THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

athumani mambosasa

inasemekana athumani mambosasa ndiye aliyekuwa kipa bora kuliko wote nchini toka wakati huo hadi sasa. wenye data za kuongeza ama kupunguza hayo tunaomba msaada tutani. pichani mambosasa akifanya vitu vyake siku ya yanga na simba uwanja wa nyamagana, mwanza, mwaka 1974 (samahani sio 1994) mbele ya kitwana manara popat wa yanga huku beki mkali shaaban baraza wa simba sc akihakikisha hakuna linaloharibika. mnazungumziaje pia upigaji picha wa enzi hizo na hizi?


Kuna Maoni 33 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Joke Of The Day:
  Redneck Divorce...
  A hillbilly walked into an attorney's office wanting to file for divorce.

  Attorney: "May I help you?"

  Hillbilly: "Yea, I want to get one of those dayvorces".

  Attorney: "Well do you have any grounds?"

  Hillbilly: "Yea, I got about a hundred acres."

  Attorney: "No, you don't understand, do you have a case?"

  Hillbilly: "No, I don't have a Case, but I have a John Deere."

  Attorney: "I mean, do you have a grudge?"

  Hillbilly: "Yea, I got a grudge. That's where I park my John Deere."

  Attorney: "No sir, I mean do you have a suit?"

  Hillbilly: "Yes sir, I got a suit, I wear it to church on Sundays."

  Attorney: "Well sir, does your wife beat you up or anything?"

  Hillbilly: "No sir, we both get up about 4:30 in the morning."

  Attorney: "Well, is she a nagger or anything?"

  Hillbilly: "No she's a little white gal, but our last child was a nagger. That's why I want this dayvorce."

 2. Anonymous Anasema:

  1.Golikipa bora kuliko wote aliepata kutokea Tanzania ni Omar Mahadhi Bin Jabir.
  2.Hio match ilichezwa 1974 na Yanga walishinda 2-1,Gibson sembuli alisawazisha dakika za majeruhi then Sunday Manara akafunga goli la pili.
  3.Upigaji picha wa wakati ule ulikuwa bab kubwa just proffessional kama uionavyo picha hio.
  Wapigaji walikuwa wakali kama jinsi ulivyo wewe,na wapigaji wengi uchwara wa sasa....I mean bongo flavour.

 3. nukta77 Anasema:

  Sikushuhudia kazi yake uwanjani lakini jina lake lilivuma kiasi cha kushindwa kujizuia kumsoma habari zake.... enzi hizo mpira wa miguu ukiwa mpira wa miguu tu!
  ...am Simba SC & Liverpool FC fan!

 4. Anonymous Anasema:

  Idi Pazi
  Hamisi Kinye
  Juma Pondamali
  Omar Mahadh Bin Jabir

  Wote hao walikuwa makipa wazuri kuliko mambosasa

 5. Anonymous Anasema:

  Doh!!1994!!!mambo sasa!!sio mchezo,mwameja mwaka huo alikua anadakia tim gani?

 6. Anonymous Anasema:

  Mr.Misupu hebu sahihisha huo mwaka wa pambano la hao watani wa jadi.bila sha ilikuwa ni 1974 na siyo 1994.wenye kumbukumbu nzuri za data saidieni hapo.

 7. Anonymous Anasema:

  Hiyo ilikuwa 1974(au miaka ile ya 70) siyo 1994.Hata hivyo asante kwa picha inayoleta memories kibao.

 8. PM Anasema:

  Du! Jamaa ananyaka kavu kavu bila gloves? balaa huyo alikuwa!

