THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

JK atembelea maonesho ya nane nane dodoma

JK akikagua matunda aina ya topetope wakati alipotembelea viwanja vya maonesho ya Nanenane huko eneo la Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma.
JK akiangalia mafuta ya Alizeti yaliyozalishwa na wakulima wadogowadogo mkoani Dodoma jan wakati alipotembelea baadhi ya mabanda katika viwanja vya Nanenane.


Kuna Maoni 19 mpaka sasa.

 1. Wutasa Anasema:

  MKubwa hiyo sio topetope bali ni Stafeli,Nawakilisha

 2. Anonymous Anasema:

  kila jambo au kila kitu kinakuwa na mara ya kwanza ,kwa upande wangu leo kwa mara ya kwanza tunda litwalo stafeli kusikia wezetu wanalita Topetope ,si madogo :-)))

 3. Anonymous Anasema:

  Topetope ndio tunda gani?Hayo yanaitwa Mastafeli!

 4. Julius (Dodoma) Anasema:

  Hilo tunda siyo topetope! Linaitwa "Staferi"
  Michuzi unapotosha watoto wetu ambao wangependa kuelewa matunda!

 5. KIPILI Anasema:

  Michuzi unachanganya mambo bwana, ni sawa na "chungwa" kuita "chenza"

  Hayo yanaitwa "MASTAFELI", Uliza waztu wa Tabora hayo yapo mengi sana, hujulikana kama STAFELI. yapo mengine ambayo ni madogo madogo jamii moja ila huitwa "TOPETOPE" Ni hayo mkuu.

 6. Anonymous Anasema:

  Hata kule Bagamoyo yapo kwa wingi sie twayaita mastafeli, wewe mwezetu waita topetope?

 7. Anonymous Anasema:

  wakati mwingine huwa naamini wachangiaji wa safi hii kuitwa mambumbumbu. ona walivyobishana jina tu, na kusahau mada na madhumuni ya picha hizo kuwekwa hapo. kwa jina lolote, rais alitakiwa kujiuliza mmea huo ulivyotoa tunda dhaifu huku majani yake yakionyesha kunyauka, hapo ujumbe nini.
  Aidha, angalia mafuta hayo yalivyo na pack yake, rais anaujumbe gani kwa maskinihao wanaotumia vinu na machujio kupaki kwa mikono yao, wasidiweje,kukuza soko na uzalishaji.
  samahani kwa kuwaita member wako vile, kwani wanaubishi usio wa msingi.

 8. Anonymous Anasema:

  Michuzi usinibanie hii. Nampenda sana rais wangu kikwete, lakini sipendi anapotembelea mahali huku akiwa ameweka mikono mifukoni. Naona na ndugu yake Pinda nae ameanza kumwiga bosi wake katika kitabia hiki cha kuweka mikono mfukoni katika shughuli ya hadhara. Nawasilisha

 9. Amos (UK) Anasema:

  sasa nakubaliana na dr shayo alipokuja tanzania kuwashauri wakulima, na kuwaambia kuwa packing ya bidhaa zetu ndiyo tatizo kubwa. au tayari mmeshasahau yale aliyosema?
  hivi michuzi, hiyo report ya utafiti wa shayo iko wapi? inapatikana wapi? na ni nani mmiliki?

  Unajua tunapohimiza kilimo vile vile tuhimize namna ya kuweka pamoja mfumo wa kupack hiyo product.

  Kutokana na hiyo picha namuona mkuu ameridhika na hiyo packing ya mafuta! au aliwapa somo?

 10. Hildebrand Shayo Anasema:

  Hilo tunda aliloshika Muheshimiwa rais wa jamhuri ya Tanzania linaitwa CUSTAD APPLE yaani kwa lugha ya kiswahili STAFERI

  Topetope linaitwa Fruit Horoscope

  Ila michuzi hujafanya kosa, kwa umesema tunda aina ya topetope.

  Kuna aina nyingi za jamii ya tunda hili.

