Wazalendo na Wanataaluma Wenzangu;

Kwa unyenyekevu wa hali ya juu naomba niwaalike wote katika Mkutano wa Wanataaluma waliopo ndani na nje ya nchi kama tangazo nilinavyoonyesha hapa chini. Tunalo deni kubwa la kutambua kubwa, Wasomi na Wanataaluma tunayo sehemu kubwa sana katika kuleta maendeleo na mabadiliko ya kweli katika nchi yetu.

Ni kweli kuwa Serikali na Viongozi wanayo sehemu yao ya kufanya katika kubuni mikakati na sera za kuleta maendeleo ikiwa ni pamoja na kuleta maendeleo ya ujumla. Lakini ikumbukwe pia kwamba, kila mtu binafsi anayo nafasi yake ya kuleta maendeleo ya nchi kwa kuanzia yeye binafsi, familia, jamii nk.

Haitoshi kwetu sisi kuridhika kuwa kwa kuwa tunazo kazi nzuri na bora, na kwa kuwa tuna viapato vya kuridhisha na nyumba za kuishi na usafiri na kusomesha watoto katika shule tunazopenda, basi suala la maendeleo zaidi halituhusu sana japokuwa tunao uwezo mkubwa sana wa kuleta mabadiliko .

Umefika wakati sasa lazima tukubali kuwa Wanataaluma na wasomi sasa tunayo nafasi kubwa sana ya kufanya kuliko wakati mwingine wowote. Kila mtu anayo sehemu yake na tunatoa wito kuwa Wakati tuliokuwa tunausubiri sasa umefika. Tafakari sana na amua sasa kuunganisha nguvu zetu za kiakili, kitaaluma na kisomi kuleta mabadiliko ya kweli.

Fanya kila uwezalo kuhudhuria mkutano huu ambao utakuwa ni wa vitendo na wala si siasa ambazo hazijatufikisha kunakostahili. Jiandikishe sasa na tuma mialiko kwa Wanataaluma wengine wengi waliopo ndani na nje ya nchi. Tarehe ya mwisho ya kujiandikisha ni 15-11-2005. Pia tunachukua nafasi hii kuwaomba udhamini wale wote wanaoweza kufanya hivyo ili kufanikisha yote yaliyokusudiwa.

Kwa yeyote atakayehitaji taarifa za ziada bila ya shaka anaweza kufanya mawasiliano kupitia details zilizoonyeshwa hapa chini. Kila mmoja nayo sehemu yake ya kufanya na nafasi ni sasa. Tafadhali soma Tangazo hapa chini ya barua pepe hii au lililoambatanishwa.

NB: Zingatia kuwa mkutano huu utakuja na mambo endelevu na ya kiutendaji ambayo yatafanyiwa kazi kwa vitendo wakati wote ili kuleta mabadiliko ya kweli.

Wasalaam

EMPOWERMENT

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Inaleta matumaini sana, basi na tutekeleze hilo!

    ReplyDelete
  2. Acheni siasa nyie. Nyimbo za Diaspora tumezichoka. Juzi walishafanya DICOTA.

    ReplyDelete
  3. Una maana deadline ni 15/11/2009? naona umeweka 15/11/2005 hapo.
    Pili, ukitaka kujiandikisha unajiandikisha wapi?

    ReplyDelete
  4. Empowement asante kwa ubunifu huu. Hili ni muhimu sana kuliko mambo ya BBA na kulumbana tu hapa oh sijui mabox na vumbi n.k

    Empowerment, hakikisha Wachokozi wa mada wanazungumza juu ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima nchini na pia kuongeza uzalishaji kwa ajili ya kuinua uchumi na hali ya maisha ya Watz.

    Mimi naanza hapa hapa kupendekeza (hata kama yana machungu):

    1. Hatuna haja ya kuwa na Bunge kubwa sana tulilo nalo. Kila Mkoa unaweza kuwa na Mbunge mmoja tu na Wakatunga sheria bora, wakapitisha makisio na kusimamia shughuli za serikali n.k kwa gharama nafuu kabisa

    2.Suala la kuwa na Mamlaka za Halmashauri na za Wakuu wa Wilaya ni mkanganyiko mtupu. Kila Wilaya iwe na Mkuu wa Wilaya aliyeajiriwa (sio kuteuliwa) kutokana na job specifications zitakazowekwa na yeye awe ndiye Kiongozi Mkuu wa masuala ya maendeleo katika Wilaya yake akisaidiana na watendaji wengine wa kila idara na diwani mmoja tu aliyechaguliwa (Mbunge wa Wilaya).

    Wananchi wote tufanye kazi kwa bidii kila mtu sehemu yake na tupunguze siasa na kutoa nafasi kwa Wataalamu kutushauri ili tuwe na ufanisi katika kilimo, viwanda, maofisini, katika biashara na kila mahala.

    ReplyDelete
  5. Una maana gani unapoandika "Tunalo deni kubwa la kutambua kubwa, Wasomi na Wanataaluma tunayo sehemu kubwa sana katika kuleta maendeleo na mabadiliko ya kweli katika nchi yetu"?. Binafsi sina deni lolote, ila ninaidai hiyo serikali mali asili kibao ambazo mafisadi wamegawana na Wageni!!