 9. Anonymous Anasema:

  yuko tight kinoma jamaa. Ni kweli jinsi alivyoruka sidhani tumeshawahi kuwa na golie kama huyo tena. Really impressive

 10. Anonymous Anasema:

  I don't think kama hii ni ya mwaka 1994, 94 simba walikuwa na mwameja golini. Enzi hizo soccer la simba na yanga ilikuwa ndumba tu

 11. Anonymous Anasema:

  kaka nanihii xzamani ndo soka lilikuwa linapigwa mpaka unafurahi...wachezaji walikuwa na nidhamu ya mchezo...siyo cku hizi hakuna kitu..mbwembwe kibao mchezaji anaingiza mambo ya uswazi katika kazi..mpira...erti mchezaji anagombana na refa wakati wa mechi kisha wanadaiana walichokopeshana nje ya uwanja..that is the highest form of unprofessionalism...ndo maana weengine tumeamua kushabikia timu za nje because u get entertained that is all about footbal!!! pourly my views and instict bro Michuzi

 12. Anonymous Anasema:

  Picha hii nilikuwa nayo zamani,wakati ule tulikuwa tukiokota magazeti tunakata picha tunabandika kwenye mabuku makubwa, it was so funny. Turudi kwenye hili la ubora kwa bahati njema nimebahatika kumuona mambosasa akiishia, mahadhi akiishia, pondamali akiwa kwenye form,idd pazi akiwa kwenye form na wengine.
  Kwa vigezo vya soka wengi wanampa mahadhi kwa kuwa alichaguliwa, timu ya africa. Lakini kwa nilivyowaona mimi, nwapanga hivi:- Mambosasa, Pondamali, Mahadhi, Idd Pazi, Mwameja. Wafuatao walikuwa Standard level, Nemes, Riffat, Lly Bushiri,na kidogo haka ka Kaseja ila aondoe ubinafsi. Kuhusu upigaji picha hakika kina mwalimu omari wangepata hii mitambo ya siku hizi wangetisha.

 13. Anonymous Anasema:

  Jamani acheni masihara! enzi hizo mpira ilikuwa ni vita! magolikipa walikuwa wanaogopwa! eti mtu unaingia ndani ya kumi na nane unaleta gozigozi kipa anakuua. Wakati wa kona ndo balaa! Kipa anaruka juu amenyoosha daluga lake kifuani kwa mtu. Mambosasa tulikuwa tunamkubali kwa ku-dive! alikuwa ni noma! hawa makipa wetu sijui walikuwa na vifua vya namna gani, kwa sababu utakuta mchezaji kama Sembuli, alikuwa anapiga makombora kweli, lakini utakuta kipa kama Mambosasa ananyaka mikwaju hiyo ya nguvu kifua, hakuna ku-punch![anonymous wed 16, 10:56 am - hata mimi nilikuwa nalo buku la mapicha kama hilo mpaka kwenye mwaka 1980]

 14. Anonymous Anasema:

  MPIRA ULIKUWA ENZI ZETU,TIMU INA WACHEZAJI 450 NA NYENGINE 450,TIMU INA KIPA 35,REFA ANACHEZESHA MPIRA HUKU KAPANDA PIKI PIKI,UWANJA MKUBWA KUTOKA POSTA HADI MBAGALA..WADAU WA ENZI ZANGU MPO,NINA UMRI WA MIAKA 129,NIMEANZA KUCHEZA MPIRA NIKIWA NA UMRI WA MIAKA 10.ILIKUWA NI 1890

 15. miram3 Anasema:

  Enzi hizo wachezaji walikuwa wakijituma, na walicheza kiwito, lakini sasa mchezo ni pesa. Wachezaji wa sasa wanacheza kutafuta masilahi, kwahiyo ile ari hasa haipo kama hakuna masilahi.
  Kinachosikitisha ni kuwa wachezaji hawa wa siku nyingi wengine wanahali mbaya kiuchumi, wakati walikuwa msitari wa mbele kuliwakilisha taifa. Nimeshangaa hata hawa zekomedy wanawazihaki hawa wasanii wa siku nyingi kuwa ni choka mbaya, jamani sio hivyo hali ile ilikuwa vile sio hali ya sasa. Kuliko kuwasimanga, ni bora tukawapa maneno ya matumaini,tukawaenzi kwa kuwatafutia vitega uchumi.
  M3

 16. Anonymous Anasema:

  ni kweli kabisa kuwa athumani mambosasa ni kipa bora kabisa kuwahi kutokea tanzania sawa na diego maradona alivyokuwa mwanasoka bora kabisa kuwahi kutokea

