Babu Seya (mwenye bazee kulia) akiwa na wanawe kizimbani leo Mahakama ya Rufaa jijini Dar
Askari magereza akiwatia pingu Babu Seya na mwanae Papii Kocha Mtoto wa Mfalme tayari kurudishwa gerezani leo baada ya rufani yao kuahirishwa

Rufaa ya mwanamuziki maarufu, Nguza Viking (pichani kulia) maarufu kwa jina la Babu Seya na wanawe watatu, imehairishwa hadi Desemba 3 mwaka huu, ili upande wa Jamhuri uweze kupitia nyaraka mbalimbali zilizowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi.
Katika rufani hiyo pia wamo watoto wake ambao ni Papii Nguza, Nguza Mbangu na Francis Nguza ambao wanapinga hukumu waliyohukumiwa kutumikia jela maisha iliyotolewa mwaka 2004 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.
Rufani hiyo iliahirishwa jana mbele ya jopo la majaji watatu lililokuwa likiongozwa na Nathalia Kimaro pamoja na wenzake ambao ni jaji Mbarouk Salim Mbarouk na Salum Massati.

Awali upande wa utetezi uliokuwa ukiongozwa na wakili wa kujitegemea Mabere Malando aliiomba Mahakama hiyo ya Rufaa kupokea maombi yake yakurekebisha maombi ya rufani iliyowasilishwa Mahakamani hapo na iweze kusomeka kesi namba 56/2005 ya makosa ya jinai badala ya kesi namba 56/2009.

Mbali na ombi hilo pia aliiomba Mahakama kuongeza sababu nne za kufungua rufani hiyo na hivyo kuwa na sababu 19, alidai kuwa ameamua kuongeza sababu hizo kutokana na kuona baadhi ya vitu vilisahaurika katika rufaa iliyowasilishwa awali na wakili Nyange.

“Licha ya kuongeza hizi nne baadhi ya sababu nitaziacha wakati tukiendelea kusikiliza rufaa hii,” alidai Marando.

Upande wa Jamuhuri uliokuwa ukiongozwa na Justuce Mlokozi, ulikubaliana na maombi hayo na kudai kuwa maombi hayo waliyapokea wiki iliyopita.

Mlokozi alidai kuwa baadhi ya vielelezo vya ushahidi vilichelewesha kufikishwa katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) ambapo alidai nyaraka hizo alizipata Novemba 27 wakati muda wa kazi ukiwa umeisha.
Alidai kuw akutokana na hali hiyo hajaweza kuzipitia kwa haraka kutokana na kuwa nyingi ambapo alidai kuwa nyaraka hizo ni zaidi ya 20 ambako alidai kuwa atakuwa akisoma taratibu.

Pia alidai kuwa kabla ya kesi hiyo kuanza jana Mahakamani hapo Malando alimpatia nyaraka nyingine ambazo bado hajajua zinasema nini ambapo alidai kuwa kutokana na uwingi huo aliiomba Mahakama kuhairisha shauri hilo ili kuweza kupata muda wa kusoma.

Mbali na hayo Mlokozi alidai kutoelewa sababu ya 14 na 15 ambapo alidai kuwa sababu ya 14 inashambulia Mahakama ya Mkoa kwakutoweka kumbukumbu vizuri wakati sababu namba 15 nayo pia inashambulia Mahakama Kuu kwa kutokuweza kumbukumbu vizuri.

Wakili huyo wa Jamuhuri alidai kuwa kutokana na sababu hizo aliutaka upande wa utetezi kuelezea kwa kina sababu hizo kutokana na kutokuwa wazi na pia aliiomba Mahakama kuruhusu upande wa utetezi kuleta mashahidi ambao wataweza kuthibitisha madai yao yaliyotolewa katika sababu ya 14 na 15.

Kwa upande wake Marando aliiomba Mahakama kuongeza muda ili kuweza kupata muda wa kuweza kusoma nyaraka hizo ambapo alipoulizwa na Jaji Mbarouk kama kunamawakili waliojitoa katika kesi hiyo alidai kuwa hakuna aliyejitoa zaidi ya idadi ya mawakili kuongezeka.

