujenga moyo wa kuitumia nchi yetu."we should not rule, but we should learn how to serve the nation".
    hainidhuru kusema hivi,ilikuwa vizuri kwa vyama vya upinzani na wao wakatayarisha vijana wake,ili kuletea ushindi wa siasa hapo baadae,ambao ndio chimbuko la kijiletea maendeleo.
    Pia,ccm vijana tujaribu kuacha siasa za malumbano na publicity,na kuzingatia siasa za kiutendaji ambazo ndio msingi wa modern politics of 21c,kwasababu ukitoa mchango kwa chama na taifa kwa ujamla,hautajificha utaonekana tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 12, 2009

    Tumeona balozi wa naniii,mbona wewe hukuonekana au hukuwepo? Sasa wawe na mawazo ya kujenga Tanzania na sio kukimbilia kuifisadi nchi, ndio hapo sipendi ccm

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 12, 2009

    Ni kweli mkuu tumewaona ila je wengi wao wana maanisha kweli au kwa kuwa siasa ni deal bongo?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2009

    January Makamba, a future potential leader of Tanzania. Chaaange is coming to Tanzania!
    Hallellujah!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 13, 2009

    ndugu wadau, mimi natoa ushauri wa bure. january ndiye anayefaa kuwa rais 2015. john mashaka na dr. shayo hawafai kwa sababu wao siyo wana ccm, licha ya hayo mashakareza na marekani . january yeye anakaa hapa nchini na wakulima. january ni mtoto wa mkulima wakati mashaka ni mtoto wa fisadi. january ndiye anayefaa kuongoza hii nchi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 13, 2009

    Kaka Michuzi, mbona hayo majina yamekaa kiaina fulani?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 13, 2009

    January mikonozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 13, 2009

    Lord , please forgive them because they don't know what they are doing.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 13, 2009

    Nataka kusema tu kwamba huyu mtu aliyepiga hizi picha ama anajali kazi yake, au yuko makini katika kazi yake ya upiga picha. Pamoja na heshima zote nilizonazo kwa DC wa nanihii katika fani yake ya upiga picha, mara nyingi anapenda kuminya "shutter button" kwenye "auto" setting ya kamera anazotumia. Ndo mara nyingi kwenye blog hii tunapata picha ambazo tunazithamini sana ila huwa ni "snap shots" tu na si picha za mpiga picha anayepaswa kuwa mahususi. haya si maneno mazuri lakini endeleza libeneke DC -- ila ukiweza na we japo mara moja moja upige picha kama hizi kwani unaziweza sana!! (Nitashangaa kujua kwamba ni wewe uliyepiga hizi picha!!)

    ReplyDelete
  12. Michuzi,
    Mimi ninaona CCM wanajaribu kujenga CCM ilijengwa na Umoja wa Vijana wakati kina Mohamedi Seif Khatibu, Kikwete, Ditopile, Komba, lakini wapi chuo cha siasa Kivukoni. Makada wote wakereketwa wa CCM walipigwa msasa kwanza JKT na baadaye Chuo cha siasa kivukoni. Mimi ninaona ni wakati huu sasa Tanzania kuanzisha vyuo vya masomo ya jamii ambavyo vitakuwa na watalamu ambao watafanya hizi bila ya kuwa na kujadili maswala ya jamii na kuwakilisha jamii na watu wachache (group-misclassification-cofounding-biases). Sasa upati ukweli juu ya matatizo ya jamii.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 13, 2009

    Eti January ni mtoto ni mkulima. Thubutu. Hakuna mtoto wa mkulima anayeweza kuingia anga hizo. Mara ya mwisho mtoto wa mkulima kuingia anga hizo alikuwa Nyerere mwaka 1960.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 13, 2009

    Kwenye picha ya juu kabisa Michuzi umeandika January Makama ndiyo maana watu wanadhani huyo Makama ni malalahoi ambaye hajawahi kusikika katika ulimwengu wa wenye nazo. Kwa wewe uliyesema January ni mtoto wa mkulima, anaitwa January Makamba.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 13, 2009

    wadau, huyo aliyeshika hicho kitabu cha TUJISAHIHISHE kanifurahisha kama hapo alikuwa anawaambia wajumbe wakisome kitabu hicho. inabidi viongozi wetu nao wasome hilo desa na maneno yaliyopo humo wayaelewe na yafanyiwe kazi. Viongozi wetu ni WAOGA kukubali kuwa wamekosea pale inapotokea hivyo (NIJUAVYO NI MWALIMU TU NDIYE ALIWAHI KUKUBALI ALIPOKOSEA) I stand to be corrected.

    mdau desilamu

    ReplyDelete
  16. Kumbe CCM can be cool! Hongereni vijana wa CCM kazi nzuri. Mdau Misupu hii ilikuwa wapi?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 13, 2009

    Hii kitu mbona haijakaa ki-CCM kabisa! Hapa ni wapi? Kama ni hivyo basi CCM kweli wamezinduka. Hongereni. John Mashaka na Dr. Shayo mko wapi?