 17. Anonymous Anasema:

  mhhh kweli enzi hiyo kulikuwa balaa naomba kuwaulizia makipa wafuatao HAMIS MAKENE alishezea coastal Union yupo wapi AGREY CHAMBO,HUSSEIN MWAKURUZO,IDRISA NGULUNGU,JUMA MGUNDA - JANGURINO walikuwa wanamuita JANGRAA, wakina ABUU YASIN NAPILI,RAZAK YUSUPH aka KAREKA ebwana eheee nimewakumbuka sana hawa jamaa walikuwa tanga kipindi icho nasoma kule JOSEPH LAZARO, MCHUNGA BAKARI, VICTOR MKANWA, HAMIS GAGA walikuwa wanamuta GAGARINO, kuna beki alikuwa matata sana kitambo icho alikuwa anaitwa SAID KOLONGO huyu jamaa ilikuwa ni mawili upite wewe mpira ubaki au wewe ubaki mpira upite ebwanaa sio mchezo yupo wapi KAMPIRA jamani duhhh, Yanga walikuwa wakija Tanga lazima waumie na coastal akicheza kipindi icho lazima mvua inyeshe kubwa sana kuna habari kuwa walikuwa wanafukia ZERU ZERU kule baharini kuna siku mpira uliisha wakamsahau akaokolewa na mpita njia,

  jamani hebu tukumbushane kama kuna mtu alikuwa tanga anakumbuka nini mambo ya BWANA KAKA huyu alikuwa ndio mwimbishaji wa timu.. jamani mmeni kumbusha mbali sana sio siri

  Mwenye kiujua mengi zaidi amwage UPUPU

 18. Athumani Mambosasa, Zamoyoni Mogella! THOSE WERE THE DAYS!

 19. Anonymous Anasema:

  Wewe Anony wa Wed Sep 16, 04:47:00 PM, umenikumbusha mbali sana. Waja leo waondoka leo, nyumbani kwetu huko ati. Good memory! Bwana Kaka (Hamisi) alishafariki muda mrefu sana.

 20. Anonymous Anasema:

  yanga na simba nyamagana,nchi yote ilishikwa na kigugumizi,simba walimbebesha jini saad ali,alimanusura afariki dunia,ilibidi mganga wa yanga aliyekuwa bagamoyo anaangalia mpira live kwenye ndoo ya maji,afanye kazi ya ziada ili saad ali apone kwa kupunguza magoli ambayo simba angefungwa siku hiyo

 21. Anonymous Anasema:

  Mkuu,

  Mambosasa alikuwa golikipa mzuri lakini sidhani kama ataweza kuwa mzuri zaidi ya Omar Mahadhi Bin Jabir na Juma Pondamali Mensah. Kwa hiyo kwa mpangilio wangu ningesema:
  1: Omar Mahadhi
  2: Juma Pondamali na
  3: Athumani Mambosasa.

 22. Anonymous Anasema:

  Natamani DC angesoma comment yangu hii kuhusu upiga picha wa wakati huo na wakati huu. Katika hii picha kikubwa alichopatia mpiga picha huo mwaka 74 ni kutumia shutter speed stahiki kwani aliweza "kufreeze action" kama tunavyoona. Na ambacho naamini hakupatia na mpaka leo picha nyingi zinapigwa hivi hivi ni kutotumia/kutojua atumie aperture ipi ili background ya picha iwe "blury and beautiful". Hapa tunaona vizuri mpaka watu waliokaa kwenye majukwaa kwa nyuma. Picha nzuri za kispoti hazipigwi hivyo

  DC mwenyewe Michu huwa "akiamua" ndo anapiga picha za kitaalam otherwise anatusnapiaaga tu snapshots ambazo pia tunashukuru sana kizipata.

  Sijui kama exposure iko sawa make picha inaonekama kama iko washed up ila sababu ni black and white si rahisi kujua

  Picha ni nzuri overall

 23. Anonymous Anasema:

  Katika Umri wangu wa Nina Miaka 10 nilianza kuwa Golikipa hawa Ndio walikuwa Makipa wangu Bora 3
  1.Mohammed Mwameja Jamaa Ingekuwa Umri Mdogo Basi Reading angekuwa Number 1.
  2.Rifat Said - Mwenyezimungu Amrehemu
  3.Pazi
  Na Ndio Niliobahatika kuwaona kwa Macho Na pazi nilibahatika Kukutana Naye na Kumpa Mkono wakati yupo Pan African. Katika Ambao Nimehaidthiwa na Kukubali ni Mkali basi ni Pondamali. MZ.