Akitoa amri ya Mahakama kwa niaaba ya Majaji wenzake, Mbarouk alisema kuwa Mahakama imekubaliana na maombi ya upande wa utetezi ikiwa ni pamoja na kuongeza sababu nne katika rufaa hiyo.

Pia alisema kuhusu maombi ya Jamuhuri ya kutaka kuongezewa muda ili kuweza kupitia nyaraka zilizotolewa na upande wa utetezi alisema Mahakama imekubaliana na ombi hilo kwakuwa ni haki yake ili rufaa hiyo iweze kuendeshwa kwa haki.

Mbarouk alihairisha rufaa hiyo hadi Disemba 3 mwaka huu ili pande hizo mbili ziweze kupitia nyaraka za rufaa hiyo.

Babu seya na watoto wake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2004, baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa Jamuhuri dhidi ya kesi ya kudhalilisha kijinsia watoto wa kike.

Kesi hiyo iliyovuma kwa wakati huo ambayo ilikuwa ikisikilizwa na kutolewa hukumu na Hakimu Mkazi Addy Lyamuya ambaye amestaafu hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Igwe igwe lelele leee ah...ah, igwe le le leee. Masikini namkumbuka sana Papi kocha katika ile raping yake pale ndani ya FM academia!

    Kwa kifupi huyu mshikaji ana kipaji lakini ndio hivyo tunai - miss ile mikogo yake.

    Munu awasaidie washinde rufani yao

    Mdau

    Nachingwea

    ReplyDelete
  2. Kikwete mafisadi wako wapi?

    ReplyDelete
  3. Fanta wangu (papalampapapa...) uliamua, kuniacha pekeyangu fanta kwa ajili ya pesa aah, mwenye pesa kanipoooraa naweee eh...
    duh naukumbuka huu mwimbo wa papii kocha, namuangalia hapa sura yake, naona machozi yananitoka.
    eeeh mungu uliye juu wewe ni muweza wa yote, baba naomba uwasaidie hawa watoto watoke, kosa lao ni lipi baba??
    humu duniani sote tunapita tu, baba na siku ya mwisho wengi wetu watakuwa na maswali mengi magumu ya kujibu. tuwaonee huruma watoto hawa. ee bwana ukatende miujiza yako ukawasaidie watoto hawa wawe huru, tazama baba mmoja wao huyu mdogo anaumwa sana huko gerezani. ahsante baba, naamini katika jina la yesu na mtume muhamad s.w tarehe 3 dec matokeo yatakuwa mazuri. amina.
    kihancha, sweden.

    ReplyDelete
  4. Huyu Baba mwalimu mzuri sana kule Gerezani anafundisha Kifaransa.

    ReplyDelete
  5. Kwa wale mnaoamini kwamba hii kesi hawa jamaa walibambikiwa, Hivi inawezekanavipi watoto, polisi, walimu, madaktari, wazazi,na wote walioathirika na kutoa ushahidi kwenye kesi hii wawe walinunuliwa? Kwa sababu za kishirikina inawezekana kabisa babu Seya na wanae walifanya hiki kitu kwa ushirikiano! Kwa sababu za kawaida za kibinadamu haiwezekani.

    ReplyDelete
  6. Kutokana na juhudi zinazofanywa na hawa jamaa kujaribu kupata haki yao mahakamani kuna ushawishi fulani hivi unaonyesha labda walibambikiziwa hii kesi. Mara nyingi watu waliofanya makoso hawa hawaangaiki kukata rufaa kwa sababu hata mioyo yao tu huwa inawashitaki.

    Mahakama kazi yake ni kusikiliza ushadi unaoletwa kwake na kufanya maamuzi kutokana na sheria inavyoelekeza.

    Lakini kama hawa jamaa wana hatia au la, wanajua wenyewe na Mungu wao.

    ReplyDelete
  7. watu wanaua watu kwa kukusudia hawafungwi maisha, wengine wanawanyanyasa kijinsia hata watoto wao nao hawafungwi maisha, mmh hapo inaonekana hukumu yao ina matashi ya kisiasa!.. kweli duniani hakuna haki!