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 13, 2009

    Inasitikisha sana kuona blog ya jamii inageuka kuwa ya wateule maana ukiweka views and comments ambazo zinamwelekeo wa kutetea maslahi ya watanzania siyo vingunge basi information hiyo inabaniwa ....anyway this is normal for Tanzanian media system lakini hata upipo i-publish hapa copy na natuma kwenye blg nyingine and iam sure my message will reach my audience.
    Thanks for support and effort to educate Tanzanian society.
    Mkereketwa

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 13, 2009

    CCM inatisha mjomba! hivi hawa wenye mawazo ya kuwa na vikao elekezi wametoka wapi? ama kweli CCM ni chama kubwa, hawapigi kelele wao wanachukua kelele za zinazopigwa na huko nje wanaziweka katika vitendo.
    Na kama hawa jamaa wate niliowaona katika picha hizo hapo juu wako active katika mambo hayo basi CCM iko juu sana kwani huwezi kuwasikia hao wakilumbana hata siku moja.
    CCM iko matawi ya juu sana mjomba, keep it up!!!! chapeni kazi vijana.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 13, 2009

    Vijana wa ccm my ass, wote watoto wa vigogo halafu mnaita Tanzania ni ya watanzania kumbe ni kurithishana tu madaraka, ushenzi mtupu ndio maana vijana wanaojua hili wote wanaukana UTZ wao, hauna maana.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 13, 2009

    Asante sana kaka Michuzi kwa kutuletea taarifa ya Michakato ya vijana katika harakati za kuliendeleza taifa letu Tanzania. Kwanza kabisa hongereni sana for those initiatives ambazo zinaonyesha jinsi gani mlivyo na upendo wa dhati kwa watanzania. Ni kweli vijana lazima tusimame kwa nguvu na kutetea masilahi ya watanzania wote bila kujali rangi zetu, itikadi zetu pamoja na uwezo wetu (Kifedha). Nimeshawishika sana kutoa mchango wangu baada ya kusoma comments mbalimbali zilizotolewa hapo juu. Nasikitika sana kusoma baadhi ya comments kweli inaonyesha ni jinsi gani tulivyo wavivu wa kufikiri na siipatii picha Tanzania ya baadaye (15 years to come).Mimi binafsi siyo mfuasi wa chama chochote kile cha siasa, ila ni muumini wa yeyote yule mwenye nia ya dhati na ya kweli kabisa katika kulisaidia Taifa letu la Tanzania. Na kuona kweli watu wake wanapata Maisha bora kama invyoainishwa na serikali ya CCM. Natoa wito wangu kwa vijana wenzangu huu ni wakati wa pekee katika historia ya ulimwengu ambapo mabadiriko ya kifikra yanazidi kuchukua nafasi yake. Tanzania ya leo sio sawa na ile ya miaka mitano iliyopita, wananchi wamechoshwa na kerere za kwenye majukwaa za kunadi sera ili kupata nafasi na sio kuwajibika kwa ajili yao. Tunachotaka sasa ni mabadiriko ya kweli yenye nia ya kumkomboa mtanzania kutoka katika hali ya utegemezi mpaka kujitegemea.Nchi yetu ni moja kati ya nchi zilizojaliwa kwa kuwa na rasilimali kibao ambazo kiuhalisia hazitusaidii watanzania. Leo mwananchi wa Nyamongo hafaidiki na Dhahabu iliyopo kwao. So we need to come with very concrete and innovative ideas ni jinsi gani tutawasaidia watanzania na tusikimbilie kwenye siasa kwasababu may be Baba yako ni mtu maarufu (Mwanasiasa) ama kutafuta ulaji kama ilivyo hivi sasa. Siasa za ukoo katika nchi hii hazina nafasi tena tunahitaji viongozi wenye vision nzuri na nia ya dhati kabisa dhidi ya watanzania. Tumechoka na malumbano ya hoja mara hii ya CCM, CHADEMA wametuibia. So an advice to my combrades lets stop all those we need to see changes wananchi tunataka maendeleo. Kwa mwenendo huu mnaoenda nao sasa wananchi tumewachoka CCM, otherwise you guys mbadirike lakini still mmelelewa katika misingi ya kifisadi na kubaguana. Na ndiyo maana majina ni yale yale kila kukicha utasikia some body Makamba amechaguliwa kuwa mwekahazina wa UVCCM. Tubadilike siyo lazima kuingia kwenye siasa ndiyo utaweza kuisaidia Tanzania. CCm isiwe kisima cha kwenda kutafutia ulaji kama mlivyo hivi sasa. Aluta continua.
    Activist Non-politician
    Nyagonde Stephen.