    ReplyDelete
  6. I hate this things paying in Dollars! did umemsoma mashaka kweli humu ndani kuhusu dollars and shilings? nyie ndio mnaoukandamiza uchumi wetu. for that am not cumn! good luck

    ReplyDelete
  7. Michuzi naomba umwambie aliyeweka tangazo hili amekosea tarehe, pili angetoa maelezo zaidi kwa kuwakaribisha watu wnaotaka kutoa mada. Maana tuko watanzania tuliorudi nyumbani tunataka na tunaweza kutoa mchango mkubwa katika kongamano kama hili hasa pale tunapoweza kuchangia experience zetu juu kuchangia katika maendeleo baada ya kukaa nje kwa mda mrefu. Tafadhalini tunaomba maelezo zaidi!

    ReplyDelete
  8. kumekuwa na desturi ya muda mrefu miongoni mwa wasomi na watu walioko nje ya nchi, kulalamika na kukosoa sana,wakati mwingine unashindwa kuelewa kweli wamesoma au wamesomewa an wamebahatisha tu? Toka lini maneno yakabadili kitu? Vitendo hukidhi haja. Utaweza sasa kuonyesha kuwa wasomi wetu si waoga na wanakitu wanaweza kufanya badala ya kelele za mlango!

    ReplyDelete
  9. kwanza nianze kwa kutoa hongera kwa juhudi za akili ya kundi au mtu binafsi kwa jamii ya watanzania ambao wanaitaji mchango mkubwa wa wasomi wao hii inaweza kusaidia kutoa MENTAL REVOLUTION kwa wasomi wetu wa tanzania maana kuna nchi nyingi sana duniani zimewekeza kwenye RASILIMALI WATU na sasa wako mbali sana kiuchumi na ni vinchi vidogo sana km malyasia
    pili mimi nigeomba hii ADA ni kubwa sana kwa wasomi hawa maana mi nafikiri walegwa pia kuanzia UFUNDI STADI VETA mpaka PhD maana ndio wasomi wetu hao sasa kipato kinatofautiana sana baina yao ni bora tukafaniye pale mkrumah UDSM kwa gharama nafuu ya maji lkn tukaelewana nini tumeonge mbona REDET wanafanikiwa mikutano yao gharama ni maji tu
    kwa zoezi hili naomba lisiwe dili tu maana watz tuna project nyingi sana ambazo atujui zinaishia wapi ilimradi tu mtu kapata alichokuwa anataka pesa basi utaona kimya hasa sisi tunaojiita wasomi tuna theories nyingi sana hila utendaji hakuna kwenye sekta nyingi sana

    ReplyDelete
  10. msisahau kuzungumzia maswala ya uwanja wa ndege kuibiwa,bandari kutozwa fedha nyingi,posta ukituma vitu havifiki,barabara hazitoshelezi foleni sehem nyingine hamna taa,serikali za mtaa kupewa computer kwa kuhifadhi nyaraka muhim,pia zikarabatiwe viongozi wawe na elimu ya kutosha,juu ya mlima wetu kilimanjaro kibao chake kibadilishwe,wanaovamia mbuga za wanyama wafukuzwe kuwekwe mikataba yenye kueleweka maarufuku waarabu watatuteka,kuchimba mashimo na kuachwa wazi barabarani au mjini,wafanyakazi wa takataka waweke tank za taka tanzania nzima ipewe kampuni inayoweza,wanaojenga barabara wamalizie kuweka mauwa mazuri mji upendeze,wanaojenga nakuacha mabati au vitendea kazi baada ya kumaliza ujenzi wachukuliwe hatua,kuweka vituo vya basi nchi nzima,kamera sehemu muhimu kama barabara kuu,mabenki,sehemu muhimu za mitambo au maduka makuu iwe sheria ya lazima kuepusha ujambazi,kuweka faya kila wilaya ziwepo nne sio kungoja za kariakoo tuu,kila hospitali lazima kuwe na ambulance nne ikiwezekana,jeshi letu la poloce wapewe mkopo wa kompyuter ili waweze kujifunza na kujionea ulimwengu unavyoenda kwa kasi,tupewe vitambulisho vya uraia ambavyo tunaweza kupigia kura na kucheki imfomation zote kuhusu muhusika,kama tarehe yakuzaliwa kazi gani anakaa wapi nyumba namba ngapi ofice gani mshahara wake inakua kama id yake.pia ma supermarket yaongezwe viwanda vijitahidi kutengeneza vitu mbali mbali kuweka hali ya nchi kuwa safi angalau kwa mjini,sina mengi nina machungu na nchi yangu natamani ninavyoongea ndio vifanyike ni hayo tu watusaidie kukuza uchumi haraka.

    ReplyDelete
  11. Tuanze kupenda na kujenga uchumi kwa kuthamini SHILING. WHY PAY IN $$$$$$$$?

    ReplyDelete
  12. 1.badili tarehe ya mwisho wa kujiandikisha
    2.tangazo lako dogooo sana hatuwezi soma maandishi mengine
    3.kwanini dollar fees?jamani mbona wezetu wengi tu tena uko nje kila kitu almost walipa kwa feza yao,Tz kuna wazimu gani?
    4.hujaainisha ukilipa iyo pesa(dollar?) yajumuisha nini?vingine watu wajitegemee au?na muda wa meeting waanza na kuisheje?

    ukue wee mtoa tangazo alaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...