    ReplyDelete
  8. Tanzania kweli kwa mtu mdogo wanamfinya kabisaa,sasa huyu mzee na watoto wake,siwangepewa hata miaka 30?Yani kufungwa maisha yao yoote !!mimi sikubaliani na hicho kifungu cha hii sheria kabisaa,,kwasababu hata wauwaji wapo hapo na hawajaenda kufia jela,,sio kesi kama hio yakawaida tu mbona huku ulaya yanatokea lakini sio mpaka watu wafie jela..No hiyo shelia sio nzuli kwa nchi maskini kama tanzania.Kesi ya huyu mzee huwa kila nikiikumbuka naumia sana.Michuzi utupe habali za huyu kaka nakuomba jinsi zitakavyoenderea.

    ReplyDelete
  9. Na vipi wale ndugu ambao watoto wao waliathirika na hawa wauwaji????kwa nini watu wapumbavu sana mnaangalia upande mmoja tu wa shillingi???KAMA HILI KOSA WALILIFANYA KWELI, NI HAKI YAO KUKAA HUKO MILELE EBOOO....Sheria lazima ifuate mkondo wake.

    ReplyDelete
  10. moyo ungekuwa na mfupa mabaki ningeyapata lakini moyo umeumbwa na nyama, nyimbo hii inanikumbusha mbali sana jamani dah siamini kama kweli papii nae muona hapa ndio yeye jamani mahakama fanyeni haki kwa binaadam hawa mnawaonea.anzeni adhabu kama hizi kwa mafisadi ndio mje kwa wanyongeeeee jamani inaniuma sanaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  11. moyo ungekuwa na mfupa mabaki ningeyapata lakini moyo umeumbwa na nyama, nyimbo hii inanikumbusha mbali sana jamani dah siamini kama kweli papii nae muona hapa ndio yeye jamani mahakama fanyeni haki kwa binaadam hawa mnawaonea.anzeni adhabu kama hizi kwa mafisadi ndio mje kwa wanyongeeeee jamani inaniuma sanaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  12. hawa jamaa nasikia walikua si wabakaji ila kuna wanawake wa vigogo ndio walikua wakienda nao sambamba na ndio maana wakabambikwa,kisheria haiwezekani hata siku moja watu 4 kupatikana na same hatia,na wote wakafungwa maisha,Hata mungu hakuumba sawa ila na hawa hata kama walitenda hilo basi mahakama ingepitia uzuri kesi na tungeona tu kuwa baadhi yao wamekula miaka kidogolabda kwa kusaidia,na huyo alosema walimu polisi na watoto wamenunuliwa,naona bado ni mpumbavu kwa sababu wagombea tu hununua jimbo zima la wapiga kura je hao vigogo wa serikali kununua watu chini ya 10 unafikiri ni tabu?ANZANIA MTU ANAKUOMBA 200 TU JE UKIMPATIA ELFU 10 SI YUPO TAYARI KSEMA UONGO?NA MBONAHUKUMU YA HAWA WATU IMEKWENDA CHAP CHAP NYENGINE ZINACHUKUA MUDA?HAPA UONEVU MTUPUU

    ReplyDelete
  13. Wewe Anon wa kwanza, toka lini kunajisi watoto ni kosa la kawaida? Una watoto weye? vipi wangekuw wanao? au wadogo zako?

    Hebu angalieni pande zote za shilingi, sio kushabikia tu Muziki. Vitendo kama hivyo vimekithiri katika jamii yetu na hii ni njia mojawapo ya kuvikomesha. Ushahidi umetolewa, wameonekana wana makosa, sheria imechukua mkondo wake!!

    ReplyDelete
  14. sishabikii uhalifu na hasa udhalilishaji wowote wa watoto au wanawake lakini naona hii kesi ina walakini!! hivi familia nzima ilionekana ina hatia kwa vigezo vipi?? kulikuwa na DNA evidence iliyoonyesha familia nzima kufanya huo mchezo mchafu?? kama hakukuwa na DNA evidence,hao madaktari walithibitishaje kuwa ni familia ya Nguza wamefanya huo uhalifu?? kaka Michu tupatie update hiyo Dec 3...

