Hello Kaka Michuzi,
pole na kazi ya kuelimisha na kuburudisha jamii.
Sisi tunahitaji gari sana, ila namna ya kupata gari tuitegemeayo sisi hatujaona mahali wanafanya. Ni kwamba: Tunatafuta mtu/commission agent/duka ambapo tunaweza kuchukua gari na kulipia kidogo kidogo kila mwezi (mfano Tsh 400,000/= -laki nne kila mwezi) kisha tukikimaliza kulipa gari linakuwa letu.
Kwa mfano tukichukua gari la 9.6m/= ina maana ndani ya miezi 24 tu tunakuwa tumemaliza kulipia. Tupo tayari documents zote za gari ziwe za/kwa mmiliki mpaka tutakapomaliza deni hilo. Bima tutalipia sisi likila mzinga isiwe hasara kwa muuzaji. Pia tuna mishemishe zetu huenda saa yoyote mambo yakikaa sawa tunamalizia bila kungojea muda wote au tukawa tunalipa mara mbili ya hiyo laki nne mfano.
Je, kuna sehemu wanapokea utaratibu huu?

Tumechunguza kivyetu tumegundua kuna gari zinakaa yard/dukani zaidi ya miezi hiyo 24, kwa hiyo tunaamini ni suala linalowezekana kabisa. . Mikopo ya benki mhhh, watuwie tu radhi!
Tufahamisheni tafadhali wadau.
Ahsanteni,
Dada M na Kaka D
tzpekee@gmail.com
Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Kutokana na hesabu zenu za malipo naona mmesahau kitu kidogo kinachoitwa interest

    ReplyDelete
  2. mnaoneka wazi kuwa mnataka kufosi mambo yaliyo juu ya uwezo wenu!!! inaoneka uwezo wa kutumngua usafiri hamna ila mnalataka kulazimisha mambo. kama mnaweza kuwa mnalipa hizo au x2 iweje mshindwe kutungua kimkoo chenu na hali cku hizi magari bei cheee tu. acheni nyie bibi na bwana zoeeeni daladala tu hizo laki nne nne zenu muwe mnaziweka benki baada ya hiyo miezi 24 zitakuwa zimetimia mnazi-download mnaagiza kimmkoko chenu saafi.

    ReplyDelete
  3. Ni wazo zuri sana na binafsi hushangaa na sipati majibu ya kutosha ya je kwanini bidhaa nyingi Tanzania zinauzwa cash,vitu kama magari,runinga, pikipiki n.k. Ni kwamba Tanzania watu wana hela sana? Watu hata wakienda kwenye shoping mall pale MC waweza kwenda kwenye duka leo pale MC ukakuta bidhaa yauzwa labda alf 45 kesho unakuta ile karatasi ya bei haipo ukichukua ukifika sehemu ya malipo unaambiwa ati alfu60 aaaah!
    Eti tiketi ya ndege inauzwa kwa dola na si shilingi, laptop pia yauzwa kwa dola khaaa!
    Anyway hii hoja ya mdau ni nzuri hata na mimi nasubilia jibu kama ikiwezekana nafikiri itakua jambo la heri sana hasa kama ile riba nayo haitakua kubwa sana kwani ni kweli gari za yard haziukiki kiivyo na mbaya zaid ikizidi kukaa wanauchumi mnafahamu inakuaje.

    ReplyDelete
  4. Hata mimi nadhani utaratibu huu ungenifaa, mkuu michuzi hebu tusaidie hapo