 24. Anonymous Anasema:

  Ma Kipa wazamani bwana Wanamikwala Mbuzi anamwambia Kiungo hapo Tizama Mistari Mitatu(Adidas). Pazi.

 25. Anonymous Anasema:

  Omari Mahadhi alikubali goli nne DAR kwenda Zambia Mambo akatinga golini na Wazambia hawakuambulia chochote. Hivyo kwa upande wangu Mambo first.

  Picha na hata gazeti la zamani la Daily news lilikua bora. Sielewi pamoja na technologia ya sasa unasoma gazeti unabaki na wino mikononi.
  Enzi hizo hakukua na digital cameras lakini picha zilikua bomba

 26. media Anasema:

  jamaa kavaa njumu ya miraba mi 3(adidas) bongo iliendelea zamani,

 27. Anonymous Anasema:

  ALIKUWA MTU WA TOTOZ, HE WAS AGREAT FRIEND OF MY BROTHER THOSE DAYS.

 28. Anonymous Anasema:

  mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!..mnapowaorodhesha hao makipa wakubwa hebu jaribuni kuorodhesha walidaka katika daraja la juu kiasi gani kimashindano na ugumu wa mechi zenyewe! Ni rahisi kujua kwa nini inahisiwa na wengi kuwa Athman Mambosasa 'Mambo' ni kipa mahiri pengine kuliko woote kwa Simba ('mnyama'/'lunyasi') na bongo (akifufuka leo ukamwambia 'Bongo' atashangaa, wakati wake hakukuwa na jina kama hilo – lol!)..ni kwa sababu kuanzia 1972 (alipokwenda simba akitokea Morogoro) hadi kunako 1978 (japo aliendelea kudaka ikiwa ni pamoja na kusajiliwa na Yanga! -dalili ya wachezaji wengi wa TZ kuisha ni kutambuka klabu hizi 2 wababe: linganisha golden boy mogella, lunyamila, kizota, hussein mmachinga, super kiwelu, nk nk; japo masuala ya akina jujuman greyson, method mogella, deo njohole, athumani idd na kaseja ni tofauti) ni muda ambao kihistoria ya soka la Bongo kulikua na mechi na matukio mengi yanayojipambanua (ikiwa na pamoja na nchi kupata uwezo mkubwa zaidi wa kurekodi matukio hayo tofauti na kabla - enzi za akina Yunge Mwanansali, ambao visa vyao kwa kukosa uthibitisho wa kimaandishi [kwa kupotea ama kutonakiliwa] vinabaki kama hekaya na ngano tu!). Hapo ndipo watoa hoja na maoni na wataalamu wa duru za gozi mtakubaliana name, ilikuwa kilele cha mafanikio ya soka letu (kwa kilele sina maana kuwa enzi haitarudia, inaweza hata ikaja kupita, ila hadi sasa bado hatujashuhudia hivyo)..”Mambo” alihusika na mambo ya Mehalla al-Kubra ambapo inasemekana alinyaka kila walomrushia golini mwa Lunyasi hadi wamanga wakathubutu kumtolea 'jamvia' kulazmisha magoli, ili mnyama achabangwe..kama sikosei (unajua uzee tena!) Mambo pia ndo alowaliza 'walungushi' kule Mufulira, Simba walipoenda Ndola na kuwatoa patupu jamaa wa kaunda. Nikitoka nje ya ‘inshu’, ndani ya uelewa wangu, soka la Tanzania limegusa 'mbinguni' mara kama tano hivi. mbili katika hizo zilimhusisha Mambo..#1. Hii ya nusu fainali na Mehalla al Kubra na ile #2. ya Mufulira (japo kwa maoni yangu, wiki 2 kabla ya hapo, wakati mnyama alipoelekezwa qibla kwa kupigwa 4 mtungi hapo shamba la bibi, “Mambo” alikuwa off-form, na kama bao 2 hivi alitia kwenye 'glovu'). matokeo mengine makubwa kwa taifa ni Yanga kutolewa na Accra Hearts of Oak kwa shilingi na nyingine kwa goli la ugenini; Simba kucheza fainali za makombe ya klabu bingwa afrika - x 2? (1 kumhusisha mwameja, na nyingine pazi) na pia la juu kuliko yote lilitokea Zambia tena, pale shujaa Peter Tino alipofanya vitu vyake nasi tukatinga Lagos, langoni akiwa Pondamali (ndo ambayo inafanya wadau hapa wamtaje sana). Msidhani nimesahau mambo ya Cote d’Ivoire mwaka jana lakini hayo kwangu mimi, mmmm mmmm mmmm!.. Lunyasi pia hawawezi msahau “Mambo” kwa mipambano yao na mwafrika baina ya 1974 na 1975 (hadi februari, kwani baada ya hapo, mwafrika akatimiza kauli mbiu yao ya 'Yanga Imara' – iliwa kizaramo wanasema 'Yanga Imala', maana yake 'yanga kwishnehi!!!! – lol!!')..mwafrika akawayawaya jangwani hadi alipookolewa 1981 na, kama nakumbuka sawaswa, bao 1 la Abdalla Burhani!!Mahadhi Bin Jabbir alimpa ushindani zaidi “Mambo” haswa katika timu ya taifa..na Mwenyezi Mungu amrehemu “Mambo” alikuwa anajiharibia mwenyewe kwa kujulikana kuwa ‘anavuta pochi’ na kuachia magoli, sifa ambayo Mahadhi alifanikiwa kuiepuka kabisa..vinginevyo mtu atakayemtaja Kaseja sijiui itabidi atuletee data za kukata na shoka hapa.. ngoja niishie hapa, 'ngano' zingine, siku ingine – mdau UzenG!