    ReplyDelete
  15. hata kama wamefanya kweli lakini adhabu waliopewa kubwa sana wewe anon kwanza huyo mmoja alikuwa mwanafunzi akiwa na mika 17 sasa kwann akawekwe na watu wazima? kama kweli walifanyiwa haki hapo kuna walakini vyombo vya kutetea haki za binadamu mmelala fofooo angalieni hili swala kwa kina jamani wameonewa inshaallah m/mungu atawasaidia mtatoka tu kwake hakuna linaloshindikana amin

    ReplyDelete
  16. Kama kweli walifanya basi wajibu mapigo lakini kama hawakufanya mungu amgeuzie kibao aliyowaweka ndani.Ni case ngumu kuamini lakini

    ReplyDelete
  17. we anoy wa 10:56 pm nov 30,inaonekana hujaifuatilia hii kesi na wala hujui sheria hata kidogo na ndo maana ushabiki umekupumbaza mpaka unamuita mwenzio mpumbavu.Laiti ungekuwa na access na mambo ya maahakama,na ungefuatilia kuanzia mwanzo muenendo wa kesi hii,mpaka wale watoto wote(tena wadogo)walivyokuwa wanatoa ushahidi,askari,daktari,mpaka wazazi wao.na watuhumiwa walivyokuwa wakijitetea.WEWE KAMA MTANZANIA USINGETOA COMMENT YA KISHABIKI HIVYO

    ReplyDelete
  18. IN ORDER FOR AN ACCUSED TO BE CONVICTED THERE SHOULD BE AN EVIDENCE THAT PROVES BEYOND A REASONABLE DOUBT THAT THE ACCUSED COMMITED THE CRIME,SO IN THIS CASE WHERE THESE PEOPLE WERE ACCUSED OF RAP THERE SHOULD BE EVIDENCE THAT SEAMENS OF THESE SAID PERSONS WERE FOUND IN THE GIRLS BIOLOGICAL STRUCTURES BY EVIDENCE OF A DNA TESTING,THATS ONLY THE REASON THESE PEOPLE WOULD GET JAIL TIME BUT IF THIS WAS NOT THE CASE THEN THIS CASE IS VERY EASY TO WIN AND GET THEM FREED.ONLY THE EVIDENCE THAT THE GILS HAD A TESTING RESULT OF BEING PENETRATED WOULD NOT PROVE BEYOND REASONABLE DOUBT THAT NGUZA AND SONS WERE RESPONSIBLE FOR THAT COZ THEY MIGHT HAVE GOT PENETRATIONS FROM SOMEONE ELSE.SO BOTTOM LINE IS IF THERE'S NO EVIDENCE OF DNA THEN THESE PEOPLE ARE NOT GUILT AND SHOULD BE FREED NO MATTER WHETHER THEY COMMITTED THE CRIME OR NOT.THERE SHOULD BE STRONG EVIDENCE AGAINST THEM,PERIOD,COZ A LIFE SENTENSE IS TOO BIG FOR SOMETHING WITHOUT DNA EVIDENCE

    ReplyDelete
  19. Binafsi nililidhishwa na ushaidi wa watoto wadogo sana waliojieleza kuwa "walituambia tunyonye madudu yao halafu tumeze maziwa"

    Kama una mtoto hawa jamaa wanastahili kunyongwa.

    Lile kundi la watoto ni wadogo sana kufundishwa maneno mazito kama hayo na kuyatoa ushahidi mahakamani.

    Watanzania tuwe serious na tuache kuamini kila kitu ni majungu. Tunahitaji kusisitiza utawala wa sheria ili hata wale walimu wanaowalamba watoto wetu ktk umri mdogo mashuleni nao wawekwe ndani. Na mabosi wanaolala na wake zetu pia wachukuliwe hatua kali.

    Kumbukeni Tanzania inanuka kutokana na uozo wa wajinga na kukosa utawala wa kisheria.

