a
Shafi Adam Shafi
IJUMAA YA KUKUTANA NA MWANDISHI
Wiki hii katika mjumuiko wetu wa kila Ijumaa katika Mkahawa wa Vitabu Soma tunawakaribisha kukutana na mwandishi maarufu Ndugu Shafi Adam Shafi.
Mwandishi wetu atazungumzia riwaya yake maarufu ya “Vuta n’kuvute” na zinginezo kama Kasri ya Mwinyi Fuad na Kuli. Riwaya ya Vuta n’kuvute imepata tuzo kadhaa ikiwemo tuzo ya mswada bora wa riwaya za kiswahili kabla hata kuchapishwa, kwenye tamasha la vitabu nchini lililofanyika jijini Dar kwa mwaka 1998 na pia kutumika katika mtaala wa shule za sekondari nchini hadi hivi sasa.

Siku: Ijumaa 24 Julai 2009
Muda: Saa Kumi na Moja na nusu Jioni hadi Saa Mbili usiku
Mahala: Soma Mkahawa wa Vitabu
Tafadhali njoo na daftari au shajara yako.
Njoo na maswali yako.
Vitabu vitakuwepo kwa ajili ya kununua.
Nyama choma toka mgahawani itakuwepo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2009

    MGAHAWA UKO WAPI? KWA TUSIOJUA

    ReplyDelete
  2. BIBI UMEMEJuly 23, 2009

    nilikuwa nangojea kwa hamu sana kwa nafasi hii, what about the other 'gwiji' who used a local sleuth Bwana Msa ?? i'd give anything to read the books, kisima cha giningi, kosa la bwana msa etc etc, i grew up reading books and I LOVE READING BOOKS, kudos mgahawa !

    ReplyDelete
  3. Jamaa fulani hiviJuly 23, 2009

    Huyu mzee yuko makini sana katika fani yake...Kuli nilijibia mtihani form 4 enzi hizo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2009

    Hakika nianze kwa kuwapongeza waanzilishi wa wazo la kuandaa mijadala na kuwakaribisha watu muhimu katika mghahawa wa SOMA. Pili nimpongeze Shafi A.Shafi kwa kazi zake nzuri! Swali mmoja je yupo tayari kuandika kitabu kinachohusu Tanzania ya leo na michakato ya ukuzaji waUCHUMI wa watu wakubwa? Mafsadi?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2009

    kwa kweli tunapaswa kujivunia watanzania kua na waandishi mahiri kama shafi Adam shafi, unastahili pongezi kwa vile sijaona aliyevunja rikodi yako ya uandishi.
    nilitokwa na machozi wakati nasoma riwaya yako ya HAINI nikioanisha na historia ya kweli ya kesi ya mwanzo ya uhaini.
    Mungu akupe maisha marefu utuandikie tena na tena.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2009

    go shaffy, thats my uncle

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2009

    Yana mwisho haya.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2009

    HONGERA SANA SHAFI ADAM SHAFI VITABU VYAKO VIMENIFUNDISHA MENGI NA PIA VIMENIFANYA NIPENDE KUSOMA HISTORIA.NI JAMBO LA KUJIVUNIA KWA WATANZANIA KUWA NA MTU KAMA WEWE...TUNAKUENZI.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2009

    ningekuwa bongo lazima ninge hudhuria mjadala huo. namfagilia sana huyu mzee!!hasa nikikumbuka riwaya yake ya kuli,haswa pale rashid alipokuwa anambembeleza amina amfungulie mlango wakati amelewa anasema kiulevi ulevi "amina mpwenzi" akimaanisha mpenzi!hahaha miaka mingi sana imepita but i still remember that.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...