JK akikagua matunda aina ya topetope wakati alipotembelea viwanja vya maonesho ya Nanenane huko eneo la Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma.
JK akiangalia mafuta ya Alizeti yaliyozalishwa na wakulima wadogowadogo mkoani Dodoma jan wakati alipotembelea baadhi ya mabanda katika viwanja vya Nanenane.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. MKubwa hiyo sio topetope bali ni Stafeli,Nawakilisha

    ReplyDelete
  2. kila jambo au kila kitu kinakuwa na mara ya kwanza ,kwa upande wangu leo kwa mara ya kwanza tunda litwalo stafeli kusikia wezetu wanalita Topetope ,si madogo :-)))

    ReplyDelete
  3. Topetope ndio tunda gani?Hayo yanaitwa Mastafeli!

    ReplyDelete
  4. Julius (Dodoma)August 03, 2009

    Hilo tunda siyo topetope! Linaitwa "Staferi"
    Michuzi unapotosha watoto wetu ambao wangependa kuelewa matunda!

    ReplyDelete
  5. Michuzi unachanganya mambo bwana, ni sawa na "chungwa" kuita "chenza"

    Hayo yanaitwa "MASTAFELI", Uliza waztu wa Tabora hayo yapo mengi sana, hujulikana kama STAFELI. yapo mengine ambayo ni madogo madogo jamii moja ila huitwa "TOPETOPE" Ni hayo mkuu.

    ReplyDelete
  6. Hata kule Bagamoyo yapo kwa wingi sie twayaita mastafeli, wewe mwezetu waita topetope?

    ReplyDelete
  7. wakati mwingine huwa naamini wachangiaji wa safi hii kuitwa mambumbumbu. ona walivyobishana jina tu, na kusahau mada na madhumuni ya picha hizo kuwekwa hapo. kwa jina lolote, rais alitakiwa kujiuliza mmea huo ulivyotoa tunda dhaifu huku majani yake yakionyesha kunyauka, hapo ujumbe nini.
    Aidha, angalia mafuta hayo yalivyo na pack yake, rais anaujumbe gani kwa maskinihao wanaotumia vinu na machujio kupaki kwa mikono yao, wasidiweje,kukuza soko na uzalishaji.
    samahani kwa kuwaita member wako vile, kwani wanaubishi usio wa msingi.

    ReplyDelete
  8. Michuzi usinibanie hii. Nampenda sana rais wangu kikwete, lakini sipendi anapotembelea mahali huku akiwa ameweka mikono mifukoni. Naona na ndugu yake Pinda nae ameanza kumwiga bosi wake katika kitabia hiki cha kuweka mikono mfukoni katika shughuli ya hadhara. Nawasilisha

    ReplyDelete
  9. sasa nakubaliana na dr shayo alipokuja tanzania kuwashauri wakulima, na kuwaambia kuwa packing ya bidhaa zetu ndiyo tatizo kubwa. au tayari mmeshasahau yale aliyosema?
    hivi michuzi, hiyo report ya utafiti wa shayo iko wapi? inapatikana wapi? na ni nani mmiliki?

    Unajua tunapohimiza kilimo vile vile tuhimize namna ya kuweka pamoja mfumo wa kupack hiyo product.

    Kutokana na hiyo picha namuona mkuu ameridhika na hiyo packing ya mafuta! au aliwapa somo?

    ReplyDelete
  10. Hildebrand ShayoAugust 03, 2009

    Hilo tunda aliloshika Muheshimiwa rais wa jamhuri ya Tanzania linaitwa CUSTAD APPLE yaani kwa lugha ya kiswahili STAFERI

    Topetope linaitwa Fruit Horoscope

    Ila michuzi hujafanya kosa, kwa umesema tunda aina ya topetope.

    Kuna aina nyingi za jamii ya tunda hili.

    ReplyDelete
  11. Anon wa Mon Aug 03, 02:48:00 PM

    Inavyoonekana wewe ndiyo mbumbumbu tena mzungu wa reli. Yaani kule kwetu tunasema umedandia gari kwa mbele. Kama wewe una cha kuchangia si uchangie tu?, japo kuna "matypo" kibao yanakudefine. Watu makini kwanza tunaangali range ya muda wa wachangiaji wote.
    observation ni kuwa:

    1 kuanzia 11:44 am mpaka 12:56 pm takriban saa moja huenda michuzi alikuwa idle, haku-update blogu, hivyo kufanya watu wengi wenye mawazo sahihi kuchangia na yeye alipo-update akawaweka online wote kwa pamoja.