    ReplyDelete
  20. Tuacheni ushabiki hasa kutokana na uzembe na ku-implicate kila kitu na majungu. Ushahidi waliotoa wale watoto ni wa kutosha sana

    Inatisha. Na walifanya hivyo kutokana na uzembe wa sheria za nchi yetu na kwa umaarufu wao na vijipesa.

    Pamoja na kifungo cha maisha waongeze tena miaka baada ya rufaa

    Na kama walisingiziwa then poleni
    Ila ushahidi ulitosha.
    Hakuna kigogo sijui wala nini
    Ushabiki utatumaliza

    ReplyDelete
  21. Bwana Yesu...
    aya tunasubiri

    ReplyDelete
  22. Itakuwa walifanya kweli na ushahidi upo. nakubaliana na waliosema kwamba walikuwa wanapiga picha wakati wanafanya ufedhuli huo na kwenda kuziosha ng'ambo ndipo mbongo mmoja akazirudisha kwa kaizari. hakuna hakimu aliyesoma atakayehukumu kipuuzi ili ahatarishe kazi yake. vinginevyo basi, kuomba rehema za mungu zitendeke kwao ili watoke au wapunguziwe adhabu.

    ReplyDelete
  23. The absence of the evidence is not the evidence of the absence...there are unknowns unknows that we all don't know!

    ReplyDelete
  24. Mimi watanzania wengine nawashangaa sana! hivi wewe anonymous wa dec01,12:01:00 mimi sikuelewi unaposema eti ni ushabiki,,hivi wewe ukitumia akili yako unaweza kumwambia nani kwamba familia yababa na watoto watatu eti walihusika kwahili tendo?mimi ni mzazi tena najua uchungu wa mtoto ,lakini hii kesi sijakubali kama ndani yake kuna ukweli,,halafu kitu kingine jua kwamba uhalifu kama huu sio wakufia jela familia nzima hivo, kipindi kuna wahalifu wameshindikana hata kufikishwa mahakamani,,huyu anonymous naye wa dec 01,09:08:12:00 unataka kujifanya mjuaji saana wa mambo ya mahakama kipindi hujui,,,hivi wewe unavyofikilia hii kesi ulifuatilia peke yako ee?Hapa hakuna cha ushabiki wala nini ila tu ni mambo ya kiongozi kufinya mtu mdogo,,,je mbona kesi ya Zombe imeisha na ikaonekana kwamba ameshinda serekali?ni jambo gumu sana kuhusiana na hii kesi eti familia yoote ifie jela,,kipindi wanaochinja watu wanaachiwa kiholela.Watanzania jamani tukubali sheria nyingi za nchi yetu zinamfinya mtu mdogomdogo tuuu.Samahani mithupu usiniweke kolokoloni.

    ReplyDelete
  25. watoto kufundishwa uongo inawezekana sana tena vinajuaga na kukremu na kulia juu uspime kabisa hamuonagi maigizo sio enhhe?? na baloon boy je?? acheni tu hii ishu wanajua wakulukulu wa nnji

    ReplyDelete
  26. HAPA DAWA NI ALIBADILI TU KUKATA MZIZI WA FITNA ISOMWEEEEE??????

    ReplyDelete
  27. Mapenzi au ushabiki kwa mtu au kitu fulani kuna wakati ushangaza sana. ushabiki huu unawez\a kupofusha watu wasione ukweli an hata wakiuona wanaweza wakajikuta wasiukubali ukweli wenyewe. Hivyo pengine mapenzi au ushabiki wetu kwa muziki wa Nguza na mwanae Papii Kocha umeweza kutupofusha na hivyo kutokuwa tayari kuamini kwamba walitenda makosa hayo pamoja na kwamba ushahidi uliotolewa mahakani ulitosheleza kuwatia hatiani Nguza na wanae.

    Mimi naukubali sana muziki wa Nguza na Papii. Kiasi kwamba ningekuwa hakimu kwa huruma ya kibinadamu pengine ningepata huruma japo kidogo na kuwapa adhabu ya miaka inayohesabika (jela miaka 20, 25 au 20) kuliko kuwafunga maisha baba na watoto wake wote watatu.

