Mwenyekiti wa Simba SC Mzee Hassan Dalali (kati) akiwa na Mwina Kaduguda katibu mkuu Simba (kulia ) na Mratibu wa Tamasha Mulamu Nghambi
Timu ya Simba Sports Club imeandaa tamasha la kuukaribisha msimu mpya linalotarajiwa kufanyika jumamosi tarehe 8 Agosti katika katika uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo mgeni rasmi atakuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mh. Samwel Sitta.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo Mzee Hassan Dalali amesema leo kuwa tamasha litaanza saa 12 asubuhi ambapo milango itakuwa wazi na kutakuwa nashughuli mbalimbali za Burudani. Waalikwa mbalimbali wakiwemo wabunge na mawaziri na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu, hususan Simba SC, pia wamealikwa.


Kasema siku hiyo kutakuwa na mechi ya utangulizi kati ya timu ya simba U20 na Africa Lyon U20 na baadae itafuatia mechi katika ya Simba na Sports Club Villa ya Uganda ambayo inatarajiwa kuwasili nchini tarehe 6 Agosti.


Mzee Dalali amesema kuwa katika tamasha hilo pia kutakuwa na ugeni kutoka Norway kwenye Timu anayochezea mchezaji Henry Joseph aliyekuwa akiichezea timu ya Simba kabla ya kununuliwa na timu hiyo.


Wageni toka Norway ni pamoja na Rais wa timu hiyo Henrik Mohn, wakala wa FIFA nchini humo, Glenn Shiller na Azzedin Soud wa Grand Canaria Football Centre ya Norway ambao nao pia watawasili tarehe 6 agosti.

Mzee Dalali kasema tiketi zitauzwa kati ya shilingi 50.000 VIP , 20.000 Main Stand, 8.000 Green Stand na 3.000 mzunguko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mulamu Mzizima academy production naona unafanya mavituzz!Ongera sana hivi mzizima wote mko wapi? mbona hatuonani , Mulamu organize mzizima united! watu wakutane!

    ReplyDelete
  2. Wizi mtupu hakuna cha simba day wala swala day hiyo ni njia ya hao viongozi kupata hela kwa manufaa yao.Badala ya kuitisha harambee ya ukarabati wa jengo lao wanaleta simba day!WIZII MTUPUU!!!

    ReplyDelete
  3. Bro Michuzi, naomba uwashauri hao wana wa Msimbazi mimi nafikiri pia katika ratiba yao ya siku hiyo ya birthday ya club katika matukio muhimu yangekuwepo pia na Timu ya wachezaji wa zamani wa miaka hiyo ambapo simba alianzishwa kama bado wapo au wachezaji wowote wa zamani kama ni huyo Gumbo wangecheza mechi na timu nyingine ya wazee wa miaka hiyo, kwakweli ingependeza sana na ingeleta msisimko tofauti kabisa na wao wanavyofikiri. Naomba jitahidi Bro Michuzi ujumbe huu ufike mapema maana siku za maandalizi bado zipo. Naomba kuwakilisha

    ReplyDelete
  4. Hili ni wazo zuri linalofaa kuigwa.

    ReplyDelete
  5. Naona pia huu utakuwa muda muafaka wa six kutoa duku duku zake za watu wanaosema kwamba angatuke.

    ReplyDelete
  6. Wazo la anon saa 11.29 pm ni zuri sana, ingependeza sana kama wazee waliochezea SSC miaka hiyo wangecheza hata kwa muda mfupi. Wanaweza kuchukuliwa waliocheza kati ya 1970 hadi 1990 wakatengeneza timu mbili na baadaye wakapewa kitu kidogo maana nafahamu wengi wapo ktk hali mbaya. Kama wazo hili halijachelewa ni vyema likafanyiwa kazi haraka.

    ReplyDelete
  7. Naunga mkono kabisa wazo hili na ikiwezekana iwe kila mwaka. ni wakati wa mashabiki, wapenzi na wanachama wa simba kuunga mkono klabu yao.

    Mara nyingi viongozi wameomba michango, lakini wana simba wameshindwa kuchangia klabu, sasa ni wakati muafaka kwa wanasimba kuichangia klabu yao kwa ajili ya kuleta maendeleo.
    Naungana na mdau hapo juu kuwa, ingefaa sana kama siku hiyo kukawa na mechi ya wachezaji wa zamani wa simba, watu kama akina malota soma, mwameja,king kibadeni,Adam sabu, Martin kikwa n.k wangecheza mechi na timu kama ya wazee wa Dar, ama Wabunge, ama wawakilishi naona ingevutia sana.

    ReplyDelete
  8. Anon wa 9.30 am trh 4.8.09 wazo lako la ziada ni safi sana ila kwa taarifa yako Adam Sabu na Martin Kikwa walikwishatangulia mbele ya haki. Mwenyezi Mungu awarehemu.