    ReplyDelete
  5. HIVYO NDIVYO INAVYOFANYIKA HUKU KWA WENZETU NI WATU WACHACHE SANA HUNUNUWA GARI KWA CASH AT ONE GO HATA AKINA DAVID BECKHAM WANANUNUA MAGARI KWA MTINDI HUO, HUKU KINACHOFANYIKA NI KWAMBA KAMA GARI SEMA RANGE ROVER VOGUE NI £155,000UNATOA SEMA £10,000. WANAITA DEPOSIT THEN WANAKUFANYIA MAHESABU UTALIPAJE KWA MWEZI KWA MUDA GANI, LAKINI KATIKA MAHESABU HAYO WANAWEKA NA INTEREST/RIBA ZAO SO UKIMALIZA UNAWEZA UTAJIKUTA UMELIPA ZAIDI YA £155,000. UNAWEZA KULIPA HATA £165,000. HILO NDILO TATIZO LA MKOPO LAZIMA KUNA RIBA, LAKINI NI KWAMBA KWA VILE HUNA FUNGU LA KUNUNUA KWA MARA MOJA THEN UNA OPT MKOPO, NI HUKO NYUMBANI NA NCHI NYINGI ZA DUNIA YA TATU AMBAKO WATU WANANUNUA MAGARI CASH AT ONCE, WATU WANAJENGA NYUMBA ZAO KWA PESA YAO AT ONCE, HUKU WATU VITU VIKUBWA VYA AINA HIYO HUKOPA TU HATA WALE WENYE PESA HUKOPA PIA. PESA KAMA WANAZO HUFANYIA SHUGHULI ZINGINE ZA UZALISHAJI. NI WAO ZURI NA KAMA KUNA MTU WA MAGARI AFANYIE UTAFITI JUU YA SWALA HILI KWANI ATAFANYA BIASHARA SANA, PAMOJA NA KWAMBA DUNIA YA TATU NI RISK KUFANYA HIVYO LAKINI ANAWEZA KUFANYA RESEARCH NA KUBUNI NJIA YA KU-FEND HIYO RISK, RISK ANALYSIS YA KUTOSHA INAWEZA KUMPATIA NJIA YA KUZUWIA HATARI HIYO YA KUTORUDISHA PESA YAKE. KWA UJUMLA NI WAZO ZURI SANA NA LINAWEZEKANA, NJIA NYINGINE NI KWAMBA MABENI YANAWEZA KUBUNI KITU KAMA HICHO, MTU UNATAKA KUNUNUWA GARI UNA KAZI YAKO YA SHUGHULI YAKO BINAFSI YA KUAMINIKA INAYOKUPATIA KIPATA UNAENDE BENKI UNAOMBA MKOPO WA GARI MAOFISA WA BENKI WANAKUTADHIMINI ALAFU WANAKUAMBIA NENDA KATULETEE INVOCE YA GARI MNAKUBALIANA BENKI WANALIPA GARI CASH KWA MUUZAJI NA WANAANDIKIANA NAO MKOPO WAO KADI YA GARI INABAKI KWAO PENGINE NA DHAMANA NYINGINE HIVI KAMA HATI YA NYUMBA INAKAA BENKI HADI UNAMALIZA MKOPO UNARUDISHIWA.

    ReplyDelete
  6. DADA M AND KAKA D,I DO NOT THINK THE SORT OF ARRANGEMENT YOU REQUEST WOULD BE ACCEPTED BY ANYONE WITH FINANCIAL KNOWLEDGE AND WHO DEALS WITH FIXED ASSETS.

    THE FOLLOWING REASONS WOULD CLARIFY THE TREATMENT OF YOUR PROPOSAL AND TRY TO ASCERTAIN THE RELATIONSHIP YOU WILL HAVE WITH THE LENDER.

    IF YOU GET THE CAR AND USE IT,YOU WILL HAVE NOT BOUGHT IT YET SINCE THE SALE(IAS 18) OCCURS WHEN RISKS AND REWARD OF OWNERSHIP PASS,SELLER WILL NOT HAVE MANAGERIAL INVOLVEMENT AND THE SALE MUST HAVE RELIABLE MEASURE.

    THEREFORE,GETTING THE CAR THROUGH LENDING ARRANGEMENT(EITHER FROM BANK LOAN TO BUY A CAR OR CAR DEALERS WHO PROVIDE FINANCE) IS AN EXAMPLE OF FINANCE LEASE(IAS 17) WHERE THE LENDER STILL HAS RISKS AND REWARD OF OWNERSHIP OF THE ASSET(risk interms of your monthly non repayment,reward is interest you get charged for usage).IN FINANCE LEASE,SALE COMPLETES WHEN LEASE TERM LAPSES(matured)THE CAR BECOMES YOURS.