    Suala la hii familia kwa kiasi kikubwa limetawaliwa na minong'ono inayodai kwamba Nguza alikuwa akimchukua bibi wa mkubwa fulani na kwamba mkubwa huyo ndiye aliyetumia wadhifa wake hadi nguza na hao wanae wote wakafungwa maisha!

    Sitaki kuamini hili kwani kwa jinsi ilivyo si rahisi idadi yote hiyo ya watoto isingeweza kutoa ushahidi imara mbele ya mahakama na wakati huo Nguza akitetewa na Wakili maarufu vile ambae angewayumbisha na maswali na kama watoto walikuwa wamefundishwa kusema uwongo lazima tu ingekuja kudhihirika mahakamani.

    UKISTAAJABU YA MUSA UTAONA YA FIRAUNI....

    Kuna watu wengi sana kwa sababu mbalimbali wamejikuta wakifanya mambo ya ajabu na jamii kutoamini kama kweli yametokea huku ukweli ukibaki kwamba yametokea. Tena katika nchi zetu hizi ambazo sehemu kubwa ya jamii inaamini ushirikina ndiyo usiseme.
    Mfano;
    1. Mwanzoni mwa miaka ya 2000Ilipata kulipotiwa kuhusu watu waliojifanya waganga waliokuwa wanawatapeli watu mamilioni ya mapesa na kisha kwenda kuwakata mishipa ya shingoni kwa vifaa vya ncha kali na kuwaulia mbali kando ya bahari hapa hapa Bongo.Waliwaua wengi na wakawa wanawafukia huko huko kando ya bahari.

    2. Kibaha miaka michache iliyopita kuna mganga aliyekuwa kachimba shimo ndani ya nyumba yake akawa anawatapeli watu mapesa. akishawadhurumu baadae anawaulia mbali na kuwatumbukiza kwenye shimo na aliuwa zaidi ya watu kumi.pia kuna mwingine alikuwa anawaua watu na kuwabanika ili kupata mafuta ya binadamu na akakutwa na ndoo za mafuta hayo kama samli.

    Mauaji ya albino n.k

    Hayo hapo juu ni makubwa zaidi hata ya waliyoyafanya Nguza na wanae na kwa maana nyingine kama Nguza alikuwa ni muumini wa ushirikina ilikuwa rahisi tu kwake kufanya hayo yaliyomtia hatinani.n Hivyo tusishangae kwamba si rahisi kwa mtu kama Nguza na wanae kufanya mambo ya kulawiti watoto na kuwabaka.

    Yote hayo yanatokana na imani za kishirikina. Mtenda anajua jamii aliyomo inaamini ushirikina na mtendewa ni sehemu ya jamii inayoamini ushirikina.

    Sasa linapokuja suala la Nguza na wanae inamaminika kuwa yeye na wanae walikuwa wakilawiti watoto ili nyota yao ya muziki izidi kung'aa ili kusaka pesa zaidi kupitia muziki wao.

    Kama walitenda makosa hayo ni vema sheria ikachukua mkondo wake na jamii isikimbilie tu kuamini maneno ya mitani kuwa ooh wameonewa. Basi wale wanaodai Nguza kaonewa na wanaewajitokeze wakathibitishe mahakani kuwa jamaa wameonewa. Watu wlisema kipindi kile wanafungwa na sasa kwa vile kesi imerudi tena mahakani wajitokeze basi mahakamani wakathibitishe uonevu uliofanyika ili ndugu yetu aachiwe nasi tupate nafasi nyingine tena ya kupata na kusikiliza miziki yake mipya.Tusipende sana story za vijiweni jamani!