    2. Ukiangalia hakuna ubishi dhidi ya wachangiaji, bali ni katika kumuelewa Michuzi usahihi wa Jina la matunda.

    3. Kama wewe ulikuwa na mtazamo tofauti ulitakiwa kuutoa bila kuita wenzeko mambumbumbu kwani kwa kufanya hivyo umewakumbusha watu msamiati unaofaa wewe uitwe, kutokana na post yako kwani haieleweki ulichotaka kuelezea ni nini hasa.

    ReplyDelete
  12. Hongera mdau Hildebrand shayo kwa kutupa hiyo dose

    jamani, tunapochangia hoja changia ukiwa umefanya kautafiti kidogo siyo unakurupuka kama mwizi au ulikuwa usingizini

    ReplyDelete
  13. Jeans na T-shirt ingemtoa sana raisi wetu na tena hivyo wanavyosafiri kila leo lazima wana viwalo vya nguvu ila suti shambani?? well..

    ReplyDelete
  14. Hilo tunda linaitwa Stafeli au kwa kiingereza Soursop tofauti na mdau Hilderbrand Shayo alivyosema ambalo huwa na kama miiba midogo isiyochoma, na tope tope ni jamii moja ya hayo mastafeli sema lenyewe huwa na ganda lenye maumbo ya pods(sifahamu kiswahili chake) na mbegu huwa katika kila uvimbe mmoja wake.

    ReplyDelete
  15. Ndugu yangu usiye na jina (Aug 3, 02:48 PM)kama kwako kuna kioo cha kujitazamia nenda kajiangalie kwa makini utaona wapi umbumbu wako ulipolalia, "HII NI KWA FAIDA YAKO"

    ReplyDelete
  16. mimi siko kwenye hoja ya stafeli wala topetope ila nakuungana mdau uliyesema mr president sehemu kama hizo za maonyesho iwe ni ya viwanda mashambani awe anavaa kama jeans na shati hii mambo ya suti kila wakati hainogi, simfagilii mtu hapa tizazameni tu obama ameshindwa tu kuvaa kipens ila uvaaji wake huwa unaendana na mazingira halisi ya eneo husika, annoy wa Aug 04,21:00 AM umenichekesha hadi basi
    mdau CANADA

    ReplyDelete
  17. Mhesh. Rais kumbuka kuwa suti hizo nyingi zinatokana na mfuko wa Pesa za mavazi ya Rais (Kodi zetu watokwa jasho mgogo, basi si vizuri mara kwa kuvaa na kuzichosha na mwishoe utajikuta bajeti ya masuti ni sawa na gharama ya kujenga shule ya msingi huko Kidodi na kulipa mishahara ya walimu wa shule hiyo kwa muda wa miezi sita hivi. Basi kama kwenye maonyesho ya bidhaa basi vaa suruali la khaki na shati jeupe, utapendeza tu, Mbona mama mama yetu Salma anapendeza ma vitegenge vya ubungo, sasa suti za 5th Avenue (sakis ) New York kila wakti nini cha mno?

    ReplyDelete
  18. Hayo ni mastafeli au soursop fruit (Annona muricata)kwa Kiingereza, yanafanana na matoptope ambayo maganda ni tofauti. Topetope kwa Kiingereza ni custard-apple (Annona reticulata)ni jamii moja na mastafeli.

    ReplyDelete
  19. hayo ni mastaferi ni matunda matamu sana kwa kutengeneza juisi ingelikuwa la maana sana kuyatumia kwa kutengeneza juisi wakulima wangepata mafanikio makubwa kwani juisi za staferi ni bei mbaya sana hapa nilipo nipo na boks la juisi ya staferi nakunywa kwani nayapenda sana.....naomba msimlaumu kaka michuzi kwa kuita matopetope kwani kila mtu anaweza kukosea ...mdau uholanzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...