    YOU MIGHT HAVE NOT ENVISAGED THE IDEA AND MY NARRATION BEHIND YOUR CASE.WHAT I EXPLAIN,ARE FINANCIAL TECHNICAL STANDARDS FOR RECOGNITION,MEASUREMENT AND TREATMENT OF TRANSACTIONS ACCORDING TO INTERNATIONAL ACCOUNTING STANDARDS(IAS).

    IF NOT BORED,PLEASE READ FURTHER ON HOW ASSETS PROVIDED THROUGH FINANCE ARRANGEMENT ARE TREATED.(have you ever heard of magari ya mikopo?)YOUR CASE RELATES TO THEM AND IT IS SUBSTANCE THAT IS RECOGNISED OVER LEGAL FORM.THE LOAN TO BUY AN ASSSET.

    IF YOU WERE A COMPANY OR A TRADER AND MOST INDIVIDUALS DO HAVE THEIR OWN FINANCIAL STATEMENTS SUCH AS BALANCE SHEET(currently known as statement of financial position) AND INCOME STATEMENTS AND SOMETIMES CASH FLOW STATEMENT.SO,THROUGH FINANCE LEASE,

    LESEE(BUYER)(YOUR) BALANCE SHEET WILL SHOW AN ASSET VALUE(DR)(A Car) AND LIABILITY (CR)(amount outstanding) AND YOUR INCOME STATEMENT WIL SHOW FINANCE CHARGE(DR)(interest you paid) AND A YEAR DEPRECIATION EXPENCE (DR)!you need to know about this?.

    LESSOR(LENDER)BANK,A CAR DEALER WHO DEFINITELY MUST HAVE FINANCIAL STATEMENTS WILL SHOW AN INVESTMENT OR LOAN OR RECEIVABLE(DR) ON THEIR BALANCE SHEETS AND INTEREST RECEIVABLE(The charge you paid) ON THEIR INCOME STATEMENTS.

    I PITCHED THE ABOVE MORE IN FINANCIAL IMPLICATIONS OF THESE SORTS TRANSACTION UNFAMILIAR TO MANY TANZANIANS AND ON OUR EMBARKMENT ON EAST AFRICA COMMON MARKET,THERE WILL BE MULTITUDE OF SME'S SOME OF WHICH WILL HAVE FEATURES OF THESE BUSINESSES.MORTGAGE FINANCING HAS SIMILAR FEATURES OF FINANCE EXCEPT THAT IT IS LONG TERM AND HAS PRODUCT VARIETY.

    PLEASE NOTE,THE IAS 17 LEASES IS COMPLEX STANDARD SIMPLY IT PROVIDES FOR CREATIVE ACCOUNTING BY CLASSIFYING FINANCE LEASES AS OPERATING LEASE WHERE PROFIT COULD BE SMOOTHENED AND THEREBY SHOWING FAVOURABLE FINANCIAL POSITION.

    ANYWAY,I MIGHT HAVE OVER ELABORATED,I MEANT TO SHOW FINANCIAL TREATMENT OF YOUR CASE.

    Mdau(John)UK
    daskim@hotmail.com

    ReplyDelete
  7. Kwa kweli huyo ndio utaratibu wa manunuzi mengi huku ughaibuni, kuanzia magari, simu na kadhalika. Hata nyumba huwa wanapewa pesa na kununua baadae wanalipia kidogo kidogo kila mwezi kwa miaka kadhaa. Ila sasa kimsingi inavyokuwa sio kila mtu anaweza kupewa hiyo mikopo hadi waridhike kwamba kweli utaweza kulipa, istoshe kitu chechote unachokinunua kwa kulipia kidogo kidogo kinakuwa bei juu ukilinganisha na bei halisi ya kulipa mara moja.