 29. Anonymous Anasema:

  Mimi Mdau mbegu nachotaka kusema tu kwamba tuliwaza vijana hao wa msimbazi 2-1 katika mechi hiyo, wafungaji wetu sunday manara, na Gibbson Sembuli, msimbazi ndio walioanza kufunga, tulirudi na mchaka mchaka na Dundiko letu huku tukiimba" Simba karuka kenda Poland kurudi Mwanza kala Magoli" michuzi upo hapo? yanga tulitokea Romania Na kocha wetu Victor.

 30. Anonymous Anasema:

  Kwangu mimi Mwameja ndo number One, kwanza handsome, kenda hewani akivaa jezi unaona kweli kipa amekaa golini. Ah! Mwameja niseme nini mie

 31. Anonymous Anasema:

  Yanga alitolewa na accra hearts of oak AU ni ASANTE KOTOKO,chini ya golikipa robert mensah

 32. Anonymous Anasema:

  Mkuu wa nanihii, nimekwishatoa comments zangu hapo juu, lakini naomba kwa hisani yako niwakumbushe wadau waliokuwa S'wanga wakati wa enzi za Mwalimu, ukiachilia mbali mambo ya Mambosasa, hivi wanamkumbuka mzee Simbakavu? Huyu mzee alikuwa akitangaza mpira kuliko hata Chars Hilary!, wachezaji wote wa timu za "Komweksi", Kantalamba, Kaengesa n.k alikuwa anawafahamu!na wakati huo mind you, timu ilikuwa inaweza kuchezesha wachezaji kibao! sio siku hizi substitute wanne tu, waaapi!! enzi za mwalimu ni hiari yako kuingiza "nguvu mpya" unavyoweza!

 33. Anonymous Anasema:

  pamoja na sifa zote mlizotoa kwa wote hao mlio wataja inaonyesha kila mtu ametoa maoni yake kwa yule anayemfagilia kwa hiyo nami natoa sifa zangu kwa Omari Massoud kama yupo anayemkumbuka si zani kama kutakuwa na wa kupinga huyo mtu katika kipindi hichohicho cha Chars Hilary yeye ndie alikuwa mtangazaji bora wa mpira hapa nchini kwetu yeye ndie aliyeibuka na kuzibwaga ngoma ngumu za wakati huo akiwemo legend Ahmed Jongo hata huyo Chars Hilary anaelewa hilo kwani alikuwa ni kiboko yao