MUSIC MAYDAY TANZANIA KUFANYA TAMASHA KUBWA
Wanafunzi wa Sanaa ya uigizaji wa Music Mayday Tanzania wakifanya jijini
Jorging na mwalimu wao katika kituo cha talent factory cha shirika hilo
kilichopo Morroco Dar es salaam mapema mwezi huu.

Shirika lisilo la kiserikali la Music Mayday Tanzania, linatarajia kufanya tamasha kubwa linalolenga kupiga vita uuzaji na utumiaji ya Madawa ya kulevya litakalofanyika eneo la manzese kwenye viwanja vya Barccelona mtaani hapo mnamo tarehe 26/09/2009.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Afisa wa huduma kwa jamii wa shirika hilo Bi Prisca Lucas alisema, Tanzania ni moja kati ya nchi zilizoathirika sana na janga hili linalozidi kukua siku hadi siku hasa kwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 14 hadi 36. Alisema;

‘Music Mayday Tanzania ni shirika linalijihusisha sana na maendeleo ya vijana wasanii wa fani mabalimbali hapa nchini, na tumegundua kuwa kuna vijana wengi sana huko mitaani ambao wanauwezo wa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo za kisanii, lakini kwa sababu walishajiingiza tayari kwenye ubwiaji wa madawa ya kulevya, inakuwa ni vigumu sana kuwa na fikra chanya zitakazowaletea maendeleo ’’..


mkufunzi akitoa mafunzo ya kuigiza wakati wa mafunzo hayo katika semina iliyopita
Pamoja na mambo mengine, tamasha hilo linatarajia kutoa mafunzo na mbinu mbalimbali ya jinsi ya kujiepusha pia kuachana na madawa ya kulevya, yatakayotolewa na wataalam waliobobea katika fani hiyo, ambao watatoa pia huduma ya ushauri nasaha kwa waathirika.

Tamasha hilo litatumbuizwa na wasanii mbalimbali wa muziki, maigizo, pamoja na Dansi ya nguvu, likiwemo kundi zima la’ The Motherland live band’ linaloundwa na wasanii mahiri Kala jeremiah, Rogers Lucas, Malfred Mwasote na wengine, na kwamba wasanii chipukizi wa fani mbalimbali watapewa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
Music Mayday Tanzania (MM-TZ) ni shirika lisilo la kiserikali lilianzishwa mwaka 2004 na kusajiliwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) tangu mwaka 2005 ambalo huendesha Programu mbalimbali zikiwemo Bconnected festival, na cheza Tanzania.

Pia shirika hilo hutoa multimedia computer courses, kusaidia wasanii kuimba na kurekodi muziki, sanaa ya uchoraji, kutoa mafunzo ya uinjinia wa sauti( sound engineering), na utengenezaji wa filamu( video production.), kuwasaidia wasanii kupata udhamini wa masomo na ajira, pia shughuli mbalimbali za kijamii.

Mawasiliano:
Music Mayday Tanzania,
Dar es Salaam,
P.O. Box 34747,
Tanzania,
E-Mail:

T. +255 (0)22 277 11 56,
+255 (0)22 277 11 57.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mnaweza kutuambia so far mmeshasaidia wasanii wangapi?maana toka 2005 ni kitambo kidogo na kina kanumba and co. ndo hao bado wanahitaji msaada wanaponea kwa watu binafsi sasa whats the point of ur existence?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...