Habari kutoka bandari ya dar zinadatisha kwamba hivi sasa kampuni ya upakuaji makontena bandarini (ticts) hakuna kazi inayofanyika leo wala kontena kushushwa au kupakiwa melini kutokana na kile ninachosemekanaa kupuuzwa kwa madai ya wafanyakazi kwa muda mrefu.
Yaani unaambiwa kuna vipengele kama nane vya madai, ila vipengele viwili vikuu kwa sasa hivi ni:
1.meneja utumishi bwana james rhombo aondolewe kazini kwa kinachodaiwa kushindwa kutatua kero za wafanyakazi na meneja mkuu wa ticts bwana nevellie bissete nae aondoke amezidi ubabe na kutotaka kabisa kusikiliza hata kutatua kero za wafanyakazi
2.kampuni kuwanyima hisa asilimia tano za wafanyakazi wakati hisa hizo zipo kwenye kipengele cha mkataba ambapo kuna asilimia tano za hisa kwa wafanyakazi kila mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2009

    1. MKATABA WA TICTS ULIOONGEZEWA MUDA KWA MIAKA 15 BILA TENDER UVUNJWE NA BUNGE, TENDER ITANGAZWE KWA INTERNATIONAL OPERATORS WENGINE. KWAMBA TICTS WAHAKUWEKEZA KAMA WALIVYOAHIDI NI SABABU NYINGINE YA KUUKATISHA.

    2. MULTIPLE OPERATORS WARUHUSIWE KUSHINDANA, KAMA VILE SHIPPING AGENTS, ILI WATEJA WAPELEKE MIZIGO YAO KWA WALE WANAOFANYA KAZI VIZURI. THA IWE INAWAPIGA FAINI(DEMMURRAGE/STORAGE)WALE OPERATORS WATAKAOZEMBEA. KWA KUOGOGA PEBALTIES, WATAFANYA KAZI VIZURI!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2009

    Huyu james rhombo si yule jamaa alikuwa PWC? alikuwa kafulia sana wakati yuko hapo, kafika ticts kapata kacheo kidogo sasa si unajua maskini akipata matako hulia mbwata? ananyanyasa sana wafanyakazi, halafu jamaa huwa ni uncivilized vibaya sana!! anaongea kwa kuropoka, hataga points kabisa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2009

    Andolewe tu. watu kama hao michizo sana. ajui cheo ni dhamana tu ya kazi.Ni mfanyakazi kama wafanya kazi wenzie.Sasa aondolewe ndio akafulie vizuri huko mtaani.Atajiju

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2009

    Hapa wadau kama una mzigo wako wahi mombasa la sivyo utaishia kupata pressure! manake mzigo unaweza kucheleweshwa kwa sababu zao na wewe ukaambiwa ulipe storage charges bila sababu za msingi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2009

    nikiona hivi naogopa hata kufanya biashara na afrika maana watu ni wababaishaji kwelikweli yaani hapa unaweza kufa na pressure tu hakuna jambo la maana utafanya nao ni hadidhi mtimdo mmoja

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2009

    Hi ndio tatizo ya siasa kuchanganya na biashara, maadui wa akina karamagi hufanya visa na kuwachochea wafanyakazi ili walete migogoro isiyo ya lazima kwa manufaa ya wanasiasa wachache!
    At the end of the day, ni wananchi wanayopata hasara.
    MI NAOMBA HII TENDER IFANYWE UPYA NA IKATAZE WANASIASA KUPATA HISA ZA AJABU KATIKA MAKAMPUNI MAKUBWA BILA YA WAO KUTOA CAPITAL!
    All shipping lines agencies za bongo, wakubwa wana hisa, tena za kupewa bila kuingiza capital.....jiulize ni KWANINI?
    BANDARI NI RASILIMALI MUHIMU KULIKO HATA HIYO MIGODI kwasababu vizazi vijavyo wataambulia mashimo tu kwenye hiyo migodi na madini yatakuwa yameisha, bali BAHARI ITABAKI MILELE NA MILELE!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2009

    Ndugu naombeni msaada, Kufulia maana yake nini?

    Asanteni.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 28, 2009

    Kufulia maana yake ni kupigika.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 28, 2009

    anoni wa 08:35 swali lako ni simpo.
    kufulia maana yake ni pale unaposahau kitu ndani ya nguo zako kabla ya kuanza kufua. kwa mfano ukisahau hela ndani ya nguo yako say shs 1000/= ukafua nguo yako huku hela yako ikiwa ndani ya mfuko wa nguo tunasema kuwa umefulia 1000/= kwenye nguo. hiyo ndio maana halisi ya neno kufulia na ndio haswa iliyokusudiwa hapo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 28, 2009

    kufulia manake ni kuchacha na kuwa huna mpango, yani unakuwa kwishnei...huyu meneja muajiri mshenzi sana, hatetei wafanyakazi yeye anasikiliza wazungu tu yani nahisi huwa anawatawaza kabisa wakitoka ku*ya mana anawatetemekea hadi unamuona, katika wafanyakazi wote anayempa motisha na kumsujudia ni receptionist wake tu ambaye kwa sasa amempa kacheo kengine na ana mpango wa kumpa uafisa hapo ofisini kwake, hana maana hata kidogo..ndo zake tunamjua huyo!!