    ReplyDelete
  28. Anony Tue Dec 01, 03:54:00 PM kufundisha kundi la watoto wakatoa ushahidi mahakamani-that is never possible
    Culture ya watanzania wako shy kwa public na watoto ni waoga sana
    na flow ya maelezo yao hata FBI wangewafundisha wasingeweza
    Come on nw lets be more serious than arguing with impossible assumptions

    ReplyDelete
  29. NAOMBA NILULIZE SWALI.......KATIKA HII KESI KULIKUWA NA MWALIMU AMBAE INASEMEKANA NDIE ALIEKUWA ANAWAPELEKEA KINA BABU SEA WALE WATOTO ILI AWALAWITI SASA CHA AJABU NI KWANINI YULE MWALIMU YEYE ALIACHIWA HURU,NAOMBA USHAURI WAKUU

    ReplyDelete
  30. KESI INAWALAKINI, KESI YA KULAWITI/RAPE/NGONO INATAKA USHAHIDI WA KISAYANSI SI WA KUSEMA KWA MDOMO, KWANI KAMA KA MDOMO HATA MIMI NAWEZA KUSEMA BABA FULANI KANI-RAPE AKAFUNGWA, KINACHOTAKIWA KAMA KANI-RAPE NIPIMWE NDANI YA UCHI WANGU NA SEAMEN ZIPIMWE ZIWE ZAKE INAWEZEKANA NIME-RAPIWA NA MTU MWINGI JE, KUPIMA UKE NA KUONA DALILI ZA MIKWARUZO HIYO SI SAHIHI INAWEZA KUWA MIKWARUZO YA NDIZI MTOTO MWENYE ALIKUWA NAPIGA MASTERBASHENI JE. KESI INAWALAKINI MKUBWA HATA KAMA WALIFANYA,

    ReplyDelete
  31. sisi wote tuliumbwa na Mungu, mimi hainiingii akilini kabisa kuwa hawa watu woteee wamebaka,mimi nafikiri kila aliyeguswa na jambo hili afanye maombi juu yao kesi yao ili Mungu awanusuru na kifungo hiki, kama paulo na sila walivyoomba coz ninachaamini kwa maombi ya wengi wataachiliwa. otherwise inauma kuona kizazi chote cha huyu mzee kinafia gerezani. Pole mzee nguza na familia yako.

    ReplyDelete
  32. Kwenye vitabu vya Mungu imeandikwa "Ni haki kwa Mungu kuwatesa wale watutesao" hivyo basi kama kuna mkono wa mtu unawaangamiza Babu Seya na wanawe basi na asifikiri yeye ni mjanja na mshindi asubiri na fimbo ya Mungu. Mwenyezi Mungu hata acha mwenye haki ateseke milele, tumwachie Mungu wadau.

    ReplyDelete
  33. kwakweli hata mimi nawaombea kwa Mungu. Kuombea walio katika matatizo ni thawabu kwa Mungu...Mungu mwenye enzi atawasamehe kama mioyo yao ina majuto (kama ni kweli they did the deed)MUNGU WA REHEMA WEWE ULIYE MUNGU MWINGI WA REHEMA NA HAKI, TUNAKUSIHI BABA UWAHURUMIE HAWA WATU NA UWAWEKE HURU KWA JINA LA YESU. AMEN. mimi eva

    ReplyDelete
  34. naungana na anon 10:51 kweli inasemekana mwalimu wao mkuu ndo aliyekuwa anawachukua watoto na kuwapeleka kwa nguza mbona mwalimu hakushitakiwa kwa sababu kama ingekuwa ni kweli basi huyo mwalimu angeshitakiwa kwa conspirance mbona hakushitakiwa
    tufikirie vizuri wadanganyika wenzangu
    vilevile kwa mtoto kufundishwa kitu inawezekana tena sana hata mwanao mwenyewe anaweza kukufunga akifundishwa chochote especially na mama yake against u,hata kama wewe ni baba yake ataongea vizuri sana, mi imeshashuhudia mtoto wa miaka5 anafundishwa maneno na mama yake ya kumwambia baba yake na anasema kama alivyofundishwa bila kuacha neno hata moja na ,sembuse wale watoto watashindwa nini
    tuwaombee tu hawa jamaa hii kesi si yao

    ReplyDelete
  35. hii kesi sio bule,maumba akufungwa maisha;

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...