    Huko nyumbani ni vigumu kuweza kumpata mtu atakae kubali kukupa gari ya milioni 9 ulipie miaka miwili, ukizingatia itakuwa ni hasara kubwa kwa muuzaji, ndio maana kama ulivyoeleza hapo juu wanahiari yaozee katika hizo yards kwa kutegemea kuna siku watauza kwa bei nzuri kulingana na mfumuko wa bei za bidhaa. Ndani ya miaka miwili bei za ununuzi zinabadilika sana nyumbani, gari ya milioni 9 baada ya mwaka tu itastahili kuuzwa hata milioni 10+.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  8. Huo ndio utaratibu wa ughaibuni, kutoa cash labda uwe fisadi.Hata mimi ninafikiria huo mpango

    wapo wadosi hapo mjini wanafanya hiyo biashara kwa wafanyakazi wa serikalini lkn hiyo riba yake mpk ukamilishe malipo umeshapata magari mawili ya aina hiyo na pikipiki.

    au nilisikia pia kunajamaa(jina limenitoka) wanafanya hiyo bznes walishawapa magari ze comedy kwa mtindo huo na unaweza ukabadili gari na kuchukua lingine hapo hapo

    ReplyDelete
  9. BABU CHUZI MSAADA KWA MDAU.HIZO NDIO DILI HUKU NCHI ZA WATU LAKINI UKIKOPA KWA MUUZAJI DIRECTLY UTAJIKUTA MWISHONI UNALIPA INTEREST ALMOST HALF OF BEI YA GARI,UKIKOPA BENKI INAKUWA NAFUU KIDOGO LAKINI WOTE GARI INABIDI IWE NA FULL COVERAGE INSURANCE.PILI MDAU KWANINI USISAVE HADI UFIKISHE HIZO 9M.

    ReplyDelete
  10. hiyo biashara hapa bongo hamana,labda kwa vitu vidogovidogo kama baiskel/pikipiki mabat ya kujenga,TV uende pale TUNAKOPESHA wakukopeshe na interest yao ni 100% na bado hawatakupa mpaka wakutathmin kipato chako kama kunauhakika wa kulipwa,kwa vitu vikubwa kama magar NO. Hiyo nafikir kwa sababu ya uaminifu hamna na kukosekana kwa uaminifu unatokana na njaa hakuna uhakika wa kipato.Hao wanaotaka kununua gar kwa kudunduliza ni kuwa kipato chao ni kidogo hawawez kununua gar kwa mkupuo mmoja ina maana akianza kukulipa mwez wa kwanza hiyo laki nne mwez ujao mtoto akiugua au mama au baba ujue hela yako hupat mpaka apone,utapigwa story mpaka utakoma ukiamua kwenda mahakaman hiyo kes itapelekwa hata miaka miwil mpaka utasahau gar,na ukishinda bado hulipwi kwa sabab ya muundo wa sheria zetu za madai ni mbofmbof.Mchosho tu huo.

    ReplyDelete
  11. Kaka na Dada D, nadhani msaada mkubwa kwenu ni ushauri mkusanye hizo hela hadi zitimie au mfikirie kununua gari ya bei rahisi. Mambo ya mikopo ni fitna, waswahili wanasema- kukopa harusi kulipa matanga. Mimi nimekuwa nikiishi huku ughaibuni kwa miaka minne sasa, hadi leo bado natumia simu pay as you go, kitu ambacho sio common kabisa huku na ni ghali. Hali kadhalika hata credit card yangu ni prepaid haina interest wala fee yeyote, Sisi waisilam haturuhusiwi kujihusisha na mikopo inayojumuisha interests kabisa kwa vile ina madhara.

    Nchi hizi, watu wanafika kujiua kwa madeni kama hayo, mtu hujikuna ajipatapo, kama humiliki kitu ni vizuri kustahamili hadi ukipata uwezo, bila hivyo utajikuta unapata matatizo. Sijui mupo katika hali gani kimaisha, mnaweza kuwa confident kuweza kulipa hizo laki 4 leo na kesho, ila kuna mambo mengi yanaweza kutokezea ndani ya miaka miwili. Mmoja wenu anaweza kukosa kazi au mkapatwa na dharura kama ya kimatibabu na kadhalika, hela yote ikahitajika huko.

