Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Dk. John Malecela, akimtunuku Shahada ya Kwanza ya Sheria, mfungwa katika Gereza la Ukonga, Ernest Michael, wakati wa mahafali ya 21 ya chuo hicho, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza huko Ukonga jijini Dar leo. Wengine pichani ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha na Kamishna Mkuu wa Magereza Afande Nanyaro.

Bw. Semayoga Ernest anakuwa mfungwa wa pili kutoka gereza la ukonga kula nondozza, baada ya baada ya mfungwa wa kwanza Haruna Mgombela aliyekula nondozz za chuo hicho mwaka 2007.
Hizi ni juhudi za pamoja kati ya jeshi la magereza kupitia Wizara ya mambo ya ndani pamoja na wadau mbalimabli nchini katika kuwasaida wafungwa kubadili tabia wakiwa gerezani na kuhakikisha kuwa wanatoka wakiwa wema na wenye manufaa na walio tayari kujenga tiafa katika jamii zao.

Jeshi la Magereza kupitia Wizara ya Mambo ya ndani pamoja na chuo kikuu huria cha Tanzania vina mpango wa kujenga maktaba ndogo katika gereza la Ukonga pia kupita katika magerza yote nchini na kuwahamasisha wafungwa pamoja na askari magereza wajiunge na chuo hicho ikiwa ni katika kuwatoa katika dimbwi la upungufu wa elimu na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya serikali inayosema 'maisha bora kwa kila mtanzania'.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. MFANO WA KUIGWA

    ReplyDelete
  2. This guy used to be my mentor at Kigoma Secondary School in the early 90's. He then went to Azania high school and completed his high school studies.Thereafter, i do not know what happened to him, but this guy will continue to be my mentor for what he did today. Peace be upon you Ernest and may the Almighty God pour his blessings so that you can keep be the inspirational to many. Mdau-from Texas.

    ReplyDelete
  3. That is wrong from my opinion and as well as from African poor countries perspective if their studies are being funded by the public purse, it is an incentive to otthers to do wrong things as they could know that once they are in the dock they can go to school free of charge and come out with degree that otherwise they could not pay/afford by themselves when they are just good citizens. It just sends wrong signal to the public, it is politics and democracy at its best. We have so many young good people who are not able to go to school simply because of money issue/they can not afford to pay, and yet instead of helping them the government helps criminals, why not support these good young people. Discuss.

    ReplyDelete
  4. Huyu kama mimi, anapiga kitabu wakati yuko jela.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  5. tx bwana utawajua tu.sentensi ya kiswahili alafu inabadilishwa.hongera sana

    ReplyDelete
  6. Uyu mdau wa pili wa 4:07:000 kaandika nini au mimi sijui kzungu,
    Naomba nifaj]hamishwe,maana mimi ninavyojua chuo kikuu huria unasoma hata ukiwa iringa,tena bure au kwa mchango kidogo tu

    ReplyDelete
  7. Mpango mzima wa kuwasomesha wafungwa ni mzuri,kwani unasaidia kuondoa ile dhana potofu kwa wafungwa,kwamba ukiwa jela unakuwa umeshaharibu mipango yako ya maisha baada ya kutoka jela, na wengi wao hukata tamaa,hence wanazongwa na mawazo ambayo huwafanya wakonde sana japo wanakula,na wengine wanakufa,ukiondoa kusoma chuo huria,wanafundisha vitu vingi mfano-uwashi,carpentry,gardening,nursing,driving etc
    My point -je nafasi hizi zinatolewa kwa wafungwa wote wanaopenda kujiendeleza kielimu,jaribu kufanya utafiti,ndugu zake wa mfungwa wapo vipi ki-uchumi au vyeo serikalini,utakuta anatoka katika familia ya kitajili au kifisadi,may be alifungwa coz case ilikuwa na mazingira magumu wakashindwa kumtoa au ndugu zake wame-win jamaa akiwa gerezani,there IS NO FAIR DISTRIBUTION OF EDUCATION OPPORTUNITIES in Tanzania,its your convising power 'MONEY"

    ReplyDelete
  8. Huyu Ernest ni mwenyeji wa Kigoma?kama ni yeye mimi ninamfahamu sana na alikua anajulikana kama Ene enzi za Kigoma Primary School,baadae tulikuanae South Africa,alikua msanii ile mbaya,na pesa nyingi saana,sasa yupo jela bongo!!!Pole saana mchizi wa kigoma,na hongera kwa kula nondozzz, unawakilisha.Mdau Bondeni.