    ReplyDelete
  9. Mimi sipendeleagi kuzungumzia mavazi, lakini kuna mavazi maalumu kwa sehemu maalumu,nafikiri ni vyema uwe kiongozi au mtu wakawaida ukayaheshimu mavazi hayo.
    Ndio kutokana na halihalisi ni vigumu, lakini kwa dharura ni vyema tukamuogopa Mungu na kuyavua kwamuda, hadi unachokifanya kikipita basi yavae.Nafikiri mumenielewa kwa wenye kuelewa.

    ReplyDelete
  10. nawapongeza sana wana simba kwa hatua yao,lakini mimi najiuliza nini madhumuni yao? kama ni ukarabati wa jengo kwanini wasipige harambee kwa ajili ya kukarabati jengo lao? na hiyo party walioandaa wanauhakika kuwa gharama zao walizotumia zitarudi?maana tff wenywe kila mara wana pata hasara sasa sijui sisi wanasimba tumejipangaje ukiangalia jengo ndio hilo chafuuuuu wapinzani wetu yanga wamejitahidi wamekarabati jengo lao mpaka raha.

    ReplyDelete
  11. Kwa kumjibu anon wa trh 4.8.09 saa 02.08pm, Simba walitangaza harambee kwa ajili ya kusajili wachezaji wa msimu huu na walitoa namba ya akaunti ya benki lakini wapenzi hawakuchangia ndio maana wameona wabadilishe namna ya uchangiaji. Kuhusu ukarabati wa jengo la Yanga bila shaka kila mpenzi wa soka anafahamu jinsi fedha za ukarabati huo zinavyopatikana nadhani nimeeleweka na sioni kama kuna haja ya kuendelea na maelezo.

    ReplyDelete
  12. kanzu, baragashia na kirimanjaro lager wapi na wapi???

    ReplyDelete
  13. Mdau wa 02:01:00Pm Tumekusoma nafikiri unazungumzia vazi la mzee Dalali mm binafsi nina mashaka na hilo vazi nahisi kuna local believe anazoziamini yy.Kwanza analizalilisha hilo vazi nyuma tangazo la pombe yy analitinga sio ustaarabu mm nilivyoliona nikahisi siku hiyo ilikuwa ijumaa kumbe sio.Hizi klabu zetu sasa zinahitaji viongozi wasomi wenye elimu yao sio hawa wazee wamepitwa na wakati.WIZI MTUPU

    ReplyDelete
  14. HONGERENI SIMBA KWA WAZO ZURI LA KUWA NA SIKU YA SIMBA LAKINI NAWAPENI USHAURI WA BURE NI VYEMA MNGEITUMIA SIKU HIYO KWENDA KUSAFISHA JENGO KA CLABU YENU PALE MSIMBAZI LINATIA AIBU KWA UVUNDO

    ReplyDelete
  15. Kwa kuchangia tu nilikuwa napenda kuwajibu anon 02.01pm ,anon 03.26pm na anon 3.56pm nilitaka kuwakum busha tu kuwa vazi la kanzu si la kiislamu bali ni vazi la kiarabu. vazi la kiislamu ni vazi lolote lile linalostiri maungo yako. uislamu ni imani si kanzu na baraghashia . mkumbuke vazi la kitaifa Uganda kwa wanaume ni kanzu na koti je mnataka kusema waganda wote ni waislamu ? nendeni Egypt(Misri), Lebanon , Syria na Palestine. mtaona waarabu wote wanaume wanavaa Kanzu je wote wale ni waislamu ? kwa kuwajulisha tu nchi hizo nilizokutajieni ndio zinazoongoza kuwa na waarabu wengi walio wakirsto .tukirudi bongo Mrema anavaa baraghashia na Mwalimu Nyerere alikuwa akivaa je nao ni waislamu. kwa hiyo ondoeni mtazamo wenu kuwa kuvaa kanzu ni uislamu unaweza kuvaa full jeans na ukawa imamu na ukaswalisha vile vile . hapo mseme mwenyekiti wa Simba Dalali kavaa vazi la kiarabu lakini si la kiislamu. kwa kuongezea tu Dini ni imani si jina wala vazi.
    mdau Maalim Kacheche.

    ReplyDelete
  16. Mambo ya walawi yanasemaje: Tujikumbushe Any.12.05

    4.Ataivaa ile kanzu takatifu ya kitani, atakuwa na zile suruali za kitani mwilini mwake, atafungwa ule mshipi wa kitani, naye atavaa ile kofia ya kitani, hayo ndiyo mavazi matakatifu, naye ataoga mwili wake majini, na kuyavaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...