    Kweli gari, ni kitu kizuri sana kwa kurahisisha usafiri, ila kama huna uwezo unapaswa kumeza mate na kufikiria njia nyengine za usafiri. Binafsi nikiwa nyumbani nimeanza kutembelea gari nikiwa na miaka 18, ni bahati sana kwa maisha ya kitanzania. Ila sasa nipo huku miaka 4 na sina gari wala mpango wa kununua karibuni na maisha yanakwenda.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  12. wazo lenu zuri,ila mkumbuke mkipata mtu wa kuwakubalia atawapa gari bovu,baadae muanze kusumbuana,haya!

    ReplyDelete
  13. Mithupu kama nilivyokwambia kwamba mimi huwa nakufa na mawazo ya wachangiajI,naona wengi wameona umuhimu wa swala hili na kujaribu kuelimisha kwa namna moja au nyingine. Kwanza nataka niwatoe wasiwasi hao ndugu kwamba tutafikia huko wanakotaka.Wengi wetu wametoa mifano ya hapa ugaibuni ni kweli kwamba benki zinatoa mikopo kwa wanaotaka kukopa magari,Nyumba na hata kama unataka kuanzisha umamantilie.
    Wenzetu hawa wanataka kukopeshwa na mwenye biashara hiyo ya magari siyo benki. Kutokana na risk ya mali yenye kuhamishika (moverble asset)kama magari,unakuta wauzaji wanaogopa hasara.Sasa mimi nafikiri serikali idhamini watu wake badala ya benki za kigeni kuwakopesha watu kununua majumba au magari.Pia kuwepo na bima kwa kila mwananchi anayekopa hela au gari kutoka kwa mfanyabiashara wa kigeni ili kama mambo hayakwenda vizuri,serikali iingilie kati.Wenzangu wa ugaibuni mlionunua nyumba si mmeona jinsi FHA LOANS zilivyo nafuu wakati wa kurefinance? maana serikali inaingilia kati mambo yakienda vibaya.Haya utaniambia serikali yetu ni maskini siyo kweli.Inaweza kuwapunguzia kodi wafanya biashara ambao wako tayari kuwakopesha watu wa kipato cha chini.Na ilijaribu kufanya hivyo kwa kuanzisha benki za wananchi kadhaa kama MuCoBa,DCB,MWANGA COMMUNITY BANK nk.bado haitoshi.Hata mimi wakati najenga nyumba ya kwetu huko,vifaa vya finishing nilikopa kwenye duka la vifaa vya ujenzi na ilikuwa rahisi kwangu kuliko kukusanya hela zote kwa mkupuo.Pia ndugu zangu watanzania huku kutumia cash kila mnapo nunua, kunafanya wajanja kuzichenge na kuhamishia kwenye mabenki ya uswizi na Canada hau hamjui hilo? Tumieni mikopo na hela zenu wekeni kwenye Banki za hapo weka kwenye savings.

    ReplyDelete
  14. Kiboko msheliNovember 24, 2009

    Mdau UK, hapa sio sehemu ya Ku-copy na Ku-paste mambo unayosoma vitabuni.Mara nyingine uwe unanyamaza, kama wewe unatafasiri hizo fixed assets zako vibaya basi ni wewe mwenyewe. Ni sawa na wote tusome gazeti hilo hilo au tuone mpira huo huo halafu waje wengine waanze kusema lile goli halikufungwa hivyo, wakati wote tumeona mpira na goli.
    Kama uko UK, basi ujue magari, nyumba nk hununuliwa kwa mtindo huo wa kulipa kidogo kidogo. Nia ni kuhakikisha kwamba unajenga credit history na kwamba wenye fedha ni Benki na serikali na sio wananchi. Nchi ambazo hawatumii mtindo huo kama China, India, Korea NK, watu wake hupenda kuwekeza fedha zao benki, hadi dhamani halisi ya manunuzi inapotimu na wanaenda kunuanua cash. Hawapendi rib za benki.
    Mdau aliyeandika kuhusu kulipa polepole ameuliza , kama una jibu toa kama huna basi. kama hata wakikosa watasubiri tu hadi kufikisha hiyo miaka miwili na watakuwa na gari lao, sio shida kwani kwa sasa naamini hawana la kwao.
    Ndau John kumbuka sio wewe tu ndo unayesoma , wengi wamesoma na wamenyamaza. Pili kajifunze kuandika vi-english vya kwako 95% na kucopy 5% na sio sasa unavyocopy na kupaste aslimia 98(98%).