    ReplyDelete
  22. BREAKING NEWS!!!

    Kampeni ya January Makamba 2015 yazinduliwa kwa kishindo!!

    Habari zaidi tembelea http://tinyurl.com/Makamba-2015

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 14, 2009

    we Unaesema unaukana UTZ unakosea, lamsingi nawewe pigania hakiyako, nchi niyetu sote usitishike na hizo lcd projectors, hivyo nivitu vyakawaida sana sikuhizi kwenye mukutano, na kwa taarifa yenu sio huyo january, makamba wala mwingine yoyote aliye kaa hapo amefanya hayo, wana ajili kampuni tu ya kuandaa mikutano ndo wana anaandaa yote hayo, ni vijimambo tu vya kawaida sana sikuhizi!

    MIMI ninacho sema nikwamba watanznia Vijana amkeni kila mtu anahaki yakuingia umoja wa vijana wa chama chochote na akapaza sauti yake kutetea wanyonge, kwahiyo msihofu.

    Mimi kijana wenu nataka kuingia huko kuliendeleza libeneke lasiasa, mimi ni mtoto wa mlala hoi mwenzenu nta hitaji support kutoka kwenu,

    kwasasa details zingine bado kapuni!!

    Mdau.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 14, 2009

    The Finest, japo umenitosa but your work is impressive!!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 14, 2009

    Aliyeshika kitabu kilichoandikwa tujisahihishe ni Togolani Mavura. Hongera sana mdogo wangu Togolani. Mungu akujalie maisha marefu uje kuwa raisi, waziri au mbunge.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 15, 2009

    Hivi mkuu wa nanihii, naomba kuuliza kwa nini vijana wote wenye pesa na nafasi kubwa hata kwenye kampuni binafsi wako CCM, je ni kweli hakuna vijana masikini huko, au wao wenye pesa ni wakereketwa wa kweli wa CCM?, ni naogopa hawa watu wasije kuwa wanatafuta security ya chama tuu, na je ikitokea CCM ikashindwa Uchaguzi wataendelea kuwa wenzetu CCM, au wao ni wanachama wa chama tawala tu, na si CCM ? naomba kuwakilisha

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 15, 2009

    dah! jamaa wanarithishana tu, sisi makabwela tunaishia ukatibu kata na kadhalika... anga hizo utasikia majina ni hayo hayo. huo mkutano ulifanyika zanzibar, eti nasikia ulikuwa wa siri sana?!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 15, 2009

    dawa yao kuwafwata huko huko ccm.sababu hawatoi nchi kwa kura

    ReplyDelete
  29. Lyimo bedaJune 16, 2009

    Kuna mdau mmoja amedai ati Dr shayo na msahaka siyo wana CCM. Ningependa kuwaambieni kuwa ninavyomfahamu Dr shayo ni mwana CCM na pia mwana Umoja wa Vijana. Niliwahi siku za nyuma kutoa number ya kadi zake lakini michuzi ukazibania sijui kwa sababu gani labda uliona si vyema kutoa kadi za kijana wetu.

    Mashaka sina uhakika yeye yuko upande wa chama gani. Ila cha msingi
    katika kuleta mabadiliko ya kweli na mazingira ya kuwawezesha vijana kumsaidia atakayeteuliwa kuwa raisi 2010 itikadi ya chama si hoja.

    Tunataka vijana sio tu wamefika hapao walipo wa juhudi za kubebwa ila kwa uwezo wa kuweza kuona na kubuni mikakati ya kubadilisha mwelekeo wa taifa letu.

    Mashaka anao huo upeo na ndiyo maana wameshaanza kufanya vitu vyao kwa pamoja na Dr shayo, na siku zi nyingi utawaona vijana hawa wakiwa pamoja.

    Hawa ndiyo chachu ya fikra za kizazi kipya.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 17, 2009

    NANIHII NA WEWE HAUNA MPANGO WOWOTE MBONA SIJAWAHI KUONA PICHA ZA CAF HATA SIKUMOJA, ACHA UBAGUZI WA KISIASA! HALAF HAWA JAMAA MI NAONA HAWANA LOLOTE JIPYA ZAIDI YA KUSUMBULIWA NA NJAA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...