 11. Anonymous Anasema:

  Anon wa Mon Aug 03, 02:48:00 PM

  Inavyoonekana wewe ndiyo mbumbumbu tena mzungu wa reli. Yaani kule kwetu tunasema umedandia gari kwa mbele. Kama wewe una cha kuchangia si uchangie tu?, japo kuna "matypo" kibao yanakudefine. Watu makini kwanza tunaangali range ya muda wa wachangiaji wote.
  observation ni kuwa:

  1 kuanzia 11:44 am mpaka 12:56 pm takriban saa moja huenda michuzi alikuwa idle, haku-update blogu, hivyo kufanya watu wengi wenye mawazo sahihi kuchangia na yeye alipo-update akawaweka online wote kwa pamoja.

  2. Ukiangalia hakuna ubishi dhidi ya wachangiaji, bali ni katika kumuelewa Michuzi usahihi wa Jina la matunda.

  3. Kama wewe ulikuwa na mtazamo tofauti ulitakiwa kuutoa bila kuita wenzeko mambumbumbu kwani kwa kufanya hivyo umewakumbusha watu msamiati unaofaa wewe uitwe, kutokana na post yako kwani haieleweki ulichotaka kuelezea ni nini hasa.

 12. Anonymous Anasema:

  Hongera mdau Hildebrand shayo kwa kutupa hiyo dose

  jamani, tunapochangia hoja changia ukiwa umefanya kautafiti kidogo siyo unakurupuka kama mwizi au ulikuwa usingizini

 13. Anonymous Anasema:

  Jeans na T-shirt ingemtoa sana raisi wetu na tena hivyo wanavyosafiri kila leo lazima wana viwalo vya nguvu ila suti shambani?? well..

 14. Anonymous Anasema:

  Hilo tunda linaitwa Stafeli au kwa kiingereza Soursop tofauti na mdau Hilderbrand Shayo alivyosema ambalo huwa na kama miiba midogo isiyochoma, na tope tope ni jamii moja ya hayo mastafeli sema lenyewe huwa na ganda lenye maumbo ya pods(sifahamu kiswahili chake) na mbegu huwa katika kila uvimbe mmoja wake.

 15. Anonymous Anasema:

  Ndugu yangu usiye na jina (Aug 3, 02:48 PM)kama kwako kuna kioo cha kujitazamia nenda kajiangalie kwa makini utaona wapi umbumbu wako ulipolalia, "HII NI KWA FAIDA YAKO"

 16. Anonymous Anasema:

  mimi siko kwenye hoja ya stafeli wala topetope ila nakuungana mdau uliyesema mr president sehemu kama hizo za maonyesho iwe ni ya viwanda mashambani awe anavaa kama jeans na shati hii mambo ya suti kila wakati hainogi, simfagilii mtu hapa tizazameni tu obama ameshindwa tu kuvaa kipens ila uvaaji wake huwa unaendana na mazingira halisi ya eneo husika, annoy wa Aug 04,21:00 AM umenichekesha hadi basi
  mdau CANADA

 17. Anonymous Anasema:

  Mhesh. Rais kumbuka kuwa suti hizo nyingi zinatokana na mfuko wa Pesa za mavazi ya Rais (Kodi zetu watokwa jasho mgogo, basi si vizuri mara kwa kuvaa na kuzichosha na mwishoe utajikuta bajeti ya masuti ni sawa na gharama ya kujenga shule ya msingi huko Kidodi na kulipa mishahara ya walimu wa shule hiyo kwa muda wa miezi sita hivi. Basi kama kwenye maonyesho ya bidhaa basi vaa suruali la khaki na shati jeupe, utapendeza tu, Mbona mama mama yetu Salma anapendeza ma vitegenge vya ubungo, sasa suti za 5th Avenue (sakis ) New York kila wakti nini cha mno?

 18. Anonymous Anasema:

  Hayo ni mastafeli au soursop fruit (Annona muricata)kwa Kiingereza, yanafanana na matoptope ambayo maganda ni tofauti. Topetope kwa Kiingereza ni custard-apple (Annona reticulata)ni jamii moja na mastafeli.

 19. Anonymous Anasema:

  hayo ni mastaferi ni matunda matamu sana kwa kutengeneza juisi ingelikuwa la maana sana kuyatumia kwa kutengeneza juisi wakulima wangepata mafanikio makubwa kwani juisi za staferi ni bei mbaya sana hapa nilipo nipo na boks la juisi ya staferi nakunywa kwani nayapenda sana.....naomba msimlaumu kaka michuzi kwa kuita matopetope kwani kila mtu anaweza kukosea ...mdau uholanzi