    ReplyDelete
  15. Kama shida yako ni kigari ka sh9.6 nijulishe.

    Nitakukopesha unilipe baada ya miezi 24.

    Sitaki laki nne zako kila mwezi, sina muda wa kukimbiza laki nne kila mwezi.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  16. Benki ya Dunia kupitia shirika lake tanzu la IFC lilianzisha mradi ulioitwa Tanzania Leasing Project.Mradi huu ulikuwa na lengo la kutengeneza mazingira mazuri ya kisheria na kibiashara ili kuvutia wafanyabiashara kutoa huduma ya Financial Leasing na Operating leasing kwa wadau, especially SMEs. Financial Leasing ni biashara ambayo sehemu nyingi duniani inafanyika. Katika biashra hii kunakuwa na three parties, Lessor, yaani mkodisha vifaa- kwa mfano kampuni ya kuuza magari, Lessee, yaani wewe unayehitaji kifaa- gari, THEN Bank/Financial Institutions, inayotoa hela. Sehemu nyingi duniani, Lessors wanakuwa na Finacial Company ambayo inatoa finance e.g Toyota Finace kwa hapa USA. Lessee anachagua kifaa toka kwa Lessor-lets say Gari, Lessor anakuunganisha na Benki, Benki inalipa fedha kwa Lessor, then Lessee/Lessor wanaingia mkataba unaitwa Lease Agreement, then anachukua kifaa- gari, analipa Lease payments kwa muda mliokubaliana, ikiwa ni principal repayment na interest/financial charges. Kile kifaa kinakuwa ndio Collateral. Kumbuka moja ya vikwazo vikubwa kupata mikopo hapa Bongo ni kukosa Collateral (dhamana). Huo ndio uzuri wa Financial Leasing, kile kifaa kinakuwa ndio collateral. Ukishindwa kulipa, kile kifaa kinakuwa re-possesed na Lessor. Ni biashara kubwa, bahati mbaya TZ haijashamiri kwa sababu mazingira ya kisheria yalikuwa mabovu kutokana na kutokuwepo na sheria, World Bank/IFC kupitia mradi wake huo ilifanikiwa kupitisha sheria hiyo bungeni mwaka 2007. Cha kushangaza hadi leo bado hakujakuwa na mwamko sana. Tatizo lingine ni mitaji.Leasing ni capital intensive, Lessor anatakiwa awe na mtaji au credit line ya kutosha toka kwa mabenki makubwa, anunue vifaa, aviweke kwenye yard akingoje kuviuza on lease arrangement. Hilo ndilo tatizo kubwa kwa sasa nionavyo. SERO Lease ambayo ilifanya kazi bega kwa bega na huo radi wa IFC inafanya vizuri, kina mama wanakopa vifaa vingi tu vya biashara, frezers kwa wauza samaki, vyerehani, tractors, trucks etc etc. Nenda Sero Lease Mikocheni pale ukapata maelekezo