    ReplyDelete
  11. BIBI UMEMEJuly 28, 2009

    James Rhombo might be many things to TICS but i respect his valuable contributions during HR forums and his wide expertise in the profesion, HR is always tormented and thrown out of the window whether things are right or wrong, this is because you hire and fire, strikes and lock outs are permittable in teh new labour laws but by request, however crying outright that Mr Rhombo should go isnt right, he is a vessel and not decision maker...my comments

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 29, 2009

    Huyo Rhombo alikuja hapo ticts akiwa na kagari kamoja kaliko chakaa ile mbaya aina vw na mimi ni mmoja wa tuliompokea na kutuahidi ushirikiano na kubadilisha mambo hapo terminal.Baada ya kufika hapo na kuanza kupatapata vihela vya ticts akatugeuka,pasipo kuwasikiliza wafanyakazi.Ndo matatizo ya kumpa madaraka mtu mwenye njaa kwani akipewa chakula husahau makali ya njaa!Ndugu zangu wanaticts,nadhani sasa tumeanza kufumbua macho kwani mtu kama rhombo hakuanza leo kudharau sauti ya wafanyakazi,alianza siku nyingi akishirikiana na gang la watu wengine walioajiriwa kutoka mjini ambao wametajirika kwa jasho la watu wa operation

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 29, 2009

    huyu receptionist ni nani tena????? HR kuna wadada wawili

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 29, 2009

    wewee...aliyekuwa receptionist akapandishwa cheo ghafla humjui? mbona iko wazi na ni talk of ticts?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 29, 2009

    makubwa haya... WA HR Mnasemaje juu ya hili

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 29, 2009

    Huyo receptionist si ndo alisababisha wasichana flani wa billing hapo tics kufukuzwa kazi? aliwachongea mambo kwa hrm huyo na kwa vile yeye ni mtu wake wa karibu akawatimua kutumia cheo chake. ni mambo mengi tu mengine aibu kusema, ukitaka kwenda chuo ukapeleka form zako akusainie anakataa japo unajilipia mwenyewe lakini hataki, na huwa hana sababu ya msingi, ukitaka kusafiri nje ya nchi ukampelekea ile barua ya introduction kwa ajili ya visa ili tu akusainie kwamba wewe ni muajiriwa wa tics anakataa, hataki mtu meingine aendelee

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 30, 2009

    SISI WA HR TUNASEMA LIONDOKE HILI ZEE TUMELICHOKA, NI VILE TU NI BOSI WETU HATUWEZI KULIAMBIA KWA KUHOFIA KAZI ZETU ILA TUNGEKUWA NA UWEZO TUNGEMPIGA OFISINI SIKU MOJA, AONDOKEEEEEEEEEEEEE!!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 30, 2009

    tatizo lake anasikiliza majungu sana, watu wanaompelekea umbea ndo anaowapenda na kuwashabikia, ukiwa huendekezi umbea ndo hakupendi hata kidogo, safari hii imekula kwake, ajiuzuru tu bwana tumemchoka kweli, mameneja wenzie walishaondoka kwa kuona mbele, yeye kajibweteka ticts kazi yake kubwa ni kunyanyasa tu, mtu mzima hovyo sana

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 30, 2009

    jamani ila jamaa mgumu sana, juzi tulivyomzomea vile nilijua hatakaa aingie bandarini tena, kesho yake kaja kakondaaaa hadi suruali inamvuka shati linachomoka hovyohovyo tu. angepumzika sasa na kupenda watu, kwa kweli safari hii imekula kwake mkuu, kwi kwi kwi kwiiiiiiiii

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 30, 2009

    Niliangalia na kuzikiliza habari ktk TV, mgomo wa wafanyakazi TICTS umeisha, hii ina maana madai yao yamesikilizwa na kama yamesikilizwa yalikuwa ni ya kweli.

    kati ya Chanzo cha mgomo ni kunyimwa maslahi, anayekwamisha hayo ni nani, Wawekezaji nao wana policy zao inalekea huyo rombo hana sauti.

    Kutoka maisha magumu kwenda maisha bora ni safi. bigg up man, Keep it up rombo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...