    ReplyDelete
  9. We anaoy wa hapo juu embhu kafungwe na wewe uone kama utaweza kusoma na kuelewa na kufaulu.
    open uni mtu yoyote anaweza kumudu kulipia hata ombaomba maana kwa mwaka ni shilingi elfu 30 sasa unaweza kwenda jela kwa 30 ili usomeshwe?
    Acha uzuzu wewe na hapo inaonyesha huna degreee

    ReplyDelete
  10. Mbona kafanana na Laurence Masha, mheshimiwa waziri. Je ni ndugu yake??

    ReplyDelete
  11. Huyo mdau wa 04:07:00 mbona unaongea maneno ya mauz sana,yaan unataka kuzuia wafungwa wasisome?
    Sijui nikuelewesheje labda nikupe mfano,wewe unawatoto mtoto wako mmoja kafanya kosa ukampa adhabu inamaana huyo aliyefanya kosa ukamwazibu akipata nafasi ya kusoma hutampeleka kusoma kwa sababu alifanya kosa? Halafu naomba nikueleweshe mtu akiwa criminal hawezi kunyimwa haki zake za msingi kabisa na yeye ndiye anayestahili hasaa kupata nafasi ya kusoma ya upendeleo ili aelimike asifanye uhalif tena.Mwisho napenda kumpongeza sana mkuu wa chuo kikuu huria,Magereza na serikali kwa ujumla hili jambo linalofanyika ni la maana sana na nawapa big up wasikatishwe tamaa na watu wasiopenda maendeleo na ikiwezekana magereza yote watu wasomeshwe kuanzia level ya chini.

    ReplyDelete
  12. Iringa ndo umeona matakoni mwa nchi kiasi kwamba huduma kama hizi hazifiki! Shika adabu yako!

    Uliza uambiwe!

    ReplyDelete
  13. Achana na huyo mdau wa 4:07:00,ni bwege na hajui analoongea,kifupi mteme! nenda shule kaka/dada,upeo wako mdogo sana!

    ReplyDelete
  14. nahisi huyu mtu wa tatu hajui asemacho.......being a crimal doesnt men you are not suppose to get other rights including right to education, hivyio hauna ubaya wowote uliofanyika, na mimi sidhani ni serikali imempeleka ernst am sure it a self dertmination.................big up ernest, and we need more peole like him, kuwa jela si mwisho wa dunia, if you have a chance just grab it. melisa lyimo

    ReplyDelete
  15. Yaani wewe mdau uliyesema iringa ni matakoni mwa Nchi akili zako ni kama za yule aliyeandika Wafungwa wasipate degree.
    Mtu katolea mfano tu,maana hiki chuo kiko Dar,kwa iyo kama mtu anataka kusoma na yuko,Mwanza,Musoma,Iringa,Mbeya na kwengineko anaweza kusoma,
    kwani kuna wangapi wako Bongo lakini watu wanasoma chuo cha Marekani or nchi nyingine za ulaya kwa njia ya posta,kwa maana sasa Tz iko matakoni mwa Nchi?,
    Fikiri kabla ya kuandika

    ReplyDelete
  16. ..ERNEST MICHAEL,SIO NDUGU WA WAZIRI.JAMAA NI MTU WA KIGOMA,NA ANATOKA KWENYE FAMILIA KUBWA NA YENYE WASOMI WENGI.ERNEST,AMESOMA KIGOMA PRIMARY SCHOOL FRM 1981-87.AKAENDA O-LEVEL KILOSA SEC,THEN AKARUDI KUMALIZIA KGM SEC.SCHOOL.AKAENDA A-LEVEL AZANIA KUCHUKUA PCM...FROM THERE SIJUI ALIELEKEA WAPI.ILA NAMPA PONGEZI KWA ELIMU ALIYOIPATA.HUU NI MFANO MZURI.HONGERA SANA ENE-MDAU-USA.

    ReplyDelete
  17. Huyu ni mdogo wake Masha. Angalia kwa mbali utaona Masha na amekuja kushuhudia mdogo wake akichukua shahada ya sheria. Ndio uzuri wa sheria, kila mtu anaweza kusoma, na anaweza kusoma akiwa popote.

    ReplyDelete
  18. yani apa natetemeka kwa kucheka dah
    michuzi blog idumu

    annon Wed Dec 02, 01:27:00 PM u made my day dahh

    ale muyagoo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...