    ISIPOKUWA, HAO WATU WENYE YARD, WANGEWEZA KUKUBALIANA NA MABENKI,KWA SABABU HIVYO VIFAA/MAGARI YAPO YANANYESHEWA MVUA TU, SO BADALA YA KUNGOJEA CUSTOMER MMOJA KUPATA FEDHA ANUNUE GARI KWA CASH, WANGEZUNGUMZA NA MABENKI NA WAKUBALI KUFANYA LEASING. SHIDA KUBWA NI CREDIT RISK KWA NCHI YETU, BAHATI MBAYA WATZ WENGI HAWAJUA UMUHIMU WA KUWA NA CREDIT NZURI, WAKISHAKOPA HAWATAKI KULIPA TENA, WANAKUWA WAJANJA JANJA, HILO NDILO LINASUMBUA WAFANYABIASHARA. NA KWA KUWA WATANZANIA HAWANA VITAMBULISHO, AU HAWANA HATA PHYSICAL ADDRESS, AKIAMUA KUKUTOROKA KUMPATA NI SHIDA. USA WANA KITU KINAITWA SOCIAL SECURITY NUMBER, HIYO NUMBER NI KIBOKO,UKITAKA KUKOPA WANATAKA NAMBA YAKO, WAKIINGIZA TU KWENYE COMPUTER STSYEMS INAPULL OUT CREDIT REPORT YAKO, KAMA ULIWAHI KUKOPA HUKULIPA, KAMA ULISHAKWEPA KULIPA BILL YA UMEME NA JINA LAKO LIKAPELEKWA KWENYE COLLECTION ETC, KILA UCHAFU WOTE UNAONEKANA. NA HIYO CREDIT REPORT NDIYO INAKUWA BASIS YA KUAMUA KUPEWA MKOPO AU LA. TANZANIA HATA KITAMBULISHO CHA URAI HAKUNA, MTU WA KUTOKA NJE YA TANZANIA ANAWEZA KUJIFANYA MTZ NA AKAPEWA MKOPO,HILO NDILO TATIZO KUBWA LINALOFANYA MIKOPO INAKUWA SHIDA KUTOLEWA, AU IKITOLEWA INAKUWA NA RIBA KUBWA SANA SHAURI YA RISK

    ReplyDelete
  17. THATS CALLED FINANCING! LAKINI KWA BONGO BADO SANA.KWA NCHI ZILOZOENDELEA TUNANUNUA KARIBU KILA KITU KWA BANK FINANCING NI KWAMBA UNACHUKUA BIDHAA THEN UNALIPA KIDOGO DOGO KILA MWEZI BUT NOTE! LAZIMA ANAEKUKOPESHA AANGALIE CREDIT PROFILE REPORT YAKO KWANZA(HISTORIA YA UAMINIFU WA WEWE KUKOPA NA KULIPA)KAMA UNA CREDIT SCORE NZURI BASI UTAWEZA KUKOPESHWA JUST ANYTHING.LAKINI KUNA MAMBO MENGINE YA KUANGALIWA KAMA IDENTITY,PERMANENT ADRESS,SOCIAL SECURITY #(USA) NI LAZIMA UWE NA HIVYO VITU.SASA KWA BONGO NI NGUMU KIDOGO KWA SABABU ITS RISCKY DUE TO DIFFICULTIES OF ESTABLISHING SOMEONE IDENTITY,RISCK OF SOMEONE LOOSING A JOB,AND ITS NOT POSSIBLE TO DETERMINE SOMEONE CREDIBILY TO PAY(NO CREDIT REPORTS SCREENING AVAILABLE) KWA HIYO ITAKUWA NGUMU KUKOPESHANA. BONGO INASHANGAZA KWELI WATU WANAPATA WAPI PESA ZA KUNUNUA MAGARI,NYUMBA? NAFIKIRI NDO MAANA RUSHWA, WIZI,BEURACRACY WILL NEVER END IN AFRICA

    ReplyDelete
  18. kiboko msheli,you aren't forced to read my comments.whenever you see my name mdau(John)uk at the end of each comment,please,skip and move on,it is simple as that.or Write yours

    Mdau(John)UK

    ReplyDelete
  19. nendeni tunakopesha limited watawasaidia, bt mnatakiwa muwe na secured job

    ReplyDelete
  20. Dada M na Kaka D, hili ni wazo langu kwenu. Kama inawezekana, tafadhali nunua hilo gari kwa cash!! kama huna 9.6ml kwa sasa hivi (ni kwamba hauna uwezo nalo)
    *Ugaibuni magari mengi yanadumu hata miaka mitano bila na kuwa matatizo makubwa kwenye engine au transmission (ndio manake wanaweza kukopesha kwa kipindi kirefu)
    *Bongo na hali zetu hapo, mabarabara hiyo gari ikifa ndani ya mwaka mmoja, utaona uchungu sana kuendelea kulipa laki nne wakati gari limekufa!!! (ugaibuni kunakitu kinaitwa credit hivyo mkopaji hata kama limeharibika hana budi kulipa kwani anaogopa kuharibu credt yake)
    *Ushauri wa bure, kusanya hizo fedha mpaka utakapo weza kununua hilo gari kwa cash au nunua la bei ndogo lakini lipa cash... Pili, hebu jiulizeni hata ninyi wenyewe mtu angewapa hizo 9.6ml cash kweli sasa hivi, mngeenda kununulia hilo toy(gari always depreciate)? si ungejenga nyumba kwenu bwana, na kuanzisha miradi ywenye maana badala ya kukunua gari kwa ajili ya ufahari tuuu... barabra zenyewe hakuna foleni kibaoo..
    - kokoliko

    ReplyDelete
  21. 90% of Tanzania ni Blacklisted on ma eyez utamkopesha nani ? Mangi Au Mgosi unajipenda kweli wewe Nadhani Baada ya miaka elfu moja Bank zitaanza mfumo huo mdau makopeshoni

    ReplyDelete
  22. hapo ndo tatizo la wabongo linapokuja ni wagumu san kwenye maswala ya kukopa ni cash tu tena siku hizi wanabadili kwa dola hadi wanaboa anyway zunguka zunguka kwenye ma yard unaweza ukabahatika ila mkibahatika tu muwe na fundi wa ukweli msije mkabambikiwa mguu wa jini ikala kwenu kila la heri

    ReplyDelete
  23. Tusife moyo watz huenda wakawa wa kwanza watu ghafla tukaanza kudrive na kulipia taratibu. Nawatakia heri.

    ReplyDelete
  24. Hehe nina kigari changu cha kukopa mwezi ujao na maliza baada ya miaka minne kikiharibika kinatengenezwa Bure kuna kitu kinaitwa Motor plan huwa nalipia na pia insurance nalipia sasahivi nataka kuwapa wabongo wa madili wakiuze kama strap alafu naripoti kameibiwa nakula kengine kapyaaa habari ndo hio wabongo tunawakilisha ughaibuni mdau mkopaji

    ReplyDelete
  25. MDAU JOHN UK KWANINI UNAPENDA KUJIDHALILISHA? TATIZO SIO KU-COPY PASTE, TATIZO NI KUWA ULICHOANDIKA NI UPUUZI MTUPU. KAMA NI MTIHANI UTAPATA 2/10! KAMA UNGE COPY/PASTE INGEKUWA AFADHALI MAANA INGEKUWA NA MUELEKEO, LAKINI ULIVYOANDIKA NI KAMA MTOTO WA MIAKA MIWILI ANAYEJIFUNZA KUONGEA! YAANI HAILETI MAANA WALA HAINA MPANGILIO WOWOTE.

    ReplyDelete
  26. mdau mkopaji umeniacha hoi aluu

    ReplyDelete
  27. Huu utaritibu wa mambo ya kukopa kopa ndio umesababisha credit crunch kuanza huko US last year. Kwanini mtu usiishi sawa na uwezo wako??
    Mna habari kuwa hapa Ulaya watu wengi wanataifishwa nyumba na mali zao sababu ya madeni?? Watu wanapata stress/depression sana sababu ya kushindwa kulipia vitu wanavyonunua kuzidi uwezo wao wa pesa wengine hadi wanajiua?? Msione mambo rahisi.. ni magumu sana ndio maana wazungu wengi wanaugua ukichaa. Tuishi kutokana na uwezo wetu, kama huna cash ya kujenga nyumba mkupuo jenga taratibu, iwapo huna cash kununua gari hiyo maintanance utaiweza vipi?? Jamani tuacheni hizi tabia za ukiga sijui majuu wanakopesha nasi tukopeshwe magari, etc. hazina faida kwetu.

    Mdau mbeba box
    UK

    ReplyDelete
  28. Kwa hiyo mbeba box UK unataka kusema kila anayekopa ametaka kuishi zaidi ya uwezo wake? Fikiri kabla hujasema. Kinachosumbua watu ni kupata kitu kwa mkupuo yaani upate ela yote ya gari, kumeinteni gari ni vijiela vidogo wengi wanaweza. Mtu alite tayari kutoa laki nne kwa mwezi hashindwi kuhudumia kagari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...